ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 1, 2009

HASHEEM THABEET IPEPEE MWANA


AKIZALIWA KAMA HASHIM THABIT MANKA FEBR16/1987 DAR ES SALAAM JAMAA KESHA INGIA KTK MOJA YA LIGI YENYE USHINDANI NA ILIYO MAARUFU ULIMWENGUNI(NBA). ANAUREFU WA FUTI 7 NCHI 3 NA UZITO WA KILO 119. THABEET AMESHAWEKA HISTORIA YA KUWA MCHEZAJI WA KWANZA KUCHEZEA HUSKIES KWA UREFU HUO. HAKUWAHI KUCHEZA BASKET WALA KUWA NA MAPENZI NA MCHEZO HUO HADI ALIPOTIMIZA UMRI WA MIAKA 15 AKIWA KATIKA SHULE YA SEC YA MAKONGO. JAMAA MMOJA ALIVUTIWA NA UREFU WAKE AKAMWAHIDI KUMPATIA VIATU VYA KUCHEZEA NA KUMUALIKA KATIKA TIMU YAKE SIKU ILIYOFUATA, HAKULAZA DAMU, MCHEZO UKAMKOLEA! AKIWA KAMA MEMBA WA TIMU YA KULI AKACHAGULIWA KUWA MMOJA WA WAKILISHI KTK MICHEZO YA AFRIKA MASHARIKI ILIYOFANYIKA NAIROBI NCHINI KENYA AMBAPO MMOJA WA MAAJENTI ALIMWONA NA KUMPA OFA KWENDA KUPIGA KITABU KWENYE MOJA YA SHULE ZA BASKETBALL NCHINI MAREKANI. NDO IMETOKA.......

Monday, June 29, 2009

MASWALI MENGI YAZUKA KIFO CHA NGULI WA POPKIFO CHA NGULI WA MUZIKI WA POP DUNIANI KIMEZUA MASWALI MENGI KUHUSU NINI KILISABABISHA AFYA YAKE KUBADILIKA HATIMAYE KIFO, NA HATA NINI HATMA YA JAMII ILOKUWA IKIMTEGEMEA. WATOTO WAKE WATATU ALOWAACHA NI MIONGONI MWA WATU WANAOTAJWA ZAIDI. NAMNA GANI WATAISHI, NANANI ATAKAYEKUWA MLEZI BAADA YA BABA YAO KUAGA DUNIA? DEBBIE ROWE NESI ALIYEOLEWA NA MICHAEL 1996 NAKUTALIKIWA 1999 NA MAMA WA PRINCE MICHAEL(12) NA PARIA(11) NA PRINCE MICHAEL II (aka BLANKET) HUYU ANARIPOTIWA KUWA ALIZALIWA NA MAMA AMBAYE MPAKA LEO JINA LAKE HALIJATAMKWA HADHARANI. MSEMAJI MKUU WA JACKSON AMBAYE PIA NI RAFIKI WA FAMILIA BWANA BRIAN OXMAN AMEMTAJA MAMA MZAZI WA MICHAEL (pichani kulia) NDIYE ATAKAYEKUWA MWANGALIZI WA WATOTO KWA SABABU ANAWAJUA KIUKARIBU NA AMEKUWA AKIKAANAO MARA KWA MARA. YOTE HAYA YANASEMWA LAKINI KWA VYOVYOTE VILE KUNA JAMBO LITAZUKA TOKA KWA DEBBIE ROWE MAMA WA WATOTO.