Mkuu wa mkoa wa ARUSHA,MRISHO GAMBO,ameonya shule kutogeuzwa kuwa matawi
ya siasa na walimu wakuu kuacha kuruhusu hali hiyo na iwapo watabainika
kukiuka agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.
Gambo anatoa onyo hilo wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa wakuu
wa shule za sekondari ARUSHA-TAHOSA-na kutoa angalizo kuwa shule ni eneo
kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi na si kitovu cha siasa.
Amesema kuna tabia imeanza kuibuka ya baadhi ya shule kugeuzwa vijiwe
vya siasa na kuyataka mashirika yasiyo ya kiserikali endapo yanalengo la
kusadia wanafunzi wanaopata mimba mashuleni ni vyema wakaweka mawakili
wakuwaadhibu watu wanaowapa ujauzito wanafunzi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.