ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 23, 2022

MREMBO MBARONI KWA DAWA ZA KULEVYA WENGINE WASHIKWA NA MENO YA TEMBO IRINGA

 

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa habari juu ya matukio mbalimbali ambayo yametokea katika mkoa huo
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha silaha aina ya mapanga ambayo hutumiwa na waalifu
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha silaha aina ya bunduki ambazo hutumiwa na waalifu.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

JESHI la polisi mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Askari wa Uhifadhi kutoka hifadhi ya Taifa Ruaha wanamshikilia Cyprian Kasula miaka 42, mkulima na mkazi wa kijiji cha Kipera kwa tuhuma za kukutwa na Kichwa cha Tembo kikiwa na meno yote mawili katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Akizungumza na waandishi wa habari Iringa, Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi alisema kuwa wanamshikilia Cyprian Kasula miaka 42, mkulima na mkazi wa kijiji cha Kipera akiwa na Kichwa cha Tembo kikiwa na meno yake mawili,Nyama ya Tembo,Mkia wa Tembo,Silaha tatu za kienyeji aina ya Gobore,Vipande vya nondo 35,makopo matatu ya unga wa baruti na Panga moja.

ACP Bukumbi alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa amekaa porini chini ya mti pamoja na mwenzake mmoja ambaye alifanikiwa kukimbia baada ya kuona Askari wamefika eneo hilo na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa alisema kuwa Agnes Chaula miaka 38, mama lishe na mkazi wa Mwangata D kwa tuhuma za kukutwa na vipande vitano vya meno ya Tembo.

ACP Bukumbi alisema kuwa Mama lishe huyo anatuhumiwa kujihusisha na uwindaji haramu na taratibu za kumfikisha Mahakamani zinaendelea.  

Alisema kuwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Christina Mponzi, miaka 34, mkulima na mkazi wa Kihesa akiwa na Madawa ya kulevya yanayodhaniwa kuwa ni Heroine kete 33, mtuhumiwa alikutwa ameweka kete hizo kwenye mkoba baada ya kufanyiwa upekuzi aligundulika kuwa na hayo na anashikiliwa kwa ajili ya upelelezi zaidi na kielelezo kimehifadhiwa kituoni.

Katika hatua nyingine Jeshi la polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Gwelino Mwanzasi miaka 91, mkulima wa Image mkazi wa kijiji cha Kilangali Kata ya Image Tarafa ya Mazombe Wilaya ya Kilolo kwa kukutwa na Silaha nne aina ya Gobore na Shortgun moja,Gololi za Gobore thelathini,Risasi za Shortgun nne,Risasi za G3 tatu,Risasi ya Rifle 404 moja,Ganda la risasi Rifle 375 moja,Baruti ujazo wa nusu lita pamoja na Jino la kiboko moja,Kipande cha ngozi ya Nyati kimoja naGamba la kakakuona moja.

Kamanda polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi alimazia kwa kusema kuwa wanamshikilia Raymond Mgao miaka 28, mkulima wa kijiji cha Mapogoro na Brown Sangwa kwa kukutwa na Meno ya Tembo mazima sita baada ya kuwekewa mtego ambapo watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa kuelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka tutaendelea kufanya misako na operesheni ya nguvu zaidi ili kudhibiti uhalifu wa kijinai na ajali za barabarani na walitoa wito kwa wakazi wote wa mkoa wa Iringa kujiepusha na vitendo vya kihalifu kuelekea sherehe za sikukuu za mwisho wa mwaka.  

TANGA UWASA YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI

 

 





Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza mara baada ya kutembelea mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa maji katika eneo la Mowe unaotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (Tanga Uwasa)
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akionyesha katika ramani muonekano wa ujezi unaoendelea wa mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa Tanga uliopo kwenye eneo la Mowe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly (katikati) akizungumza jambo na mstahiki meya wa jiji la Tanga Abdurahman Shillow (kushoto) pamoja Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamis Mkoba wakiwa katika ziara ya kutembelea mradi wa maji unaotekelezwa na mamlaka hiyo.



Na Oscar Assenga,TANGA

MAMLAKA Maji safi na Usafi wa Mazingira (Tanga uwasa) imepongezwa kwa namna inavyoendelea kutekeleza na kuboresha mradi wa kuongeza huduma ya maji kwa wananchi katika Mtambo uliopo Mowe unaoghalimu kiasi cha shilingi Bilioni 9.18 ambapo kwa sasa upo katka hatua nzuri ya utekelezaji ukitarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2023. 

Pongezi hizo zilitolewa na Kamati ya Siasa ya CCM pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Tanga ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa wakati ilipofanya ziara kutembelea bwawa la Mabayani pamoja na eneo la Mowe kwenye mtambo wa kusafishia maji ambapo mradi huo utakapokamilika  unatarajiwa kuboresha huduma ya maji ikiwemo pembezoni mwa jiji la Tanga pamoja na wilaya za Pangani na Muheza. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kujionea mradi huo pamoja na Bwawa la Mabayani Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashimu Mgandilwa alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ambaye aliridhia na kutoa fedha Shilingi Bilioni 9.9  kwa ajili ya mradi huo ambao umelenga kupunguza au kuondoa kabisa adha ya maji iliyopo ndani ya jiji la Tanga. 

"Tanga ni moja ya miji ambayo inakuwa kwa kasi sana, sasa ukuwaji wa mji wa Tanga unatakiwa kwenda sambamba na ukuwaji wa miundombinu mingine na hiyo ikampendeza Rais wetu Samia Suluhu Hassan kutoa fedha kwaajili ya Mradi tunaamini baada ya kukamilika kwa mradi huu sasa Tanga inakwenda kutatua kabisa tatizo la maji " alisema Mgandilwa.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga (CCM)  Meja Mstaafu Hamis Mkoba ameishauri mamalaka ya maji na usafi wa mazingira (Tanga Uwasa) kuhakikisha inazidi kutatua na kuondoa kabisa changamoto ya kukatika katika kwa maji hii ikiendana sambamba na ukuwaji wa mji wa Tanga ambapo wananchi wanazidi kuongezeka.

 "Tumeridhika kama chama cha mapinduzi kwamba kazi hii inaenda vizuri, ili kusudi matatizo ya kukatika katika kwa maji yasitokee tulikuwa tunawashauri muwe na mipango ya muda mrefu sana ushauri wetu kama chama kwa mamlaka pamoja na kuwapa watu taarifa panatokea changamoto ya kukatika kwa maji lakini tunawapongeza sana Tanga Uwasa kwa jitihada nilizoziona ambazo zinaendelea vizuri kama tutaendelea hivi ninaamini Tanga tutakuwa hatuna shida ya maji" Alisema Meja Mkoba 

Naye kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema kuwa miradi wanayoitekeleza katika kituo kikubwa cha kutibu maji cha Mowe ina lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa maji inaendele vizuri ambapo ifikapo mwezi January 2023 wanatarajia kuanza kuyafanyia majaribio ya kupeleka huduma ya maji kwa wananchi. 


Mamlaka hiyo kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kuboresha mtambo wa kusafisha maji katika kituo kikubwa cha Mowe pamoja na kujenga tanki za kuhifadhia maji ambazo zitasaidia kupeleka maji kwa wananchi hata panapotokea changamoto ya kukatika kwa umeme au uzalishaji wa maji kupungua kutoka kwenye vyanzo vinavyoyegemewa . 

"Hali ya utekelezaji mradi mpaka sasa tunaenda vizuri na tunatarajia kwamba mpaka mwishoni mwa mwezi huu December na mwanzoni mwa January miradi yote itakuwa imekamilika na January mwishoni tunatatajia kufanya majaribiao ya kutumia mradi mpya ambao tumeujenga, lengo kuu hasa ni kuboresha hali ya upatikanaji wa maji kwa jiji letu la Tanga lakini pia maji haya yataweza kuhudumia mji wa Muheza pamoja na vijiji vya njiani" alisema Hilly.

 Alisema kuwa changamoto ya kukatika kwa umeme inaathiri utendaji wa mamlaka hiyo katika kuwafikishia wananchi huduma ya maji ikisababisha kusimama kwa kazi za uendeshaji wa mitambo ya kuzalisha maji ambapo hata hivyo mamlaka ipo kwenye hatua za kuongea na shirika la umeme Tanzania TANESCO katika kuona njia bora ya itakayotumika kuondokana na adha hiyo.

 "Kuna changamoto ya umeme kipindi hiki ambapo inasababisha mitambo yetu ishindwe kuendeshwa hivyo kusababisha upatikanaji wa maji kuwa hafifu sana, sasa hivi tuna tatizo la kukatika kwa umeme kwa takribani masaa matatu hadi matano kwa siku na inaathiri sana uendeshaji wa mitambo"

 " Kwa sasa tuna changamoto ya kutokuwa na tanki kubwa la kuhifadhia maji kwahiyo umeme ukikatika pia na hali ya upatikanaji maji baada ya masaa mawili au matatu hali inakuwa ni tete kwa wananchi lakini tuko katika mipango ya kuongea na Tanesco waangalie namna gani ya kutusaidia lakini pia sisi tupo katika mipango ya kutafuta vifaa madhubuti vya kudhibiti mapungufu ya umeme" alisema Mkurugenzi huyo. 

Bwawa la Mabayani ambalo ni moja wapo ya chanzo kikubwa kinachotegemewa na mamlaka ya maji na usafi wa mazingira (Tanga uwasa ) katika kuwahudumia wananchi wa jiji la Tanga lilianza kujengwa mnamo mwaka 1976 hadi 1978 likiwa na ujazo wa mita bilion 7.7 kwa sasa ,ambapo lina uwezo wa kuzalisha maji lita Milion 30 kwa siku. 

Thursday, December 22, 2022

JEH NI YANGA AU AZAM KUVAA JEZI NYEUSI MCHEZO UJAO AFISA HABARI AZAM FC AFUNGUKA.

 NA ALBERT G.SENGO/ MWANZA

1. Ice cream na Dhahabu haviendani kabisa kwanini hamkuvuna pointi zote 6 za Kanda ya Ziwa? 2. Vipi Mbio za Ubingwa wa NBC Premium League, Jeh bado mnaamini kuwa Azam mpo pazuri? 3. "Pointi 7 siyo nyingi kwetu, 3 kati ya hizo tunazichukuwa Christmas mbele yao zinabaki 4" 4. Mmetangaza mapema kabisa kwamba mtavaa jezi nyeusi mchezo dhidi ya Yanga, Jeh msimamo wenu bado ni huo huo? 5. Dirisha la usajili lijalo, Feisal anakwenda Azam? Afisa Habari wa Azam Fc, Hashim Ibwe amezungumza na Drive Mix ya Jembe Fm Mwanza.

INGIA 2023 NA SIRI YA KUTUNZA SIRI ILI MALENGO YAKO YASIBUME TENA.


INGIA 2023 na Siri ya Kutunza Siri Ili Malengo Yako Yasibume Tena! 

 Denis Mpagaze 

_________

Mafanikio ni siri. Watu wakijua siri za mipango yako watakutoboa macho usione mafanikio yako kama Samson. Samson alitobolewa macho baada ya kushare siri zake na Delila.


Imeandikwa katika Biblia Takatifu kwamba hata mwanamke anayelala kifuani kwako asijue siri zako (Mika 7:5-6). Unaona mambo hayo?


Yusufu aliuzwa na ndugu zake kwa sababu ya kuropoka ndoto zake hovyo. Sasa washirikishe  wazazi wako ndoto zako wakawatambie majirani zenu uone kama utatoboa!😀


Ulisema 2022 ni mwaka wako lazima ununue gari, mwaka wako umeisha hata tolori huna. Unaumia sana konda anavyokwambia kaa chini trafiki asikuone! Wewe kweli ni wa kuambiwa kaa chini!🌝


Ulisema 2022 ni mwaka wako lazima uhamie kwenye nyumba yako, ukaishia kumwaga mchanga site. Sasa unaogopa hata kwenda site. Hata picha za ujenzi hupost tena.Jamanii!


Ulisema 2022 ni mwaka wako lazima ufunge ndoa lakini mwaka wako umeisha na mchumba ndo kwanza hasomeki. Hata online haonekana na wakati alikuwa anashinda huko. Sijui kakublock Mungu wangu!! Sasa kwa nini na wewe ulitangaza?


Ulisema 2022 ni mwaka wako lazima ufungue duka lakini mwaka unaisha huna hata hamu ya kufanya biashara. Hata mkopo uliochukua umeula. Unachenga kuulipa.Taabu tupu!


Ulisema 2022 ni mwaka wako lazima

uende shule, ukamtangazia kila mtu, ukaishia kujaza fomu tu. Ziko mezani kwako! Ukiziona unamind. Wenzako waliokwenda shule ukiwaona roho inaumaaa!


Ulisema 2022 ni mwaka wako lazima

uanze ufugaji wa kuku wa mayai, uliowatangazia wakakukomesha, ukaishia kujenga mabanda. Yerewiiii!!


Ulipandishwa cheo, ukashushwa kwa sababu ulishindwa kutunza siri. Labda nikwambie, hata kama una akili nyingi kiasi gani huwezi pewa nafasi za maana kama huna siri. 


Huwezi kuwa Nabii Mkuu kama huna siri; huwezi kuwa Daktari Bingwa kama huna siri; huwezi kuwa Tajiri Mkubwa kama huna siri, huwezi kuwa Mwandishi Nguli kama huna siri!


 Nimekusikia tena umeanza kutangaza kwamba 2023 ni mwaka wako. Tayari umejiwekea malengo mengine ili yakabume tena maana bado hujaacha kumwaga mchele kwenye kuku wengi. Friji haligandishi. Bado unaongea mnooo!


Mwaka 1926, Kurt Lewin, Baba wa Saikolojia, alisema unapotangaza mipango yako unaifanya akili ione kama tayari limeishafanyika na hivyo kukosa hamu ya kufanya. 


Umetangaza mwaka huu lazima usome vitabu vya kutosha mara unashangaa kila ukishika kitabu unaishiwa hamu ya kusoma, unaacha. Mwaka unaisha hujasoma. 


Ukianza kutekeleza jambo unajisikia uvivu kweli. Uvivu ni kupumzika kabla ya kuchoka. 


Usipotunza siri zako, 2023 utapita tena kapa nakwambia. Bila kutunza siri kila kitu kitakuwa kigumu kwako. Hata ndoa itakuwa ngumu.Utauchukia mwaka nakwambia.


 Unatakiwa kuelewa kwamba siyo kila unayemshirikisha mipango yako akasema hongera ukadhani inatoka moyoni. Wengine zinatoka mdomoni, moyoni inatoka "ushindwe." Na akiishasema ushindwe unashindwa kweli. 


Kuna mtu utamuona dhaifu kwa macho lakini katika ulimwengu wa roho ana mamlaka makubwa ya kuzuia mipango yako. Ndiyo maana ni hatari kuwa na marafiki wengi maana wakiona unaelekea kuwashinda wanakimbia kukuvuta shati huko kwenye ulimwengu wa roho. 


Kumbuka mambo yote yanaanzia huko kwenye ulimwengu. Kwani hujawahi kuota ajali imetokea na kweli ikatokea? Sasa ile siyo ndoto. Ule ni uhalisia, uko kwenye ulimwengu wa roho, au tuseme ulimwengu wa akili. 


Jifunze kufanya mambo yako kuwa siri. 

 Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo (Mithali 25:2). Hata sadaka yako iwe kwa siri. Hakikisha mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume. Baba yako aonaye sirini atakujazia.


Siri ni ulinzi. Mtu asiye na siri hana ulinzi. Kazi ya siri ni kufanya mambo yako yaende  kama ulivyopanga. Usirudie kosa mwaka 2023. Siri ipo kwa ajili ya mafanikio.


Matajiri wote wanaficha mipango yao. Tunawaita washirikina kwa sababu ya usiri wa mambo yao. Na kama unavyojua tena, jamii yetu watu wasipokujua, watakupa utambulisho mbaya ili uropoke siri zako. 


Utaskia anauza watu; anakunywa damu; analala makaburini utadhani ulilala naye. Lakini matajiri hawadanganyiki. Waite majina yote lakini hutoona wakijibu ng'oo!


 Utajiri ungekuwa ni ushirikina basi Sumbawanga, Kigoma na Pemba pangekuwa kama Ulaya.  Wachawi wamenielewa.


Tajiri atakwambia "nilinunua basi nikiwa na umri wa miaka 19 na pesa sikurithi kutoka kwa mtu yoyote;" lakini kamwe hatakwambia alinunuanunuaje! 


Maskini unaweza kukutana naye leo akakusimulia hadi idadi ya vichaa katika ukoo wake utadhani kaulizwa. Sasa kwa hadithi mbaya kama hizi nani atakupa mchongo?


Waliovumbua ndege hawajatoa siri hadi leo. Jifunze kwa hao. Acha kujianika. Hata kama una mpango wa kufuga kuku usiwaambie watu, anza kimyakimya washitukie unauza mayai. Ukianza kutangaza hutofuga, na ukifuga watakufa. Nani kawaua? Utajua hujui.


 Usiwaonyeshe watu ng’ombe anayekupa maziwa,watampa sumu ukose maziwa. Kumwambia mtu mipango yako kabla ya kutenda ni kutoa siri! Hii imewagharimu watu wengi. Ficha mipango yako; fichua matokeo. 


Siri ni hatima ya maisha yako. Coca cola ingetoa siri zake isingekuwa namba moja kimauzo duniani kwa vinywaji baridi. Utamu wa kuku kwenye migajawa ya KFC kote duniani imebaki kuwa siri tangu mwaka 1930 ugunduliwe na Herland huko Kentucky.


" Man is not what he thinks he is, he is what he hides ," alisema André Malraux. Maisha ni siri. Wazungu wamefanikiwa sana katika hili. Mpaka leo siri za kutengeneza ndege zimebaki mikononi mwao. Utatengeneza ndege lakini haitaruka.


 Wazungu wameunda mpaka jamii za siri. Wanaziita Secret Society. Hawa ndo wanatawala dunia. Ni muunganiko wa familia 13 tu, google utazijua. 


Wametengeneza historia ya dunia kutuaminisha kwamba hatuwezi kufanikiwa bila kutegemea huruma za Mungu. Na kweli kila kinachotokea tunasema ni mipango ya Mungu.


Hata mtu akifa kwa kula kinyesi tunasema ni mpango wa Mungu. Kwani kipindupindi si ugonjwa unaosababishwa na kinyesi? 


Wametutengenezea skripti za maisha kama wasanii. Hatutakiwi kutoka nje ya hizo skripti, tutaharibu muvi na director atachukia. Ndani ya hizo skripti za maisha tumeambiwa kuoa wake wengi ni dhambi lakini nje ya hizo skripti mtu anamichepuko ya kutosha. Hapa nature inataradadi. 


Leo ukimwambia Mswahili unaweza kuongea na Mungu bila kupitia dini yoyote hawezi kukuelewa. Ukimwambia Mungu ni mkubwa sana kuliko walivyotufundisha kupitia dini utaambiwa una kufuru. 


Tumepandikizwa ujinga kwamba vitu vizuri vyote ni vya shetani.  


Halafu hawa secret society walivyo wajanja, hawaruhusu watoto wao kuoana na watu wa kawaida.Wanawachagulia watoto wao wachumba. Sisi tukifanya hivyo tunaambiwa ni ushamba. Matokeo yake watoto wetu wanaingia kwenye ndoa na mijitu ya ajabu. Lengo ni kutuvuruga. 


Halafu wako serious sana katika hilo. Mtoto atakayekaidi wanamuua. Kilichomtokea Princess Diana baada ya kumpenda Dodi Fayed kijana wa Uswahilini wote tunajua. Sasa wametuletea ushoga na wakati wao hawafanyi kabisa.


 Mafanikio ni mchezo wa kuangushana, ukiweza kutunza siri huwezi kuangushwa. 


Kwahiyo kabla hujaanza safari ya kutimiza malengo yako ya mwaka 2023, anza na safari ya kutunza siri. 


Huna siri unaonekana mtu wa hovyo sana. Mungu mwenyewe mambo kibao ameyafanya siri, wewe ni nani unaropoka kila unachokifanya. Ndiyo, kwani nani aliishamuona Mungu? Hata kifo Mungu ameendelea kukifanya siri. Hakuna anayejua atakufa lini. 


Siri ni maisha. Vitu vyote vya thamani na vitamu vimewekwa sehemu za siri. Siri huwa haisemwi. Siri inatekelezwa. 


Kwa nini Mungu alikuwa anaongea na Musa peke yake na kumpa maagizo akiwa peke yake? Siri!


Herode alishindwa kumuua Yesu kwa sababu wazazi wake walifanya siri. Mwenzangu ukipata mimba unatembea unatema mate njia nzima, unapiga picha tumbo na vichupi unashare. Huyo mtoto unamuweka hatarini. 


Siri ni msingi wa maisha.Hata maisha ya ndoa yana siri zake; usidhani ni uvumilivu tu. Kuna waliovumilia wakafia humo. Waulize walidumu watakwambia.


 Usijitenge na watu lakini watenganishe watu na siri zako. Kitu chochote cha thamani kimejificha. Msanii anayeonekana hadharani kila mara anapoteza thamani. 


 Hata Mungu angekuwa anaonekana mitaani kuna wapuuzi wangemzoea na kumchukulia poa. 


Moyo ni wa thamani ndiyo maana umefichwa. Mipango yako ni ya thamani ifiche. Kuitangaza inaishiwa thamani. Premature announcements attracts evil spirits. Acha kupiga mayowe: subiri wayaone wenyewe. Michongo mingi huharibika unapoisema.


Usiri ni hatua muhimu sana kuelekea kwenye mafanikio. Ukianza kutunza siri zako mambo mengi yatanyoka na mwaka 2023 utakuwa mwaka wa baraka kwako.


Utajiri hupenda watu wenye tabia ya kujificha. Utajiri unahitaji usiri; umasikini unahitaji uwazi uchaguzi ni wako. Tajiri hapendi aonekane ana pesa kama maskini. 


Masikini atafanya hivyo kwa kuvaa vizuri kwa sababu kuvaa vizuri kunaficha umaskini. Matajiri wanaficha utajiri kwa kuishi kimaskini, maskini anaficha umaskini kwa kuishi kitajiri! 


 Ni hatari kuishi kitajiri na wakati unafikra za kimaskini kichwani. Ingia mwaka 2023 na fikra za kitajiri.Kanyaga mwaka 2023 kwa maringo na mbwembwe maana siri umeijua. 


Pokea zawadi ya vitabu 8 kwa Sh 15,000 tu.  Mpesa 0753665484; 


1. Ukombozi wa Fikra; 

2. Wasomi Huru Gerezani

3. Maisha ni Kutafuta Siyo Kutafutana

4. Ukombozi wa Fikra za Mwafrika

5. Viongozi Wanaoishi Baada ya Kufa

6. Fahamu ya Ndoa Kabla ya Ndoa

7. Miamba ya Afrika

8. Fungua Ubongo


 Happy New 2023 

 Mwl. Denis  Mpagaze 

 Muhenga wa Karne ya 21

KAMA MBAPE ANASEMA HIVI BILA SHAKA 'MESSI ANAHITAJI MAADUI WAPYA'


 Kylian Mbappe wakati akirejea mazoezini huku vyombo vya habari vikiwa na shahuku ya kutaka kujua atamtizama vipi aliyekuwa mpinzani wake kwenye Kombe la Dunia Leonel Messi:

"Tutakuwa na wasaa mzuri na Messi. Huu ni wakati mwingine bora zaidi. Nilifunga penati mbili na ya 3. Alifunga moja na ya 2.

"Alikuwa anafanya kazi zake Qatar na mimi nafanya yangu pia"

Katika ngazi ya Klabu tunafanana shauku zetu na matamanio, na tukifanya kazi pamoja yeye na Neymar... Tutafanya vivyo hivyo tena.....

Aliwahi kuniambia kazi yake ni kunisaidia ili nifanikiwe kama yeye, na kwa hilo ninamwamini.

Kwa huduma na msaada anaotoa kwangu na timu kwa ujumla....kamwe siwezi kumsema vibaya.

Na huwa analiongelea hili kwa kutuambia .. "Soka ni mchezo rahisi" .. Na ndiyo maana nami nafanya mambo kadhaa kuonekana rahisi.... siwezi kuukata mkono unaonilisha eti kisa vyombo vya habari, najifunza mengi kutoka kwa huyu mkongwe.

"Tulisawazisha ikawa 1-1 katika mchezo wa Kombe la Dunia, kisha 2-2, na baadaye 3-3 ,, lakini yeye yuko mbele kwa kila kitu,, kazi yangu ni kumsikiliza hata iweje....." alimaliza Mbape.

Wednesday, December 21, 2022

#Updates ZA MKUTANO LEO YANGA.


💥Rais wa Young Africans SC Eng.Hersi Ally Said leo amekabidhiwa rasmi ofisi na Uongozi uliopita chini ya Mwenyekiti Dkt. Mshindo Msolla baada ya zoezi la ukaguzi wa hesabu za Klabu kukamilika.


-💥Kwenye dirisha hili dogo Yanga tutafanya usajili wa wachezaji wawili pekee wa kimataifa.


-💥Tumepokea maombi mengi ya wachezaji wetu kutakiwa kwa mikopo Kutoka Kwenye vilabu vya hapahapa Tanzania.Bado hatujafanya maamuzi ila sisi Kama Viongozi tutakaa na kocha Nabi kuona Kama tutaweza kuwaruhusu kwenda sehemu nyingine ili wapate muda mwingi wa kucheza.


-💥Maandalizi kwa ajili ya michezo ya kimataifa tumeshaanza tumekipanga,,tuna nia ya dhati kabisa kufika mbali sisi Kama Yanga.


-💥Chini ya Uongozi wangu na watendaji wenzangu tutakwenda kukamilisha mambo yote ambayo tuliwaahidi wananchama wetu na mashabiki wetu ambayo tutakwenda kufanya ndani ya Yanga.


-💥Bado zoezi la usajili wa wanachama pamoja na mashabiki Kwenye mfumo mpya wa mabadiliko unaendelea niwaombe Wananchi waendelee kujiandiki

WAZIRI NDAKI ASEMA MABORESHO YA MWONGOZO WA UWEKEJI HERENI YATAMFIKIA KILA MDAU

 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.  Mashimba Ndaki  akizungumza (20.12.2022) wakati akifunga mkutano wa Wadau wa sekta ya Mifugo uliofanyika kwa siku mbili kwenye jengo la PSSSF, Makole jijini Dodoma


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda akifafanua moja ya maazimio yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa wadau wa sekta ya Mifugo uliofanyika Disemba 19-20, 2022 kwenye jengo la PSSSF Makole, jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Mbaraka Stambuli akisoma maazimio yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa wadau wa sekta ya Mifugo uliofanyika Disemba 19-20, 2022 kwenye jengo la PSSSF Makole, jijini Dodoma.



Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.  Mashimba Ndaki amebainisha kuwa Wizara yake inaendelea kufanya maboresho ya Mwongozo unaosimamia zoezi la uwekaji wa hereni za kielektroniki kwenye mifugo ili kufanya zoezi hilo kuwa shirikishi kwa pande zote zinazohusiana na sekta ya ufugaji.

Mhe. Ndaki ameyasema hayo jana (20.12.2022) wakati akifunga mkutano wa Wadau wa sekta ya Mifugo uliofanyika kwa siku mbili kwenye jengo la PSSSF, Makole jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa kuboresha mwongozo huo utakabidhiwa kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu ili atoe hatma ya zoezi hilo.

“Kwenye maboresho ya mwongozo huu tutamfikia kila mdau anayehusika na sekta ya mifugo kwa nafasi yake ili baada ya kukamilika kwake kusiwe na malalamiko ya baadhi ya wadau kutoshirikishwa” Amesisitiza Mhe. Ndaki.

Mhe. Ndaki ametoa rai kwa wafugaji wote walioshiriki kwenye mkutano huo kuwafikishia wafugaji wenzao elimu waliyoipata kupitia mada mbalimbali zilizowasilishwa wakati wote wa mkutano huo ili waweze kutekeleza kwa pamoja maazimio yaliyofikiwa.

“Ni lazima wote kwa pamoja tuelewe sekta ya Mifugo inapaswa kwenda kwenye mwelekeo mpya, hatuwezi kuwa walewale kwa sababu tunalazimishwa kubadilika sasa hivi kwa namna yoyote ile kutokana na mazingira tuliyopo, mabadiliko ya tabia nchi na ongezeko la watu” Amesema Mhe. Ndaki.

Akizungumzia kuhusu marufuku ya uingizwaji wa vifaranga vya kuku kutoka nje, Mhe. Ndaki amesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo ili kuwalinda wawekezaji na wafanyaiashara wa ndani ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan zinazolenga kuongeza idadi ya wawekezaji nchini.

“Lakini natoa rai kweu mhakikishe mnaboresha mazao yenu ili yawe shindani kwenye masoko ya ndani na nje kwa sababu hivi sasa tupo kwenye ushirikiano wa Afrika Mashariki na hivi karibuni tutaingia kwenye sarafu moja hivyo ni lazima mjipange” Ameongeza Mhe. Ndaki.

Akizungumzia ubora wa nyama inayozalishwa hapa nchini na namna inavyokubalika katika masoko ya nje, Mkurugenzi wa Kiwanda cha kusindika nyama cha Eliya kilichopo mkoani Arusha Bw. Irfhan Virjee amesema kuwa kwa sasa nyama inayozalishwa hapa nchini na kusafirishwa kwenye masoko ya nje ina ubora na kuhitajika hasa kwenye soko la nchi za falme za kiarabu  kiasi cha kushindwa kukidhi mahitaji ya soko hilo.

Naye Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la kimataifa la Heifer ambao ni moja wa wadau wakubwa kwenye sekta ya Mifugo nchini Bw. Mark Tsoxo amesema kuwa ili kufanikisha  mwelekeo mpya wa sekta ya Mifugo ni lazima Serikali na wadau wote kufanya mabadiliko ya teknolojia na mifumo inayoratibu sekta hiyo.  

“Jambo jingine ni muhimu kuhakikisha kwenye mwelekeo huu mpya wa sekta ya Mifugo tunawajumuisha kwa kiasi kikubwa vijana ambao wanakadiriwa kufikia asilimia 31 ya idadi ya watu wote nchini  na wanawake ambao ni asilimia 51 ya idadi ya watu wote waliopo nchini, kinyume na hapo tutatengeneza changamoto kubwa wakati tukitekeleza mwelekeo huu” Amesisitiza Bw. Tsoxo.

Mkutano huo wa wadau wa sekta ya Mifugo ulifunguliwa Disemba 19 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambapo wadau mbalimbali walioshiriki mkutano huo walifanikiwa kutoa maoni mbalimbali yaliyolenga kutekeleza kauli mbiu ya Mkutano huo ya “ Mwelekeo Mpya wa Sekta ya Mifugo nchini 

TIMU YA UFARANSA YAKARIBISHWA NYUMBANI KISHUJAA LICHA YA KUPOTEZA KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa ya soka ya Ufaransa imewasili nyumbani kutoka Qatar salama salmini na kupokelewa na umati mkubwa wa watu jijini Paris kwa mbwembwe. 

Kikosi hicho kilikumbatiwa kwa shangwe na nderemo Jumatatu, Disemba 19, baada ya kushindwa na Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia Jumapili, Disemba 18. 

Deschamps na Hugo Lloris waliongoza timu hiyo wakifuatwa na fowadi pilipili Kylian Mbappé ambaye alifungia Ufaransa hat-trick katika fainali ambayo ilikuwa kubwa zaidi katika historia ya michuano hiyo. 

Kisha wachezaji wengine walifuata wakiwa wamevalia tabasamu la ujasiri kuonyesha shukrani kwa maelfu waliojitokeza kuwapokea. 

 Licha ya kupoteza Kombe la Dunia, takriban mashabiki 50,000 walikusanyika katika Place de la Concorde ili kuwapa wachezaji wao makaribisho ya kifalme wakiachia fataki. 

Hata hivyo, Mbappe alionekana kutojali na kununa baada ya kushuka kutoka kwenye ndege.

 Alionekana kukasirika na kukata tamaa katika muda wote baada ya kukamilika kwa michuano hiyo ya kimataifa. 

Meneja wake pia alionekana kumsaidia kuinua mkono wake ili kuwapungia mashabiki waliokuwa wakimsifu. 

Makovu ya kushindwa Jumapili, yalikuwa bado hayajamtoka nyota huyo wa klabu ya PSG. Mbappe, ambaye alikua mchezaji wa kwanza baada ya Geoff Hurst kufunga hat-trick 1966, kwenye fainali ya Kombe la Dunia, ameapa kuwaa Ufaransa 'itarejea' tena. Juhudi zake, za kimiujiza kama zilivyokuwa, hazikutosha kusaidia upande wake kutetea taji lao. 

Ufaransa ilisawazisha mara mbili katika fainali iliyomalizika kwa mabao 3-3, kabla ya Argentina kushinda kwa mikwaju ya penati 4-2. 

 Kuwasili kwao nyumbani kunajiri huku Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikosolewa vikali kwa kuwafariji wachezaji baada ya kupoteza Kombe la Dunia. 

Vyombo vya habari vya Ufaransa vilimkosoa mwanasiasa huyo namna alivyojaribu kumfariji Mbappe alipokuwa akibubujikwa na machozi katika uwanja wa Lusail Stadium. 

Wakati huo huo, huku hatma ya kocha Deschamps ikiwa inayumba na kandarasi yake ikikaribia kumalizika, inaripotiwa kwamba anataka kufanya mazungumzo ya mkataba wake kurefushwa ili kusalia kuinoa timu ya Ufaransa kwa michuano ijayo ya Kombe la Dunia.

Tuesday, December 20, 2022

CHRISTMAS HII MWANZA TUKUTANA HAPA.

 Siyo suala la kupepesa macho............

Monday, December 19, 2022

PASTA APIGWA MAWE MPAKA KUFA BAADA YA KUPATIKANA ENEO LA MAUAJI.


Mhubiri mmoja kutoka nchini Uganda alikumbana na mauti yake mikononi mwa wanakijiji waliokuwa na hasira baada ya kupatikana karibu na eneo la mauaji.

 Pasta Julius Mugisa anasemekana alikuwa katika kundi la wauaji waliompiga risasi mtu mmoja na kumuua. 

 Inaripotiwa kuwa Mchungaji Julius Mugisa alikuwa miongoni mwa genge lililomuua Tobias Komunda nyumbani kwake katika kijiji cha Igogonya mnamo Ijumaa, Desemba 16. 

Washukiwa hao walikuwa wamesafiri hadi nyumbani kwa mwathiriwa wakitumia gari ambalo bado nambari lake la usajili haijajulikani. “Inadaiwa genge la watu watano wasiojulikana waliokuwa wakisafiri na gari jeupe na namba ya usajili ambayo haijajulikana, walikwenda nyumbani kwa marehemu (Komunda) mwendo wa saa kumi na moja jioni. 

Wote walienda nyuma ya nyumba ya Komunda ambapo walitumia takribani dakika 30." 

"Walianza kutofautiana kabla ya Komunda kuwaambia waondoke nyumbani kwake. Yeye (Komunda) alijaribu kuwapiga kwa jiwe lakini alipigwa risasi ya kichwa na kufa,” mtu aliyeshuhudia aliwaambia polisi. 

Chanzo cha mzozo huo bado hakijajulikana, kama Daily Monitor inavyoripoti. Baada ya mauaji hayo, washukiwa hao walitoroka katika eneo la tukio wakitumia gari na kumwacha Mugisa. Jitihada zake za kuhepa kama wenzake ziliambulia patupu baada ya wakazi wa waliokuwa na hasira kumpata na kumvamia. 

“Mchungaji alikimbia kutoka eneo la tukio lakini tayari alikuwa ametambuliwa na wakazi waliokuwa wakijibu milio ya risasi. 

Alishambuliwa na kupigwa na umati mkubwa wa wakazi wenye hasira ambao waliwazidi nguvu maafisa wa polisi wa eneo hilo waliojaribu kumwokoa,” mtu mwingine aliyeshuhudia alisema. 

Majambazi wamuua polisi Kwingineko, undi la Wakristu waliokuwa wamekusanyika kusali katika eneo la Diepsloot, Afrika Kusini waligeuka kuwa waathiriwa wa wizi wa kimabavu baada ya majambazi kuwavamia na kumuua pasta wao. 

Ripoti zinaonyesha kuwa Wakristu 50 walikuwa wamekusanyika katika kanisa lao kwa ajili ya maombi na kukesha wakati majambazi hao wenye silaha walipowashambuli.

NEYMAR AMPONGEZA MESSI NA KUMKAUSHIA MBAPPE BAADA YA ARGENTINA KUSHINDA KOMBE LA DUNIA.


Neymar katika ujumbe mfupi kwenye mitandao ya kijamii, alimpongeza Lionel Messi kufuatia ushindi wake wa Kombe la Dunia nchini Qatar.

Messi aliongoza Argentina kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1986 kupitia mikwaju kali ya penalti dhidi ya Ufaransa. Ilikuwa ni mechi babu kubwa ambayo iliwakutanisha mafowadi nyota wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe na Messi ambao walionyesha umahiri wao kwenye fani y soka. 

Messi alifunga mabao mawili huku Mbappe akidaka hattrick na kulazimisha mchezo kwenda kwa mikwaju ya penalti ambapo Emi Martinez alifunga bao moja kwa kuokoa. 

Ujumbe wa Neymar kwa Messi Neymar alimpongeza Messi kwa ujumbe mfupi wa 'Hongera Kaka.' Lakini mashabiki walikuwa wepesi kugundua kwamba hakuandika ujumbe wa kumfariji Mbappe ambaye licha ya umahiri wake wa kufungamabo alishindwa kutetea taji lao usiku huo. 

Inakumbukwa kuwa Neymar na Mbappe walikuwa na vita vya ubabe vilivyoripotiwa jijini Paris mwanzoni mwa msimu. 

Nyota hao wawili walisemekana kuwa na kinyongo huku Mbappe akiripotiwa akishinikiza kuuzwa kwa Neymar Timu ya Brazil ya Neymar, iliondolewa kwenye Kombe la Dunia katika hatua ya robo fainali na Croatia licha ya kuwa moja ya timu zilizokuwa zinapigiwa upatu kushinda taji hilo. Iwapo wangeliishinda Croatia, Neymar angelimwenyana na Messi katika nusu fainali. 

Nyota hao watatu sasa wanatarajiwa kurejea Paris hivi karibuni wakati miamba hao wa Ufaransa wakiendelea na harakati zao za kuwania taji la kwanza kabisa la Ligi ya Mabingwa. 

Paris Saint-Germain sasa wanajivunia kuwa na mshindi wa Kombe la Dunia na mshindi wa pili wa Kombe la Dunia katika kikosi chao.

Sunday, December 18, 2022

KUMBE MAYELE ALITINGIA NA SIMU UWANJANI AKICHEZA DHIDI YA POLISI

 Yanga 3-0 Polisi Tanzania | Highlights | NBC Premier League 17/12/2022

Yanga imetumia kipindi cha pili kufunga magoli matatu ikiipa kichapo cha 3-0 Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Dimba la Benjamin Mkapa. Wafungaji wa mabao hayo ni Jesus Moloko dakika ya 47, Fiston Mayele dakika ya 77 na Clement Mzize dakika ya 86. Katika mchezo huu pia, Polisi Tanzania walipata pigo kwa mshambuliaji wao Ambrose Awio kutolewa kwa kadi nyekundu kufutia kadi ya pili ya njano.