ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 25, 2019

VIDEO... WAZIRI MPINA:- DAMU YA WANANCHI ILIYOMWAGIKA SHAMBULIO LA UKEREWE 'VITA MPYA DHIDI YA UVUVI HARAMU'



SIZA-UKEREWE, MWANZA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ametangaza oparesheni Mpya Dhidi ya Uvuvi haramu katika ziwa Victoria kufuatia vifo vya wananchi wanne akiwemo Afisa Mfawidhi Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi kanda maalum ya Ukerewe Ibrahim Jalali.

Waziri Mpina amesema kuwa vifo hivyo vimewaongezea watendaji wa wizara yake hali na kasi Mpya ya Kupambana na wavuvi Haram lengo likiwa kukomesha kabisa matumizi ya zana haramu ndani ya ziwa Zictoria.

Akitoa tamko la serikali wakati wa kuaga Mwili wa afisa huyo Mfawidhi usimamizi wa rasilimali za uvuvi katika Hospitali ya wilaya ya Ukerewe mjini Nansio, Mpina amesema watendaji wa wizara hiyo wakitumia mbinu mpya, wataendelea na oparesheni ya kuwasaka kwa hali na mali, wavuvi haramu pamoja na wafanyabiashara haramu wa rasilimali za ziwa mpaka hapo vitendo hivyo vitakapo koma. 






Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.