ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 27, 2019

MADRID YAPIGWA WIKI NA ATLETICO



Real Madrid vs Atletico madrid 3-7 - Highlights & Goals Resumen & Goles 2019 HD

MABONDIA TWAHA KIDUKU NA TSHIBANGU KAYEMBE KUZIPIGA KESHO JULAI 27 ESCAP ONE

Promota Kaike Siraju katikati akiwainua mikono juu mabondia Twaha Kiduku kushoto na Tshibangu Kayembe kutoka Kongo baada ya kupima uzito na afya kwa ajili ya mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia utakaofanyika katika ukuimbi wa Escap One  Mikocheni B 

Bobondia Twaha Kiduku kushoto akitambiana na bondia kutoka Kongo Tshibangu Kayembe baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa Dunia utakaofanyika Julai 27 katika fukwe za Escap One Mikocheni 

Bondia Ibrahimu Makubi akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Adamu Yusufu utakaofanyika Escap One julai 27

Mabondia Adam Yusufu kushoto akitambiana na Ibrahimu Makubi baada ya kupima uzito na Afya kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika fukwe za Escap One Mikocheni 

BONDIA TSHIBANGU KAYEMBE AKIPIPWA AFYA NA DR DOLNARD MADONO


BONDIA TSHIBANGU KAYEMBE AKIPIPWA UZITO

LIVE Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkoa Mwanza


Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/20 kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu 2019 Mkoa Mwanza. Matangazo haya yanakujia #Mubashara kutoka ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza.

Friday, July 26, 2019

WAZIRI NDALICHAKO AITUPIA KOMBORA COSTECH


Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekonolojia, Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Tume ya Sayansi na Teknolojia kubadili utendaji wake na kutokufanya kazi kwa mazoea. Waziri Ndalichako ameyasema hayo JANA jijini Mwanza wakati akizindua kituo cha Teknolojia cha Jema Tech kilicho chini ya Jema Afrika.



HUGO SANTILLAN: BONDIA WA ARGENTINA AFARIKI KUFUATIA MAJERAHA ALIYOYAPATA KATIKA PIGANO.

 Bondia wa Argentina Hugo Santillan amefariki kutokana na majeraha aliyopata katika pigano , siku chache baada ya kifo cha bondia wa Urusi Maxim Dadashev.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 23 alizirai katika ukumbi siku ya Jumamosi baada ya pigano lake la ukanda wa WBC dhidi ya Eduardo Javier Abreu nchini Argentina kuisha kwa sare.
Alipelekwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini akafariki siku ya Alhamisi.
''Lala kwa amani, Hugo Santillan'' ,alisema afisa wa ukanda wa WBC katika ujumbe wake wa Twitter.
Santillan ni bondia wa pili kufariki kutokana na majeraha aliyopata katika ulingo wa ndondi wiki hii baada ya kifo cha Dadashev kuthibitishwa siku ya Jumanne.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 28 alipelekwa hospitalini akitokwa na damu katika ubongo baada ya pigano lake la IBF ukanda wa Welterwieght dhidi ya Subriel Matias kusimamishwa mwisho wa raundi ya 11 Ijumaa iliopita.
Alifanyiwa upasuaji wa dharura lakini ukafeli.

TAHA WATAKIWA KUFANYA TAFITI ZA KUWAKOMBOA WAKULIMA NCHINI TANZANIA

 Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) iliyofanyika katika mjini Morogoro. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro. Meneja miradi Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) Bi. Elianchea Shanga akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa taasisi ya TAHA iliyofanyika katika mjini humo. Wakulima wa Mboga Mboga akinyoosha mikono kujitambulisha.
 Meneja mradi Naimana akizungumza wakati akitambulisha mradi huo huku wakulima na wageni waalikwa wakifuatilia.
 Mmiliki wa shamba la nyanya la kisasa akiongea machache.
Meneja miradi TAHA Bi. Elianchea Shanga akiwatambulisha mabwana shamba wanaosaidia kufundisha wakulima.
 Wafanyakazi wa TAHA wakitoa elimu kwa wakulima.
 Kilima cha kisasa cha nyanya.
 Mgeni rasmi Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akipewa maelezo juu ya kilimo cha kisasa cha nyanya kutoka kwa Meneja mradi huo Naimana.
 Vingozi wa kijiji wakiwa na Mgeni rasmi.
Wakulima wakiwa na mgeni rasmi.

TURUDISHE FARAJA KWA DJ STEVE B A.K.A DJ SKILLS

Ndugu yetu Dj STEVE B a.k.a Dj Skills anasumbuLiwa na Maradhi ya FIGO, leo tulienda kumjulia Hali' na tulipoingia katika chumba alicholazwa tukapiga Story sana, katikati ya Maongezi alisema, “Mtu ukiwa mzima ni jambo la kumshukuru Mungu sana”, hii ni kutokana na Situation anayopitia.

Steve anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila, natoa Taarifa kwa Marafiki, Wasanii na Wadau wote wa Muziki, wengi hawana TAARIFA, kama tunavyojua Maradhi ya FIGO ni aghali sana.

Sisi kama MaDj/ndugu/marafiki Wenzake tunaangalia Jinsi ya Kushirikiana na Wadau ku-Raise Fund ili kufanikisha aweze kupata Tiba sahihi nje ya nchi, kwani Familia imefika pahala wanahitaji Msaada wa hali na mali.

Wapo waliochangia Matibabu tutawashukuru sana kwa Majina na Tutapeana Taarifa zaidi jinsi ya Kumsaidia mwenzetu Matibabu yake. 

Kwa Mawasiliano Zaidi wasiliana na Kaka yake 0687536015 #RudishaFarajaKwaDjSteve

MUBASHARA KUTOKA IKULU TANZANIA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akitekeleza majukumu ya kiserikali na kuzungumza na Wananchi wa maeneo mbalimbali kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bwawa la kufua umeme la mto Rufiji

Thursday, July 25, 2019

VIDEO... WAZIRI MPINA:- DAMU YA WANANCHI ILIYOMWAGIKA SHAMBULIO LA UKEREWE 'VITA MPYA DHIDI YA UVUVI HARAMU'



SIZA-UKEREWE, MWANZA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ametangaza oparesheni Mpya Dhidi ya Uvuvi haramu katika ziwa Victoria kufuatia vifo vya wananchi wanne akiwemo Afisa Mfawidhi Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi kanda maalum ya Ukerewe Ibrahim Jalali.

Waziri Mpina amesema kuwa vifo hivyo vimewaongezea watendaji wa wizara yake hali na kasi Mpya ya Kupambana na wavuvi Haram lengo likiwa kukomesha kabisa matumizi ya zana haramu ndani ya ziwa Zictoria.

Akitoa tamko la serikali wakati wa kuaga Mwili wa afisa huyo Mfawidhi usimamizi wa rasilimali za uvuvi katika Hospitali ya wilaya ya Ukerewe mjini Nansio, Mpina amesema watendaji wa wizara hiyo wakitumia mbinu mpya, wataendelea na oparesheni ya kuwasaka kwa hali na mali, wavuvi haramu pamoja na wafanyabiashara haramu wa rasilimali za ziwa mpaka hapo vitendo hivyo vitakapo koma. 






TAHA WATAKIWA KUFANYA TAFITI ZA KUWAKOMBOA WAKULIMA NCHINI TANZANIA

 Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) iliyofanyika katika mjini Morogoro. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro. Meneja miradi Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) Bi. Elianchea Shanga akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa taasisi ya TAHA iliyofanyika katika mjini humo. Wakulima wa Mboga Mboga akinyoosha mikono kujitambulisha.
 Meneja mradi Naimana akizungumza wakati akitambulisha mradi huo huku wakulima na wageni waalikwa wakifuatilia.
 Mmiliki wa shamba la nyanya la kisasa akiongea machache.
Meneja miradi TAHA Bi. Elianchea Shanga akiwatambulisha mabwana shamba wanaosaidia kufundisha wakulima.
 Wafanyakazi wa TAHA wakitoa elimu kwa wakulima.
 Kilima cha kisasa cha nyanya.
 Mgeni rasmi Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akipewa maelezo juu ya kilimo cha kisasa cha nyanya kutoka kwa Meneja mradi huo Naimana.
 Vingozi wa kijiji wakiwa na Mgeni rasmi.
Wakulima wakiwa na mgeni rasmi.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.

Watafiti wa mazao ya kilimo nchini wametakiwa kuhakikisha tafiti zao zinawafikia wakulima wadogo wadogo hasa waliopo vijiji ili wakulima hao waweze kulima kilimo chenye tija ikiwa ni katika kubabiliana na changamoto ya ushindani wa masoko kitaifa na kimataifa.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba, wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) iliyofanyika katika mjini Morogoro.

Bi. Chumba amesema kuwa watafiti hao endapo watafanya zao vyema zinaweza kumkomboa mkulima na akaweza kupata soko bora la mazao yao na itawakwambua kiuchumi.

"Niwashukuru wataalamu maana nyie mmekuja wakomboa wakulima wadogo ambao mara nyingi huwa ni  ngumu kufikiwa matokeo yake wamekuwa wakilima kilima cha mazoea ambacho hakina manufaa kwao," amesema.

Nae Meneja Miradi ya Taasisi ya TAHA, Bi. Elianchea Shanga amesema kuwa kwa sasa wamesambaa mikoa mbali mbali ya Tanzania na lengo lao kubwa ni kumkomboa mkulima kutoka katika kilimo cha mazoea na kulima kilimo cha tija.

"Sisi lengo kubwa mkulima aone dhamani ya kile anachokilima maana tunasimamia kuanzia kuandaa shamba, madawa na mbolea huku tukimpa ushauri na kumtafutia soko," amesema.

Kwa upande wao wakulima Mwajuma Abdala wamefurahishwa na ujio wa Taasisi ya TAHA huku wakielezea kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa mwiba kwao kwa sasa ni mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yamepelekea ukosefu wa mvua huku wakiiomba serikali kuongezea nguvu katika kusaidia kilimo cha umwagiliaji.