NDOMANAKE.
Friday, October 01, 2010
BANGO
Mwimbaji na rapa machachari, mdogo kuliko wote mwenye maajabu katika stage wa Mwanamuziki Ferre Gola kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo anayejulikana kama (Shikitu) akihojiwa na wanahabari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K,Nyerere, Kiongozi wao mwanamuziki Ferre Gola yeye anatarajiwa kuwasili LEO mnamo saa 12 jioni na anatarajia kufanya onyesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee LEO Ijumaa akishirikiana na bendi ya Mashujaa inayoongozwa na Mwanamuziki Jado Field Force na kisha jumamosi mchana jijini MWANZA katika uwanja wa ccm KIRUMBA.
Wednesday, September 29, 2010
BANGO
MASHUJAA GROUP LTD NA NY PRODUCTION USPIME KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA BURUDANI WANAKULETEA BURUDANI YA MTIKISIKO FERRE GORA NA SHIKITO TOKA KONGO LIVE AMBAPO WATASINDIKIZA UZINDUZI WA ALBUM YA SAFARI YA VIKWAZO YA BENDI YA MASHUJAA MUZIKA TOKA JIJI LA DAR ES SALAAM
ONYESHO NI NI MOJA TU JUMAMOSI HII TAREHE 2OCT2010
CCM KIRUMBA KIINGILIO SH 5,000 WATU WAZIMA NA 3,000 WATOTO
NI KUANZIA SAA 8 MCHANA NA KUENDELEA
MARAFIKI WASTAARABU WOTE WA MWANZA WATAKUWA PALE!
KUMPOKEA FERRE GORA AMBAYE ANAKUJA LIVE KUZINDUA NA MASHUJAA MUZIKA
UZINDUZI NI JUMAMOSI HII CCM KIRUMBA MWANZA,
USIKOSE!!!
Tuesday, September 28, 2010
HABARI
Jeshi la Tanzania limesema limemkamata mshukiwa mmoja wa Uharamia raia Somalia, kufuatia makabiliano makali ya ufyatulianaji wa risasi katika bahari ya Hindi.
Ripoti zinasema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili iliyopita katika eneo la Kusini mwa pwani ya Tanzania, eneo ambalo meli ya kampuni ya kuchimba mafuta ya Ophir inafanya utafiti ili kubainisha ikiwa eneo hilo lina utajiri wa mafuta ya Petroli.
Msemaji wa jeshi la wanamaji nchini Tanzania, Steve Buyuya, amesema manuawari ya kijeshi ilishambuliwa kwa risasi na maharamia waliokuwa kwenye mashua ndogo.
Lakini baada ya ufyatulianaji wa risasi uliodumu kwa muda, maharamia kadhaa walifanikiwa kutoroka huku mmoja wao akikamatwa na wanamaji wake.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.