NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Benki ya CRDB katika kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa elimu ya fedha kwa taasisi zisizokuwa za kiserikali zipatazo 22 za Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa zaidi juu ya umuhimu wa kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo.
Pia benki hiyo sambamba na hilo imeweza kuzipa mbinu mbali mbali pamoja na kuzishauri taasisi hizo kuweka mikakati ya kufungua akaunti ya NIA MOJA ambayo ni akaunti mahsusi kwa vikundi na haina makato yoyote ya kila mwezi.
Hayo yamebainisha na Meneja wa biashara wa CRDB tawi la Kibaha mjini Richard Mkakala wakati wa kikao kazi maalumu ambacho kilizikutanisha taasisi zizosokuwa za kiserikali kwa ajili ya kujadili mambo mbali mbali yanayohusiana na uchukuaji wa fedha na utunzaji wake kupitia mfumo wa kufungua akaunti.
Meneja huyo Mkakala alisema kwamba kwa sasa benki ya CRDB wameanzisha akauniti ya NIA MOJA ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuweka fedha za taasisi ili ziwe katika hali ya usalama katika kipindi chote bila wasiwasi.
Kadhali Meneja huyo alifafanua kwamba wanachama hasa kwa upande wa wanawake wanashauriwa kufungua akaunti ya iMBEJU ili wazitumie katika kuweka akiba zao na kupitisha mapato ya biashara zao mbali mbali kwa urahisi zaidi.
" Ninyi wanachama mkiwa na akaunti za CRDB, mnayo fursa kubwa zaidi kupitia katika hizi taasisi zenu kuweza kunufaika na mpango wa uwezeshaji unaowalenga wanawake kuwapa mitaji midogogo kwa ajili ya kuendeleza biashara zenu ili ziweze kukua na kuwa kubwa,"alifafanua Meneja huyo.
Kadhalika aliongeza kuwa lengo lao kubwa ni kuziwezesha taasisi hizo ili ziweze kujikwamua kiuchumi kwa masharti nafuu ambayo wanaweza kuyamudu lengo ikiwa waweze kutimiza malengo yao waliyojiwekea.
"Kwa kweli sisi kama benki ya CRDB kwa sasa tuna uwezeshaji huu wa kuziwezesha taasisi mbali mbali mbali zisizokuwa za kiserikaki na kiukweli unatolewa kwa masharti nafuu sana na benki yetu,"aliongeza Meneja huyo.
Katika hatua nyingine alizishauri na kuzihimiza taasisi zote ambazo zimesajiliwa rasmi hiyo nazishauri kuhakikisha zinafungua akaunti ya CRDB ili kuwa na uhakika zaidi juu ya usalama wa fedha zao.
Pia aliongeza kuwa wananchi wanapaswa kuhakikisha wanajiunga katika vikundi mbali mbali na kuvisajili ili viweze kutambulika na kupata fursa ya mikopo katika benki hiyo kwa masharti nafuu zaidi.
Benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu mbali mbali kwa taasisi zisizokuwa za kiserikali pamoja na wanachi juu ya umuhimu wa kufungua akaunti ili kuweza kutunza fedha zao zikiwa katika hali ya usalama.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.