Mpenzi mtazamaji wa IBM CHANNEL endelea kutufuatilia kwa ajili ya kupata elimu zaidi ya uzalendo, ukombozi wa kifkira na ukuu wa Mwaafrika hapa hapa. tunakupa pia makala mbalimbali zinazohusiana na ulimwengu tunaoishi na taarifa zetu ni za ukweli na uhakika sio za uongo. karibu tuendelee kuwa pamoja. kama hauja-subscribe tafadhali fanya hivyo ili usipitwe na chochote.
Saturday, June 29, 2024
Friday, June 28, 2024
KATIBU CCM PWANI-WAGOMBEA WATAKAOTEULIWA NA VIKAO VYA CHAMA KWENYE CHAGUZI WATENDEWE HAKI
NA VICTOR MASANGU, PWANI
Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu kimejiwekea mipango kabambe ya kuhakikisha kwamba wanapata wagombea wazuri na wenye sifa ambao wanakubalika katika jamii na kuweza kusabisha kuweza kuibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa (CCM) Mkoa wa Pwani Bernad Ghathy wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya (CCM) Mkoa ambapo amesema kuwa lengo kubwa la chama ni kuweka misingi imara ya kuwapata viongozi wazuri ambao watakwenda kuipeperusha vyema bendera ya chama kwa kushinda katika mitaa yote ndani ya Mkoa wa Pwani.
Katibu Ghaty alisema kwamba kikao hicho cha Halmashauri kuu kimeelekeza kwamba katika vikao vyote vya uteuezi vitakavyofanyika katika ngazi ya chama vihakikishe kwamba vinatenda haki bila upendeleo wowote katika kuwapata viongozi ambao watagombea katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa.
"Tumekutana katika kikao cha Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani na hiki kikao ni cha kikatiba kabisa na tumeweza kuzungumzia mambo mbali mbali ya utekelezaji wa ilani pamoja na kupokea taarifa ya serikali ya Mkoa ikionyesha kazi na miradi mbali mbali ambayo imetekeleza katika sekta tofauti, ikiwa sambamba na kujadili hali ya kisiasa katika Mkoa wa Pwani,"alisema Katibu Ghathy.
Aidha Katibu huyo alifafanua kwamba Halmashauri hiyo imempongeza kwa dhati Mwenyekiti wa (CCM) Taifa ambaye pia ndiye Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwatumikia wananchi katika nyanja mbali mballi za miradi ya maendeleo ikiwemo elimu, wananchi kuweza kupata huduma ya maji safi na salama, miundombinu ya barabara sambamba na uboreshawaji wa huduma ya afya.
Kadhalika hakusita kutoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge pamoja na wasaidizi wake kwa kuweza kuhakikisha kwamba wanajitahidi kupambana kuboresha miundombinu ya barabara ili iweze kupitika kwa urahisi hata katika kipindi cha mvua zinaponyesha.
Pia amebainisha kuwa chama cha mapinduzi Mkoa wa Pwani wanajivunia kupata Mwenyekiti wa Taifa ambaye ni msikivu na shupavu kwani ameweza kufanya mambo makubwa mbali mbali ya kukisaidia chama ikiwemo kuchangia katika mradi wa jengo la kitega uchumi ambalo linatarajiwa kuzinduliwa ifikapo Julai 30 mwaka huu na kuanza kutumika.
Katika hatua nyingine amesema kuwa mikakati ambayo wamejiwekea ni kuendeleza sera ya chama ya kuweka mifumo ya kujiimarisha kichumi kuanzia ngazi za chini kwa kushirikiana bega kwa bega na wanachama wote wa chama cha mapinduzi lengo ikiwa ni kuweza kuletaa mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia vitegaa uchumi vilivyopo.
MAMA AANGUA KILIO MOCHWARI BAADA YA KUMUONA MWANAWE ALIYEPIGWA RISASI KWENYE MAANDAMANO.
Mama akilia nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha City (l). Waandamanaji wakifanya ishara kwa mikono wakati wa maandamano (r).
Mwanamke mmoja ni miongoni mwa Wakenya wanaoumia baada ya mpendwa wake aliyejitokeza kwa maandamano hayo kuathiriwa na dhuluma za polisi.
Je Rex Mmasai alikufa vipi?
Katika kisa sawia, Rex Masai, kijana kutoka kaunti ya Nairobi, alidaiwa kuuawa na afisa wa polisi alipokuwa akiandamana kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.
Kijana huyo alipopigwa risasi, alikimbizwa katika Kituo cha Matibabu cha Bliss katikati mwa jiji, na baba yake, aliyetambulika kama Chrisphine Odawa, akaenda kumtazama.
Cha kusikitisha alipoteza maisha na Chrisphine ambaye alihuzunika sana alieleza kuwa kifo cha mwanawe kilikuwa hasara kubwa kwa familia.
Nini kingine unahitaji kujua kuhusu maandamano ya kupinga Muswada wa Fedha Baadhi ya Wakenya walionyesha kufadhaika baada ya Rais William Ruto kuwashukuru polisi waliojibu maandamano hayo.
Nyumba ya Mbunge wa Molo Kimani Kuria ilichomwa moto na waandamanaji waliokuwa na hasira.
Charlene Ruto aliwakumbusha Wakenya kuzingatia Mswada wa Fedha wa 2024 kufuatia hotuba ya rais Mwigizaji.
Lupita Nyong'o aliwapongeza Gen Zs kwa kushiriki maandamano ya amani na kuitaka serikali kuwasikiliza waandamanaji.
Thursday, June 27, 2024
DC KIBAHA AMPA KONGOLE RAIS SAMIA UJENZI WA DARAJA LA MTO MPIJI
HABARI NA VICTOR MASANGU/PWANI. SAUTI YA ALBERT G. SENGO Jeshi la nchi kavu limekabidhi rasmi daraja la muda la mto Mpiji linalounganisha Wilaya.mbili za Kibaha Mkoa wa Pwani na Manispaa ya Ubungo kwa mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon ambaye naye amelikabidhi kwa uongozi wa Tarura.
VIDEO: KILICHOJIRI NCHINI KENYA ASUBUHI YA LEO BARABARA KADHAA ZIMEFUNGWA
Wednesday, June 26, 2024
DC KIBAHA AMPONGEZA RAIS SAMIA NA MBUNGE KOKA UJENZI WA DARAJA JIPYA LA MTO MPIJI
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
VIJANA WENYE BUNIFU MBALIMBALI TANGA KUPATIWA FURSA ZA RUZUKU
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akizungumza na baadhi ya madereva Bajaji wakati wa mafunzo hayo
Afisa Vijana Jiji la Tanga Fadhili Secha kulia akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Na Oscar Assenga, TANGA.
VIJANA wanaofanya shughuli za Ubunifu Jijini Tanga wamewekewa bayana uwepo wa mambo mazuri kwao ikiwemo fursa za kupatiwa ruzuku ili waweze kufanya bunifu ambazo zinaweza kuwaingiza wenzao kwenye ajira na maisha bora zaidi.
Hayo yalisemwa leo na Mwakilishi wa Shirika la Botnar Foundation Philotheusy Mbogoro wakati akifungua mafunzo maalumu ya ufundi na Udereva wa Bajaji za Mfumo wa Umeme yaliyoanza leo kwenye Shule ya Sekondari Tanga School ambapo vijana zaidi ya 40 wanapata mafunzo hayo.
Kati ya vijana hao 35 ni kutoka chuo cha Ufundi Veta na wengine ni kutoka mitaani wenye kutakuja kuwa ufundi wa Bajaji ambapo mafunzo hayo yanaendeshwa na Kampuni ya Robotech Labs kwa kushirikiana na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization chini ya ufadhili wa Tanga Yetu.
Mafunzo yaliyotolewa ni namna ya kuweza kutumia vyombo hivyo kwa urahisi, ufungaji ikiwemo uunganishaji wa bajaji kwa kila sehemu kabla ya kukamilika na kuwa chombo kamili ambayo itawasaidia kujua hata jinsi ya kufanya marekebisho yake.
Alisema kwamba wao wanawasaidia kupata ruzuku hizo ili kuwawezesha vijana wengi waweze kutumia fursa zilizopo Jijini Tanga na kuweza kujikwamua kiuchumi.
Alisema vijana hao wanapaswa kutumia fursa hizo zilizopo ikiwemo kujitahidi kuwa wabunifu na wasilale kutokana na uwepo wa vitu vingi vya kufanya ambavyo vinaweza kuwaondoa kukaa kijiweni kutokana na kukosa kitu cha kufanya.
Akizungumzia mafunzo ya Bajaji za umeme alisema kwamba zinawapa fursa ya kuunganisha bajaji za umeme ambazo wanaweza kupata biashara ya kuziunganaisha, kufanya matengenezo, vituo vya kuzifanya marekebisho.
“Lakini pia zinatoa fursa wengine kuchaji, kuziuza na fursa za ajira ambazo zinakwenda kwa vijana ni wengi kupitia bajaji na pikipiki za umeme zinazokuja na hata magari umeme kwa hiyo wamekuwa kuwa na teknolojia hiyo uwezo mkubwa wa kukamata biashara ya kuhudumia bajaj,pikipiki na hata magari ya umeme itakuwa mikono mwenu hivyo mzingatie mafunzo haya”Alisema
Awali akizungumza katika mafunzo hayo ni Mmoja kati ya Washirika na Wafanyakazi wa Tanzania Open Innovation Organization na Robotech Abdulwahab Issa alisema kwamba wapo kwenye mafunzo ya bajaji wao waona namna gani bajaji zinazounganishwa zikiwa zimetoka kutoka kiwandani.
Alisema pia waweze kuona mifumo ya umeme na mota vinavyofanya kazi lengo kubwa na mahususi vijana hao waweze kuona na kupata uelewa namna vyombo hivyo vinavyoweza kufanya kazi na wao jinsi gani ya kuweza kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku na kuokoa kipato.
Alisema bajaji hiyo inaweza kutembea kwa umbali wa kilomita 80 mpaka 100 kwa kutumia chaji ya asilimia 100 kwa bajaji iliyochajishwa kwa sh 3000 hivyo inaweza kuokoa kipato cha matumizi kuokoa mafuta kuhamia huko kwa sababu ya masuala ya kimazingira.
Awali akizungumza katika mafunzo hayo Afisa Vijana Jiji la Tanga Fadhili Secha alisema wamekuwa wakishirikiana na vijana na wadau wa maendeleo kuwatumia vijana kutoka sehemu mbalimbali kuwaunganisha na wadau kuweza kupata vitu mbalimbali vinavyoendelea na Ubunifu wa Teknolojia.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Bajaji Mkoa wa Tanga Rahim Makange alisema bajaji za umeme ni fursa kubwa kwa vijana wa Jiji hilo na wamepata elimu nabajaji hizo zinarahisisha mambo mengi na hazina gharama kutokana na kwamba gharama zake ni umeme hakuna kuingia sheli.
Alisema kwamba wameelewa umbali betrii ikichajiwa ikijaa inaweza kutoka Jijini Tanga hadi Korogwe kwa kuchaji lakini petroli ingekuwa ni gharama kubwa na hiyo itawaondolea ugumu wa maisha hivyo vijana wachangamkie fursa hiyo muhimu.
MBAO FC WAANZA UPYA NA KOMBE LA MBUZI
NA ALBERT GSENGO/MWANZA
Mbunge wa jimbo la Ilemela Angeline Mabula anatajwa kuwa mgeni rasmi wa fainali itakayofanyika Jumatatu ya tarehe 1 July 2024 katika viwanja vya Sabasaba Ilemela jijini Mwanza.Tuesday, June 25, 2024
BUNGE LASHIKA MOTO HUKU WAANDAMANAJI WAKIKABILIANA NA POLISI
Sehemu ya Bunge la Kenya imechomeka moto huku waandamanaji wa kupinga Mswada wa Sheria ya Fedha 2024 wakivamia jengo hilo.
Maafisa wa polisi waliokuwa wamejipanga kuzunguka bunge walifurika haraka huku umati ukiharibu lango lake.
Baada ya muda mfupi wa milio ya risasi kushamiri hewa kutoka kwa maafisa wa usalama, umati wa watu ulipata ufikiaji wa Jumba hilo.
Monday, June 24, 2024
NILITOROSHWA KIPINDI CHA MAPINDUZI |NILIPANDISHWA MELI YA NG’OMBE|NILIKUTANA NA MUME WANGU MSIKITINI
Aunty Asha ameeleza safari ya maisha yake kutoka Zanzibar mpaka kufika Marekani
Kipindi cha mapinduzi aliweza kuondoka kuelekea Dubai kupitia meli ya kusafirisha Ng’ombe ambako alitumia miezi mitatu baharini mpaka kufika Dubai. Alienda kusoma India na baadae kuendelea na masomo nchini Marekani ambapo alikutana na mume wake msikitini ambako alikua akifundisha Quran. Kwasasa ni Mkurugeni katika sekta ya afya na kua miongoni mwa Mkurugenzi wa kwanza wa kiafrika katika mahala anafanyia kazi. Subscribe to her YouTube channel ili kujifunza kuhusu Afya na kisukari @ashafaulkner Thank you Aunty Asha for allowing this to be online www.oda.internationalCCM KIBAHA MJI YATOA TAMKO LA KULAANI VITENDO VYA MAUAJI YA BODA BODA
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Sunday, June 23, 2024
VIJANA, WAKINA MAMA TANGA WATANGAZIWA FURSA YA KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organazation (TOIO) Shaukatali Hussein akikagua moja ya bajaji ambazo zinatarajiwa kuunganishwa na baadae kutengenezwa kwa ajli ya kutumia umeme
Na Oscar Assenga, TANGA
VIJANA na Wakima mama waliopo katika Jiji la Tanga wametangaziwa fursa za kuchangamkia mafunzo ya namna ya kuviunga, kuvirekebisha na kutengeneza Bajaji za Umeme, Pikipiki, na Baiskeli hatua itakayowawezesha kujikwamuaa kiuchumi.
Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organazation (TOIO) Shaukatali Hussein wakati akizungumza kuhusu namna walivyojipanga kuendelea kuiwezesha jamii ya wakazi wa Jiji hilo.
Alisema kwamba ili kufikia lengo hilo wameona waanze kutoa mafunzo ya kuunga vitu vya umeme na mafunzo hayo yatatolewa June 26 na 27 mwaka huu jinsi ya kuunga bajaji za umeme na kuanzia saa 4 asubuh hadi saa nane mchana .
“Kwa sasa tumeona njia nzuri ya kuweza kuwakwamua kiuchumi wakina mama na vijana ni kuwapa mafunzo hayo na tunaamini watakapomaliza watapata mwanga mzuri wa kuona namna ya kuzichangamkia fursa hizo”Alisema
Aidha alisema mafunzo ya vijana na wakina mama jinsi ya kuviunga na kuvitengeneza na kuvirekebisha na namba ya kuviendesha kwani hiyo ni fursa mpya ambazo zinaweza kuinua uchumi wao.
Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka vijana waliopo mtaani kutumia fursa za kidigitali mpya wanapoelekea pikipiki za umeme na bajaji za umeme,baiskeli zinaingia mtaani.
TFS WAPONGEZWA UHIFADHI WA MISITU NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA