ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 30, 2016

JIMBO LA CHATO LACHANGIWA NA WADAU WA MAENDELEO JIJINI MWANZA SH MILIONI 305.7 ZA KUTENGENEZEA MADAWATI



















NA:- PETER FABIAN MWANZA
MBUNGE wa Jimbo la Chato, Dk Medard Karemani achangisha na kufanikiwa kukusanya kiasi cha Sh milioni 305.7 kwa ajili ya kusaidia utegenezaji wa upungufu wa madawati 10,000 yanayotakiwa katika shule za msingi 131na sekondari 28 jimboni humo.
Dk Karamani alisema kwamba hali ya wanafunzi kukaa chini katika jimbo la Chato linatokana na tamko la serikali la Elimu kutolewa bure na kusababisha wanafunzi walioandikishwa kuingia shuleni kuongezeka kwa aslimia 150 jambo ambalo limeleta mahitaji ya madawati 28,000 .
“Tulihamasisha wananchi na wadau wengine kuchangia na kufanikisha kutengeneza madawati 18,000 hivyo tunahitaji kutengeneza madawati 10,000 ili kukabiliana na changamoto hiyo wanafunzi 100,000 wanaosoma kuweza kukaa kwenye madawati wakati wa kusoma madarasani,”Alisema.
Mgeni rasmi katika harambee hiyo iliyofanyika juzi jijini Mwanza, Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Wasanii, Nape Moses Nnauye, alisema kwamba ni wajibu wa Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Wilaya kushirikiana kuhamasisha wananchi kujitokeza kuiunga mkono kuchangia maendeleo.
“Rais Dk John Magufuli alisitisha michango yenye kero kwa wananchi lakini wananchi wanaweza kushiriki kuchangia kwa hiali miradi ya maendeleo iliyopo katika maeneo yao kwa kushirikiana na serikali, hivyo viongozi na wawakirishi wa wananchi tunao wajibu wa kuwahamasisha ili kutekeleza kwa ufanisi miradi na kupata huduma zinazositahili,”alisema.
Nnauye alisema kwamba suala la madawati linahitaji kuwepo msukumo wa kuwaelimisha wananchi kuchangia madawati pamoja na kuwashirikisha wadau mbalimbali ndani ya wilaya, mkoa na nje ya mikoa ili kufikia malengo yanayotokana na changamoto hiyo ambapo binafsi naunga mkono kwa mchango wa Sh milioni nne huku baadhi ya marafiki wakiwa nao wanachangia .
Katika harambe hiyo Kampuni ya Busolwa mine ya Mkoani  Geita ilichangia madawati 1,000, Saimon Group madwati 1,000,  Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM taifa (NEC) Christopher Gachuma madawati 300,  Dk Karamani Sh milioni 4, Kampuni ya Waja dawati 500, baadhi ya Wabunge wa Kanda ya Ziwa walioalikwa kila mmoja milioni moja huku baadhi ya Kampuni za wachimbaji wadogo wa madini wakichangi.

Waziri Nnauye akitangaza matokeo ya michango ya fedha zilizopatikana katika harambe hiyo ya kuchangia madawati katika jimbo la Chato yaliyoratibiwa na Dk Karemani alisema kwamba waalikwa wakiwemo wadau na wa Wilaya ya Chato na kutoka maeneo mbalimbali nchini kuunga mkono na kupatika fedha taslimu Sh milioni 120.

Alieleza wachangiaji kuwa zingine ni ahadi na jumla kuu ya michango yote kufikia kiasi cha Sh 305,721,500/=. Ambazo zitaendelea kutekeleza ukamilishwaji wa madawati katika Jimbo lote la Chato na kutoa wito wadau kuendelea kuhamasika kuchangia pindi wakifuatwa tena na kukamilisha ahadi zao kwa kipindi kifupi ili kukamilisha zoezi hilo ifikapo Agusti 30 

KAKA WA RAIS MAGUFULI AFARIKI

KAKA wa Rais Dk. John Magufuli, Anthon Lubambagwe, amefariki dunia kutokana na maradhi ya kifua.
Taarifa ya kufariki kwa Lubambagwe ilitolewa jana na msemaji wa familia, Nebart Mlambi, aliyeeleza kuwa marehemu huyo alifariki saa 8:30 mchana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure, jijini Mwanza alipokuwa amelazwa akitibiwa.

Mlambi alisema marehemu Antony ni mtoto wa Helman Gwape Lubambagwe ambaye ni baba mkubwa na Rais Magufuli.

“Mzee alianza kuugua Aprili mwaka huu na kutibiwa katika Kituo cha Afya cha Igoma, akapata nafuu lakini alizidiwa tena Julai 27, mwaka huu tukampeleka Hospitali ya Sekou Toure.

“Alipokelewa pale lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya wakamhamishia chumba cha wagonjwa mahututi ambako alifariki,” alisema Mlambi.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Rais Magufuli zimeeleza kuwa marehemu Anthon ndiye aliyempokea Rais Magufuli na kuishi naye wakati akianza masomo katika Shule ya Sekondari ya Lake jijini Mwanza.

Wakati Rais Magufuli akijiunga na Shule ya Sekondari ya Lake, marehemu alikuwa akiishi Mtaa wa Majembe Makali uliopo Kata ya Igogo na baadaye alihamia Mtaa wa Kishiri akiwa pamoja na Rais Magufuli.

Aidha, mtoto mkubwa wa marehemu huyo, Masumbuko Anthon (30), alisema maziko ya baba yake yatafanyika leo (Jumamosi) katika makaburi ya familia yaliyopo Igelegele, Kata ya Mahina, wilayani Nyamagana, ikitanguliwa na Ibada ya Misa itakayofanyika nyumbani kwake Kishiri, Kata Igoma ambako mwili wake utaagwa.

Marehemu ameacha mjane, Selina Masanja (60) na watoto saba ambao ni Masumbuko (30), Helman (34), Anna (28), Dotto (28), Paschal (26), Shija (22) na Mitimingi (12).

HUU NI UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO JULY 30, 2016.


Majengo ya serikali Dar kupigwa mnada, Dkt. Magufuli awakunjulia makucha CHADEMA, Sumaye asema CCM inaweweseka, Pata undani wa dondoo hizi hapa; 

Mpina akitoza faini kiwanda cha Dangote, JPM na CHADEMA jino kwa jino, Chirwa augawa uongozi Yanga, Dewji autega mkutano mkuu Simba, Pata dondoo hizi za magazeti ya leo hapa; 

RITA YAJA KUZIKAGUA TAASISI NA ASASI ZA KIJAMII MKOA WA MWANZA

Wakala wa Usajili Ufilisi naUdhamini (RITA) unapenda kuwatangazia wadhamini wote wa Taasisi na Asasi za kijamii Mkoani Mwanza kwamba kutakuwa na zoezi la kukagua na kuhakiki uhai na utekelezaji wa Majukumu ya taasisi hizo. 

 Zoezi hili litahusisha Watendaji wa RITA kupita katika Ofisi za Asasi na taasisi zao kama ilivyooneshwa katika Fomu za maombi ya usajili.

 RITA inawakumbusha wananchi kwamba ni lazima taasasi na Asasi yoyote ya kijamii inayomiliki mali kuwa chini ya Usimamizi wa Bodi ya Wadhamini ambayo nilazima isajiliwe kwa Mdhamini Mkuu (RITA) naitatakiwa kutekeleza majukumu yake kama ilivyoainishwa katika katiba na kufanya marejesho kila mwisho wa Mwaka. 

Taasisi zinazohusika ni pamoja na Misikiti, Makanisa, taasisi za kidini, Vyama vya Siasa, Klabu za Michezo, Shule na nyinginezo. 

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba 0719 017 217 

Tangazo hili Limetolewa na Emmy K. Hudson 
KAIMU MSIMAMIZI MKUU WA WADHAMINI

Friday, July 29, 2016

AIRTEL YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO VYA THAMANI YA MILIONI 200 KWA MAENDELEO YA SOKA LA VIJANA.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) Selestine Mwesigwa tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.
katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF)  Selestine Mwesigwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu wa chama cha soka cha Ilala Daud Kanuti tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.
katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF)  Selestine Mwesigwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa katibu wa chama cha soka cha Kinondoni Isack Mazwile tayari kwa msimu wa sita wa Airtel Rising Stars unaotarajiwa kuanza Jumamosi Julai 30.

Taarifa kwa Vyombo Vya Habari   
Airtel yakabidhi vifaa vya michezo vya thamani ya Milioni 200 kwa maendeleo ya soka la vijana.

Kampuni ya simu za mikononi Airel Tanzania leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu zikaoshiriki michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ngazi ya mkoa ambayo inatarajiwa kuanza Julai 30 mpaka Agosti 30 2016 kwenye mikoa tofauti hapa nchini.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni 200 vimekabidhiwa kwa Wasimamizi wa vituo vyote vya mikoa na Taifa. Vifaa hivyo hivyo ni pamoja na jezi za wachezaji, shin guards, soksi, jezi za marefa, mipira pamoja na glovu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Katimu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Celestine Mwesingwa alisema ‘ Kwa kutoa vifaa hivi vya michezo,mdhamini ametimiza moja kati ya majukumu yake na ni matarajio yangu kwamba mtarudi kwenye vituo vyenu na kuongeza bidii ya kutafuta vipaji vinavyoibuka vya mpira wa miguu’.

‘Tunatarajia kuona mechi zenye ushindani na za kuvutia na natoa wito kwa viongozi wa vyama vya mikoa kuwa makini wakati wa kuchangua timu kombaini ambazo zitakuja kucheza kwenye fainali za taifa ambazo zitafanyika Dar es Salaam tarehe 6 mpaka 11 Septemba mwaka huu.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema ‘Airtel Rising Stars inaungana pamoja na promosheni yetu ya Airtel Fursa ambayo ilizinduliwa mwaka jana ikiwa na lengo la kuwasaidia vijana kukuza vipaji vyao. Kwa mwaka, michuano hii inatoa fursa nyingine kwa wavulana pamoja na wasichana kutambua uwezo wao wa kucheza soka na kuweza kufanikisha ndoto zao. Kwa mantiki hiyo, Airtel Tanzania inatumia program hii kuwezesha vijana wenye vipaji vya mpira wa miguu kuvionyesha kwa makocha na hatimaye kufakinisha ndoto zao’.

Airtel Rising Stars ni mpango kabambambe kwa Afrika nzima yenye lengo ya kutoa nafasi kwa vijana kuonyesha vipaji vyao mbele ya makocha, na hatimaye kupata fursa ya kuviendeleza na kuvikuza.

ERIC OMONDI KUVUNJA MBAVU ZA WAKAZI WA MWANZA HII LEO.

Mchekeshaji maarufu Afrika Mashariki Eric Omondi kulia akiwa na mwanahabari wa Jembe Fm G.Sengo mapema leo katika kipindi cha 'Kazi na Ngoma' . Eric Omondi anatarajiwa kufanya tumbuizo la kiburudani usiku waleo ndani ya jiji la Mwanza katika ukumbi wa Nyerere Hotel Gold Crest. Kiingilio ni shilingi 50,000/=.
Na Mansour Jumanne.
Bango na mpango mzima.
Kwa hewa.

CLINTON: TRUMP HAWEZI KUTATUA MATATIZO MAREKANI.

Hillary Clinton amekubali rasmi kuwa mgombezi wa Urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, huku akisema wakati wa kupambana na mpinzani wake sasa umeanza rasmi.
Alitoa wito kwa wanachama wote wa Democratic kuungana naye huku akimkebehi mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump, katika madai yake kuwa ni yeye pekee anayeweza kuyasuluhisha matatizo ya Marekani.
Alisema kuwa Wamarekani hufanya kazi kwa pamoja kyatatua yote yanayonufaisha taifa.
Awali, bintiye Chelsea Clinton alikuwa ametoa hotuba na kumsifu sana mamake. Alisema ni mwanamke ambaye huwa hasahau anawapigania akina nani.
"Watu huniuliza kila wakati, huwa anawezaje kufanya haya? ... ni kwa sababu huwa hawasahau watu anaowatetea," amesema.
"Najua kwa moyo wangu wote kwamba mamangu atatufanya tujionee fahari."

Thursday, July 28, 2016

Dk. KIGWANGALLA AKUTANA NA WAKUU WA IDARA ZA MAENDELEO YA JAMII, WATOTO ATOA MAAGIZO

DSC_3248
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akipitia madokezo mbalimbali ya Idara za Wizara hiyo muda mfupi kabla ya kukutana na Wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na ile Idara ya Watoto.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amekutana na Wakuu wa Idara za Maenedeleo ya Jamii pamoja na ile ya Watoto katika Wizara hiyo na kupanga mikakati mbalimbali ya kiutendaji kazi.

Katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla amewataka wakuu hao wa Idara kuhakikisha wanaandaa mpango kazi kabambe ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi ndani ya Wizara hiyo ikiwemo kutoa maagizo maafisa Maendeleo ya na Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanatoka maofisini na kwenda ngazi ya chini kufanya kazi hasa Vijijini.
DSC_3279
Pia katika kukabiliana na suala la mmong’onyoko wa maadili hasa suala la vitendo vya watu kujihusisha na mapenzi ya Jinsia moja, amebainisha kuwa mikakati hiyo kwa sasa wataanzia ngazi ya chini katikakuhakikisha wanadhibiti vitendo hivyo.

“Tunataka kuhakikisha vitendo vya unyanyasi na ukatili hasa vile vinavyoanzia mashuleni tunavikomesha mara moja. Imebainika zipo baadhi ya shule watoto wanafanya vitendo visivyo fa ambavyo pia baadae vinapelekea tabia hii ya ushoga.

Hivyo miongoni mwa mikakati ni kuhakikisha tunaandaa masunduku ya maoni kwa kila shule ili kubaini vitendo hivi na vingine visivyofaa kwa Wanafunzi ambavyo vinapelekea mmong’onyoko wa maadili.” Alieleza Dk. Kigwangalla.

DSC_3261
Afisa wa Idara ya Watoto, Emmanuel Batoni akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (Hayupo pichani) wakati wa tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo.
Dk. Kigwangalla amekutana na wakuu hao ni katika mikakati ya kuhakikisha anasimamia ipasavyo majukumu ya Idara hizo ambazo zinaunda Wizara hiyo.
DSC_3275
Mkutaano huo wa Naibu Waziri na Wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na ile ya Watoto ukiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla 
DSC_3288
Sehemu ya Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla
DSC_3281
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoaa maagizo kwa Wakuu wa Idara mbalimbali wa Wizara hiyo.(Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog).

AKUTWA AMEKUFA ZIWANI BAADA YA KUPOTEA KWA MUDA WA SIKU 3 MWANZA.

Raia mmoja aliyetambulika kwa jina la Silas ambaye ni mkazi wa Sengerema mkoani Mwanza ameokotwa ziwani leo baada ya kupotea kwa muda wa siku tatu.

Marehemu Silas amepatikana kando mwa Ziwa Victoria katika Mwalo wa Kamanga wilaya ya Nyamagana Mwanza mjini  ambapo mpaka sasa chanzo cha kifo chake hakija fahamika.

Hali aliyokutwa nayo marehemu:- Amekutwa kifua wazi (hana shati) bali suruali pekee na viatu mfukoni akiwa na Simu na Pesa.

PAPA FRANCIS AMEANHGUKA GHAFLA WAKATI AKIENDELEA NA MISA HUKO POLAND.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameanguka gafla wakati akiendelea na misa huko nchini Poland baada ya kujisikia vibaya.

SPEED YA KUFA MTU NYUMBA ZA WATUMISHI WA SERIKALI KUKAMILIKA IFIKAPO MWEZI SEPTEMBA.

SIMU.TV: Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa, amemuagiza wakala wa majengo nchini TBA kuhakikisha anakamilisha majengo yote ya watumishi wa serikali ifikapo Septemba.

NGOMA MPYA 'ADO ADO' - MO MUSIC

Hello pipo huu ndo wimbo mpya wa Mo-Music uliotoka rasmi hii leo tarehe 28 July 2016.


Umetayarishwa na Deey Classic  Hight Table Sound
Pata nafasi kuusikiliza.
Asantee...

UZEMBE NA UDANGANYIFU WAWATIMUA WATUMISHI ZAIDI YA 50 WA JIJI LA ARUSHA.

Watumishi zaidi ya 50 wa halmashauri ya jiji la Arusha wamechukuliwa hatua za awali na huenda wakafukuzwa kazi kutokana na uzembe na udanganyifu ukiwemo wa kutoa taarifa za uongo za utekeezaji wa miradi.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa jiji la Arusha Bw Athumani Juma Mhamia amesema tatizo ni kubwa zaidi kwa watendaji wa idara ya fedha na mipango miji na idara ya usafi.

Aidha Bw Mhamia amesema pia halmashauri hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la mtandao wa kuuza kujenga maeneo ya wazi na amewataka wote wanaojijua kuwa wanahusika kujisalimisha kwani hakuna atakayepona.

Kuhusu tatizo la kukithiri kwa uchafu meya wa jiji la Arusha Bw. Kalst  Lazaro amesema tatizo kubwa ni ukosefu wa vitendea kazi na kwamba  halmashauri imenunua magari sita ya kuzolea taka ambayo yanatarajiwa  kupunguza tatizo hilo kwa kiasi kikubwa.

HUAWEI WAJA NA MAONYESHO YA SIMU ZA MKONONI.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Huawei Afrika Kusini, Ian Ellis akizungumza na Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali walipotembelea Kontena maalumu kujifunza mambo ya Sayansi Tekinolojia wakati wa maonyesho ya nne ya wadau wa Simu za mkononi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Huawei Afrika Kusini, Ian Ellis akizungumza na Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali walipotembelea Kontena maalumu kujifunza mambo ya Sayansi Tekinolojia wakati wa maonyesho ya nne ya wadau wa Simu za mkononi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Huawei Afrika Kusini, Ian Ellis akizungumza na Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali walipotembelea Kontena maalumu kujifunza mambo ya Sayansi Tekinolojia wakati wa maonyesho ya nne ya wadau wa Simu za mkononi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Huawei Afrika Kusini, Jeo Zhao akizungumza na Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali walipotembelea Kontena maalumu kujifunza mambo ya Tekinolojia katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

MZUNGU WA ZAMANI WA SIMBA SASA ANAINOA AFRICAN LION ILIYOPANDA LIGI KUU MSIMU HUU.

Kocha wa zamani wa Simba Dragan Popadic ameendelea kukinoa kikosi cha timu ya African Lion ambayo imepanda katika ligi kuu ya Tanzania bara.

MRADI WA HARAMBEE NI MKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHOLE, MAFIA - PWANI

Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha Chole ikiwa ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta mkanganyiko hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya kale kinyume cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile linachafua sura ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. --

- Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog - CHOLE, MAFIA. Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia - Pwani wameusifia mradi wa Harambee unaowapatia elimu watoto wao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog iliyoweka kambi kijijini hapo kujionea hali halisi ya kisiwa hicho, wananchi hao walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi wa wanachi kwa vile ni mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao amekuwepo mwekezaji kijijini hapo.

 Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman alisema mpaka sasa zaidi ya Sh. milioni 500 zimetumika kugharimia ada na mahitaji muhimu ya wanafunzi shuleni wa kijiji cha Chole, kupitia mradi huo. Aliongeza kuwa pesa hiyo imeweza kuwafikia jumla ya wanafunzi wapatao 300.
Mwenyekiti mstaafu wa kijiji cha Chole (kulia) ambaye alianza kazi yake 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. Pembeni ni mwenyekiti wa sasa Shehari Ahmadi. Mkazi wa kijiji cha Chole, Bi. Riziki Hassan Selenge ambaye anasomeshewa watoto wake wawili na Mfuko wa maendeleo wa Harambee.  Mkazi wa Chole, Bw. Johari Rajabu Fadhil ambaye ndiye mmoja ya waasisi waliompokea mwekezaji, na aliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma masomo ya kufundisha watoto ya miaka 2.
 Mkazi wa kwanza wa kijiji cha Chole wilayani Mafia kijiji cha Chole Mjini kupata digrii ya chuo kikuu, Zubeda Bhai akiwaelezea waandishi wa habari abato Kasika na Florence Mugarula waliotembelea eneo hilo la kihistoria jinsi ambavyo taasisi ya Chole Mjini Conservation and Development ilivyomsaidia gharama zote za kupata elimu ya juu. --- Alisema kuwa miaka ya nyuma wakazi wa Chole hawakuwa na mwamko wa elimu, lakini baadaye wakapata mwekezaji ambaye amechangia shughuli mbalimbali za maendeleo na kuwafanya wakazi wa kisiwa hicho kuwa nma mwamko wa elimu. "Tuna mwekezaji ambaye ni kampuni ya Chole Conservation & Development inayosimamia na kutunza magofu ya Kijerumani, ametusaidia sana kutuamsha na sasa hapa Chole kuna mwamko mkubwa wa elimu," alisema Kingi. Alisema kuwa mwekezaji huyo aliwahamasisha kuanzia kamati hiyo ndipo ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba ukaanza kuongezeka kuanzia mwaka 2007 na umekuwa ukizidi kupanda kadri miaka inavyokwenda.
 Wanafunzi wa Chekechea wakifundishwa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari wanaonufaika na mfuko wa maendeleo wa Harambee. wakiwa pamoja na mkurugenzi wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development Bi. Anne K. de Villiers.
Moja ya usafiri wa boti unaotumika kuwavusha wakazi wa Chole kwenda Mafia Mjini.
Wageni waliofika kutembelea kisiwa cha Chole kujionea majumba ya kizamani yenye histori za mababu zetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee, Hamis Musa Athuman akielezea maendeleo ya kijiji cha Chole katika upande wa elimu akiwa na  katibu wa kamati hiyo Mohamed Kingi (kulia).
Shule ya msingi ya Chole iliyojengwa na Mwekezaji wa Kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development. Majengo ya kale yanayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development yakionekana katika sura nzuri ya utunzaji wa hali ya juu. Mkazi wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia mkoani Pwani, Faharani Shomari, akiwaonyesha picha ya magofu ya kihistoria yalivyokuwa yameharibika na yalivyo sasa baada ya kufanyiwa ukarabati na kampuni ya Chole Mjini Conservation & Development wakati waandishi hao walipoenda kutembelea eneo hilo. 
Picha zikionyesha jinsi majengo ya kale yalivyoonekana kabla hayajakarabatiwa na kufanyiwa usafi.
Katibu wa Harambee wa Kijiji Cha Chole Mjini kilichopo Mafia Mkoa wa Pwani, Mohammed Kingi akiwafundisha wanafunzi wa Shule ya Msingi Chole. Shule hiyo pamoja na masomo hayo yanafadhiliwa na kampuni ya Chole Conservation and Development
Kituo cha elimu ya watu wazima, hapa ndipo hujifunza kingereza. --- Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Chole Mjini Conservation, Development, Anne K. de Villiers, alisema kuwa wafadhili wa Kamati ya Harambee wako nchini Uingereza. 

 Alisema kuwa aliwatafuta baada ya kubaini kwamba wakazi wa kijiji hicho hawana mwamko wa elimu na wamekuwa wakifadhili hata ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa nyumba za walimu na mambo mengine ya muhimu kwa ajili ya elimu. 

 "Mbali na hilo kwa sasa tuna shule ya chekechea, kituo cha wanawake cha kujufunza kusoma, kituo cha kujifunza kompyuta na kituo cha wanafunzi na watu wengine kujifunza lugha ya Kiingereza na maktaba," alisema mkurugenzi huyo na kuendelea: Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmad alisema kuwa serikali imekuwa ikifaidika kwa kupata dola 10 kwa kila mgeni anayeingia na kulala katika hoteli ya Chole mjini inayosimamiwa na kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development sambamba na dola 5 kwa kila mgeni anayetembelea majengo ya kale ya mapango ya Chole ambayo yakikuwa yakitumika katika biashara ya watumwa. 

 Nae Bi. Riziki Hassan Selenge alisema kuwa hapo mwanzo mambo yalikuwa magumu tokea kuingia kwa mwekezaji huyo ndiye amekuwa mwasisi wa maendeleo kijijini kwao kwa vile asilimia 99 wakazi wa Chole hali zao ni masikini na hawakuweza kupeleka shule watoto wao. 

 Upande wake Mwenyekiti mstaafu, 1999 - 2014, Bw. Maburuki Sadiki aliishukuru kampuni ya Chole Mjini Conservation and Development kwa kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kuwajengea shule ya msingi, Zahanati, shule ya ChekeChea, Darasa la watu wazima kujifunza kingereza, watoto kwenda sekondari na mengine mengi. 

 Akitoa historia fupi Bw. Sadiki alisema mchakato wa kumpokea mwekezaji huyo ulifanyika Desemba 4, 1993 kwa kueleza dhamila yake na tulimkubalia kwa kufuata sheria zote na makubaliano tuliwekeana nae tokea kipindi hicho ambapo tokea ameingia mwekezaji huyo amekuwa akitekeleza mkataba aliyopewa na kijiji.