Akizungumza na wadau wa maendeleo leo Jijini Dar es Salaam kutoka ndani na nje ya nchi Waziri Simbachawene amesema mfuko wa maendeleo umezorota kwa miaka kadhaa sasa, hivyo serikali kwa kuliona hilo wameamua kuupitia upya mfuko huo na utendaji wake ili waweze kurejesha uhai wa maendeleo vijijini hasa kwa barabara, nyumba za walimu, zahanati na madarasa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji amewataka maafisa kodi kuhakikisha wanabuni njia mpya za mapato ili kujazia mfuko huo kwakuwa lengo la nchi ni kujitegemea yenyewe na sio kutegemea nchi wahisani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.