ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 1, 2024

Mashujaa FC 0-1 Simba SC | Highlights | NBC Premier League 01/10/2024

 Steven Mukwala ameifungia Simba goli pekee na la ushindi dakika ya mwisho ya mchezo, dhidi ya Mashujaa FC, kwenye Dimba la Lake Tanganyika, Kigoma.....

Tazama matukio yote muhimu ya mchezo huu.... Hii ni #NBCPremierLeague

MADKATARI WABOBEZI HOSPITALI YA MUHIMBILI WAREJESHA SAUTI YA MTOTO MALIKI KWA ASILIMIA 100

 


NA VICTOR MASANGU, DAR


Sauti ya mtoto Maliki Hashimu (6), mkazi wa Goba, Jijini Dar es Salaam imerejea kwa 100% baada ya kukamilisha hatua zote za matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na majeraha makubwa aliyopata yaliyotokana na kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni Julai mwaka huu, kilichotenganisha njia ya hewa chini ya sanduku la sauti na kusababisha ashindwe kupumua, kuongea, kupata maumivu pamoja na kupoteza damu nyingi.  


Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu maendeleo ya kitabibu ya mtoto huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi amesema matibabu ya mtoto Maliki yamefanyika hatua kwa hatua na watalaam wamejiridhisha kulingana na huduma alizopata mtoto huyo kwa kurejesha kila kilichokuwa kimepata hitilafu kwenye shingo yake na kwamba sasa yupo salama kuendelea na shule na maisha yake ya kawaida.

Naye Mbobezi wa Upasuaji Shingo na Mkuu wa Idara ya Pua Koo na Maskio, Dkt. Aslam Nkya, amesema mtoto huyo alipofikishwa hospitalini alikua na jeraha mbele ya shingo, lililoharibu tezi la mbele liitwalo (thyroid gland) baada ya kukatwa katikati na kusababisha mtoto huyo kuvuja damu kwa wingi, kupata maumivu makali sehemu iitwayo (trachea) ambako hewa inayotoka kwenye mapafu hupita ili iweze kwenda kwenye sanduku la sauti kumuwezesha kuhema na kuongea kwa mantiki ambavyo vyote vimerejeshwa katika hali yake ya kawaida.

Mama mzazi wa mtoto huyo Bi. Shani Charles kipekee amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kulipa gharama za matibabu ya mtoto huyo kiasi cha TZS. 15Mil, watoa huduma wote wa Hospitali walioshiriki kumuhudumia mpaka hatua aliyofikia leo kuruhusiwa moja kwa moja, jamii ya watanzania walioguswa na tukio hilo pamoja na vyombo vya habari vilivyofuatilia kwa karibu jambo hilo.

CHAMA TAWALA BOTSWANA CHAKATALIWA BAADA YA MIAKA 58 MADARAKANI.

Wapiga kura nchini Botswana wamekikataa chama tawala cha muda mrefu cha nchi hiyo katika matokeo ambayo yanaashiria mtikisiko wa kisiasa katika taifa hilo lenye utajiri wa almasi kusini mwa Afrika.


 Chama cha Kidemokrasia cha Botswana (BDP) kilichokuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1966 kilikuwa kimeshinda kiti kimoja tu cha ubunge kufikia mapema Ijumaa asubuhi, matokeo ya awali ya uchaguzi yanaonyesha. 

 Chama cha Umbrella for Democratic Change (UDC), kinachoongozwa na wakili wa haki za binadamu Duma Boko, kilishinda viti 20, kulingana na hesabu za awali. UDC kinaonekana kitaunda serikali huku kikitarajiwa kupitisha kizingiti cha viti 31 kwa wingi wa wabunge.

 Wabunge wanapomchagua rais nchini Botswana, Duma Boko yuko mbioni kuwa mkuu wa nchi mara tu bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza. Boko, ambaye anagombea kwa mara ya tatu, amewataka wafuasi wake "kudumisha umakini na nidhamu". 

 Licha ya kusimamia mabadiliko makubwa nchini Botswana, ukuaji duni wa uchumi wa hivi karibuni na ukosefu mkubwa wa ajira ulidhoofisha umaarufu wa BDP. 

 Atachukua nafasi ya Mokgweetsi Masisi ambaye aliingia madarakani tangu 2018 na kuongoza kampeni ya BDP iliyoshindwa kupata matokeo mazuri ya kura. Katika kampeni yake Rais alinadi ujumbe kwamba chama chake kinaweza kuleta "mabadiliko", lakini hakuna wapiga kura wa kutosha waliokuwa na imani kwamba BDP knaweza kufanya kile ambacho nchi inakihitaji.

Wednesday, October 30, 2024

HOSPITALI YA TAIFA MLOGANZILA YAJIZATITI KUBORESHA HUDUMA KWA WAGONJWA WA KIHARUSI

 


VICTOR MASANGU,MLOGANZILA


Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tawi la Mloganzila katika kukabiliana  na changamoto ya wimbi la kuwepo kwa  idadi kubwa ya wagonjwa wa ubongo,mishipa ya fahamu  na  kiharusi imeamua kutoa elimu  maalumu  kwa wananchi kwa lengo kujikinga na magonjwa hayo.

Hospitali hiyo  mbali na kutoa elimu hiyo pia imeweza kutoa huduma mbali mbali za upimaji wa afya wa magonjwa kutoka kwa madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila.


Hayo yamebainishwa na Naibu mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila Dkt. Judith  Magandi wakati wa maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa kiharusi duniani.

Naibu Mkurugenzi huyo ametumia fursa hiyo kuwahimiza  wagonjwa wenye changamoto za kiharusi wajitokeze  ili waweze kupatiwa tiba sahihi kwa wakati kwa lengo la kuepuka madhara zaidi.

Dkt. Magandi amesema  kwamba  tatizo la kiharusi ni kubwa na kuongeza kuwa kwa MNH-Mloganzila katika kliniki ya ubongo na mishipa ya fahamu ambapo kwa  siku moja  wanaona  wagonjwa kati ya 140 hadi 170 ambapo kati ya wagonjwa hao asilimia 60 wanabainika kuwa na kiharusi.

“Baada ya kuona ukubwa wa tatizo la kiharusi Muhimbili Mloganzila tumeamua kuboresha huduma za magonjwa ya kiharusi kwa kuanzisha kitengo maalum cha kuhudumia wagonjwa wenye kiharusi ambapo tumeweka vifaa tiba vya kisasa vyenye uwezo wa kufuatilia mwenendo wa mgonjwa kwa wale wagonjwa ambao wamelazwa wodini.

Kwa Upande wake Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Ubongo na Mishipa ya Fahamu MNH-Mloganzila Dkt. Mohamed Mnacho amesema kuwa ugonjwa wa kiharusi ni moja kati ya magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo na ulemavu duniani.

Pamoja na hayo, amesema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kuwa zaidi ya watu milioni 12 duniani wanatatizo la kiharusi ambapo kati ya hao watu milioni 6 hupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo kwa mwaka. 

Aidha ameiomba  jamii kuacha kabisa na  baadhi ya tabia ambazo zinaweza kuchangia watu kupata ugonjwa wa kiharusi ikiwemo uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi, uzito mkubwa pamoja kutokufanya mazoezi.



Nao baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbali mbali  ambao wamepatiwa mafunzo ya kujikinga na ugonjwa huo wamesema kwamba elimu waliyoipata kutoka kwa madaktari bingwa itakwenda kuwasaidia.


Siku ya kiharusi Duniani uadhimishwa Oktoba 29 kila mwaka ambapo kwa Muhimbili Mloganzila imeadhimisha siku hiyo kwa kutoa huduma mbalimbali bure ikiwemo upimaji wa shinikizo la damu, elimu ya lishe pamoja na ugonjwa wa kiharusi.


SERIKALI YAENDELEA KUTENGA FEDHA KUTEKELEZA MIRADI 77 YA MIUNDOMBINU YA BARABARA NCHINI

 


NA MWANDISHI WETU,DODOMA


Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na utekelezaji wa miradi 77 ya ujenzi wa barabara na madaraja kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) yenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.6.

Aidha, Serikali kupitia TANROADS tayari imekamilisha kwa asilimia 100 miradi 25 ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1,198 iliyogharimu Shilingi Trilioni 1.68 katika kipindi cha utawala wa Rais Dkt. Samia.


Haya yamebainishwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Mohamed Besta wakati wa akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma (Dodoma Outer Ring Road) kwa kiwango cha lami sehemu ya pili inayoanzia Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (km 60).

Eng. Besta ameeleza tangu Rais Samia aingie madarakani ameweka kipaumbele katika ujenzi wa barabara na madaraja ili kurahisisha usafiri na usafirshaji na kwa sasa Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi 77 ya ujenzi wa barabara na madaraja yenye thamani ya takribani Triloni 4.6.


“Kazi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja inaendelea kwa kasi maeneo mbalimbali nchini na hakuna mradi uliokwama kwasababu Serikali ya Rais Samia imekuwa ikilipa wakandarasi kulingana na mikataba”, amesema Besta.

Besta ameongeza kuwa hadi sasa Shilingi Bilioni 101.1 zimelipwa kwa Makandarasi katika miradi 24 ya barabara inayoendelea kutekelezwa pamoja na miradi ya minne (4) ya ujenzi wa viwanja vya ndege nchini.

Kadhalika, Besta ameeleza kuwa ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigogo Busisi) ambalo linagharimu Shilingi Bilioni 717 limefikia zaidi ya asilimia 94.

Amefafanua kuwa kutokana na mafanikio ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja nchini imeifanya Tanzania kuwa nafasi ya 6 kati ya nchi 54 za Afrika kuwa na mtandao bora wa barabara ikipanda kutoka nafasi ya 16 iliyokuwapo katika mwaka 2022 kulingana na Takwimu za Statista.com.

Monday, October 28, 2024

JUNGULU-CCM KATA YA PICHA YA NDEGE KUNOGILE TUMEJIPANGA KUSHINDA MITAA YOTE

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 



Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Picha ya ndege iliyopo katika Halmashauri ya Kibaha mji Grace Jungulu amewahimiza wanachama wote kuhakikisha kwa sasa wanavunja makundi yote na kuungana kwa pamoja na kueleleza nguvu ili kushinda kwa kishindo  katika uchaguzi wa serikali za mtaa.

Jungulu ameyasema hayo wakati akizungumza na baadhi ya viongozi na wanachama wa ccm ikiwa ni baada ya kumalizika kwa zoezi la kura la maoni kwa ajili ya kuwapata wagombea ambao watakiwakilisha chama katika uchaguzi huo.

Alisema kwamba mchakato wa kura za maoni umeshafanyika na kumalizika  hivyo.mgombea ambaye atakwenda kukiwakilisha  chama wa CCM inapaswa apewe ushirikiano wa kutosha na kuweka kabisa tofauti ambazo zilikuwepo hapo awali kwani wote lengo ni moja katika kukijenga na kikiimarisha  chama.

"Kwa kweli mimi ninashukuru Mungu kama Mwenyekiti tumeweza kushirikiana bega kwa bega na wana ccm wenzangu tangu hatua za awali kwenye matawi lakini kitu kikubwa kwa sasa inapaswa kuvunja makundi yote ili tuungane kwa pamoja katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na nia yetu ni kushinda mitaa yote,"alisema Jungulu.


Aidha Mwenyekiti huyo hakusita kuwapongeza kwa dhati viongozi wenzake pamoja na wanachama wote kwa kuanzia ngazi za mashina na matawi hata ngazi ya kata kwa kushirikiana bega kwa bega katika suala zima la kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la makazi kwa ajili ya kupiga kura.


Katika hatua nyingine alibainisha kwamba yeye kama Mwenyekiti wa CCM Kata ya Picha ya ndege ataendelea kukijenga na kukiimarisha chama ikiwa pamoja na anashinda kwa kishindo katika mitaa yote katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Nao baadhi ya wana chama wa CCM Kata ya picha ya ndege walimshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wao kwa kujitahidi kwa hali na mali katika kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo ikiwa pamoja na kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa wingi katika daftari la makazi kwa ajili ya kupiga kura.

BASHUNGWA ACHARUKA AMPIGIA SIMU KATIBU MKUU AMTAKA KUPIGA KAMBI MAFIA

 

 
“Msitoke Mafia mpaka Kivuko kianze kutoa huduma kwa Wananchi”

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amempgia simu na kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Eng. Aisha Amour na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ufundi na Umeme (TEMESA), Lazaro Kilahala kufika mara moja katika Kisiwa cha Mafia kupiga kambi kusimamia matengenezo ya Kivuko cha MV Kilindoni na kuhakikisha hawatoki mpaka huduma ya usafiri wa kivuko kati ya Nyamisati - Mafia itakaporejea na kutoa huduma kwa wananchi.

Bashungwa ametoa maelekezo hayo wakati akitoa ufafanuzi kwa Wananchi kuhusu kusimama na kukosekana kwa huduma ya usafiri wa vivuko katika Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani ambapo Wananchi wamelalamikia kukosa huduma ya vivuko na kupelekea kutumia vyombo vya usafiri visivyo salama na uhakika pamoja na kushindwa kusafirisha bidhaa na huduma nyingine.

“Katibu Mkuu kufika kesho kutwa wewe au Naibu Katibu Mkuu uje hapa Mafia uambatane na Mtendaji Mkuu wa TEMESA mpige kambi muone kilio na uchungu wa wananchi wa Mafia wanaoupata, Msitoke hapa mpaka kivuko kianze kutoa huduma kwa wananchi. Kivuko kikianza kufanya kazi ndio mnipigie simu niweze kuwaruhusu kutoka huku Mafia”, amesisitiza Bashungwa.

Waziri Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inatambua usafiri unaotumika kufika katika kisiwa cha Mafia ni usafiri wa vivuko na ndege ambapo sasa Serikali inaendelea na jitihada za kurejesha huduma ya usafiri wa vivuko kwa kuwa sio wananchi wote wana uwezo wa kutumia usafiri wa ndege.

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inaendelea na ukarabati wa Meli ya TNS Songosongo itayosaidia kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi wa Mafia wakati Kivuko cha MV Kilindoni kikiwa kwenye matengenezo.

Bashungwa ameeleza kuwa Serikali imetenga fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 9 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma za usafiri kati ya Mafia na Nyamisati na hivyo kuongeza idadi ya vivuko kuwa vitatu.

Katika nyakati tofauti, Wananchi wa Kilindoni Wilayani Mafia wameiomba Serikali kusimamia na kutatua kero ya huduma ya usafiri wa vivuko wanayoipata katika Wilaya hiyo ambayo imesababisha kuongezeka kwa gharama za maisha na wananchi kushindwa kupata huduma nyingine za kijamii.

Benki ya CRDB Yatunukiwa Tuzo za 'Benki Bora' na 'Benki Salama' Tanzania na Jarida la Global Finance

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto), akipokea tuzo ya 'Benki Bora Tanzania' kutoka kwa Joseph Giarraputo, Mwanzilishi na Mhariri Mkuu wa Global Finance, katika hafla iliyofanyika Washington D.C. tarehe 26 Oktoba 2024. Katika hafla hii, iliyofanyika sambamba na Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, Benki ya CRDB pia ilitunukiwa tuzo ya 'Benki Salama.

Na Mwandishi Wetu.

Washington D.C., 26 Oktoba 2024 – Benki ya CRDB imetambuliwa kwa mara nyingine kama kinara katika sekta ya benki Tanzania kwa kushinda Tuzo ya ‘Benki Bora Tanzania’ na ‘Benki Salama Tanzania’ zilizotolewa na Jarida la Global Finance kwenye hafla ya 31 ya Mwaka ya Tuzo za Benki Bora.

Tuzo hizo zimetolewa katika hafla iliyofanyika sambamba na Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia huko Washington, D.C. Hii ni mara ya tano mfululizo kwa Benki ya CRDB kushinda tuzo ya Benki Bora Tanzania na mara ya pili mfululizo kwa Benki Salama Tanzania – ikidhihirisha uimara wa Benki hii katika sekta ya fedha.

Mafanikio haya yanadhihirisha mkakati wa Benki ya CRDB wa kukua kwa njia endelevu inayowanufaisha wateja, wawekezaji, na uchumi wa Tanzania kwa ujumla.

Aidha, tuzo hizi ni kielelezo cha uongozi thabiti wa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Group, Abdulmajid Nsekela, na zinadhihirisha mchango wa Benki ya CRDB katika kuimarisha sekta ya fedha nchini Tanzania na ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Kati.

“Tunajivunia sana kwa kutambuliwa kwa mara nyengine kama Benki Bora Tanzania na Benki Salama katika tuzo za Global Finance,” alisema Nsekela. “Tuzo hizi ni ishara kwamba tupo kwenye njia sahihi ya ukuaji – kutoa huduma za kipekee kwa wateja wetu, thamani kwa wanahisa wetu, na kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya fedha nchini.”

Benki ya CRDB imekuwa na mwaka wa mafanikio makubwa kutokana na maboresho ya miundombinu ya kidijitali, ambayo imeongeza ufanisi na ubunifu katika utoaji wa huduma. Nsekela alisisitiza kuwa ukuaji wa Benki umetokana na mikakati madhubuti, hali ambayo imeifanya Benki hiyo kuwa chaguo la kwanza kwa Watanzania.

“Tuzo hizi hazionyeshi tu dhamira yetu ya kuwa Benki kinara katika utoaji wa huduma bora na zinazokidhi mahitaji halisi ya wateja – bali pia zinaonyesha namna gani tumekuwa tukisikiliza na kufanyika kazi maoni ya wateja na washirika wetu, na jinsi ambavyo wafanyakazi wanajitoa katika kutoa huduma bora,” aliongeza. “Ni heshima kubwa kuwa Benki Salama na Benki Bora Tanzania, tuzo hizi zinatupa nguvu ya kusonga mbele katika kuwawezesha Watanzania na kuimarisha nafasi yetu kimataifa.”

Ikiwa na rasilimali za zaidi ya Shilingi trilioni 14, Benki ya CRDB inashikilia nafasi kama benki kubwa zaidi Tanzania, inayotambulika kwa mafanikio endelevu katika viashiria vyotevya kiutendaji vya biashara.

Joseph Giarraputo, Mwanzilishi na Mhariri Mkuu wa Global Finance, amesema tuzo hizo pia zinatambua jitihada za Benki ya CRDB katika kukuza ujumuishi wa kifedha na kujenga imani ya wateja na wawekezaji akisema, "Katika mwaka uliopita, Benki ya CRDB imepiga hatua kubwa katika kutoa huduma bora na kujenga imani miongoni mwa wateja na wawekezaji ndani na nje ya nchi.”

Wakati wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) huko Washington D.C., Nsekela alishiriki pia kwenye mjadala maalum kuhusu mifumo ya malipo kidijitali ambapo alisisitiza dhamira ya Benki ya CRDB katika kukuza suluhisho za kidijitali zinazoboresha upatikanaji wa huduma za kifedha.

Aidha, Nsekela alishiriki vikao vya kimkakati na taasisi za kimataifa kama vile Benki ya Dunia, Exim Bank ya Marekani, MUFG, Yaatra Ventures, na TIAA Mfuko wa Pensheni wa Marekani unaolenga uwekezaji wa kimkakati barani Afrika, akilenga kufungua njia mpya za mitaji na kuiweka Tanzania kama kiungo muhimu kwenye uchumi wa dunia.

SMAUJATA TANGA YAWATAKA VIJANA KUCHAGUA VIONGOZI WATAKAOKUWA SAUTI YA WANANACHI

 

 


Na Oscar Assenga, TANGA

VIJANA Mkoani Tanga wametakiwa kuhakikisha wanawachagua viongozi ambao watakuwa sauti ya wananchi kwenye maeneo yao na sio wachuma tumbo wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu .

Wito huo ulitolewa leo na Mkuu wa Idara ya Vijana Hamasa Smaujata Mkoa wa Tanga Athumani Sheria wakati akizungumza na mtandao huu ambapo alisema vijana ni muhimu kuhakikisha wanashiriki kwenye uchaguzi huo kwa wingi ili waweze kuwachagua viongozi ambao watawapa maendeleo.

Alisema kwa sababu lazima viongozi wanaowachagua wawe ambao wanajitokeza na kuwa mstari wa mbele katika kusimamia maendeleo katika maeneo yao kwa kushirikiana na wananchi.
“Ndugu zangu vijana katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa tuhakikishe tunatumia haki yetu ya msingi kuwachagua viongozi ambao watakuwa sauti ya wananchi kwa kuchochea maendeleo na sio wachuma tumbo”Alisema Sheria

Hata hivyo aliwataka vijana kuhakikisha wanajitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi huo kutokana na kwamba mchango wao kwenye maeneo yao unaweza kuwa na tija kubwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo

Aidha pia alisema kwamba wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa uwekezaji wa Bilioni 429.1 katika Bandari ya Tanga ambayo yamewezesha maboresho makubwa na hivyo kuufungua kiuchumi mkoa huo.

Alisema maboresho hayo yamewasaidia kupata ajira lakini Serikali kuongeza pato pamoja na kuwainua kiuchumi vijana wa bodaboda na mama lishe ikiwemo wafanyabiashara mbalimbali mkoani humo.

Sunday, October 27, 2024

"BWANA SUKARI' ATUA JIJINI MWANZA KWA KISHINDO - KUTATUA TATIZO LA WANAOHARA KISA UCHAFU WA MIZANI!

 

NA. ALBERT G. SENG0/MWALONI/MWANZA 

IMEZOELEKA ukifika dukani ukaagiza bidhaa mathalani ya sukari, mara nyingi utapimiwa kwa mizani inayotumiwa pia kupimia bidhaa nyingine hasa nafaka kama vile maharage, mchele, na unga wa aina mbalimbali, hali inayozua hofu kuhusu usafi wa bidhaa ya sukari inayopimwa na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na bidhaa hizo kuacha unyevunyevu na kuganda kwenye sahani ya kipimio. Aidha, sukari hiyo huuzwa kwenye vifungashio visivyo salama, na mara nyingi mizani imekuwa haina majibu ya uhakika wa vipimo sahihi kwa wateja. #uchumi #samiasuluhuhassan #ikulumawasiliano #mwanza #morogoro #harmonize #zuchu #kanda #kilombero_sugar #Jembefm