ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 24, 2024

CCM KIBAHA MJI YATOA TAMKO LA KULAANI VITENDO VYA MAUAJI YA BODA BODA

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 


Chama cha mapinduzi Wilaya ya Kibaha mjini (CCM) kimelaani vikali vitendo vya  matukio ya mauaji ya madereva wa boda boda yanayoendelea katika maeneo  mbali mbali.

Akitoa tamko hilo katika kikao cha halmashauri kuu ya chama Mwenyekiti wa (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka alisema kwamba wameamua kwa pamoja kutoa tamko hilo kutoka na kukithiri kwa matukio hayo.

Nyamka alisema kwamba matukio hayo ya unyang'anyi wa kuporwa pikipiki na kufanya mauaji yanafanywa na kikundi cha majambazi.

Alifafanua kuwa hivi karibuni kumetokea tukionla Katibu wa CCM tawi la Miswe kata ya Mbawa ambapo ndugu Sitaki Pazi kuporwa pikipiki na kuuwawa.

Pia Mwenyekiti Nyamka alisema kwamba chama pia kinalaani vikali mauaji ya kikatili aliyofanyiwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albino)  Asimwe Novat mwenye umri wa miaka miwili na nusu.



Katika hatua nyingine chama cha mapinduzi kimetoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa hatua ambazo limeanza kuzichukua na kuwatia mbaroni baadhi ya watuhumiwa na kuomba waongeze kasi ili hali hiyo itoweke kabisa nchini.

Pia katika tamko hilo limempomgeza kwa dhati Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka kwa kuweza kusaidia familia yenye watoto wawili wenye ulemavu wa ngozi(Albino).

Alisema kwamba Mbunge Koka amewasaidia watoto hao wawili kwa kuwavutia huduma ya maji safi na salama kutoka Dawasa pamoja na kuwapatia jiko la gesi.

Nyamka alisema kwamba Mhe.Mbunge ameguswa kwa kuinarisha ulinzi kwa familia zenye uhitaji maalumj na watu wenye ulemavu wa ngozi.

Pia aliongeza kuwa siku zote chama cha mapinduzi kinaubiri amani na utulivu hivyo wanaliomba jeshi la polisi kuebdelea kuimarisha ulinzi kwa wananchi pamoja na mali zao.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka alisema kwamba atahakikisha anaweka mipango ya kuwalinda na kuwatunza watu wenye ulemavu wa ngozi.

Koka alisema kwamba ataendelea kuwasaidia kwa hali na mali watu wenye ulemavu ili waweze kuishi katika mazingira ambayo ni rafiki na katika hali ya ulinzi na usalama.

Aidha Koka alitoa wito kwa wananchi wa Jimbo lake kuwa na umoja na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola endapo wakibaini watu ambao wanahusika katika matukio ya mauaji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.