Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela akimpigia simu mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda ambaye anasababisha mgogoro wa shamba la familia ya mzee Mwenda
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela akitoa maelezo kwa familia ya marehemu mzee Mwenda katika kata ya Nduli mkoani Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha
anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda kwa kuika makubaliano ya kuumaliza mgogoro huo.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela amemuagiza mkuu wa polisi wilaya ya Iringa (OCD) kuhakikisha
anamkamata popote alipo Ayubu Mwenda ambaye anasababisha mgogoro wa familia ya
Mwenda kwa kumkimbia mkuu wa wilaya na kamati yake walipokifika kusuhisha mgogoro
huo.
Akizungumza kwenye shamba la
familia mzee Mwenda Kasesela alisema kuwa Ayubu Mwenda ameleta dharau kwa
kukimbia katika eneo usika la kutatua mgogoro ambao ameusababisha kwa makusudi
kwa kutaka kuwadhurumu wanafamilia wenzake.
“Haiwezekani mtu aseme mara
yupo mahakamani mara yupo msibani mara anazima simu huu ni utovu wa nidhamu kwa
kuwa jana nilikaa nao na tukaongea nao vizuri na yeye akiwepo nay eye ndio
chanzo cha mgogoro huo kwanini leo hayupo hapa” alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa familia
hiyo inagombea hekali mia moja na hasini na tisa (159) ambazo waliachiwa na
marehemu mzee wao mzee Mwenda na kusema kuwa Ayubu ambaye ndiye kaka yao mkubwa
amekuwa kisababishi cha mgogoro huo.
Aidha Kasesela alimtaka afisa
mtendaji na afisa tarafa kuhakikisha shamba hilo linagawawiwa kwa wake wote
sita wa mzee Mwenda ili kuondo na kumaliza mgogoro huo kwa kugawa kwa usawa na
haki ili kila mmoja apate haki yake.
“Mzee Mwenda alikuwa na wake
sita hivyo shamba hilo litagawiwa kwa kufuata familia za akina mama wote kwa
haki ili kumaliza hili tatizo na hakuna mtu mwingine ataleta mgogoro kwa kuwa
nitalipeleka shauri hili mahakamani kuweka zuio la kuanzisha kesi yeyoyte ile
katika shamba hilo” alisema Kasesela
Kwa upande wake msimamizi wa mirathi
hiyo Sadiki Abdalah Mwenda alimshukuru mkuu wa wilaya ya Iringa Richard
Kasesela kwa kuasidia kutatua mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi bila
kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.
Naye askari mstaafu Hawa Mwenda
ambaye ni mwanafamilia alimshukuru mkuu wa wilaya na kumuomba awafikishie
salaam kwa Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuongoza vizuri na kufanikisha
wananchi wanyonge wafikiwe kirahisi na kutatuliwa matatizo yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.