Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa jiji la Arusha Bw Athumani Juma Mhamia amesema tatizo ni kubwa zaidi kwa watendaji wa idara ya fedha na mipango miji na idara ya usafi.
Aidha Bw Mhamia amesema pia halmashauri hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la mtandao wa kuuza kujenga maeneo ya wazi na amewataka wote wanaojijua kuwa wanahusika kujisalimisha kwani hakuna atakayepona.
Kuhusu tatizo la kukithiri kwa uchafu meya wa jiji la Arusha Bw. Kalst Lazaro amesema tatizo kubwa ni ukosefu wa vitendea kazi na kwamba halmashauri imenunua magari sita ya kuzolea taka ambayo yanatarajiwa kupunguza tatizo hilo kwa kiasi kikubwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.