NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa tatu hii leo jijini hapa, licha ya kusababisha uharibifu na upotevu wa mali za wafanyabiashara katika soko la Mlangommoja wilayani Nyamagana, pia athari za mvua hizo zimesababisha huduma za usafiri na usafirishaji kupitia barabara ya Musoma kipande cha Nata-Mabatini kusimama kwa muda. Ufinyu wa matundu ya daraja uliochangiwa na mlundikano wa taka ngumu chini ya daraja hilo sanjari na lundo la mchanga vimesababisha maji yenye kasi kufurika juu ya njia hiyo kiasi cha kufikia kina cha juu ya magoti kwa mtu anayepita usawa wa barabara. Wananchi na wafanyabiashara wa maeneo hayo wamedai kuwa mvua hiyo, iliyonyesha kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00 alasiri, ni mwendelezo wa mvua za El Nino zinazoendelea kushuhudiwa katika kipindi hiki. Taarifa kutoka maeneo mengine zinaeleza wafanyabiashara na wamiliki wa maduka katika mitaa ya Liberty na Uhuru nako hawajaachwa salama baada ya mafuriko hayo kusomba bidhaa zao zilizopangwa nje ikiwemo mapipa, madumu, samani za ndani huku maboksi yenye bidhaa mbalimbali yakionekana kusombwa na maji hayo yanayopita Mto Mirongo unaomwaga maji yake ndani ya Ziwa Victoria. Licha ya ubovu wa miundombinu, eneola Mabatini hukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na ujenzi holela uliobana kingo za Mto Mirongo. Mto Mirongo unapita katikati ya Jiji la Mwanza ukikusanya maji yake kutoka Wilaya za Nyamagana, Ilemela, Misungwi na Magu umekuwana historia ya kufurika mara kwa mara mvua zinyeshapo. #samiasuluhuhassan #jembefm #mwanza #mvua #ElNinoTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.