ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 13, 2019

ZAMU YA KULA MUZIKI WA INJILI - SOLOMONI MKUBWA FT KIGUSILE - Neno (Official Video)


Mbingu ni kiti chako cha enzi Baba Dunia ni mahali pa kukanyanga miguu yako Isaiah 66:1 Nini nikupe kishinde kutii NENO lako Maana ni NENO lako limeyafanya yote Sauli alipoasi NENO alipoteza ufalme 1sam 15 Abraham alipotii NENO alipata mwana wa uzee Genesi 18: Naamani alipotii NENO alitakazwa ukoma 2kings 5 Gehazi alipoasi NENO alipokea ukoma 2kings 5 Maana waheshimu NENO lako kupita jina lako Ndani ya NENO lako Kuna laana na baraka Deutr 28:1–2 Katika NENO lako Kuna uzima na mauti Deutro 28:15-16 NENO ndio siri la mafanikio yako Jere 7:23 NENO lako limeumba mambo yote John 1:3 Pasipo NENO lako hakuna kiliumbwa John 1:3 NENO lako linaumba ata leo NENo lako Continues .........

LIVE:- ZIARA BINAFSI YA RAIS YOWERI KAGUTA MUSEVENI WA UGANDA HAPA NCHINI. CHATO GEITA


Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni afanya Ziara Binafsi ya siku 1 moja hapa nchini.
Mhe. Rais Museveni anamtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kijijini kwake Mlimani katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Akiwa Chato, Mhe. Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli. Jumamosi tarehe 13 Julai, 2019

Friday, July 12, 2019

TIGO YATANGAZA MSHINDI WA KITITA CHA MILIONI 10 KUPITIA PROMOSHENI YA SOKA LA AFRIKA

 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael, (kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo wakati wa kumtangaza mshindi wa mwezi wa shilingi milioni 10/, kupitia promosheni ya SOKA la AFRIKA , Omary Ahmed Bwenda, (Kulia) mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam ameibuka mshindi na kukabidhiwa fedha zake.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael, (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10/- Omary Ahmed Bwenda (27 (kulia) mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, kutokana na kuibuka mshindi kupitia promosheni inayoendelea ya Tigo inayojulikana kama SOKA la AFRIKA katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya mawasiliano ya Tigo, baada ya kufanikisha ndoto za wateja wake 10 kushuhudia mashindano ya soka ya Afrika, mubashara kupitia promosheni yake ya SOKA la AFRIKA, imetangaza mshindi wa fedha taslimu shilingi milioni 10 kupitia promosheni hiyo.

Akiongea katika mkutano na waandishi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael, alimtangaza mshindi huyo wa mwezi kuwa ni Omar Ahmed Bwenda (27) mfanyabiashara na mkazi wa jijini Dar es Salaam.

Amesema kupitia promosheni hii iliyoandaliwa na Tigo kwa ajili ya kuwashukuru wateja kwa kuendelea kuiunga mkono kwa kununua bidhaa na kutumia huduma zake imewawezesha pia wateja 28 kujishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- kila siku na wateja wanne kujishindia milioni 1,000,000/- kwa mwezi.

Kupitia promosheni hii itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu washiriki wataendelea kujishindia zawadi za fedha taslimu kila siku, kwa wiki na kwa mwezi. Ili kushiriki kinachotakiwa ni kutuma neno SOKA kwenda namba 15670 au tembelea tovuti ya  www.tigosports.co.tz na kujibu maswali kuhusiana na michuano ya soka ya Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Misri.

“Natoa wito kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo kuendelea kuchangamkia na kushiriki promosheni hii ya SOKA la AFRIKA   ili waweze kujishindia zawadi, na kadri wanatavyoshiriki na kujibu maswali ndivyo watakavyokuwa na nafasi kubwa zaidi ya kupata ushindi” alisema Shisael,  na kuongeza kuwa na kuongeza kusema kuwa hadi kufikia mwisho wa promosheni hii, zaidi ya wateja 100 watajishindia zawadi ya pesa taslimu.

Mashindano ya promosheni ya SOKA LA AFRICA ni sehemu ya jitihada za Kampuni ya Tigo, kuwashukuru wateja wake kwa kutumia bidhaa na huduma za Kampuni.

Pia promosheni hii ni sehemu ya ubunifu ambao umelenga kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha wateja.

BARCELONA YALAMBA DUME YAINASA SAINI YA GRIEZMANN.


Klabu ya Barcelona imemsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann baada ya kukubali kulipa ada ya mchezaji huyo 120m euro (£107m).

Griezmann mwenye miaka 28 amesaini mkataba wa miaka mitano amabo unajumuisha kipengele cha 800m euro (£717m) ikiwa ataondoka klabu hiyo.

Griezmann alijiunga Atletico Madrid akitokea from Sociedad mwaka 2014 na kufunga magoli 133 kwenye michezo 256.

Mwaka mmoja uliopita, Juni 2018, alisaini mkataba mpya na Atletico wa miaka mitano, hata hivyo ilipofika mwezi Mei mwaka huu akatangaza kuwa ataihama klabu hiyo katika dirisha la usajili la majira haya ya joto.
Griezmann sasa anakuwa mchezaji wa sita ghali zaidi duniani kusajiliwa nyuma ya Neymar, Kylian Mbappe, Philippe Coutinho, Joao Felix na Ousmane Dembele.
Ameshinda mataji kadhaa na Atletico kama Kombe la Europa, kombe la Super Cup la Uhispania, pamoja na Uefa Super Cup.
Pia amekuwa kinara wa magoli wa klabu hiyo katika misimu mitano iliyopita klabuni hapo.
Griezmann anakuwa mchezaji wa nne mkubwa kusajiliwa na Barcelona katika dirisha hili la usajili baada ya kiungo Frenkie de Jong kutoka Ajax, golikipa Neto kutoka Valencia na beki Emerson kutoka klabu ya Atletico-MG ya Brazil.

MAHAKAMA INAYOTEMBEA KUCHOCHEA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI WA MWANZA.


ILI MAHAKAMA nchini zisiendelee kuonekana kama sehemu ya kupoteza muda wa wananchi ambao badala yake wangeweza kujikita katika shughuli za maendeleo, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imezindua mahakama inayotembea (Mobile Court) ambayo itatoa huduma katika maeneo ya Buswelu, Igoma na Buhongwa ikiwa ni mpango mkakati wa Mahakama Kuu nchini kupunguza changamoto za msongamano wa mashauri mahakamani sanjari na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Akizindua Mahakama hiyo, Jaji mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda hiyo ya Mwanza, Sam Rumanyika ambaye alitangulia kwa kutoa Salamu za rambirambi kwa Kampuni ya Azam Media kufuatia msiba wa wafanyakazi wake watano na madereva wawili amesema Mahakama hiyo ni ya kisasa na ya pili nchini na itakayorahisisha utoaji wa huduma na haki kwa wananchi.

Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ambaye alikuwa mmoja wa waalikwa na mdau mkubwa wa Mahakama amesema ili Nchi ifikie malengo yake ya kuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi ni lazima migogoro inayowasilishwa Mahakamani ikamilike kwa haraka na wananchi watumie muda wao mwingi zaidi na rasilimali zao, kuzalisha mali na kutoa huduma badala ya kupoteza muda mwingi wakitafuta utatuzi Mahakamani.







"SINGIDA MASHARIKI HAIKUWA NA MWAKILISHI MWAKA WA 9 SASA" - AFUNGUKA DC ANAYEWANIA KITI CHA LISSU.



 "Ukiangalia Jimbo hili limeishi bila mwakilishi mzuri tangu mwaka 2010, Leo hii tunavyoongea maendeleo ya jimbo la Singida Mashariki yamekuwa duni sana, kwa maana mwakilishi hakuwahi kupata nafasi hata siku moja kuongelea mahitaji ya Jimbo lake zaidi ya kushughulika na masuala ya kitaifa"

"Wananchi walitegemea mwakilishi wao angezibeba shida zao na kuzipeleka Bungeni kuiomba Serikali kusaidia kuondosha changamoto za nyanja mbalimbali, lakini hatimaye Jimbo lime kosa mwakilishi takribani mwaka wa 9 sasa"

Ni maneno ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu ambaye siku ya Jumatano July 10 mwaka huu 2019 amepitishwa na mkutano mkuu wa CCM wa Wilaya hiyo kuwania ubunge wa Singida Mashariki, na hapo alikuwa akijibu ya baadhi ya maswali ya  Albert G. Sengo, mtangazaji wa kipindi cha KAZI NA NGOMA cha Redio Jembe Fm Mwanza, 

Mtaturu alipata kura 396 akifuatiwa na Mugoto Kitima aliyepata kura 79 huku mkuu wa Mkoa wa zamani wa Songwe, Chiku Galawa akipata kura 40. Kura 600 zilipigwa na hakuna hata kura moja iliyoharibika.

BOFYA PLAY kusikia hoja nyingine.

Thursday, July 11, 2019

DC KASESELA ALIAGIZA JESHI LA POLISI IRINGA KUMKATA AYUBU MWENDA POPOTE ALIPO

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpigia simu mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda ambaye anasababisha mgogoro wa shamba la familia ya mzee Mwenda
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa maelezo kwa familia ya marehemu mzee Mwenda katika kata ya Nduli mkoani Iringa.
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda kwa kuika makubaliano ya kuumaliza mgogoro huo.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda ambaye anasababisha mgogoro wa familia ya Mwenda kwa kumkimbia mkuu wa wilaya na kamati yake walipokifika kusuhisha mgogoro huo.

Akizungumza kwenye shamba la familia mzee Mwenda Kasesela alisema kuwa Ayubu Mwenda ameleta dharau kwa kukimbia katika eneo usika la kutatua mgogoro ambao ameusababisha kwa makusudi kwa kutaka kuwadhurumu wanafamilia wenzake.

“Haiwezekani mtu aseme mara yupo mahakamani mara yupo msibani mara anazima simu huu ni utovu wa nidhamu kwa kuwa jana nilikaa nao na tukaongea nao vizuri na yeye akiwepo nay eye ndio chanzo cha mgogoro huo kwanini leo hayupo hapa” alisema Kasesela 

Kasesela alisema kuwa familia hiyo inagombea hekali mia moja na hasini na tisa (159) ambazo waliachiwa na marehemu mzee wao mzee Mwenda na kusema kuwa Ayubu ambaye ndiye kaka yao mkubwa amekuwa kisababishi cha mgogoro huo.

Aidha Kasesela alimtaka afisa mtendaji na afisa tarafa kuhakikisha shamba hilo linagawawiwa kwa wake wote sita wa mzee Mwenda ili kuondo na kumaliza mgogoro huo kwa kugawa kwa usawa na haki ili kila mmoja apate haki yake.

“Mzee Mwenda alikuwa na wake sita hivyo shamba hilo litagawiwa kwa kufuata familia za akina mama wote kwa haki ili kumaliza hili tatizo na hakuna mtu mwingine ataleta mgogoro kwa kuwa nitalipeleka shauri hili mahakamani kuweka zuio la kuanzisha kesi yeyoyte ile katika shamba hilo” alisema Kasesela

Kwa upande wake msimamizi wa mirathi hiyo Sadiki Abdalah Mwenda alimshukuru mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kuasidia kutatua mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi bila kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

Naye askari mstaafu Hawa Mwenda ambaye ni mwanafamilia alimshukuru mkuu wa wilaya na kumuomba awafikishie salaam kwa Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuongoza vizuri na kufanikisha wananchi wanyonge wafikiwe kirahisi na kutatuliwa matatizo yao.

Wednesday, July 10, 2019


BAADA YA DAU NONO HATIMAYE MBWA WA MCHEZAJI WA ZAMANI LIVERPOOL APATIKANA.


TAARIFA ZA AWALI

Mchezaji wa zamani wa Liverpool atangaza dau nono kwa atakayewezesha kupatikana kwa mbwa wake

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge ametoa ofa ya mpaka pauni 30,000 kama zawadi akirejeshewa mbwa wake.

Sturridge,29, ambaye ameondoka Liverpool mwezi uliopita baada ya mkataba wake kuisha amesema mbwa wake huyo aliibiwa baada ya wezi kuvunja nyumban yake jijini Los Angeles Marekani akiwa matembezini.

Mchezaji huyo amepakia video kwenye mtandao wake wa Instagram akionesha jinsi nyumaba yake iliyopo eneo la West Hollywood iivyoharibiwa.

"Tutalipa kiasi chochote kile ili kumpata mbwa wetu," amesema Sturridge.

"Yoyote atakayemrudisha mbwa wangu (atapata) elfu 20, elfu 30 (pauni), kiasi chochote kile."

Sturridge pia ametuma picha nne za mbwa huyo na pia video zinazoonesha wanaaume watatu waliojifunika uso wakiingia kwenye nyumba hiyo.

Amesema tukio hilo limetokea alipokuwa kwenye matembezi Jumatatu usiku.

Sturridge amewaambia wafuasi wake: "Yeyote anayewajua waliovunja nyumba yangu, nitakulipa utakacho. Ninamaanisha nisemacho.

"Nitatoa pesa yeyote ile - haijalishi thamani."

Sturridge, kwa saasa anahusishwa na uhamisho kuelekea klabu ya Aston Villa ambayo inarejea EPL msimu ujao utaoanza Agosti.

WAZIRI MKUU APOKEA PICHA YA RAIS MAGUFULI NCHINI MISRI.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea picha ya Rais Magufuli, iliyochorwa na Binti wa Dereva wa Ubalozi wa Tanzania nchini Misri, Hadeer Mohamed, kwenye mkutano na Watanzania waishiyo nchini Egypt, uliyofanyika katika hoteli ya Almasa, mjini Cairo, Julai 9.2019. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Misri, Meja Jenerali Mstaafu, Issa Suleiman.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa ya ngozi, wakati alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki, kilichopo katika mkoa wa Sharkia, nchini Misri, Julai 9.2019.

WAWEKEZAJI VIWANDA VYA NGOZI WAKARIBISHWA TANZANIA.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Misri ikiwemo kampuni ya Cairo for Investment and Development inayoshughulika na usimamizi wa kiwanda cha ngozi waje kuwekeza nchini Tanzania.

Ametoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki kilichoko katika mkoa wa Sharkianchini Misri, ambapo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji hao waje wawekeze nchini kwani kuna malighafi za kutosha.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi nchini Misri alisema Tanzania ina mifugo mingi hivyo inahitaji wawekezaji watakaojenga viwanda vya kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazo na mifugo hiyo ikiwemo ngozi.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeboresha mazingira ya biashara na ya uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma, hivyo Tanzania ni mahali bora na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kampuni ya Cairo for Investment and Development ya nchini Misri, ambayo inasimamia kiwanda cha ngozi cha Robbiki, Yasser Mohamed Ahmed Al Maghraby alisema kiwanda hicho kinauhitaji mkubwa wa ngozi kutoka Tanzania.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea mradi mkubwa wa mabwawa ya kufugia samaki, mradi wa upanuzi wa awamu ya pili ya mfereji wa suez canal, ambapo aliipongeza Serikali ya Misri kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa kwa kutumia fedha za ndani (Dola bilioni 8.2).

ASASI ZA KIRAIA ZISHIRIKIANE NA SERIKALI MCHAKATO WA BOMBA LA MAFUTA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ameziomba asasi za kiraia kuwa mdau mkubwa kwenye mchakato wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano hasa ujenzi wa bomba la mafuta litokalo  Hoima Uganda hadi Tanga, Tanzania.

Waziri Mhagama alisema hayo kwenye ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu local content katika sekta ya uzinduaji Mikoani  iliyoandaliwa na baraza la uwezeshaji la Taifa na Asasi ya HakiRasilimali inayofanyika Mkoani Shinyanga.

" Tunaziomba asasi za Kiraia zinazofanya kazi katika eneo la mafuta na madini zikiongozwa na HakiRasilimali zitusaidie kwenye kuwaanda watanzania kunufaika na mradi huu wa bomba la mafuta ghafi.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji la Taifa Bibi Beng'i  Mazana Issa alisema kuwa baraza limeanza tayari kuandaa miundombinu ya kufanikisha mradi huo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bibi Zainabu Telack alisema kuwa, Mkoa wa Shinyanga utanufaika zaidi kwenye warsha hiyo kwa kuwa bomba la mafuta litapita Mkoani humu na kutakuwa na kituo kikubwa cha kuongeza kasi ya msukumo wa mafuta katika Wikaya ya Nzega hivyo wadau wasaidiane kwenye kuwajengea uwezo wananchi ili wachangamkie fursa hizo.

Mwenyekiti wa bodi ya HakiRasilimali Bwana Donald Kasongi alisema kuwa, sera ya local content ndiyo nguzo muhimu ya kunufaika na miradi hii ya kimakati na vyema sasa tuikubali kwa kutunga sheria zake mathubuti.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga bwana Gulam Hafeez Mukadam alisema kuwa kufanyika kwa warsha hiyo Shinyanga ni fursha kwao.

Edwin Soko

NGOMA MPYA TOKA CONGO KWA 'MOPAO'.



Koffi Olomide - feat Naza & Keblack - Pi Pi Pi (Clip Officiel)

IGP SIMON SIRRO AKAGUA NYUMBA ZA KISASA ZA MAKAZI YA POLISI SHINYANGA

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini Tanzania Simon Sirro ametembelea na kukagua nyumba 10 za kisasa za makazi ya askari polisi zilizojengwa katika eneo la Kambi ya polisi Kambarage Mjini Shinyanga na kugharimu shilingi milioni 225.

MTANDAO WA 4G WA TIGO KUWANUFAISHA WAKAZI WA KIBAIGWA-DODOMA

Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba (wa tatu kutoka kulia), akishirikiana na Diwani wa Kata ya Kibaigwa, Richard Kapinye, kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa mtandao wa 4G uliozindulliwa jana katika Mji wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma.
Diwani wa Kata ya Kibaigwa Wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma, Richard Kapinye akizungumza wakati wa uzinduzi wa rasmi wa mnara wa 4G wa kampuni ya Tigo katika eneo hilo.
Baadhi ya wakazi wa Mji wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma, walishiriki katika hafla ya uzinduzi wa mnara wa huduma ya 4G ya kampuni ya mawasiliano ya Tigo. ---

 Katika jitihada zake za kuboresha mawasiliano na kurahisisha maisha ya watanzania kupitia teknolojia ya kidigitali, kampuni ya mawasiliano ya Tigo, imezindua mnara wa mawasiliano wa 4G katika mji wa Kibaigwa mkoani Dodoma. 

 Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliohudhuriwa na wakazi wa mji huo, Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Aidan Komba, alisema uboreshaji wa mtandao kutoka 3G kwenda 4G unatarajiwa kufungua fursa mpya za kibiashara ambazo zitakuza maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo. “Kwa kuzingatia kwamba Kibaigwa ina shughuli nyingi muhimu za kiuchumi hususani za kilimo na ufugaji na pia ni kiunganishi muhimu na maeneo mengine ya nchi, sasa ni wakati wa wakazi wa Kibaigwa na vitongoji jirani kutumia Intaneti yenye kasi zaidi ili kuendeleza biashara na shughuli mbalimbali za kiuchumi,” alisema Komba. 

 Uzinduzi huu unaenda sambamba na ofa maalum kwa ajili ya wateja watakaobadili laini zao kwenda mtandao wa 4G. Wateja hawa watazawadiwa kifurushi cha 4GB cha Intaneti ya bure itakayotumika ndani ya siku 7. Vilevile, wateja watakaonunua kifurushi chochote cha intaneti kwenye mitandao uliyoboreshwa kutoka 2G kwenda 3G watazawadiwa MB100 kila wanaponunua kifurushi. 

 Pia kufuatia uzinduzi huu, wateja sasa wataweza kunufaika na huduma mbalimbali za kibunifu kutoka Tigo kama vile “Saizi Yako” ambayo inawapatia wateja ofa mbalimbali za SMS, Intaneti na kupiga simu kulingana na mahitaji na matumizi ya mteja. Kwa mfano mteja anayetumia dakika nyingi zaidi kuliko Intaneti na SMS atapata kifurushi cha dakika za muda wa maongezi. 

Mteja anayetumia zaidi Intaneti kuliko dakika za maongezi na SMS atapata kifurushi cha Intaneti kinachoendana na matumizi yake. Tigo inaendelea kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa hususani 4G+ ili kukidhi mahitaji makubwa ya data na Intaneti yenye kasi kutokana na ongezeko la matumizi ya simu janja za bei nafuu. --

MASAUNI,SIRRO WAWASILI SHINYANGA KWA ZIARA YA KIKAZI

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Terack (katikati), baada ya kuwasili mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi.kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Terack, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Masauni amewasili mkoani Shinyanga leo kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana  na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Terack  baada ya kuwasili mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Tuesday, July 9, 2019

DC KASESELA MAJANGIRI HAWANA NAFASI KUFANYA UHARIFU KWENYE MBUGA ZA WILAYA YA IRINGA.

 Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti majangili wote na akiwa ameshika silaha bora ambazo wanazitumia walinzi wa hifadhi Village Game Scouts ambao wanafadhiliwa na shirika la STEPS
 Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela akiwa pamoja na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Hashimu Komba  wakiwa kwenye picha moja na viongozi na walinzi wa hifadhi Village Game Scouts
MKUU wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti majangili wote ambao wamekuwa wakifanya uharifu kwenye maliasili na misitu iliyopo katika wilaya hiyo.

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MKUU wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti majangili wote ambao wamekuwa wakifanya uharifu kwenye maliasili na misitu iliyopo katika wilaya hiyo.

Akizungumza wakati alipofanya ziara ya ghafla ya kuwatembelea na kuwapa moyo walinzi wa hifadhi Village Game Scouts ambao wanafadhiliwa na shirika la STEPS  kwa kazi kubwa wanayofanya ya kulinda maliasili zilizopo katika wilaya hiyo.

“Mimi niwapongeze sana maana mnafanyakazi kubwa sana kupambana na majangili huko porini jambo ambalo mnapaswa kupongezwa kwa namna yoyote ile” alisema Kasesela
  
Kasesela alisema kuwa hifadhi hizo zimekuwa zikivamiwa na majangili hasa pembezoni mwa hifadhi hizo kutokana na kuwa jirani na wakazi ambao wamekuwa wakifanya uharifu huo kutokana na tamaa zao.

Kasesela aliwaonya majangili kwamba sasa wasirogwe kuingia kwenye mbuga za wanyama kutaka kufanya ujangili wa aina yoyote kwakuwa wanamifumo ya kisasa zikiwemo kamera zimefungwa kwenye maeneo ya mbuga hizo.

“Yoyote atakaye kamatwa kwa ujangili atafikishwa kwenye vyombo husika na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa atakuwa amefanya uharifu ambao haukubariki kisheria” alisema Kasesela

Aidha Kasesela  alilipongeza shirika la STEPS kwa kuwafadhili walinzi wa hifadhi Village Game Scouts kwa kuwapa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kazi hiyo ya ulinzi kwenye mbuga zilizopo katika wilaya ya Iringa.

ZURA YATOA BEI MPYA ZA MAFUTA YA SASA.



Na Thabit Hamidu,Zanzibar.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) imefanya mabadiliko ya bei za mafuta ambazo zitaanza kutumika rasmi kuanzia Tarehe 10/07/2019.

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ZURA Khuzaimat Bakari kwa waandishi wa habari, Amsema kuwa bei za mafuta kwa mwezi wa Julai zimeshuka kutokana na kushuka kwa bei za bidhaa katika soko la dunia, gharama za usafirishaji pamoja na bima.

Amesema kuwa bei mpya ya mafuta ya Petroli sh.2,338 ambayo sawa na asilimia 1.59%, mafuta ya dizeli yatauzwa kwa bei sh.2,319 sawa na asilimia 0.42%.

Aidha amesema kuwa bei mpya ya mafuta ya taa ni sh.1,753 sawa na asilimia 0.075% na mafuta ya Banka yameshuka na itakuwa ni sh.2.145 sawa na asilimia 0.46%.

Hata hivyo Khuzaimat amesema kuwa bei hiyo ni halali ambazo zitaanza kutumika hapo kesho.

UWT MANISPAA YA IRINGA WANAWAKE KOPENI KWA MALENGO


 Mwenyekiti wa umoja wa wanawake manispaa ya Iringa (UWT) Ashura Jongo akizungumza wakati wa baraza la UWT manispaa ya Iringa akiwaasa wanawake kukopa kwa malengo
Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya akitoa neno kwa wanawake wa UWT manispaa ya Iringa. 
 

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Kukosekana kwa elimu ya matumizi bora ya mikopo kwa wanawake kumetajwa kuwa sababu ya wanawake wengi wa manispaa ya Iringa kushindwa kurudisha mikopo katika taasisi za kifedha.

Akizungumza kwenye baraza la UWT manispaa ya Iringa,mwenyekiti wa umoja huo Ashura Jongo  amesema kuwa wananwake wamekuwa wanakopa bila ya kuwa na elimu ndio maana wanashindwa kurejesha mikopo ambayo wamekopa kwenye taasisi za kifedha.

“Changamoto za wanawake kutokuaminika katika vyombo au taasisi za kifedha ni kutokana na hali ngumu,wanawake wanaweza wakakopa wakiwa na malengo lakini wakirudi nyumbani wanakutana na matatizo mengi yanahitaji matumizi ya fedha” aliema Jongo

Jongo alisema kuwa wanawake wanatakiwa kuendelea kuwawezesha kwa kuwa wanauwezo wa kutmia vizuri fedha ambazo zinapatikana hivyo ukimuwezesha mwanamke umewawezesha watu wengi kwa kuwa wanawake ndio nguzo ya familia hasa kwenye maswala ya kiuchumi.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi Rose Tweve amezitaka taasisi za kifedha kutoa elimu kwa wakopaji ili waweze kuzitumia vizuri fedha hizo.
“Shida moja wapo ya wanawake kushindwa kurudisha mikopo ni kutokana na kutokuwa naelimu ya matumizi ya fedha kwa kuwa pesa hiyo inahitaji nidhamu na matumizi bora ya fedha hizo za mikopo” alisema Tweve

Tweve alisema kuwa tasisi za kifedha zinatakiwa kutoa elimu kwanza kabla ya kutoa mikopo kwa wanawake ili waweze kuzirejesha kwa wakati kwa kuwa tayari ameshapata elimu ya matuzi bora ya mikopo waliyokopa.

“Pale wanapokopa lazima wajue matumizi ya hizo pesa la sivyo watazitumia bila nidhamu fedha hizo na kushindwa kuzirejesha na kujikuta wakiwa matatani kutokana na kushindwa kulipa mkopo huo” alisema Tweve

Naye mgeni rasmi kwenye baraza hilo mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya amewataka wanawake kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ili kufikia malengo waliyojiwekea kabla ya kwenda kukopa.

“Kwa kwali wanawake wa CCM manispaa ya Iringa wengi mnakopa mikopo lakini hamrejeshi kwa wakati na hili ni bomu kubwa kwa chama hivyo mnatakiwa kuwa na nidhamu ya matumizi ya mikopo hiyo” alisema Rubeya