Saturday, January 18, 2025
Thursday, January 16, 2025
RAIS SAMIA AFANYA KWELI KIBAHA TC ATOA PIKIPIKI 37 KWA MAAFISA UGANI
YANGA YAFUNGA DIRISHA DOGO KWA USAJILI WA JONATHAN IKANGALOMBO KAPELA.
SIMBA KUIKABILI CS CONSTANTINE UWANJA MTUPU BILA MASHABIKI
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeifingia klabu ya Simba kuingiza watazamaji katika mechi zake mbili za Kombe la Shirikisho Afrika baada ya vurugu zilizotokea kwenye mechi dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia Desemba 15, 2024 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Tuesday, January 14, 2025
MSIGWA ALIONEWA CHADEMA NDIYO AKAAMUA KUTIAMKIA CCM
NA ALBERT G.SENGO
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Januari 14, 2025.LEMA AMTEMA MBOWE HADHARANI AMSHAURI KUPUMZIKA NA KUMWACHIA LISSU UENYEKITI.
NA ALBERT G.SENGO
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amemshauri mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kusikiliza ushauri wa familia yake wa kumtaka kutogombea tena nafasi hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema hii leo Jumanne, Januari 14, 2025 Lema amesema anamheshimu Mbowe kutokana na kazi kubwa ya kukijenga chama hicho, lakini kwa sasa asikilize zaidi ushauri wa familia yake. Lema amesema Mbowe mara kadhaa amekuwa na nia ya kupumzika na kuwaachia nguvu mpya vijana kuendeleza mapambano, lakini watu wanaoitwa wanachama wamekuwa wakimshauri kuendelea kuwa mwenyekiti.Monday, January 13, 2025
VIONGOZI KUTOKA CHATO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO TFS - SHAMBA LA MITI SAOHILL
Sunday, January 12, 2025
Kamwe asema Yanga yaweza kumaliza kinara kwenye kundi lao
“Sisi tunaweza kumaliza pia tukiwa kinara kwenye hili kundi” maneno ya Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe akilichambua kwa undani kundi lao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).
Kamwe pia ameuchambua mchezo wao wa leo dhidi ya Al Hilal huku akimtaja Kocha Florent Ibenge. Kamwe amesema wachezaji wa Yanga wanaogelea pesa kutokana na motisha ambayo amekuwa akiitoa Mfadhili na Mdhamini wao Ghalib Said Mohamed (GSM) #YangaSafarini #YangaMauritania #AlHilal #YangaSC #AlHilalYanga #CAFCL #CAFChampionsLeagueSERIKALI YASISITIZA UMUHIMU WA MAFUNZO YA UFUATILIAJI NA TATHIMINI KWA MAENDELEO YA MIRADI YA SERIKALI
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) imezitaka halmashauri, taasisi, na wadau mbalimbali wanaonufaika na mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini kutumia vyema fursa hizo. Imepongeza ushirikiano uliopo baina ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, ambacho kimeendelea kutoa mafunzo wakishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuongeza ufanisi wa kufuatilia na kusimamia maendeleo ya miradi ya serikali.
Kauli hiyo imetolewa leo Januari 10, 2024, na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, na Uratibu, John Bosco Quman, wakati wa kufunga mafunzo ya uelewa kwa watumishi wa serikali ngazi ya halmashauri. Quman amehimiza washiriki kushiriki kikamilifu hatua zote tatu za mafunzo ili kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Aidha amekipongeza Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Quman amesema chuo hicho kimefanya kazi nzuri katika kutoa mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini, bila malalamiko yoyote kuhusu utekelezaji wa mpango huo unaosimamiwa na serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kwa upande wake, mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu Huria, amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo wafanyakazi wa serikali. Hadi sasa, mikoa yote nchini imefaidika na mafunzo hayo katika ngazi ya kwanza. Ameongeza kuwa washiriki 67 kutoka halmashauri mbalimbali wamepata maarifa ya kutafsiri miongozo, kusimamia utekelezaji wa miradi, na kuandaa miongozo inayosaidia kutatua changamoto za kijamii katika mafunzo yaliyotolewa Mkoani Morogoro .
Naye, Caroline Marila, mshiriki wa mafunzo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, amesema mafunzo hayo yataboresha utekelezaji wa miradi ya serikali na usimamizi wa rasilimali fedha, hivyo kuleta mabadiliko chanya katika utoaji wa huduma kwa jamii.
Mafunzo haya, yaliyoanzishwa na serikali kupitia Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, yalianza mwaka 2024 kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa umma katika kufuatilia na kutathmini miradi ya maendeleo ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi wa matumizi ya rasilimali.