Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella (kulia) akizungumza na viongozi
kutoka
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) walipomtembelea Ofisini
kwake jijini Mwanza. Viongozi hao walikuwa kwenye ziara rasmi ya
kukabidhiwa jengo litakalotumiaka kama Ofisi ya TADB Kanda ya Ziwa.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa
TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (wapili kushoto).
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akizungumza na
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella (hayupo pichani) wakati wa ziara
rasmi ya kukabidhiwa jengo litakalotumiaka kama Ofisi ya TADB Kanda ya
Ziwa.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella (mwenye kofia) akifuatana na
Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyevaa) kuelekea kwenye
makabidhiano ya jengo litakalotumiaka kama Ofisi ya TADB Kanda ya Ziwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (mbele kulia) akipokea funguo
za kukabidhiwa jengo litakalotumiaka kama Ofisi ya TADB Kanda ya Ziwa
kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Majengo ya Serikali mkoa wa
Mwanza, Mhandisi Yohana Mashausi (kushoto). Wanaoshuhudia ni Mkuu wa
mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella (mwenye kofia) na Mkurugenzi wa
Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha
(kulia).
Kanda ya Ziwa kuneemeka na Mikopo ya TADB
Na Mwandishi wetu,
Katika
kutimiza ahadi ya Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria
kuwaneemesha wakulima wa Kanda ya Ziwa kwa kufungua Ofisi ya Kwanza ya
Kanda yenye lengo la kuwapatia mikopo yenye gharama nafuu wakulima wa
Kanda ya Ziwa.
Akizungumza
wakati wa makadhiano ya jengo litakalotumika kama Ofisi ya TADB Kanda ya
Ziwa, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella
alisema kuwa Benki ya Kilimo ikiwa ni taasisi ya umma ina wajibu
kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini nchini Tanzania hasa katika kuchagiza mapinduzi na maendeleo
katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri zaidi ya
asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia kutoa
kiasi cha zaidi ya
asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda vya nchi.
“Uanzishwaji
wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija
kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati
ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu
ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” amesema.
Mhe.
Mongella alisema kuwa Kanda ya Ziwa ina utajiri mkubwa kwenye
uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ambayo ni mojawapo wa
minyororo ya thamani ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili
ya uongezaji wa thamani mazao mbalimbali na Benki ya Kilimo.
Aliongeza
kuwa maendeleo ya sekta ya kilimo inahitaji msaada mkubwa wa
uwezeshwaji wa mikopo kutoka TADB kwa kuzingatia kuwa ni chombo cha
serikali kilichoanzishwa ili kusaidia upatikanaji wa
utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania.
“Kwa kutambua jukumu kubwa la TADB katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye
ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini, Ofisi ya Mkoa wa Mwanza iliona
kuna umuhimu wa kuipatia Benki hii jengo hili iweze kuwafikia wakulima
wa Kanda ya Ziwa na maeneo ya jirani,” aliongeza.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis
Assenga alisema Benki ya Kilimo imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha
inachangia kwa kiasi kikubwa katika
kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa
kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri
zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.
Bw. Assenga aliongeza kuwa TADB imejipanga
kutekeleza malengo ya Serikali katika kuanzisha Benki hiyo ili kusaidia
kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika
sekta
ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo nchini.
“Kanda ya Ziwa ni eneo la kimkakati hivyo
ujio wetu ni kutimiza dhamira ya dhati ya serikali katika kutatua
changamoto za ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya
maendeleo
ya kilimo nchini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka
taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa;
riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti
magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya
sekta ya kilimo na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema.
Aliongeza kuwa Benki ya Kilimo imejipanga
kushirikiana na Serikali, wabia wa kimkakati na wadau wengine katika
kuendeleza sekta ya kilimo, hasa kuboresha na kutekeleza na juhudi
zozote sera
zinazohusiana na kuhisha ushiriki wa wananchi kwenye mifumo ya kifedha.