ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 20, 2011

HARUSI HARUSI... NI ISAAC NA JANET

Si wawili tena bali ni mwili mmoja Isaac Abraham Nyanda na Janet Jilungu Yemba sasa ni Mr&Mrs Isaac Nyanda mara baada ya ndoa yao takatifu iliyofungwa leo katika kanisa la AIC Njiro mkoani Arusha.

Maadhari tulivu kanisani.

Sehemu umma waliohudhuria ibada hiyo ya ndoa.

Isaac akimvisha pete Janet.

Janet akimvisha pete Isaac.

Sahihi ya bwana harusi.

Sahihi ya bi harusi.

Maharusi wakitoka kanisani.

Taswira zaidi.

Wanameremetajeeeee!!!!!

Safu ya wapambe.

Mara nkabaaaaa!!! Ukumbini.

Moja kati ya burudani za ukumbini zilizotikisa ile kinomanoma chekshia...hapa ni Mama Paul na Jeremiah.

Jografia ya ukumbi.

Friday, August 19, 2011

CHEREKO LA SENDOFF YA DADA JANET ILIVYOFANA

Dada Janet Kushoto akiwa na best wake sis Jackline.

Poz la keki,,

Dada Janet akimlisha keki mama yake mzazi.

Janet akisoma neno kwa mumewake mtarajiwa.

Shangwe na kujimwayamwaya....

Wakati wa Zawadiz'

Hapa nikiwa na Bwashee' Mr & Mrs Isaac.

Janet na mtarajiwa wake bwana Isaac Nyanda.

Nikiwa na dada zangu kutoka kushoto Sister Catherine, Leah na Rodha.

Bibi Ng'wana Mashauri akimpongeza Bi harusi mtarajiwa Janet.

Best couples - Mr & Mrs Joshua.

Utamaduni wetu na Kapu la mama...


Mama mzazi wa Janet akitunzwa kulishehenesha kapu lake...


Safu kamili...


Wanakamati haoo....
Wanakamati waliofanikisha sendoff ya bi Janet ndiyo hawa...


Thursday, August 18, 2011

HAPA NA PALE PANDE ZA ARUSHA

Mtaani kwetu.

Bar ya Ngiwaranecha inayopatikana levolosi jijini Arusha moja kati ya maeneo maarufu kwa firigisi.

Stendi ndogo ya Vifodi arachuga.

Huduma zinazopatikana ndiyo hizi.. Stendi ya Vifodi.

Mitaa ya magoro' Kambi ya Fisi.

SIMBA ARARUA MWANAKIJIJI!!!!!

Siyo kitu ya kuuliza!!.

Mchezaji wa Simba, Uhuru Selemani akinyanyua juu ngao ya hisani mara baada ya kukabidhiwa rasmi katika mchezo wa ngao ya hisani, uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam jana usiku.

Hapa ni raha ya ushindi wakisakata mayenu kutoka kulia tena ni Victor Costa, Uhuru Selemani, Felix Sunzu na Juma K. Juma. Mmmmmh!... FULLSHANGWE

AIRTEL YAHAMASISHA VIJANA KUPENDA SOKA

"Bado nipo nipo" ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abass Kandoro akipiga danadana mbele ya mkuu wa wilaya ya Ilemela Saidi Amanzi.

· Ni kupitia Tangazo la luninga la Airtel linafanya vijana kuwa na shauku kubwa ya mpira wa miguu na matokeo ya kupitia Airtel Rising Stars.

· Tangazo la Airtel kwenye luninga ni kiashirio kizuri jinsi Airtel ilivyojikita na kuendeleza vijana wenye vipaji katika nchi 15 ambazo Airtel inafanya biashara.

· Michuano ya Airtel Rising Stars ni mpango unaosaidiwa kwa pamoja na Klabu ya mpira wa miguu ya Manchester United ya Uingereza.

Airtel Tanzania, Agosti 16, 2011 – Tayari Airtel Africa imezindua tangazo la luninga kwa Afrika nzima ambayo madhumuni yake ni kuhamasisha vijana kuwa na shauku ya mchezo wa mpira wa miguu kwa kushiriki kwenye michuano ya Airtel Rising Stars. Michuano hiyo, ambayo kwa sasa inaendelea kwenye nchi 15 za Afrika ambapo Airtel inafanya biashara, ina lengo la kutafuta na kukuza vipaji vya mpira wa miguu kuanzia ngazi ya chini.

‘Airtel ina shauku kubwa sana na Afrika, na Afrika ina shauku kubwa sana na mpira wa miguu’. Mpango kama huu unaifanya jamii inayotuzunguka kuwa na mtazamo chanya na kuwawezesha vijana kujiendeleza kupitia mpango huu wa Airtel Rising Stars, anaelezea Andre Beyers, Meneja Masoko wa Airtel Afrika.

Akielezea juu ya hilo tangazo la luninga, Bw. Beyers alisema: Kinachofanya michuano ya Airtel Rising Stars kuwa tofauti na michuano mingine ya mpira wa miguu ni jinsi mpangilio mzima na upana wa mpango huu. Michuano hii inachezwa na maelfu ya vijana Bara nzima la Afrika na inatia moyo sana. Huu ndio ujumbe tunaotaka kuufikisha kwa kupitia tangazo hilo.

Tangazo hilo linaanzia kwa watu binafsi katika mandhari mbalimbali katika bara huku wakitazama ndege ikuruka juu. Ndege hii inaangusha maelfu na maelfu ya mipira kwenye Kata tofauti vijijini na mjini, kwenye milima na mabonde na pia kwenye jangwa. Wakati wa kudodosha mipira, mpira mmoja unajitenga kutoka kwenye mipira mingine na kuanza kusonga mbele peke yake kupitia kwenye mitaa na vichochoro. Hatimaye unasimamia kwenye miguu ya mwanafunzi akiwa kwenye kiti chake cha kusomea.

Tangazo linaishia kwa ujumbe usemao, ‘Kama wewe ndio staa wa Afrika unayefuata, basi tutakufikia.’ Michuano hii tayari inaendelea kwenye nchi 15 barani Afrika, ambapo timu zaidi ya 3,000 zinashiriki.

‘Michuano ya Airtel Rising Stars imejikita kwenye kutafuta na kukuza vipaji vya soka kwa vijana wenye umri chini ya 17 ambapo pia watapata nafasi ya kuonyesha umahiri wao kwa wataalamu na waalimu wa mpira wa miguu’ anasema Cheikh Sarr, Meneja Masoko wa Airtel Tanzania na kuongeza kuwa kwa hapa Tanzania peke yake, timu 24 zilishiriki kwenye ngazi ya mkoa ambapo timu 4 bora zitasonga mbele kwenye ngazi ya Taifa. Tunatarajia kufanya kazi kwa ukaribu na wachezaji wanaoshiriki kwenye michuano hii na kuwapa nafasi ya kukuza vipaji vyao.

Kwa hapa Tanzania, Airtel Rising Stars ni mpango wa Airtel pamoja na Klabu ya Manchester United. Ushirikiano huu na Manchester United ni mpango wa miaka minne uliosainiwa Desemba mwaka jana. Manchester United kwa kutumia nembo yake ya shule za soka ya aegis itatoa msaada wa kiufundi katika kambi za soka zitakazofanyika Gabon na Tanzania mwishoni mwa mashindano.
Bofya hapa kutazama tangazo hili.

KUHUSU Airtel Barani Afrika:-
Airtel ni nembo mpya ya iliyokuwa Zain ambayo ilikuwa ikifanya biashara kwenye nchi 16 Barani Afrika ambayo ilinunuliwa na Airtel International Juni 2010. Airtel inaendesha kwa madhumuni ya kutoa huduma ya simu za mkononi kwa bei rahisi na nafuu, na kwa Afrika inafanya biashara kwenye nchi zifuatazo: Burkina Fasso, Chad,DRC, Ghana, Gabon, Kenya, Malawi, Madagascar, Niger, Nigeria, Seychelles, Sierra Leone, Tanzania, Uganda na Zambia. Airtel International ni kampuni tanzu ya Bharti. Kwa habari zaidi, tembelea
http://www.airtel.com/

Wednesday, August 17, 2011

WAKUFUNZI WA SOKA TOKA ARSENAL WATUA KUFUNDISHA SOKA JIJINI MWANZA

Wakufunzi wawili wa soka toka Club ya Arsenal ya London nchini Uingereza wamewasili jana jioni majira ya saa 1:30 jijini Mwanza kwaajili ya kutoa mafunzo kwa timu za soka za vijana wadogo wenye umri wa miaka 17 kwenda chini.

Wakijiandaa kwaajili ya mahojianao mafupi uwanja wa ndege Mwanza.
Wakufunzi hao Harry Webb na Francesca Miles wameitonya bogu hii kuwa wamekuja kutoa mafunzo ya sok yatakayodumu kwa muda wa wiki sita kwenye kituo kilichotoa mualiko cha Tanzania street children academy.

Mkurugenzi wa TSC ya jijini Mwanza Mutani Yangwe katikati katika picha ya pamoja na wakufunzi hao ambao watajigawa kufundisha soka upande wa wanaume na wanawake kituo hicho cha watoto wa mitaani.

Kutoka kushoto mkurugenzi wa TSC Mutani Yangwe, kocha Harry Webb, Albert G. Sengo na kocha Francesca Miles.

Kutoka shoto Benard, G.Sengo, Harry Webb, Magasha na Francesca.

Tuesday, August 16, 2011

HAPA NA PALE PANDE HIII!!

Kitanda full na godoro lake, tuna hama mchana kweupeeee...!

Kunako barabara ya halmashauri ya jiji mjengo Umekamilika, wapangaji tayari wamekwisha anza kuhamia.

Mjengo unakwenda kwa jina la.....

Mara baada ya kupigwa marufuku kwa Express kusimamisha au kupakia abiria kwenye kituo cha Chai bora mataa, Kituo hiki cha daladala kilichopo karibu na soko kuu kilianza kutumika huku matengenezo yake yakifanyika kimtindo papo hapo..

Ofisi za Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Mwanza (MWAUWASA).

Barabara yenye mishemishe ya Lumumba kama inavyoonekana leo..