ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 13, 2024

TAASISI ZA KIFEDHA ZASHAURIWA KUJA NA PRODUCTS ZITAKAZOSAIDIA WAFANYABIASHARA WADOGO HANANG’

 

Mkurugenzi wa Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Condrad Millinga akizungumza wakati wa kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Tarehe 11 Januari 2024. Aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Mhe. Janeth Mayanja.

 baadhi ya wafanyabiashara Wilayani Hanang’ katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara Tarehe 11 Januari 2024.
Mwenyekiti wa Soko la Hanang’ Bw. Mathia Jonisi akizungumza katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Mnyara Tarehe 11 Januari 2024.



Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Tarehe 11 Januari 2024.

Bw. Godfrey Chacha Afisa Vijana Mwandamzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akizungumza katika kikao cha mafunzo cha wafanyabisha na wawakilishi kutoka kwenye mabenki na Taasisi za fedha kilichofanyika Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Tarehe 11 Januari 2024.


NA; MWANDISHI WETU HANANG’

Taasisi za kifedha Hususani Mabenki, yameshauriwa kuja na Dirisha maalum na Products zitakazosaidia wafanyabiasha wadogo walioathiriwa na maafa ya maporomoko ya tope, miti na mawe yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana Wilayani Hanang’ Mkoa wa Manyara.

Hayo yamesemwa tarehe 11 Januari 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Bi Janeth Mayanja alipokutana na Wafanyabiashara wilaya hiyo na wawakilishi wa mabenki na Taasisi za kifedha katika Mkutano wa Mafunzo Ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC).

Bi. Mayanja alisema ni wakati sasa kwa mabenki kuwafikiria wafanyabiashara wadogo wasiyo na mali ya kuweka rehani katika kupata mikopo yenye unafuu kuja na Products zitakazowawezesha wafanyabiasha hao kukopesheka kwa riba nafuu kwani wafanyabiashara hao wanakopa kwenye taasisi nyigine za kifedha zenye masharti magumu na kwa watu binafsi na wanaweza kulipa.

“Inawezekana mikopo hivyo kwa mabenki ikaonekana ni midogo midogo kwa sababu wafanyabiahara hao ni wengi lakini bado mabenki yanaweza kupata faida, tukiendelea kijikita kwa wafanyabiashara wakubwa wenye mali za kuweka rehani maendeleo ya watanzania wanaojikita kwenye biashara ndogondogo yatachelewa.” Alisema Mhe. Mayanja

Kwa wakati huo huo Banki ya NMB imekabidhi hundi ya fedha ya Tsh 269,000,000 (Milioni Mia Mbili sitini na tisa) kwa Waathirika kumi na nane wa maporomoko ya Mlima Hanang , ambapo fedha hizo ni sehemu ya fidia kwa wateja wa Benki hiyo waliokata Bima kwenye Biashara na Bima za Mikopo Kupitia Bank ya NMB, na imeelezwa kuwa Benki hiyo itaendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa Bima.
Awali Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo Wilayani Hanang’ kuchangamkia fursa zitakazotolewa na mabenki hayo na kuachana na mikopo yenye masharti kandamizi ili kuwainua kiuchumi

Friday, January 12, 2024

HILI HAPA BALAA LA LEO NA MVUA ZILIZONYESHA LEO JIJINI MWANZA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa tatu hii leo jijini hapa, licha ya kusababisha uharibifu na upotevu wa mali za wafanyabiashara katika soko la Mlangommoja wilayani Nyamagana, pia athari za mvua hizo zimesababisha huduma za usafiri na usafirishaji kupitia barabara ya Musoma kipande cha Nata-Mabatini kusimama kwa muda. Ufinyu wa matundu ya daraja uliochangiwa na mlundikano wa taka ngumu chini ya daraja hilo sanjari na lundo la mchanga vimesababisha maji yenye kasi kufurika juu ya njia hiyo kiasi cha kufikia kina cha juu ya magoti kwa mtu anayepita usawa wa barabara. Wananchi na wafanyabiashara wa maeneo hayo wamedai kuwa mvua hiyo, iliyonyesha kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00 alasiri, ni mwendelezo wa mvua za El Nino zinazoendelea kushuhudiwa katika kipindi hiki. Taarifa kutoka maeneo mengine zinaeleza wafanyabiashara na wamiliki wa maduka katika mitaa ya Liberty na Uhuru nako hawajaachwa salama baada ya mafuriko hayo kusomba bidhaa zao zilizopangwa nje ikiwemo mapipa, madumu, samani za ndani huku maboksi yenye bidhaa mbalimbali yakionekana kusombwa na maji hayo yanayopita Mto Mirongo unaomwaga maji yake ndani ya Ziwa Victoria. Licha ya ubovu wa miundombinu, eneola Mabatini hukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na ujenzi holela uliobana kingo za Mto Mirongo. Mto Mirongo unapita katikati ya Jiji la Mwanza ukikusanya maji yake kutoka Wilaya za Nyamagana, Ilemela, Misungwi na Magu umekuwana historia ya kufurika mara kwa mara mvua zinyeshapo. #samiasuluhuhassan #jembefm #mwanza #mvua #ElNino

Thursday, January 11, 2024

TANESCO YASHIRIKI MAONESHO YA 10 YA KIMATAIFA YA BIASHARA ZANZIBAR

 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeshiriki kwenye maonesho ya 10 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar.

Maonesho hayo yamezinduliwa Januari 10, 2024 na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi, ambapo alizipongeza Taasisi zote ziizoshiriki katika maonesho hayo.

Wednesday, January 10, 2024

KAYA ZAIDI ZA 130 ZILIZOVAMIA SHAMBA LA SERIKALI LA MITAMBA KIBAHA MJI ZATAKIWA KUONDOKA HARAKA

 VICTOR MASANGU/PWANI


Uongozi wa Halmashauri ya Mji Kibaha mkoani Pwani imetoa onyo kali na kuzitaka   kaya zaidi ya 130 ambazo zimepatiwa  notisi  mara mbili kuondoka haraka iwezekanavyo  kwenye eneo la  mitamba  kiwanja namba 34 lililopo kata ya  Pangani  ili kupisha zoezi la ubomoaji  lisilete hasara kwa wavamizi hao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa  Halmashauri ya mji wa Kibaha
 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na  wavamizi wa  eneo hilo la shamba la mitamba  muda wa notisi  umeshapita na  kilichobaki ni  upimaji.

Tuesday, January 9, 2024

NAIBU WAZIRI MKUU DKT. BITEKO ATETA MAZITO NA UMOJA WA VIJANA CCM ZANZIBAR

 NA ALBERT G. SENGO

NAIBU WAZIRI MKUU DKT. BITEKO AWATAKA UMOJA WA VIJANA CCM ZANZIBAR KUSHIKAMANA KULETA MAENDELEO.

Monday, January 8, 2024

RC KUNENGE ATEMA CHECHE AAGIZA WATOTO WOTE KUPELEKWA SHULE HATA KAMA HAWANA SARE

 VICTOR MASANGU/ PWANI

MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewagiza walimu wa shule za msingi na sekondari kuwapokea wanafunzi wote waliojiunga kidato cha kwanza na darasa la kwanza bila kujali changamoto  za ukosefu wa sare za shule badala yake watoe  muda wa kukamilisha  taratibu zote za kujiunga na masomo.

Kunenge ametoa Maagizo  hayo wakati alipotembelea baadhi ya shule za msingi na sekondari katika  halmashauri ya mji wa Kibaha na kuzungumza na baadhi ya  wanafunzi waliojiunga na muhula Mpya wa masomo wa mwaka 2024.


Nao baadhi ya walimu wameelezea namna  mwamko wa wanafunzi waliojiunga na muhula huo Mpya wa masomo huku wanafunzi wakiahidi kufanya vizuri katika masomo yao. FIDELIS HAULE ni Mkuu wa  shule ya sekondari Tumbi.

Nao baadhi ya wanafunzi wa wa shuke ya sekondari Tumbi na Kibaha  hawakusita kuzungumza ya moyoni. MOSES DAMAS NA LIBYA OMARY ni wanafunzi walio wawakilisha wenzao.