ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 29, 2017

MUUMINI MWINJUMA NI CHUMA CHA RELI AISHTUKIZA MWANZA KWA SHOW YA HATARI USIKU WA KUAMKIA LEO.

Mwanamuziki mkurugenzi wa Double M Plus Muumini Mwinjuma akiimba katika show yake iliyofanyika jana ijumaa ndani ya Villa Park Mwanza na kusisismua wengi waliohudhuria.
Kwa mara nyingine tena, Double M Plus tena kama mashambulizi ya kustukiza hivi usiku wa kuamkia leo yaani jana ijumaa wameangusha mbungi la burudani katika kiota cha Villa Park Mwanza.

Bosi wa bendi hiyo Mwinjuma Muumin akiwa na wakali wengine wa bendi hiyo amefunika tena sana kwa masauti yake matamu. 

Double M Plus ilitimua vumbi ndani ya ukumbi huo kwenye onyesho la kufungua pazia ya ratiba yao ya kutumbiza Kanda ya Ziwa wakiwapa likizo fupi ndugu zao Super Kamanyola.

Double M Plus ikadhihirisha kuwa ina utajiri wa program ya nyimbo pendwa (hit songs) kuanzia zile za Mchinga Sound, Tam Tam na Double M Sound ambako kote huko Muumin alishiriki kuzalisha kazi nyingi zilizotesa ndani na nje ya Bongo. 

Nyimbo kama “Kiu ya Mapenzi”, “Tunda”, “Mgumba”, “Kilio Cha Yatima”, “Kisiki Cha Mpingo” na nyingine nyingi zilinguruma Equator Grill na kusisimua mashabiki waliofika kwenye ukumbi huo ulioko Kirumba jijini Mwanza.














SIMBA U20 YAAGA MASHINDANO YA HISANI YA ATF YATOLEWA NA TANZANIA PRISONS KWA PENATI

 BEIKI wa Simba U20, Jacob Jalala (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Mohamed Rashid, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 BEKI wa Tanzania Prisons, Michael Ismail (kushoto) akijaribu kumpita mchezaji wa Simba U20, Rashid Juma, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 BEIKI wa Simba U20, Abdallah Rashid (kulia) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Kassim Hamis, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 KIPA wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo, akiokoa moja ya hatari langoni kwake wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 WACHEZAJI wa Tanzania Prisons, wakimdhibiti mshambuliaji wa Simba U20, Abilay Issa, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
  MSHAMBULIAJI wa Simba U20, Said Hamis (kulia) akichuana kuwania mpira na beki wa Tanzania Prisons, Sharif Shaban, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 BEKI wa Simba U20 Erick Costantine (kulia) akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Cleophace Anthony, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani
 MCHEZAJI wa Simba U20, Abilay Issa (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Tanzania Prisons, Sharif Shaba, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa jana Julai 28, 2017 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Katika mchezo huo Tanzania Prisons ilishinda kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya mchezo huo kumalizka dakika 90 kwa sare ya 1-1. Picha na Muhidin Sufiani


TIMU ya Vijana wa Simba chini ya umri wa miaka 20, jana walishinda kuungana na wenzao wa Yanga katika fainali ya Mechi za Hisani kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI baada ya kufungwa na Tanzania Prisons kwa mikwaju ya penati 6-5 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu wa Sokoine jijini Mbeya.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka uwanjani bila kupata bao, huku timu zote zikicheza kwa taadhari na kufanya mashambulizi ya kushitukiza.

Katika mchezo huo Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 69 kupitia kwa mshambuliaji wake, Dadi Mbarouk, baada ya kuwatoka mabeki wa Tanzania Prisons Aron Kalambo, aliyekuwa ametoka golini akijaribu kuwahi kumzuia na  kupishana na mpira uliotinga wavuni.

Bao la kusawazisha la Tanzania Prisons, lilifungwa na Kassim Hamis, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 79, baada ya mchezaji wa Simba U20, kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na kufanya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa sare kwa kufungana 1-1.

Baada ya sare hiyo timu hizo zilikwenda katika hatua ya matuta, ambapo zilipigwa jumla ya penati 8, na Tanzania Prisons wakikosa 2 na kupata penati 6 na Simba wakikosa 3 na kupata penati 5.

Simba wameungana na wenzao Mbeya City Kikosi cha kwanza ambao walitolewa na Kikosi cha Yanga U20 kwa kukubali kichapo cha mabao 3-0 katika mechi hizo za Hisani zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, na kushirikisha jumla ya timu Nne za Yanga U20 na Simba U20 kutoka jijini Dar es Salaam, Mbeya City na Tanzania Prisons vikosi vya kwanza Ligi Kuu Bara.

Mchezo wa fainali unachezwa leo jioni kwenye Uwanja huo wa Sokoine kati ya Yanga U20 na Tanzania Prisons.

Akizungumzia matokeo hayo Kocha wa Simba U20, Nico Kiondo, alisema kuwa kwa upande wao hali ya hewa ilichangia kwa kiasi kikubwa kupata matokeo hayo lakini pia maandalizi yao hayakuwa ya kutosha kwani wachezaji wengi ni wageni ndani ya Kikosi chao.

''Kwa kweli hali ya hewa imetugharimu kupoteza mchezo wa leo lakini pia hatukuwa na mazoezi ya kutosha kabla kwani wachezaji wengi ni wageni waliojiunga na timu msimu huu''. alisema Kiondo

Kwa upande wake Kocha wa Tanzania Prisons, Abdalla Mohamed, alisemakuwa timu yake imejitahidi kupata matokeo hayo japo imecheza na kikosi cha pili cha Simba kutokana na timu zote kucheza kwa uangalifu kwani hawakuwa na maandalizi ya kutosha baada ya usajili wa wachezaji wapya ambao wengi wao ndiyo walicheza ili kuwajaribu ili kuona mapungufu, huku wengine wakitarajia kucheza katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga.

''Nimeona mapungufu kwa wachezaji wangu na hasa kwa safu ya ushambuliaji, nitayafanyia kazi ili kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo kwani wachezaji wangu wengi ni wageni ambao tumewasajili msimu huu bado hawajazoea hali ya hewa, na wengini nitawajaribu katika mchezo wa leo dhidi ya Yanga''. alisema Mohamed

CCM ARUSHA YAPATA PIGO.

KATIBU wa Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Mkoa wa Arusha, Hillal Soud amefariki dunia jana nyumbani kwake Njiro majira ya saa tatu usiku.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho mtoto wa marehemu Ramadhan Soud alisema marehemu baba yake alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu.

Alisema kabla ya marehemu baba yake kufikwa na umauti alipatiwa matibabu katika hosptali ya Shirhindu ambapo afya yake iliimarika na kurudishwa nyumbani.

Akizungumzia kifo cha Soud kwa niaba ya CCM Mkoa wa Arusha Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa, Shaaban Mdoe alisema chama kimepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa kwani juzi walikuwa naye kwenye kikao cha Sekretararieti ya mkoa.

Kwa mujibu wa Mdoe Julai 26 mwaka huu walikuwa na marehemu kwenye kikao akiwa mzima wa afya, lakini baada ya muda aliwaambia kuwa anasikia maumivu ya kichomi chini ya kifua mkono wa kushoto.

“Naisikia sauti ya marehemu kwenye masikio tangu hapo mpaka sasa baada ya kusema anasikia kichomi alitania wajumbe wa kikao nitakufa nini nina miaka 62, kisha kanigeukia na kuniambia nyie ni vijana mna nguvu ya kukimbia kimbia na kukipigania chama,”alisema.

Alisema hata hivyo aliendelea na kikao hadi kilipomalizika jioni bila tatizo lolote ambapo aliagana na wajumbe na kuelekea nyumbani kwake.

Alisema siku iliyofuata kulikuwa na kikao cha kamati ya siasa ya mkoa ambapo alimtumia ujumbe wa meseji Katibu Msaidizi wa CCM mkoa  Omary Bilal kumjulisha kuwa hajisikii vizuri hivyo hataweza kushiriki kikao na kwamba amepumzishwa kwa muda katika hosptali ya Shir Hindu iliyopo mkoani hapa.
Mdoe aliendelea kufafanua kuwa baadaye jioni majira ya saa 10  hivi alimtumia tena ujumbe katibu huyo na kumjulisha kuwa afya yake imeimarika na kwamba ameruhisiwa kwenda nyumbani.

“Baada ya kupata taarifa hiyo katibu wa CCM  mkoa Elias Mpanda  alimpigia simu kumjulia hali ambapo alijibu kuwa anandelea vizuri na ameruhusuwa kwenda nyumbani kupumzika,”alisema
Kwa mujibu wa mdoe usiku majira ya saa tatu alipata taarifa kuwa marehemu alianguka ghafla nyumbani kwake na kufikwa na mauti.

Alisema CCM imepata pigo kwa kupoteza kiungo muhimu ambaye alikuwa amebobea katika masuala ya fedha na utawala ambapo alikisadia chama katika masuala mbalimbali ya kukuza uchumi wa chama pamoja na jumiya zake.

“Tumepata pigo kubwa Soud alikuwa kwenye mchakato wa kupata wawekezaji wa kuwekeza kwenye maeneo yetu ya wazi Sakina na Njiro lakini pia kuboresha uwanja wa Sheik Amir Abeid, lakini pia alitusaidia  kurekebisha bajeti ya uchaguzi wa jumuiya za chama,”alisema

Kabla ya kuwa mchumi wa CCM mkoa wa Arusha Soud alikuwa Mkurugenzi wa NMB Kanda ya Kaskazini,mpaka alipostaafu.

Marehemu Soud ameacha  watoto sita na mjane mmoja na  amezikwa leo(jana) katika makaburi ya njiro .

Friday, July 28, 2017

BINTI WA MIAKA 17 ABAKWA KWA AMRI YA BARAZA LA KIJIJI, KISA? KAKA YAKE KABAKA.


Polisi ya Pakistan imeamuru kutiwa nguvuni wajumbe 20 wa Baraza la kijiji kimoja cha katikati mwa nchi hiyo baada ya wajumbe hao kutoa hukumu ya kubakwa na kunajisiwa binti mwenye umri wa miaka 17 ili kulipiza kisasi cha uhalifu kama huo uliofanywa na kaka yake. 
Suala hilo limefichua zaidi hali inayotawala mfumo wa kikabila nchini Pakistan. Kamanda wa Polisi ya eneo hilo, Saliim Khan Niyazi amesema kuwa, msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 alibakwa na kunajisiwa katika mji wa Multan katika jimbo la Punjab.
Baraza la kijiji hicho liliamuru msichana huyo abakwe ili kulipiza kisasi cha kitendo kilichofanywa na kaka yake cha kumbaka msichana mwingine katika eneo hilo. Msichana huyo alikamatwa na kubakwa mbele ya wazazi wake.

Mabaraza ya vijiji yanatambuliwa kuwa ni mbadala wa mahakama dhaifu za Pakistan ambazo huchelewesha kesi zinazowasilishwa huko kwa miaka mingi. Maamuzi ya mabaraza hayo yanayotegemea ada za kikabila, yanakubaliwa na wakazi wa maeneo ya vijijini, ingawa hayatambuliwi rasmi na serikali ya Pakistan.
Kamada wa Polisi, Saliim Khan Niyazi amesema mkuu wa baraza hilo lililotoa hukumu ya kubakwa msichana huyo na wajumbe wengine 20 wametiwa nguvuni na kwamba mtuhumu mkuu ametoroka.
Mkuu wa jimbo la Punjab, Shahbaz Sharif ameliamuru jeshi la polisi kuwasaka na kuwakamata wajumbe wote wa baraza la kijiji hicho

YANGA U20 MBEYA CITY FC WAKIWA KAMILI UWANJA WA SOKOINE MBEYA NA KUTANGULIA FAINALI

 MSHAMBULIAJI  wa timu ya Yanga U20, Said Mussa (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Mbeya City, Erick Kyaruzi, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0. Picha na Muhidin Sufiani

 MSHAMBULIAJI  wa timu ya Yanga U20,Yusuph Nyamiundu, (katikati), akijaribu kuwatoka mabeki wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0. Picha na Muhidin Sufiani

MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga U20,Paul Godfrey, (kulia), akimtoka mchezaji wa Mbeya City, Anthony, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0. Picha na Muhidin Sufiani

 BEKI  wa timu ya Yanga U20, Mawazo Gawasa, (kushoto) akiwadhibiti wachezaji wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0. Picha na Muhidin Sufiani

BEKI  wa timu ya Yanga U20, Mawazo Gawasa, (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0. Picha na Muhidin Sufiani

BEKI wa timu ya Yanga U20, Bakari Jomba, (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Mbeya City 'Demba Ba', wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0. Kulia ni Saad Awadh, akijiandaa kutoa msaada. Picha na Muhidin Sufiani

BEKI  wa timu ya Yanga U20, Mawazo Gawasa, (kushoto) akimdhibiti winga wa Mbeya City, Idd Nabe, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0. Picha na Muhidin Sufiani

YANGA U20 YAWADUWAZA MBEYA CITY FC WAKIWA KAMILI UWANJA WA SOKOINE MBEYA NA KUTANGULIA FAINALI

NA MUHIDIN SUFIANI, MBEYA
TIMU ya Vijana ya Yanga U20 jana iliwashangaza mashabiki wa soko waliojitokeza kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kuacha gumzo baada ya kuwaduwaza Mbeya City wanaoshiriki Ligi Kuu Bara kwa kuwachapa mabao 3-0 katika mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI.

Mechi hizo za Hisani zimeandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, ambapo zinashirikisha jumla ya timu Nne za Yanga U20 na Simba U20 kutoka jijini Dar es Salaam, huku Mbeya City na Tanzania Prisons zikiwa ni zile zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.

Kabla ya mchezo huo kuanza wakati timu zikipasha misuli, mashabiki waliokuwapo uwanjani hapo baadhi walisikika wakijutia kuingia uwanjani kwa kuhisi kukosa burudani, lakini kadri mchezo ulivyokuwa ukiendelea baadhi ya mashabiki walianza kubadilika na kuanza kuwashangilia vijana hao wa Yanga U20, waliokuwa wakionyesha kandanda safi na kuwainua vitini mashabiki wa Soka wa jiji la Mbeya.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia tayari Yanga wametangulia fainali na kusubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Simba U20 na Tanzania Prisons ambapo fainali hiyo itachezwa siku ya Jumamosikwenye Uwanja wa Sokoine.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Maka Edward, katika dakika ya 30 kipindi cha kwanza, akimalizia pasi nzuri ya Said Mussa na dakika ya 64 kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati, baada ya kipa wa Mbeya City, Fikirini Bakari, kumchezea rafu mshambuliaji wa Yanga,Paul Godfrey, ndani ya eneo la hatari, huku pazia la mabao likifungwa na Festo Greyson, katika dakika ya 79 baada ya kazi nzuri ya Paul Godfrey, aliyemtoka beki wa kushoto wa Mbeya city na kupiga krosi nzuri iliyozaa bao hilo.

Akizungumzia matokeo hayo Kocha msaidizi wa Mbeya City Mohamed Kijuso, alisema kuwa kwa upande wake amechukulia ni matokeo ya kawaida na kutokana na kwamba hakuna wanachopoteza bali ilikuwa ni kipimo tosha kwa wachezaji wake ambao baadhi ni wageni waliojiunga na timu msimu huu kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na kuongeza kuwa ameona mapungufu mengi ambayo atayafanyia kazi na Kocha mkuu atakayejiunga na kikosi hicho.

''Kikubwa ni mazoezi kwani tayari nimeona mapungufu ndani ya kikosi changu, nitayafanyia kazi na Kocha atakayejiunga nasi hapo baadaye, ila mashabiki watambue kuwa haya ni matokeo tu ya mchezo na hakuna atulichopoteza kwani ulikuwa ni mchezo wetu wa kwanza kujiandaa na kuangalia kikosi chetu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu''. alisema Kijuso.

Kwa upande wake Kocha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema kuwa amefurahishwa na matokeo hayo ambayo alikuwa akiyatarajia baada ya kuona wapinzani wake wamepanga Kikosi cha Ligi Kuu, huku yeye akiwaamini na kuwapa majukumu Vijana wa U20, ambao hawakumuangusha baada ya kufuata maelekezo waliopewa.

''Kwa kweli Vijana wangu wamenifurahisha sana na matokeo haya kwa upande wangu kama mwalimu niliyatarajia na hasa baada ya kuona wapinzani wakiwa na kikosi cha wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu, kwani nilijua watacheza kwa kuwazania vijana wangu na kujiamini sana jambo ambalo vijana wangu walilitumia kuwashangaza na hawakuamini kilichowakuta katika dakika 90 za mchezo,

Mimi nilikuwa na vijana wawili tu walicheza ligi msimu uliopita na mmoja ambaye amepandishwa msimu huu, lakini niliwaamini zaidi vijana na kuwapangia Mhilu tu aliyeshiriki ligi iliyopita ili kuwapa hamasa wenzake jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa'', alisema  Nsajigwa

NGOME YA MAALIM SEIF YABOMOKA, MAGUFULI AWAKINGIA KIFUA MACHINGA MORO, NEC YATEUA WABUNGE WA 4 WAPYA CUF.

Ngome ya Maalim Seif abomoka, Magufuli awakingia kifua machinga Moro, NEC yateua wabunge wanne wapya CUF, Pata kwa undani yaliyojiri katika magazeti ya leo hapa.

WATAALAMU WATANGAZA DAWA YA KUKINGA UKIMWI, MKUTANO WA KIMATAIFA WA UKIMWI, PARIS

Wataalamu walioshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Ukimwi uliofanyika Paris nchini Ufaransa wametangaza mbinu mpya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV na kutibu maradhi ya Ukimwi.

Ripoti zinasema mkutano huo ambao ulimaliza kazi zake usiku wa kuamkia leo, ulihitimishwa kwa kutangazwa habari za mafanikio ya kuzuia na kutibu maradhi ya Ukimwi.

Washiriki katika mkutano huo wanasema dawa hiyo mpya ya Ukimwi imetengenezwa kwa namna ambayo inapambana na virusi vya HIV na kuvifubaza, na kwamba mafanikio haya ni habari nzuri kwa watu wenye virusi hivyo au wale wenye ndugu na jaa walioathirika.
Ukimwi umeua zaidi ya watu milioni 35 duniani

Chris Beyrer wa jumuiya ya The International AIDS Association anasema kuwa, mtu mwenye mume au mke aliyeathiriwa na virusi vya Ukimwi anaweza kutumia vidonge vyake vya kila siku au kudunga sindano mara moja kwa miezi mwili na hivyo kuzuia kabisa uwezekano wa kupatwa na virusi hivyo. Amesisitiza kuwa, hayo ni mafanikio na mapinduzi makubwa katika vita na mapambano dhidi ya Ukimwi.

Nchi ya Swaziland barani Afrika ndiyo inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waathirika wa virusi vya Ukimwi na unaripotiwa kuwa, mtu mmoja kati ya kila watu watatu ameambukizwa virusi hivyo

Zaidi ya watu milioni 35 wamepotea maisha tangu vurusi vya HIV na Ukimwi ulipoeneza duniani katika miaka ya 1980.

Thursday, July 27, 2017

WAZIRI SIMBACHAWENE: UKOSEFU WA FEDHA WASIMAMISHA MIRADI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhe. George Simbachawene amesema miradi mbalimbali inashindwa kuendelea kwa sababu ya ukosefu wa fedha kwenye mfuko wa maendeleo vijijini.

Akizungumza na wadau wa maendeleo leo Jijini Dar es Salaam kutoka ndani na nje ya nchi Waziri Simbachawene amesema mfuko wa maendeleo umezorota kwa miaka kadhaa sasa,  hivyo serikali kwa kuliona hilo wameamua kuupitia upya mfuko huo na utendaji wake ili waweze kurejesha uhai wa maendeleo vijijini hasa kwa barabara, nyumba za walimu, zahanati na madarasa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amewataka maafisa kodi kuhakikisha wanabuni njia mpya za mapato ili kujazia mfuko huo kwakuwa lengo la nchi ni kujitegemea yenyewe na sio kutegemea nchi wahisani.

DK. KIGWANGALLA AKABIDHI GARI LA WAGONJWA JIMBONI KWAKE


Gari hilo la kubebea wagonjwa linavyoonekana

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge, lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.



Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge, lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.
Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) mpya na la kisasa katika Kituo cha Afya Busondo kilichopo Tarafa ya Puge ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Nzega Vijijini.

Tukio hilo la kukabidhi gari hilo limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani  Tabora, Mh. Geofrey Ngupula mapema Julai 26,2017, aliyekuwa mgeni rasmi ambaye alitoa agizo kali kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho kuhakikisha gari hilo linatumika kwa shughuli zilizokusudiwa ikiwemo za kubebea wagonjwa na akina mama wajawazito kuwawaisha sehemu muhimu za kutolea huduma stahiki.

Mkuu wa Wilaya huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Dk. Kigwangalla kwa kuweza kuwasaidia wananchi  wa Jimbo hilo kwa kuweza kuwasaidia gari hilo la Wagonjwa  kwani litasaidia kuokoa maisha ya wananchi hao ambao wapo maeneo ya mbali na kituo cha Afya huku pia likitarajiwa kuwa msaada kwa kuwapeleka wateja katika  ngazi za juu za huduma hiyo ikiwemo Hospitali za  Wilaya, Mkoa, Kanda na Taifa.

Aidha, alisema ni marufuku wagonjwa kuombwa  kuchangia mafuta ya  ambulance hiyo au gharama yoyote ile, gari hili wagonjwa walitumie bure kwani limetolewa bure na pia huduma zote zikiwemo za mafuta zinalipwa na Halmashahuri hiyo.

“Gari hilo lipatikane kituoni  wakati wote pamoja na dereva. Tumeshahakikishiwa hapa Halmshauri imesema ina mafuta ya kutosha litakuwa linajazwa lita 90, kila yatakapokuwa yametumika hivyo kusiwe na kisingizio kingine cha kuweza kudai mafuta ama kuwatoza wananchi gharama na atakayefanya hivyo Serikali hii si ya mchezo hatua kali zitafuata , tutakutumbua tu” alieleza Mh. Ngupula.

Ameongeza kuwa gari hilo ambalo ni la kisasa, litunzwe na kulindwa ili liweze kutumika kwa miaka mingi ijayo na kuwa  msaada kwa Tarafa hiyo na wananchi wote watakaopata msaada wakiwemo wale wa maeneo mengine ya jirani.

Kwa upande wake, Dk. Kigwangalla amewaomba wananchi waendelee kumuombea kwa kazi anayofanya ikiwemo jukumu la kulitumikia Taifa katika nafasi yake ya Unaibu Uwaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Dk. Kigwangalla ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli  kwa kuweza kuwa karibu na Wananchi ikiwemo kushughulikia suala la maji kutoka Ziwa Victoria na kuja Mkoa wa Tabora ikiwemo kuanzia katika Wilaya hiyo ya Nzega na kisha kwenda maeneeo mengine.

“Tunampongeza Rais wetru Dk. Magufuli kwa kuwa karibu na wananchi wake. Tulikuwa nae Mkoani kwetu hapa Tabora na amezindua miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara na ule wa maji safi yatakayotoka Ziwa Vitoria. Shida ya maji kwa wananchi wa Nzega inaenda kuwa historia kwani Maji hayo yatakuja hapa na kisha kwenda maeneo mengine. Rais wetu anatupenda na tuendelee kumuunga mkono hasa juhudi zake za kulinda rasilimali za nchi yetu na pia katika kushughulikia mafisadi na wahujumu uchumi wa Taifa letu

Mimi Mbunge wenu pia muendelee kuniombea na kila siku mawazo yangu na akili yangu ipo pamoja nanyi ndio maana nimeweza kuwaletea gari hili la wagonjwa, na pia kufanikisha kuandaa kambi maalum ya matibabu bure ya wiki moja kwa wananchi wote wa Nzega bure inayoendeshwa na Madaktari bingwa wakiwemo wale wa kutoka China na waliopo hapa nchini” alieleza Dk. Kigwangalla.

Tukio hilo la ukabidhi wa gari hilo pia lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani wa Jimbo hilo na wale wa jimbo jirani ikiwemo Bukuene, Viongozi wa ulinzi na Usalama pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nzega.

SIMBA NA YANGA KUSHUKA DIMBANI KUTUNISHA MFUKO WA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI BINADAMU

Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu,Seperatus Fella, akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha  wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu,lengo ikiwa ni kupitia Sheria mbalimbali zinazosimamia biashara hiyo.Wengine ni Mwenyekiti wa kamati hiyo () na Mkurugenzi Mradi wa kuzuia biashara hiyo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya RTI,Dk. Lyungai Mbilinyi.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mradi wa Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka Taasisi ya Kimataifa ya RTI,Dk. Lyungai Mbilinyi,akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha  wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara hiyo,lengo ikiwa ni kupitia Sheria mbalimbali zinazosimamia biashara hiyo.Wengine ni Mwenyekiti wa kamati hiyo () na Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu,Seperatus Fella.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu,() akizungumza wakati wa mkutano wa  kupitia Sheria mbalimbali zinazosimamia biashara hiyo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam
Mjumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu,() akizungumza wakati wa mkutano wa  kupitia Sheria mbalimbali zinazosimamia biashara hiyo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam
Nchi ya Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa mataifa yanayoshamiri kwa biashara haramu ya kusafirisha binadamu kwa ajili ya utumwa wa ngono duniani.

Kupitia taarifa iliyotolewa mnamo mwezi July 4 mwaka 2016 na Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya kuzuia na kupambana na biashara haramu ya bianadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Bw. Separatus Fella alipokuwa akiongea katika mkutano uliondaliwa na Shirika la Kimataifa la Msaada wa Sheria (NOLA) kwa lengo la kutoa elimu juu ya mdhara ya kusafirisha watoto.

NUKUU YAKE INASEMA "Tanzania ni mkondo na chanzo cha usafirishaji wa wanawake na watoto wanaopelekwa kwenye biashara ya utumwa wa ngono katika mataifa mengine, na hii ni kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa nchini Marekani," alisema Fella.

Aidha wasafirishaji binadamu wamekuwa wakitumia Tanzania kama chanzo cha kupitisha na kupata watoto wanawake wakufanya biashara hiyo.

Baadhi ya mambo yanayochochea biashara ya usafirishaji haramu binadamua ni pamoja na umasikini na kukata tamaa, ukatili wa majumbani, njaa na vita, ukosefu wa ajira na mishahara kidogo, ndoa kuvunjika, kukosekana kwa usawa wa kijinsia na ukosefu wa elimu.