ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 21, 2019

TPDC YAMPA TUZO PROF. MARK MWANDOSYA

 
HIVI Karibuni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), lilifanya Maadhimisho ya Miaka 50. Ambapo mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Mh. Majaliwa Kassimu Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye aliwakilishwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuuu- Uwekezaji Mhe. Angela Jasmine Kairuki. 

 Pamoja na Maadhimisho hayo, TPDC ilitoa TUZO kwa baadhi ya WASTAAFU waliokuwa na michango mbalimbali katika utumishi wao. Pichani juu Bi Marie Msellemu, MKUU wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa TPDC, akimkabidhi Prof. Mark Mwandosya TUZO ya kuutambua mchango wake mkubwa kwa TPDC kwa nafasi yake kama Kamishna wa kwanza wa Petroli nchini na Mwenyekiti wa BODI ya Shirika la TPDC katika utumishi wake.
Picha ya pamoja.

NAIBU MEYA JOSEPH LYATA ATATUA TATIZO LA BARABARA YA DODOMA ROAD

NAIBU Meya Manispaa ya Iringa Joseph Lyata kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM Manispaa wameendelea kutekeleza ahadi ya kukarabati za Mitaa iliyopo kata ya Mtwivila kama ambavyo unawaona hapo kwenye picha
NAIBU Meya Manispaa ya Iringa Joseph Lyata akiwa anaangalia ukarabati barabara za Mitaa iliyopo kata ya Mtwivila
Baadhi ya watoto na wananchi wakiangalia ukarabati wa barabara ukiendelea katika mitaa ya kata ya Mtwivira

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

NAIBU Meya Manispaa ya Iringa Joseph Lyata kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM Manispaa wameendelea kutekeleza ahadi ya kukarabati za Mitaa iliyopo kata ya Mtwivila.

Akizungumza na wananachi wa Mtaa wa Dodoma Road C wakati wa kukarabati barabara hizo, Lyata amesema kuwa wameamua kukarabati barabara hiyo kutokana na ubovu uliokuwepo awali.

Lyata amesema kuwa anashangaa kuona Diwani wa kata ya Mtwivila kushindwa kukarabati barabara za mitaa hiyo huku akiwataka wananchi wa Kata hiyo kutoa taarifa katika ofisi yake na kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili.

Awali Lyata amebainisha kuwa Chama cha mapinduzi kimekuwa kikiwafikia wananchi wa chini na kujua changamoto zao na kisha kuzitatua.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa DODOMA ROAD C Mzee Said Mwachang’a amemshukuru naibu meya manispaa ya iringa Joseph Lyata kwa kuwarekebishia barabara hiyo kwani itafungua fursa ya wafanyabiashara kufika katika mitaa yao.

“Nikushukuru Naibu meya kwa kuja kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwani umeonesha wewe ni kiongozi wa watu na tunakupongeza kwa hili” alisema Mwachang’a

Nao baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Dodoma Road C wamebainisha kuwa baada ya ukarabati wa barabara hiyo utapelekea waweze kufanya shughuli zao bila tatizo.

Lakini diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula alisema kuwa chama cha mapinduzi na naibu meya wa manispaa ya Iringa walikuwa hawalali kwa ajili ya kutatua tatizo la barabara ya Dodoma Road  kwa kuwa wananchi hao wanahitaji kufanya kazi za kimaendeleo

“Wananchi wa kata ya Dodoma Road wanahitaji kufanya maendeleo kwa kuwa wamekuwa wachapa kazi wakubwa lakini mbunge wao amekuwa hawasaidie kwa lolote hivyo ndio chama na Naibu Meya walipobebe jukumu la kutatua changamoto hiyo” alisema Chegula

Chegula alisema kuwa kipaumbele kilikuwa kutatua changamoto ya barabara ndipo wanatafuta njia nyingine ya kutatua changamoto nyingine zilizopo katika mtaa wa Dodoma Road ili wananchi wafanye kazi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyotaka.

SEKRETARIETI YA MAADILI YATINGA MWANZA TAYARI KUFANYA UHAKIKI MALI ZA VIONGOZI WA UMMA.


SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma imetinga jijini Mwanza tayari kufanya uhakiki wa mgongano wa kimasilahi wa viongozi wa umma. 

Lengo la uhakiki huo ni kuangalia taarifa za mali na madeni kupitia tamko la rasilimali na madeni walizojaza viongozi hao, wenza wao pamoja na watoto wao walio chini ya miaka 18 kama zinawiana.

Jaji Nsekela amesema shughuli hiyo ni ya kawaida kwa sababu sekretarieti ilianzishwa ili kusimamia mienendo na tabia za viongozi wa umma pamoja na utekelezaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 pamoja na marekebisho yake.






Hatua hiyo inakuja ikiwa ni muendelezo wa uhakiki unaoendelea nchini ambapo umelenga viongozi  600 walioko kwenye mikoa 12 hapa nchini. 

Mbali na Mwanza mikoa mingine iliyolengwa na uhakiki huo ni pamoja na Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Geita, Kagera, Mara, Dodoma, Tabora, Singida, Dar es Salaam na Shinyanga.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa viongozi hao 600 wanaohusika na uhakiki huo, mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini wa taasisi hiyo, Honoratus Ishengoma alisema, “sheria yetu ukiiangalia vizuri kifungu cha 4 kinataja aina ya viongozi tunaowasimamia kutoka mihimili yote mitatu. Aina za viongozi wanaohakikiwa wanatokana na mihimili hiyo.”

Ingawa Ishengoma hakutaka kuwataka moja kwa moja majina yao baadhi yao ni; madiwani, wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala wa mikoa na wilaya, mahakimu pamoja na majaji.

Wednesday, June 19, 2019

NINI TAFSIRI YA BAJETI YA SERIKALI 2019 2020 KWA WAFANYABIASHARA NA UWEKEZAJI MWANZA



SIKU 5 baada ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango kuwasilishwa Bungeni Dodoma bajeti Kuu ya Serikali  ya Tanzania,  JOHN MONGELLA ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza anakutana na wadau wa Baraza la Biashara katika ukumbi wa mikutano ofisini  pake kujadili masuala mbalimbali ya biashara, fursa, changamoto na utatuzi wake.

Yawezekana kupitia kikao hiki unaweza kuvutiwa kufanya uwekezaji mkoani Mwanza....!!

Kupata yaliyojiri na kuzijua fursa zilizopo ungana nasi kufuatilia Video hii.


WAZAZI WATUMIA ZAIDI YA MILIONI 70 KUKARABATI SHULE YA MSINGI MAPINDUZI ENGLISH MEDIUM

 Mwenyekiti wa shule ya msingi Mapinduzi English medium Haliel Abdallah akionyesha jinsi gani ukarabati wa madarasa na ofisi sita za walimu za shule hiyo kwa lengo la kuboresha miundombinu ya shule hiyo
 Mafundi wakiwa kazini kuendelea na ukarabati wa majengo ya shule hiyo ya msingi Mapinduzi English medium iliyopo manispaa ya Iringa.
Mwenyekiti wa shule ya msingi Mapinduzi English medium Haliel Abdallah akiwa na kiongozi mwingine kwenye kama hiyo wakikagua ukarabati ambao unaendelea


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wazazi wa shule ya msingi Mapinduzi English medium iliyopo manispaa ya Iringa wameamua kuikarabati ili kuboresha mazingira ya shule kwa lengo la kukuza taaluma ya wanafunzi katika shule hiyo.

Akizungumza na blog hii mwenyekiti wa shule hiyo,Haliel Abdallah alisema kuwa shule hiyo ilikuwa na miundombinu mibovu ambayo ilikuwa sio rafiki kwa walimu na wanafunzi hivyo ilikuwa inachangia kutoingia kwenye shule nyingine za aina hiyo.

“Kwa kifupi sana kamati ilibaini kwamba mazingira ya madarasa pamoja na ofisi za walimu hazikuwa rafiki hivyo tukaamua kuanza kufanya tathimini kwa lengo la kuanza kukarabati shule hiyo ili irudi kwenye ubora kama uliokuwepo hapo awali” alisema Abdallah 

Abdallah alisema kuwa lengo la kujenga darasa jipya katika shule hiyo ili kupanua wigo wa kuwa na vyumba vingi ambavyo vitatuasaidia kuleta ushindani na shule nyingine zenye mchepuo wa masomo ambayo yanafundishwa kwa lugha ya kingereza 

“Tunataka kuhakikisha kuwa shule hii inakuwa kwenye ubora wa hali ya juu kwenye miondombinu kuanzia madarasa,ofisi za walimu na mazingira ya shule lazima yawe ya kuvutiwa kwa walimu,wanafunzi na hata wazazi wawe wanajisifia watoto wao kusoma katika shule hiyo” alisema Abdallah

Abdallah aliongeza kwa kusema kuwa katika ukarabati huo utahusisha pia ukarabati wa madawati pamoja kuhakikisha walimu wanakuwa na samani  bora ambazo nazo zinakuwa rafiki na mazingira ya kufundishia na kuandalia masomo.

Aidha Abdallah amewapongeza wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule hiyo kwa kujitoa kukakikisha shule hiyo inakarabatiwa kwa lengo la kuwa nashule yenye kushindana na shule nyingine zilizopo mkoani Iringa na nje ya Iringa.

Awali akitoa taarifa ya hali ilivyokuwa hapo awali walimu mkuu wa shule hiyo Emanuel Mwakyusa alisema kuwa miundombinu ya shule hiyo haikuwa rafiki kwa kutoa elimu iliyobora kwa kuwa madarasa na majengo mengi yalikuwa chakavu sana.

“Madarasa mengi yakuwa chakavu hivyo ikawa ngumu kufanya usafi kukiwa na mashimo,paa zilikuwa zimechoka na kuvujisha maji kipindi cha vua hiyo hali ya usafi ilikuwa mbaya na kusababisha kutoa elimu ambayo ilikuwa haistahili” alisema Mwakyusa

Mwakyusaalisema kuwa ukarabati huo umefanywa na wazazi tu bila kuigusa serikali kwa kuwa wazazi hao wanapenda kufanya maendeleo kwa lengo la kuhakikisha waoto wao wanasoma katika mazingira yaliyo bora.

“Mimi niwapongeze wazazi ambao watoto wao wanasoma katika shule hii kwa kujitoa kwa moyo wao wote kuhakikisha kuwa shule hii inakarabatiwa vilivyo na kuwa na mazingira yaliyo bora” alisema Mwakyusa

Mwakyusa alisema kuwa ukarabati huo utasaidia kukuza taaluma za wanafunzi wa shule hiyo kwa kuwa miundombinu itakuwa imeboreshwa vilivyo na itakuwa rafiki wa pande zote
Kwa upande wake mwalimu Rahab Mahenge alisema uboresha wa miundombinu ya shule hiyo kutachangia kuongezeka kwa ufaulu kwa kuwa watu wote watakuwa na furaha na mazingira yaliyopo.

TANZANIA YASEMA IMETEKELEZA VYEMA MKAKATI WA EITI

Waziri Doto Biteko  akishiriki mkutano wa kimataifa wa uwazi na uwajibikaji unaofanyika jijini Paris

Waziri wa madini Doto Biteko alisema hayo kwenye mkutano wa nane wa Kidunia wa uwazi na uwajibikaji unaofanyika jijini Paris Ufaransa kuwa, Tanzania imetekeleza vyema mkakati wa uwazi na uwajibikaji kwenye kulinda rasilimali za Nchi kwa kuifanyia marekebisho sheria ya madini ya mwaka 2010 ili iendane na matakwa ya mkakati huo.

Katika kuhakikisha uwazi unakuwepo serikali iliamua kufanya marekebisho na pia kuanzisha sheria ya uwazi na uwajibikaji ya mwaka 2015 ili kuweka jambo hilo kisheria.

Pia wakati akijibu swali toka kwa wachangiaji alisema kuwa, hatua ya seikali kuanza kuweka sheria mbali na mikataba kwenye tovuti ni hatua ya mafanikio ambayo inaongesha utayari na katika kuhakikisha watanzania wanajua madhui zaidi ya sheria hizo na mikataba basi ni wazi kuwa uwepo wa asasi za kiraia unaonekana hapo kwa kuwa zinawajibu wa kufanya kazi na serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanafikia na kupata kujua nini kimeandikwa ndani ya mikataba hiyo.

Biteko ameeleza kuwa Tanzania ipo tayari kuemdelea kutekeleza makakti huo na pia hata Nchi nyingine zije kujifunza toka Tanzania.

Mkutano huo wa kidunia unajumuisha zaidi ya washiriki 1000 na nchi 100 zinazokutana na kujadili utekelezaji wa mkakati huo.

Washiriki toka Tanzania wametoka serikalini, asasi za kiraia na waandishi wa habari.

Shirika la kimataifa la Hivos Afrika ya mashiriki lilichukua jukumu la kuwasafirisha baadhi ya washiriki tika asasi za kiraia na waandishi wa habari ili wahudhurie mkutano huo na kuongeza weledi wa kufuatilia uwazi na uwajibikaji kwenye kulinda rasilimali za Nchi.

TASAF YAWAJENGEA UELEWA VIONGOZI KUHUSU MAJARIBIO YA UTAMBUZI WA KAYA ZA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI SEHEMU YA PILI MKOANI MTWARA.

.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF(aliyesimama) akizungumza kwenye kikao kazi cha viongozi ,watendaji na wawezeshaji wa majaribio ya utambuzi wa Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika  Mtwara.
Na .Estom Sanga-Mtwara. 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeanza mkakati wa kuwajengea uelewa viongozi ,Watendaji na Wawezeshaji katika ngazi ya halmashauri za Wilaya juu ya zoezi la utambuzi wa Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini ili kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa ufanisi mkubwa . 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kilichofanyika mjini Mtwara, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,bwana Ladislaus Mwamanga amesema zoezi hilo linakusudia kuboresha mapungufu yaliyojitokeza kwenye sehemu ya kwanza ya utekelezaji wa Mpango huo inayotarajiwa kukamilika hivi karibuni na kuwa majaribio hayo ambayo kwa kiwango kikubwa yatatumia njia ya mfumo wa kompyuta yatafanyika katika Halmashauri za wilaya ya Siha,Mtwara na Tandahimba. 

Bwana Mwamanga amesema baada ya kukamilika kwa majaribio hayo, kazi ya kutambua Kaya za Walengwa watakaojumuishwa kwenye Mpango itafanyika nchini kote ili kutekeleza maagizo ya Serikali ya kujumuisha maeneo yote kwenye shughuli za Mpango. Katika Awamu ya Kwanza ya Mpango serikali kupitia TASAF imeweza kutekeleza Mpango huo kwa asilimia 70 ya mitaa/vijiji/shehia na hivyo asilimia 30 iliyosalia itakamishwa katika sehemu ya pili ya Mpango itakayotekelezwa kwa takribani miaka mitano ijayo. 

Akifafanua Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema mkazo mkubwa katika sehemu ya pili ya Mpango imewekwa zaidi katika kuhamasisha Walengwa wa Mpango kufanyakazi kwenye miradi ya Maendeleo watakayoiibua na kisha kulipwa ujira ili waweze kujiongezea kipato na kupunguza adha ya umaskini. 

“…tumeweka mkakati bora zaidi ya kutekeleza maagizo ya serikali ya kupunguza dhana ya Walengwa wa Mpango kuwa tegemezi” amesisisitiza bwana Mwamanga. 

Amewahimiza Viongozi,Watendaji na Wawezeshaji kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya utambuzi wa Kaya za Walengwa ili kuondoa uwezekano wa kaya zenye uhitaji kutojumuishwa kwenye Mpango na hivyo kuondoa manung’uniko baada ya kuanza kwa sehemu ya pili ya Mpango unaotarajiwa kuzifikia takribani Kaya milioni 1.3 ikilinganishwa na Kaya Milioni 1.1 zilizoandikishwa katika sehemu ya Kwanza. 

Bwana Mwamanga amesema kutokana na usimamizi thabiti wa Serikali katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, kumekuwa na mafanikio makubwa kwa Kaya za Walengwa kuanza kuboresha maisha yao huku sehemu kubwa ya kaya hizo zikitumia fursa ya kuwemo kwenye Mpango kuanzisha shughuli uzalishaji mali jambo ambalo amesema limeendelea kuvutia Wadau mbalimbali wa Maendeleo kutaka kuchangia zaidi raslimali fedha na Utaalam. 

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara bwana Evold Mmanda amesema TASAF kwa kiwango kikubwa imekuwa kielelezo bora cha kuwafikia wananchi wanaoendelea kuishi katika mazingira ya umaskini kutokana na namna Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini walivyotumia fursa hiyo kupunguza athari za Umaskini. 

Bwana Mmanda amewataka viongozi katika maeneo ya utekelezaji wa shughuli za Mpango kuendelea kuwahamasisha wananchi kuuchukia umaskini kwa vitendo jambo ambalo amesema linawezekana ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evold Mmanga (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao kazi cha viongozi ,watendaji na wawezeshaji wa majaribio ya utambuzi wa Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika  Mtwara.
 Mtaalamu wa Mafunzo na Uwezeshaji wa TASAF Bi. Mercy Mandawa akitoa maelezo katika kikao kazi cha viongozi,watendaji na wawezeshaji kuhusu utekelezaji wa majaribio ya utambuzi wa kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
 Baadhi ya Washiriki wa kikao kazi cha kujenga uelewa wa uetekelezaji wa majaribio ya utambuzi wa kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini (picha ya juu na chini).

 Picha ya pamoja

ROTARY CLUB UDSM MLIMANI WAPATA RAIS MPYA DK HERI TUNGARAZA

UONGOZI NI KUPOKEZANA VIJITI: Rais Mpya wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Dk Heri Tungaraza (kushoto) akiwa na Rais Mstaafu Lulu Tunu Kaaya (kulia) wakionyesha ishara ya upendo mara baada ya Bi. Catherine Njuguna wa Rotary Club Dar es Salaam Mikocheni (katikati) kumaliza zoezi la makabidhiano kumalizika.
Rais Mpya wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Dk Heri Tungaraza (kushoto) akizungumza machache mara baada ya kutangazwa kuongoza kwa muda wa mwaka mmoja.
Rais Mstaafu wa Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Lulu Tunu Kaaya akizungumza wakati wa halfa ya kumsika Rais Mpya Dk Heri Tungaraza.
Mwanachana wa Rotary Club  Dar es Salaam Mikocheni, Bi. Catherine Njuguna wa Rotary Club Mikocheni (kushoto) akiongea na na Rais Mstaafu Lulu Tunu Kaaya (kulia).
Akivalishwa...
Rais Mstaafu wa Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Lulu Tunu Kaaya (kushoto) akikabidhiwa zawadi na Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi (kulia).
Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi akitoa zawadi.
Wanachama wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam wakipata burudani.
Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi (kushoto) na Edwin Mashayo (kulia).
Rais Mpya wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam, Dk Heri Tungaraza akimkabidhi zawadi Mwanachana Prof. David Mfinanga ikiwa ni heshima ya kuweza kuifanya club ya UDSM Mlimani kusonga mbele.
Mwanachana wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam Prof. David Mfinanga akitoa shukrani mara baada ya kukabidhiwa zawadi.
 Mwanachama wa Rotary Club Catherine Dar North Club akizungumza machache.
Mwanachama wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam Mona Mwakalinga.
Mwanachama wa  Rotary Club UDSM Mlimani jijini Dar es Salaam Adolpho Mascharenas akizungumza machache.
Wanachama wa Rotary Club UDSM Mlimani Prof. Abel Ishumi akitoa wosia kwa uongozi mpya.
Picha ya pamoja na Rais Mpya...

Wanachama wakibadirisha mawazo.
Burudani ikiendelea...
Picha ya pamoja na rais Mpya.