NA ALBERT G.SENGO
Mkutano wa kipekee kati ya rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy umeisha njiani huku ukiacha nyingi sinto fahamu kwa watizamaji waliokuwa wakiufuatilia mubashara baada ya rais huyo wa taifa babe duniani kumtimua kiongozi huyo wa Ukrane. Viongozi hao wawili walihusika katika mazungumzo motomoto na hadharani kuhusu mustakabali wa uungaji mkono wa Marekani kwa Ukraine huku kukiwa na vita vinavyoendelea dhidi ya Urusi. Malumbano hayo makali, ambayo yalijitokeza mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval, yalishuhudia Trump na makamu wa rais wa Marekani J.D. Vance wakimpinga Zelenskyy mara kwa mara, huku kiongozi huyo wa Ukrain akisukuma nyuma hoja zao kwa dharau.Saturday, March 1, 2025
Friday, February 28, 2025
KAMPENI YA MSAADA WA SHERIA YA MAMA SAMIA YAWAKOMBOA WANANCHI WA KATA ZA VISIGA NA MISUGUSUGU
VICTOR MASANGU, KIBAHA
Akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata hizo wakili George Banoba kutoka Wizara ya Katiba na sheria wakati wa mwendelezo wa kampeni ya msaaada wa kisheria ya Mama Samia amesema kwamba lengo kubwa ni kuwaelimisha wananchi juu ya kuweza kupata haki zao za msingi hasa katika suala zima la maeneo ya ardhi.
Amesema kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto nyingi za wananchi kukosa msaada wa kisheria katika mambo mbali mbali ndio maana Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kuanzisha kampeni hiyo kwa lengo la kuwea kuwasaidia wananchi kupata huduma hiyo ya msaada wa kisheria ambayo huduma hiyo inatolewa bure bila malipo.
"Rais wetu wa awamu ya sita ameweza kuanzisha kampeni hii ya msaada wa kwa katika amesema kwamba kampeni hiyo imelenga kupita katika maeneo mbali mbali kwa ajili ya kuwaelimisha wwananchi kuweza kutambua haki zao za msingi juu ya suala zima la msaada wa kisheria wa Mama Samia,"alisema Wakili.
Kadhalika Wakili huyo amewataka wananchi kuhakikisha wanaepukana kabisa na migogogoro ya ardhi kwa kuzingatia sheria na taratibu zote za nchi ikiwemo kufanya uhakiki wa eneo husika wanayoyanunua kutoka kwa wataalamu wa ardhi ambao wataweza kumsaidia kutambua haki zake na kuepukana na migogoro hiyo.
Kadhalika amebainisha kwamba Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia lengo lake kubwa ni kwa ajili ya kuelimisha wananchi juu ya masuala ya utatuzi mbali mbali ikiwemo migogogoro ya ardhi, mirathi,ukatili wa kijinsia, kusikiliza kero zinazowakabiliwa wananchi ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia.
Nao badhi ya wananchi wa Kata ya Visiga akiwemo mzee Ally Matimbwa kutoka mtaa wa Madafu amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuanzisha kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ambayo itaweza kusaidia kutatua mambo mbali mbali ikiwemo migogoro ya ndoa, pamoja na migogoro ya ardhi.
Amebainisha kwamba katika baadhi ya maeneo katikaKata ya Visiga tangu mwaka 1984 kuwekuwepo na changamoto kubwa ya migogogro ya ardhi na kwamba kupitia kampeni hiyo ya Mama Samia itaweza kuwa ni mkombozi kutokana na kuweza kupata fursa ya kUupewa elimu juu ya masuala ya kisheria.
Thursday, February 27, 2025
AMCOS ZA PWANI ZATAKIWA KUACHANA NA OFISI ZA MABEGI
HAWA HAPA WASHINDI WOTE WA TUZO ZA TRACE 2025
Hatimaye washindi wa Tuzo za Trace kwa mwaka 2025, wamepatikaja na kutangazwa rasmi usiku wa Jumatano Februari 26 huko Zanzibar.
Hafla hiyo iliwaleta pamoja nyota wakubwa katika tasnia hiyo kusherehekea mafanikio ya ajabu ya wasanii, watayarishaji na wasanii wa Kiafrika.
Tukio la mwaka huu liliangazia ukuaji wa ushawishi wa bara la Afrika kimataifa, huku Afrobeats, Amapiano, na aina mbalimbali za muziki za Kiafrika zikichukua nafasi kubwa.
Wasanii wawili wakali kutoka Afrika Kusini, Titom na Yuppe wametwaa tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka kupitia wimbo wao mkali wa ‘Tshwala Bam’, wimbo ambao umechezwa sana na wapendao burudani kote ulimwenguni kiasi cha kufanya Mdundo wao wa nguvu kuambukiza taifa na taifa hata ikawa kama utamaduni kuucheza wimbo huo.
Nyota wa Nigeria Rema ameendelea kuliteka anga, baada ya kushinda Tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka kwa kupitia Heis, Pia ametwaa tuzo ya Msanii Bora wa Kiume, akithibitisha tena ubabe wake katika tasnia hiyo.
Katika kipengele cha Wimbo Bora wa Ushirikiano (Best Collaboration), Raia wa Ivory Coast Tam Sir & Team Paiya wameibuka kidedea kupitia mkwaju wao ‘Coup du Marteau’, wimbo wa kusisimua uliochanganya mdundo, nishati na utayarishaji bora. Wakati huo huo, tuzo ya Video Bora ya Muziki imemwendea mwana maono, mtayarishaji Meji Alabi kwa uelekezi wake shupavu wa 'DND' ya Rema.
Nguli wa Afrika Kusini Makhadzi kwa mara nyingine tena amethibitisha uwepo wake wa kipekee katika jukwaa la washindi, kwa kushinda Mchezaji Bora wa Dansi kwa maonyesho yake ya nguvu. Katika kitengo cha DJ, DJ Moh Green kutoka Algeria alitunukiwa kama DJ Bora, na hivyo kuimarisha hadhi yake kama mmoja wa wasanii wa mchanganyiko wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.
Mkali Diamond Platnumz ameliheshimisha taifa lake na kuipeleka Tanzania duniani. akishinda kibabe kama Msanii Bora wa Kimataifa wa Afrika, huku rapa wa Ivory Coast, Didi B, akiibuka kidedea katika kipengele cha Msanii Bora wa Hip Hop kwa mtiririko mkali na kipaji chake kisichopingika.Miongoni mwa wasanii wa kike, Tyla wa Afrika Kusini alitajwa kuwa Msanii Bora wa Kike, sifa inayostahiki kwa uhalisi wake na mtindo wa kipekee ambao umevutia wasikilizaji na wapenzi wa muziki mtamu kote ulimwenguni.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Nigeria Mercy Chinwo ametwaa tuzo ya Msanii Bora wa Injili, kupitia kazi zake zenye kugusa mioyo zinazo ambatana na simulizi za kuhuisha na kuinua mioyo.
Washindi wa kanda ni pamoja na mwimbaji wa Ivory Coast Josey, ambaye ametawazwa kuwa Msanii Bora Anayezungumza Kifaransa, na mwimbaji wa Nigeria Ayra Starr, ambaye anaendelea kutawala Afrika Magharibi kwa sauti yake kali na nyimbo maarufu. Kusini mwa Afrika, Tyler ICU alipata tuzo hiyo, na kuthibitisha nafasi yake kama mchezaji muhimu katika eneo la muziki la kanda.
Msanii wa Kenya Bien alitambuliwa kama Msanii Bora wa Afrika Mashariki, akiwapoteza Diamond Platnumz (Tanzania), Joshua Baraka (Uganda), Harmonize (Tanzania), Rophnan (Ethiopia), Marioo (Tanzania), Zuchu (Tanzania) na Nandy (Tanzania)
Washindi wengine ni Chelsea Dinorath ya Angola aliibuka kuwa Msanii Bora Anayezungumza Kireno kwa kipaji chake kisichoweza kupingwa.
Kwa upande wa kipengele kilichokuwa kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu na wengi watazamaji hususani nchi wenyeji wenyewe wa tuzo, Nandy amefanikiwa kuwagalagaza wasanii wote waliokuwa kwenye kinyang'anyiro cha Msanii Bora Tanzania akiwemo Mbosso, Diamond Platnumz, Zuchu, Marioo, Alikiba, Jux na Harmonize.
IFUATAYO NI ORODHA YA WASHINDI WA TUZO ZOTE:
Tuzo za Kimataifa
Wimbo wa Mwaka
- Titom & Yuppe – ‘Tshwala Bam’ (South Africa)
- Tyla – ‘Jump’ (South Africa)
- Tyler ICU – ‘Mnike’ (South Africa)
- Tamsir x Team Paiya – ‘Coup du Marteau’ (Ivory Coast)
- Asake & Travis Scott – ‘Active’ (Nigeria)
- Tems – ‘Love Me Jeje’ (Nigeria)
- Burna Boy – ‘Higher’ (Nigeria)
- Rema & Shallipopi – ‘Benin Boys’ (Nigeria)
- Diamond Platnumz – ‘Komasawa’ (Tanzania)
Albamu ya Mwaka
- Rema – Heis (Nigeria)
- Burna Boy – I Told Them (Nigeria)
- Asake – Lungu Boy (Nigeria)
- Josey – Vibration Universelle (Ivory Coast)
- Amaarae – Fountain Baby (Ghana)
- King Promise – True To Self (Ghana)
- Stonebwoy – 5th Dimension (Ghana)
- Toofan – Stamina (Togo)
Best Collaboration
- Tamsir & Team Paiya – ‘Coup du Marteau’ (Ivory Coast)
- Titom & Yuppe & Burna Boy – ‘Tshwala Bam’ (Remix) (South Africa/Nigeria)
- Neyna & MC Acondize – ‘Nu Ka Sta Para’ (Cape Verde)
- Kocee ft. Patoranking – ‘Credit Alert’ (Cameroon/Nigeria)
- Asake & Wizkid – ‘MMS’ (Nigeria)
- Rema & Shallipopi – ‘Benin Boys’ (Nigeria)
- Odumodublvck & Black Sherif – ‘Woto Woto Seasoning’ (Ghana)
Video Bora ya Muziki
- Meji Alabi – Rema ‘DND’ (Nigeria)
- TG Omori – Kizz Daniel & Davido ‘Twe Twe’ (Nigeria)
- Director Folex – Zuchu feat Innoss’ B ‘Nani’ (Remix) (Tanzania/DRC)
- Nabil Elderkin – Tyla ‘Jump’ (South Africa)
- Kmane – Ayra Starr ‘Commas’ (Nigeria)
- Seoute Emmanuel – Toofan ‘C Pas Normal’ (Togo)
- Ach’B – Innoss’ B ‘Sete’ (DRC)
- Edgar Esteves – Asake & Wizkid ‘MMS’ (Nigeria)
Mchezaji Bora
- Makhadzi (South Africa)
- Ikorodu Boys (Nigeria)
- Dancegod Lloyd (Ghana)
- Incredible Zigi (Ghana)
- Kamo Mphela (South Africa)
- Telminho (Angola)
- Ordinateur (Ivory Coast)
- Issac Kalonji (Democratic Republic of Congo)
DJ Bora
- DJ Moh Green – ‘Kelele’ (Algeria)
- Tyler ICU – ‘Mnike’ (South Africa)
- Uncle Waffles – ‘Wadibusa’ (South Africa)
- DJ Tunez – ‘Apala Disco Remix’ (Nigeria)
- DJ Nelasta – ‘Eros’ (Angola)
- DJ Spinall ft. Tyla & Omah Lay – ‘One Call’ (Nigeria)
- DJ Neptune ft. Qing Madi – ‘Honest’ (Nigeria)
- DJ Maphorisa – ‘Mnike’ (South Africa)
- Kabza De Small – ‘Imithandazo’ (South Africa)
Best Hip Hop Artist (sponsored by Hot 97)
- Didi B (Ivory Coast)
- Nasty C (South Africa)
- Odumodublvck (Nigeria)
- Suspect 95 (Ivory Coast)
- Sarkodie (Ghana)
- Young Lunya (Tanzania)
- Maglera Doe Boy (South Africa)
Pan-African Awards
Best Global African Artist
- Diamond Platnumz (Tanzania)
- Tyla (South Africa)
- Tyler ICU (South Africa)
- Fally Ipupa (Democratic Republic of Congo)
- Burna Boy (Nigeria)
- Asake (Nigeria/USA)
- Rema (Nigeria)
- Ayra Starr (Nigeria)
Msanii Bora wa Kiume
- Rema (Nigeria)
- Dlala Thukzin (South Africa)
- Fally Ipupa (Democratic Republic of Congo)
- Diamond Platnumz (Tanzania)
- Asake (Nigeria)
- Burna Boy (Nigeria)
- Wizkid (Nigeria)
- Stonebwoy (Ghana)
Msanii Bora wa Kike
- Tyla (South Africa)
- Makhadzi (South Africa)
- Chelsea Dinorath (Angola)
- Josey (Ivory Coast)
- Ayra Starr (Nigeria)
- Tems (Nigeria)
- Yemi Alade (Nigeria)
Mtumbuizaji Bora LIVE Jukwaani
- Fally Ipupa (DRC)
- Ayra Starr – 21: The World Tour (Nigeria)
- Burna Boy – I Told Them (Nigeria)
- Tyla (South Africa)
- Yemi Alade – African Rebel Tour (Nigeria)
- Didi B – Mojo Trone Tour (Ivory Coast)
- Diamond Platnumz – Wasafi Festival (Tanzania)
Mtayarishaji Bora
- P.Priime – ‘MMS’ (Nigeria)
- Kelvin Momo – ‘Sewe’ (South Africa)
- DJ Maphorisa – ‘Mnike’ (South Africa)
- Tam Sir – ‘Coup du Marteau’ (Ivory Coast)
- Sarz – ‘Happiness’ (Nigeria)
- Jae 5 – ‘Perfect Combi’ (Ghana)
- KDDO – ‘For Certain’ (Party Next Door) (Nigeria)
- London – ‘Ozeba’ (Nigeria)
- Kabza De Small – ‘Imithandazo’ (South Africa)
Best Gospel Artist
- Mercy Chinwo (Nigeria)
- Spirit of Praise 10 (South Africa)
- KS Bloom (Ivory Coast)
- Ada Ehi (Nigeria)
- Bella Kombo (Tanzania)
- Israël Mbonyi (Rwanda)
Regional Awards
Best Artist Eastern Africa
- Bien (Kenya)
- Diamond Platnumz (Tanzania)
- Joshua Baraka (Uganda)
- Harmonize (Tanzania)
- Rophnan (Ethiopia)
- Marioo (Tanzania)
- Zuchu (Tanzania)
- Nandy (Tanzania)
Best Artist (Western Africa Anglophone)
- Ayra Starr (Nigeria)
- Seyi Vibez (Nigeria)
- Adekunle Gold (Nigeria)
- Tems (Nigeria)
- Chike (Nigeria)
- Simi (Nigeria)
- KiDi (Ghana)
Best Artist (Southern Africa)
- Tyler ICU (South Africa)
- Titom & Yuppe (South Africa)
- De Mthuda (South Africa)
- Inkabi Zezwe (South Africa)
- Dlala Thukzin (South Africa)
- Tyla (South Africa)
- Uncle Waffles (South Africa)
Best Artist Francophone Africa
- Josey (Ivory Coast)
- Didi B (Ivory Coast)
- Tidiane Mario (Congo)
- Gaz Mawete (Democratic Republic of Congo)
- Wally B. Seck (Senegal)
- PhillBill (Cameroon)
Best Artist (Lusophone Africa)
- Chelsea Dinorath (Angola)
- Calema (São Tomé and Príncipe)
- Landrick (Angola)
- Twenty Fingers (Mozambique)
- Mr. Bow (Mozambique)
- Soraia Ramos (Cape Verde)
Best Artist (Tanzania)
- Nandy (Tanzania)
- Mbosso (Zanzibar)
- Diamond Platnumz (Tanzania)
- Zuchu (Zanzibar)
- Marioo (Tanzania)
- Alikiba (Tanzania)
- Jux (Tanzania)
- Harmonize (Tanzania)
International and Diaspora Awards
Best Artist (Europe)
- Joe Dwet File (France/Haiti)
- Central Cee (United Kingdom)
- Kalash (France/Martinique)
- Darkoo (United Kingdom)
- Jungeli (France)
- Franglish (France)
- Aya Nakamura (France/Mali)
Best Artist (Brazil)
- Duquesa (Brazil)
- Racionais MC’s (Brazil)
- MC IG (Brazil)
- Péricles (Brazil)
- Tasha & Tracie (Brazil)
- Ludmilla (Brazil)
Best Artist (Caribbean)
- Lea Churro (Reunion Island)
- Venssy (French Guiana)
- Mathieu White (Guadeloupe)
- Meryl (Martinique)
- Nesly (French Guiana)
- Shenseea (Jamaica)
- Kenny Haiti (Haiti)
Best Artist (Indian Ocean)
- Barth (Reunion)
- Goulam (Comoros)
- PLL (Reunion)
- Kalipsxau (Reunion)
- Léa Churros (Reunion)
- Jamily Jeanne (Mauritius)
Lifetime Achievement Award
- D’Banj
HAZINA- MASHIRIKA YA UMMA YAMETAKIWA KUACHANA NA TABIA YA KUWA TEGEMEZI KWA SERIKALI
IMEANDIKWA NA VICTOR MASANGU, PWANI KUSOMWA NA ALBERT G.SENGO Mashirika mbali mbali ya umma nchini yameaswa kuwa na uzalendo kwa kuepuka tabia ya kuwa tegemezi wa fedha za ruzuku kutoka serikalini na badala yake Mashirika hayo yajenge mikakati imara ya kuweza kuleta mageuzi katika kuichangia gawio serikali katika mfuko wa hazina kwa ajili ya kuleta chachu ya maendeleo na kuongeza Pato la Taifa. Kauli hiyo imetolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichele, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha siku mbili kilichowakutanisha 0fisi ya msajiili wa hazina, Ofisi ya Taifa ya ukaguzi na baadhi ya viongozi wa mashirika ya umma. Aidha Mkaguzi huyo ameongeza kuwa kikao kazi hicho kimelenga kuwajengea uwezo watumishi wa mashirika ya umma pamoja na kuweka mikakati kabambe ya kuimarisha mifumo ya utekelezaji wa majukumu ya uongozi ikiwa sambamba na kuzilinda rasilimali za Taifa kwa maslahi ya wananchi sambamba na kuepuka kabisa mianya ya upotevu wa mapato ya serikali.
RUNALI WAANZA KUJENGA HOTELI YA KISASA YA ZAIDI YA MILIONI 700, CORECU WAPANGA KUIGA
Na Fredy Mgunda, Lindi.
Chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kimeanza ujenzi wa hoteli ya kisasa katika wilaya ya Liwale, lengo likiwa ni kuongeza mapato ya chama hicho kupitia vitega uchumi vipya.
Ujenzi huu utasaidia si tu kuongeza kipato cha chama, bali pia kuimarisha uchumi wa maeneo ya jirani.
Akizungumza wakati wa ziara ya viongozi wa AMCOS kutoka mkoa wa Pwani, Mwenyekiti wa RUNALI, Odas Mpunga, alielezea kuwa hatua hii ni sehemu ya mkakati wao wa kujenga na kuendeleza miradi itakayowafaidi wanachama na kuimarisha sekta ya ushirika katika wilaya ya Liwale na maeneo mengine.
Aliongeza kuwa ni muhimu kwa chama hicho kuendelea kuwa na miradi itakayowasaidia kuongeza mapato na kuboresha huduma kwa wanachama.
Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha Pwani (CORECU), Mussa Hemedi mng'eresa, alielezea furaha yake kwa kuona mafanikio ya RUNALI na kusema kuwa wao pia wanajivunia mafanikio haya. Alisema kuwa wamepanga kuanzisha miradi ya maendeleo katika chama chao, wakifuata mfano mzuri unaoonyeshwa na RUNALI, na kuwa hiyo ni ishara ya maendeleo endelevu katika sekta ya ushirika.
Miradi hii ya maendeleo inaonyesha juhudi za vyama vya ushirika katika kuboresha hali ya maisha ya wanachama na kuchangia katika maendeleo ya uchumi wa mikoa mbalimbali, hasa kupitia uwekezaji katika sekta za kitalii na huduma za kijamii.
Wednesday, February 26, 2025
#live ALLY KAMWE NA MSEMAJI WA PAMBA JIJI USO KWA USO NDANI YA JEMBE FM MUDA HUU
WANAFUNZI ZAIDI YA 2423 KATA YA TUMBI WANUFAIKA NA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA WA MAMA SAMIA
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Akizungumza na baadhi ya wanafunzi kuhusiana na kampeni hiyo Wakili George Banoba kutoka Wizara ya Katiba na sheria amesema kwamba wamefanikiwa kupita katika shule mbali mbali zikiwemo shule za msingi tatu pamoja na shule ya sekondari Mwanalugali kwa lengo la kuweza kutoa elimu ya masuala mbali mbali yanayohusiana na sheria.
Banoba amebainisha kwamba katika kampeni hiyo wameweza kuambatana na wadau mbali mbali wa sheria akiwemo pamoja na Afisa ustawi wa jamii pamoja na mkuu wa Dawati lajinsia Wilaya ya Kibaha kwa lengo la kuweza kupata elimu kwa wanafunzi na kuwaajengea uwezo juu ya kutambua haki zao za msingi ikiwemo mambo ya unyanyasaji wa kijinsia.
"Tumeanza rasmi kampeni yetu ya msaada wa kisheria ambapo tumeanza katika kata ya Tumbi na tumefanikiwa kuwafikia wanafunzi zaidi ya 2400 na wameweza kufundishwa masuala mbali mbali ya msaada wa kisheria bure na kwamba katika Halmashauri ya mji Kibaha watakwenda katika kata zipatazo 10 ambapo watatoa msaada wa kisheria katika maeneo ya migogoro ya ardhi, ndoa, miradhi, pamoja na usaidizi mwingine unaohusina na mambo ya kisheria,"amesema
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Mwanalugali Jeriko Rogers na pamoja na mwanafunzi wa shule hiyo Mwasalobo Komalumo wamempongeza Rais wa wawamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuanzisha kampeni ambayo itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwasaidia katika suala zima la msaada wa kisheria.
Naye Mkuu wa wa dawati la Kjinsia na watoto Wilaya ya Kibaha pamoja na Afisa ustawi wa jamii katika Halmashauri ya Kibaha mji wamebainisha kwamba kampeni hiyo itakwenda kuwa mkombozi na msaada mkubwa katika kuwasaidia wanafunzi pamoja na wananchi wengine kuweza kupata haki zao za msingi.
Kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia inaendelea kufanyika katika Mkoa wa Pwani ambapo itapita katika Halmashauri zote tisa kwa lengo la kuweza kutoa elimu ya masuala mbali mbali ikiwemo mambo ya migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi pamoja na mambo mengine ya msingi yanayohitaji msaada wa kisheria.
SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI YA UWEKEZAJI
Serikali imedhamiria kuendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa wawekezaji kuwekeza Mkoa wa Mwanza na Tanzania kiujumla ili kuchochea maendeleo na kukuza uchumi wa Mkoa na Taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda alipokuwa katika ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo katika kiwanda cha Ziwa Steel kilichopo Nyanguge Wilayani Magu.
Mkuu wa Mkoa amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kwani Taifa likiwa na viwanda vingi inasaidia katika upatikanaji wa ajira, ukusanyi wa kodi na upatikanaji wa bidhaa kwa urahisi zitakazozalishwa kupitia wawekezaji hao.
“Kwa niaba ya Serikali ninaomba kuwapongeza Mkurugenzi na timu yako, lakini pia nitumie wasaa huu kuwakaribisha Wawekezaji katika Mkoa wetu wa Mwanza na Mwanza ni salama sana kwa uwekezaji”.
Sambamba na hayo Mhe. Mtanda amesema kilichomfurahisha zaidi ni kusikia kuwa kiwanda hicho kina mpango wa kuanza kutengeneza nashine za uchakataji wa dhahabu ambapo kwa ukanda huu ndio ukanda wa madini hayo.
“Mtakapoanza uzalishaji wa mashine hizo basi rai yangu ni kwamba msiwasahau pia wachenjuaji wadogo wa dhahabu”.
Kwa upande wake Afisa Utumishi wa Kiwanda hicho Bw. Philip Sylivanus amesema wanamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri na kuvutia Wawekezaji, wamekuwa wakifanya kazi zao kwa urahisi hususani wakati wa kusafirisha malighafi na bidhaa zao.
Awali kabla ya kutembelea Kiwandani hapo Mkuu wa Mkoa pia alipata wasaa wa kutembelea na kukagua maendeleo katika Kiwanda Kipya cha Pepsi SBC kilichopo Nyakato Industrial Area, Wilayani Ilemela na kupongeza juhudi hizo za uwekezaji mkubwa uliofanywa na kiwanda hicho.
Monday, February 24, 2025
WAZIRI MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA UJENZI SGR MWANZA - ISAKA
NA ALBERT G.SENGO/MALAMPAKA/SIMIYU
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amelitaka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kutumia uzoefu wa uendeshaji wa reli ya SGR Dar Es Salaam - Dodoma katika kufanya maboresho kwenye ujenzi wa reli ya SGR kipande cha tano (Lot 5) Isaka - Mwanza ili kuepuka usumbufu usio wa lazima. Prof. Mbarawa ameyasema hayo leo alipotembelea mradi huo kwa lengo la kujionea maendeleo na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mradi huo wa kisasa unaotarajiwa kuleta mapinduzi katika nyanja ya usafiri na usafirishaji nchini. " Tunataka yale tuliyojifunza kule hapa yasijirudie tena, kwa mfano Dar es Salaam kuna changamoto ya maegesho ya magari pamoja na Dodoma sasa kwenye mikoa hii tuhakikishe tunajipanga vizuri hata watu wakiongezeka kusiwe na shida," Amesema Mbarawa. Aidha Waziri Mbarawa amesema kwa upande wa serikali watahakikisha wanamsimamia vizuri mkandarasi pamoja na kumpatia malipo kwa wakati ili mradi huo ukamilike kwa wakati na wananchi wanufaike kama Dar es salaam, Morogoro na Dodoma wanavyonufaika.ZIDANE SERERI AZIMA SHANGWE ZA SIMBA DAKIKA ZA JIOOoooNI.......!!
TIMU za Simba SC na Azam FC zimegawana pointi moja moja baada ya sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Azam FC walitangulia na bao la dakika ya pili tu la winga Mgambia, Gibrill Sillah akimalizia mpira uliotemwa na kipa Mguinea, Mousa Camara kufuatia krosi nzuri ya Iddi Suleiman ‘Nado’ kutoka kushoto mwa Uwanja.
Simba wakasawazisha dakika ya 25 kwa bao la winga Mkongo, Elly Mpanzu Kibisawala aloyepokea pasi nzuri ya kiungo mshambuliaji Mtanzania, mwenye asili ya Kongo, Kibu Dennis Prosper.
Kipindi cha pili ikawa zamu ya Simba kutangulia kwa bao la beki Abdurazam Mohamed Hamza dakika ya 76 akimalizia kwa kichwa mpira wa adhabu wa kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua kutoka kulia mwa Uwanja.
Aliyeinusuru Azam kupoteza mchezo wa leo ni winga mzawa chipukizi wa miaka 19, Zidane Sereri kwa kusawazisha bao dakika ya 88 baada ya kupokea pasi ndefu ya kiungo Feisal Salum na kuwatoka mabeki wa Simba kabla ya kumlamba chenga kipa Camara.
Kwa matokeo hayo, Simba inafikisha pointi 51 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
Kwa upande wao Azam FC wanafikisha pointi 44, nao wanabaki nafasi ya tatu mbele ya Singida Black Stars yenye pointi 38 baada ya wote kucheza mechi 21.
RAIS DKT. SAMIA AKIFUNGUA JENGO LA HALMASHAURI YA BUMBULI-LUSHOTO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Akifungua Jengo la Almashauri ya Bumbuli Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, leo tarehe 24 Februari, 2025.
KADI NYEKUNDU YA DERICK MUKOMBOZI DHIDI YA SIMBA YAFUTWA
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imefuta adhabu ya kadi nyekundu (Red Card) aliyooneshwa mchezaji wa Namungo, Derick Mukombozi na mwamuzi wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Namungo dhidi ya Simba Sc.
Taarifa ya leo Februari 23, 2025 iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya mapitio ya mwenendo na matukio ya Ligi katika kikao chake cha Februari 21, 2025.
Kamati imefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa maelezo yaliyopo kwenye ripoti ya mwamuzi hayana ushahidi wa kutosha unaoendana na marejeo ya picha mjongeo kuwa Mukombozi alistahili kadi nyekundu.
RAIS DKT SAMIA ATOA MAELEKEZO KWA WAZIRI MCHENGERWA

Na Oscar Assenga, HANDENI.
RAIS Dkt Samia Suluhu amemuagiza Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengerwa kuhakikisha wanapeleka kiasi cha Milioni 240 kwa ajili ya kujenga eneo maalumu la Upasuaji wa Mifupa katika Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Handeni.
Dkt Samia aliyasema hayo leo mara baada ya kufungua Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Handeni eneo la Mkata ikiwa ni ziara ya siku saba katika Mkoa wa Tanga yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo, kuweka mawe ya msingi na kuzungumza na wananchi.

Alisema kwa sababu wanataka Handeni kuwa eneo maalumu kwa ajili ya Hospitali ya Mifupa pamoja na kuwepo na tiba mbalimbali lakini libaki kuwa maalumu kwa ajili ya mifupa
Aidha alisema kwamba mpaka sasa Hospitali hiyo imeshapokea wajawazito 900 na 300 walijifungua kwa upasuaji na iwapo isingekuwepo lazima kungekuwa na Rufaa na hivyo uwepo wa hospitali hiyo umeokoa maisha ya watu wengi.

Alisema hospitali hiyo ipo barabarani na wakiweka lami kipande kinachotoka Barabarani kwenda hosputali itakuwa karibu na wameamua kujenga aeneo la kufanya upasuaji wa mifupa na nimeelekeza Waziri Tamisema aleta fedha milioni 240 ili kujenga eneo la mifupa likamilike,
“Ukiangalie kuna maeneo ya upasuaji mawli eneo la upasuaji ,upauaji wa jumla na mifupa na hakuna wodi na wanalazwa na wagonjwa wengine hivyo ni vema sehemu ya mifupa ikabakia pekee yake na Handeni ikiwa Hospitali maalumu kwa ajili ya mifupa na mambo mengine na watu wengine wake na wagonwa wengine wa mifupa na maeneo mengine waje kupata huduma”Alisema

Rais Dkt Samia aliawapongeza wana kijiji na uongozi wa kijiji cha Mkata Mashariki kwa kutoa eneo la ekari 32 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo huku akieleza jambo hilo ni la kuigwa kwani kama wangesubiri Serikali itoe eneo pengine mradi ungeweza kuchelewa.
“Mbali na hayo awamu ya sita Serikali katika wilaya ya Handeni wamepeleka Bilioni 4.37 kwa ajili ya Hospitali hiyo na fedha walizipeleka kwa ajili ya kujenga vituo vya afya na zahanati 16 kwa hiyo ni dhamira ya serikali kuwakinga wananchi wasipatwe na magonjwa .

“Ikitokea wanahitaji matibabu wapate huduma za uhakika zilizokaribu nao ndio maana wameendelea ujenzi wa Hospitali hiyo na kuleta vifaa vya kisasa kwa mkoa wa mzima “Alisema
Alisema kwamba wananchi wa handeni wanamshukuru kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuliunganisha Taifa na wannachi ikiwemo kuwapeleka wadau ambao waliwashika mkono wakajenga majengo mbalimbali na kuifanya hospitali hiyo kwa bora na yenye viwango vya hospitali ya mkoa.

Mchengerwa alisema ujenzi wa jengo hilo ni mpango wa Serikali kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi na maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu ya kuelekeza kwamba yajengwe majengo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa handeni na hiyo ni kazi kubwa ya kuunganisha Taifa na mahusiano na watu mbalimbali duniani.
“Wananchi walipata bahati ya kupata wadau wa maendeleo kutushika mkono na kujenga majengo mbalimbali na kuifanya Hospitali yetu kuwa bora na yenye viwango vya Hospitai ya mkoa na kazi hiyo imekwenda kuokoa maisha ya watoto, wakina mama wanaokwenda kujifungua na maisha ya wapiti njia”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba Serikali imewezesha ujenzi wa Majengo 15 ya huduma za maabara, majengo muhimu za huduma za nje, huduma za dharura, huduma za mionzi,jingo la huduma za wuzazi ,jengo la dawa na kipindi cha muda mfupi umweza kuokoa maisha ya wakina mama na watoto.
“Mhe Rais Sekta ya Afya inafanya kazi kubwa ya kuokoa maisha ya wakina mama na watoto na wilaya ya Handeni hakuna kifo cha mama na mtoto na wahudumu katika sekta hii wamebadilika na wanafanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanaokoa maisha ya watanzania.
Hata hivyo alisema katika Mkoa wa Tanga fedha ambazo zilitolewa na Serikali kwenye sekta ya afya wametoa Bilioni 65.6.