ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 8, 2022

WATEMI SHINYANGA WASISIMUA TAMASHA LA BUSIYA SABA SABA WANADI KISWAHILI - VIDEO

 Maelfu ya Watu wakusanyika Tamasha la Sanjo ya Busiya (7SabaFEST) Ikiwa ni kilele cha siku ya kiswahili Duniani pamoja Kilele cha sherehe za sanjo ya Busiya wilayani kishapu mkoani shinyanga ,Ntemi wa Busiya Edward Makwaia ametumia Tamasha hilo kuwataka watanzania kutunza na kuenzi Kiswahili, kwani ni Lugha ya Taifa pia ni alama muhimu inayotambulisha utamaduni wa mtanzania.

Pia nao msisitizo wa SENSA ukatolewa.

HUYU HAPA MTAALAMU WA COCTAIL.

 


𝐓𝐮𝐧𝐚𝐢𝐚𝐧𝐳𝐚 𝐰𝐞𝐞𝐤𝐞𝐧𝐝 𝐧𝐝𝐚𝐧𝐢 𝐲𝐚 #𝐝𝐫𝐢𝐯𝐞𝐦𝐢𝐱 𝐧𝐚 @𝐦𝐫𝐟𝐥𝐚𝐯𝐨𝐫𝐬𝐭𝐳 𝐦𝐭𝐚𝐚𝐥𝐚𝐦𝐮 𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐜𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐜𝐨𝐜𝐤𝐭𝐚𝐢𝐥 🍹𝐯𝐢𝐩𝐢 𝐮𝐧𝐚𝐡𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐤𝐮𝐟𝐚𝐡𝐚𝐦𝐮 𝐍𝐢𝐧𝐢 𝐤𝐮𝐡𝐮𝐬𝐢𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐜𝐨𝐜𝐤𝐭𝐚𝐢𝐥? 🤷‍♂️

𝐔𝐧𝐠𝐚𝐧𝐚 𝐧𝐚 𝐭𝐢𝐦𝐮 𝐃𝐑𝐈𝐕𝐄 𝐌𝐈𝐗 @𝐠𝐬𝐞𝐧𝐠𝐨𝐭𝐯 & @𝐦𝐜_𝐬𝐮𝐳𝐮𝐤𝐢 

.

.

.#𝐝𝐫𝐢𝐯𝐞𝐦𝐢𝐱

#𝐣𝐮𝐥𝐲

#𝐥𝐞𝐭𝐞𝐧𝐨𝐧𝐝𝐨

#𝐣𝐞𝐦𝐛𝐞𝐟𝐦𝐭𝐳

WATEMI SHINYANGA WASISIMUA TAMASHA LA BUSIYA SABA SABA KUNADI LUGHA YA KISWAHILI

Kamisaa wa Sensa Taifa Anna makinda Amezindua Tamasha la Utamaduni La Sanjo ya Busiya(7SabaFEST) wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.. Makinda ametumia Tamasha hilo kuhamasisha wakazi wa mkoani Shinyanga kujitokeza kuhesabiwa Itakapofika August 23 ili Serikali iweze kujua idadi ya watu wake na kusaidia kuleta maendeleo..

Tamasha la Sanjo ya Busiya hufanyika kila mwaka na kilele chake ni Tarehe 07/07/2022 na kauli mbiu ya Mwaka huu "Watu wote wahesabiwe Tuwe na Takwimu sahihi kwa maendeleo Yetu'

Maelfu ya Watu wakusanyika Tamasha la Sanjo ya Busiya (7SabaFEST) Ikiwa ni kilele cha siku ya kiswahili Duniani pamoja Kilele cha sherehe za sanjo ya Busiya wilayani kishapu mkoani shinyanga  ,Ntemi wa Busiya Edward Makwaia ametumia Tamasha hilo kuwataka watanzania kukitunza na kukienzi kiswahili kwani ni Lugha ya taifa  pia ni alama muhimu inayotambulisha utamaduni wa mtanzania.
Salaam salaam.
Tuzo na medali za Rais samia Suluhu zatolewa kwa washindi wa Tamasha la utamaduni kitaifai kutoka Utemi wa Busiya Shinyanga.
Tuzo na medali za Rais samia Suluhu zatolewa kwa washindi wa Tamasha la utamaduni kitaifai kutoka Utemi wa Busiya Shinyanga.
Washiriki wa shindano la mavazi asili.
Ntemi wa Busiya Edward Makwaia.
Ngoma imebamba.
Tamasha limenoga.
Dawa asili nazo zilikuwepo tamashani.
Ntemi wa Busiya Edward Makwaia akipata maelezo kutoka kwa waratibu.
Piza za juu kwa juu.
Kusanyiko likifuatilia yanayojiri tamashani.
Ze engo.
Maelfu ya Watu wakusanyika Tamasha la Sanjo ya Busiya (7SabaFEST) Ikiwa ni kilele cha siku ya kiswahili Duniani pamoja Kilele cha sherehe za sanjo ya Busiya wilayani kishapu mkoani shinyanga  ,Ntemi wa Busiya Edward Makwaia ametumia Tamasha hilo kuwataka watanzania kukitunza na kukienzi kiswahili kwani ni Lugha ya taifa  pia ni alama muhimu inayotambulisha utamaduni wa mtanzania.
 

BEI YA MAFUTA YA KULA YAANZA KUSHUKA.

 

CHANZO MWANANCHI

Baada ya machungu ya takriban mwaka mzima ya kupanda kwa bei ya mafuta ya kula nchini, nafuu imeanza kuonekana katika maeneo mbalimbali kwa bidhaa hiyo kuanza kushuka.


Bei zilianza kupanda hata kabla ya kuanza kwa vita ya Ukraine na Urusi Februari mwaka huu kwa dumu la lita 20 kufikia Sh120,000 hadi Sh130,000 kutoka wastani wa Sh55,000 hadi Sh75,000.


Kwa bei za rejareja lita moja ilifikia kati ya Sh8,000 hadi Sh9,000 kutoka Sh5,500 na baadhi ya maeneo yalipanda kutoka Sh6,500.


Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi maeneo mbalimbali umebaini bei ya mafuta imeanza kushuka na kwingine hali ikiendelea kubaki vilevile.


Godfrey James, mfanyabiashara wa duka la rejareja Kinondoni, Dar es Salaam alisema dumu la lita 20 walilokuwa wakinunua Sh115,000 hadi Sh120,000, sasa wananunua kwa Sh92,000 hadi Sh94,000. Alisema lita moja waliyokuwa wakiuza Sh6,500 sasa wanauza Sh5,500 huku Bryan Wambura, mkazi wa Chanika anayeuza kwa bei ya jumla alisema sasa dumu la lita 20 bei yake ni Sh110,000 hadi Sh100,000 kutoka Sh120,000 hadi 130,000 ya awali.


Baby Omar, mkazi wa Buguruni alisema ndoo ndogo iliyokuwa ikiuzwa Sh68,000 mpaka Sh.70,000 sasa inauzwa hadi Sh65,000.


“Hali inaanza kurejea, kwani bidhaa hii ilipanda sana hadi wengine tuliacha kuuza kwa sababu wateja walikuwa hawatuelewi,” alisema Baby.


Vita ya Ukraine imeathiri upandaji wa bei za bidhaa hii kwa sababu kwa mujibu wa ripoti ya Sampuli ya Sensa ya Kitaifa ya Kilimo ya 2019/20 inayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ilionyesha Tanzania ina uwezo wa kuzalisha mafuta yenye kukidhi asilimia 45 ya mahitaji ya mafuta nchini na kiasi kinachobaki huagizwa nje ya nchi.


Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe alisema bei hizo zinashuka kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo jitihada za Serikali kuhamasisha hata wenye viwanda vidogovidogo waongeze uzalishaji.


Alisema katika bajeti hii, Serikali imepunguza hadi asilimia sifuri ya mafuta ghafi ya kupikia kutoka nje, ili kuwawezesha kuyachakata na kuyauza kwa bei nafuu.


Jijini Mwanza, mfanyabishara Peter Maduhu alisema bei ya mafuta ya kula ya alizeti haijapanda wala kushuka na yanaendelea kuuzwa Sh7,000 hadi Sh8,0 00 kwa lita.


Naye, mfanyabishara mkoani Tabora, Jumanne Isack alisema hakuna mabadiliko katika bei ya mafuta huku akisema lita moja ya mafuta ya alizeti inauzwa Sh8,000 na lita tano kati ya Sh32,000 hadi Sh35,000.


Jijini Mbeya bei ya mafuta ya kula katika baadhi ya maeneo imeshuka kutoka Sh7,000 mpaka 5,000 na mama lishe alisema kwa sasa bei ya vyakula imeshuka kutoka Sh 2,500 kwa sahani mpaka Sh2,000 na Sh1,500.


Kwa Kilimanjaro, mfanyabiashara na mzalishaji, Mary Mosha alisema mafuta ya alizeti yamepanda bei kutoka Sh5,500 na sasa yanauzwa Sh6,500 mpaka Sh7,000.


I­­meandikwa na Nasra Abdallah (Dar), Mgongo Kaitira (Mwanza), Hawa Mathias (Mbeya), Ombeni Daniel (Moshi) na Robert Kakwesi (Tabora).

WIMBO HUU UNAKUHUSU...

 Aniset Butati-NENDA [ Official video ]

Thursday, July 7, 2022

NMB YAJA NA MWAROBAINI KWA WEZI WA FEDHA ZA WAFANYABIASHARA BUHONGWA.

 WAKAZI wa kata ya Buhongwa walilazimika kusafiri na fedha umbali mrefu hadi kuzifikia benki mbalimbali ambapo mara kadhaa walikutana na madhira ya uvamizi na kuporwa fedha zao na vibaka au wezi, lakini sasa wanayofursa kupata huduma za kifedha toka tawi lao jipya lililo funguliwa katani humo.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Sauda Msemo akihutubia katika uzinduzi wa tawi la NMB Buhongwa jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi.
Meya wa jiji la Mwanza Sima Costantine.
Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Binafsi NMB Filbert Mponzi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Buhongwa wakipoka moja ya mabati 262 kutoka NMB kwa ajili ya Shule yao, mbele ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Sauda Msemo (aliyefungu ushungi), wakati wa uzinduzi wa tawi la NMB Buhongwa jijini Mwanza.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Sauda Msemo (katikati) akikata utepe ili kuzindua tawi la NMB Buhongwa jijini Mwanza, wa tatu kutoka kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Binafsi NMB Filbert Mponzi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (wa tatu kushoto),Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (wa pili kushoto),Meya wa jiji la Mwanza Sima Costantine (wa pili kulia) na Meneja wa NMB kanda ya Ziwa Baraka Ladslaus (kulia) wakishuhudia.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Sauda Msemo (katikati) akikata utepe ili kuzindua tawi la NMB Buhongwa jijini Mwanza, wa tatu kutoka kulia ni Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Binafsi NMB Filbert Mponzi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi (wa tatu kushoto),Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (wa pili kushoto),Meya wa jiji la Mwanza Sima Costantine (wa pili kulia) na Meneja wa NMB kanda ya Ziwa Baraka Ladslaus wakishuhudia.
Picha ya pamoja wadau wa meza kuu na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Sauda Msemo.

DC TANGA ALITAKA SHIRIKA LA WORLD VISION KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA WALIOSHINDANISHWA KWENYE INSHA

 

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akigawa zawadi na vyeti kwa washindi ya Insha wakati wa kilele cha sherehe za uandishi wa Insha kwa shule za Msingi mkoa wa Tanga iliyohusisha wilaya nne za mkoa wa Tanga iliyandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania iliyoambatana na utoaji wa zawadi kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Jinsia na Uchchemuaji Makao Makuu Shirika la World Vision Tanzania Esther Mongi
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akigawa zawadi na vyeti kwa washindi ya Insha wakati wa kilele cha sherehe za uandishi wa Insha kwa shule za Msingi mkoa wa Tanga iliyohusisha wilaya nne za mkoa wa Tanga iliyandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania iliyoambatana na utoaji wa zawadi kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Jinsia na Uchchemuaji Makao Makuu Shirika la World Vision Tanzania Esther Mongi
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akigawa zawadi na vyeti kwa washindi ya Insha wakati wa kilele cha sherehe za uandishi wa Insha kwa shule za Msingi mkoa wa Tanga iliyohusisha wilaya nne za mkoa wa Tanga iliyandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania iliyoambatana na utoaji wa zawadi kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Jinsia na Uchchemuaji Makao Makuu Shirika la World Vision Tanzania Esther Mongi
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa aliyevaa suti katika akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Insha wakiwa wamebeba zawadi zao na vyeti wakiwa na watumishi wa Shirika la World Vision

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa aliyevaa suti katika akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Insha wakiwa wamebeba zawadi zao na vyeti wakiwa na watumishi wa Shirika la World Vision

 

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

MKUU wa wilaya ya Tanga mkoani Tanga Hashimu Mgandiliwa amelitaka Shirika la World Vision kuhakikisha linaendelea kuwajengea uwezo mkubwa vijana walioshindanishwa kwenye usomaji wa Insha na uandishi wa Ishana kuibuka washindi ili kuwaendeleza vipawa mungu alivyowajalia ili kufika mbali zaidi kimaendeleo.

Mgandilwa aliyasema hayo wakati wa kilele cha sherehe za uandishi wa Insha kwa shule za Msingi mkoa wa Tanga iliyohusisha wilaya nne za mkoa wa Tanga iliyandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania iliyoambatana na utoaji wa zawadi

Alisema vipaji ambavyo vimepatikana visiishie hapo bali viendelezwe ili viweze kufika mbali ikiwemo kuhakikisha fedha wanazowapa wazazi zisaidie kuwaendeleza kimasomo na kununua mahitaji ya shule.

Alisema Shirika hili limelenga kusaidia jamii na kusaidia kutimiza ndoto za watoto kusoma vizuri basi ni vyema kujikita zaidi katika kuibua vipawa na kuviendeleza katika masomo yao ili kufikia ndoto zao na kujikwamua kiuchumi endapo watahakikisha wanapata elimu bora itakayowasaidia kufika hadi vyuo vikuu na kupata wandishi wazuri wa Insha.

Aidha aliwataka watoto waliopata zawadi baada ya kuibuka washindi wa Uwandishi wa Insha kwamba wazingatie vigezo kabla ya kuhariri kazi zao wazingatie kuwashindanisha walichokiandika wenyewe badala ya kubadilisha maana na uhalisia wa mtoto ili kuweza kufanikiwa kupata washindi halisi badala ya kubadilisha maana na mantiki ya Insha yake.

“Kubadilisha maana ya uhalisia wa maana ya Insha kunaweza kusababisha mtoto kushindwa kufanya mwenyewe vizuri na kukosa kujiamini wakati wa kuwasilisha alichokiandika mwenyewe hivyo zingatieni hilo ili kuweza kupata vipawa vingi katika maeneo tofauti kwenye Halmashauri zetu.

Pia alisema watoto hao wanatakiwa kuhakikishiwa wanasoma vizuri na kuwekeza nguvu katika kusaidia familia zao kwani wengine wanatoka katika familia duni na kushindwa kutimiza malengo yao hivyo ni vyema kuliona hilo nalo ili kuhakikisha wanafika mbali zaidi na kupata wandishi wazuri kama watajengewa misingi imara kutokea wakiwa wadogo hadi kufika chuo kikuu.

Alisema Shirika linauwezo wakuwasomesha watoto hao hadi kufika vyuo vikuu nivyema kuhakikisha wanaunga nguvu ya pamoja katika kukuza vipawa hivyo alivyovitunuku vyeti vya sifa katika viwanja hivi vya Usagara.

Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa Kitengo cha Jinsia na Uchchemuaji Makao Makuu Shirika la World Vision Tanzania Esther Mongi alisema wao kama shirika wameanzisha kampeni hiyo tokea mwaka 2017 ya kupinga mimba za utotoni.

Alisema lakini baada ya kutekeleza kampeni hiyo wakaona hapana mimba pekee haitoshi changamoto iliyopo kwenye jamii kuna mimba na ndoa za utotoni hivi sasa wana kampeni yao jukumu lao sote kupinga mimba za utotoni na ndoa na mwaka huu wamekuja na zoezi la uandiskiha wa insha kwa mikoa 12 Tanzania.

Aidha alisema wapo mkoani Tanga kutoa zawadi kwa washindi wa ngazi ya wilaya za mkoa na wamepata washindi watatu ngazi ya wilaya kwenye wilaya tatu na katika mkoa wa Tanga leo washindi watatu baada ya hapo mshindi wa kwanza katarasi yake itapelekwa Tamisemi Dodoma ili kupata mshindi wa kwanza na pili na tatu.

,Sisi kama Shirika la World Vision tunaamini kabisa ni jukumu lao wote kupinga mimba za utoto na ndoa iwe mzazi,mlezi, kiongozi wa dini na serikali kupitia insha tumewajenga uwezo watoto wameweza kuwa na ujasiri kusoma insha zao mbele ya wenzao”Alisema

Hata hivyo alisema kupitia zoezi na insha wamefikia shule 544 na kwa mkoa wa Tanga wamezifikia shule 72 hivyo wanaamini kwenye mikoa iliyopita wamefanya kazi kwa karibu na waandishi na elimu hiyo itasamba na wanaamini washindi watakuwa mabalozi wazuri.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza ngazi ya wilaya alipata 300,000 na cheti pamoja na baiskeli,mshindi wa pili 200,000,cheti na baiskeli,mshindi wa tatu 100,000 cheti na baiskeli ili kuweza kuwasaidia katika masomo yao.

Hata hivyo washindi kwenye ngazi ya mkoa,mshindi wa kwanza kutoka wilayaani Korogwe Sarah Juma Mussa alipata 500,000 na cheti,mshindi wa pili 400,000 na cheti huku mshindi akipata 350,000 na cheti.

Wednesday, July 6, 2022

MBUNGE AWESO AMSHUKURU RAIS SAMIA ASEMA NI SULUHU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

 

MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Waziri wa Maji akisisitiza jambo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara ya Tanga -Pangani Saadani kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly na kushoto aliyevaa miwani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani Isaya Mbenje


MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Waziri wa Maji akisisitiza jambo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa barabara ya Tanga -Pangani Saadani kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly na kushoto aliyevaa miwani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani Isaya Mbenje
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) Mhandisi Zuhuru Amani  akisoma taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Mbunge wa Jimbo la Pangani kulia ambaye pia ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
Mbunge wa Pangani (CCM) na Waziri wa Maji Jumaa Aweso wa pili kutoka kushoto akikagua  ujenzi wa barabara ya Tanga -Pangani wakati wa ziara yake leo kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri  na Katibu wa Waziri Gibson George
Sehemu ya ujenzi wa barabara hiyo ukiendelea
Mbunge wa Pangani (CCM) na Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika akitembelea ujenzi huo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Hassan Nyange kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo


NA OSCAR ASSENGA, PANGANI.

MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kufanikisha ujenzi wa Barabara ya kutoka Tanga-Pangani –Saadan huku akieleza kwamba utawala wake umekuwa ni suluhu ya matatizo ya watanzania na wana Pangani .

Amesema ujenzi wa barabara hiyo utakapokamilika utalifungua jimbo hilo kiuchumi na hivyo kusaidia wananchi kuweza kunufaika na fursa mbalimbali za kimaendeleo kutokana na uwepo wake.

Aweso ambaye pia ni Waziri wa Maji aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua na kutembelea ujenzi wa barabara ya Tanga –Pangani-Bagamoyo kwa kiwango cha lami lenye kilomita 256.

Huku akiridhishwa na kasi ya utekelezaji wake unavyokwenda huku akiwahaidi ushirikiano wakandarasi wanaotekeleza mradi huo ili kuhakikisha ujenzi huo unakwenda kama ulivyopangwa.

Alisema kwa sababu wilaya ya Pangani walikuwa na na changamoto ya barabara na wapo ambao walikuwa hawaamini kwamba ujenzi huo utafanyia lakini leo ujenzi unaendelea.

“Wapo ambao walikuwa hawaamini kwamba ujenzi wa barabara hii utajengwa lakini leo hii hapa inajengwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu tunamshukuru sana kwa hili kubwa alilotufanyia sisi wana Pangani”Alisema Mbunge Aweso.

Aidha aliwataka wana Pangani wachangamkie fursa za ujenzi wa mradi huo wa barabara kwa kuongeza uzalishaji zaidi kwa kutumia ardhi iliyopo kwa ajili ya kilimo ikiwemo kuwataka kuacha kuuza maeneo yao kiholela,

“Niwaombeni ndugu zangu sasa ujenzi huu unafanyika hii ni fursa na maendeleo kwa sababu itafungua fursa za kiuchumi hivyo niwasihi acheni kuuza ardhi kiholela holela kwa kuhakikisha mnayasimamia kutokana na fursa za kiuchumi zitafunguka wakati ujenzi huu utakapokamilika na kuweza kupata maendeleo”Alisema

Alisema kwa sababu ujenzi wa barabara hiyo unakwenda kuitoa Pangani pangoni na kuiinua kiuchumi na hivyo kufungua fursa za kimaendeleo hivyo wananchi hakikisheni mnaongeza uzalishaji.

“Niliwahi kupiga magoti hapa kuomba barabara hii lakini naishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia kwa kutufuta machozi wana Pangani kwa kuliona hili na utekelezaji wa mradi huu kwa sasa unaendelea na kubwa zaidi unakwenda pamoja”Alisema

“Nimeanza kukagua eneo la Choba nimeridhika sana na utekelezaji wake nifikisheni salamu za pongezi kwa Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa na Watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) kwa kuwapata wakandarasi wazuri wanafanya kazi vizuri”Alisema

Aliongeza yeye kama mbunge wa Jimbo la Pangani aliwahaidi wakandarasi hao kwamba watawapa ushirikiano kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati huku akiwaeleza kwamba changamoto ambazo aliwaeleza atakwenda kukutana na Waziri wa Ujenzi kuona namna ya kuzipatia suluhu”alisema

Hata hivyo aliwapongeza Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) mkoa wa Tanga kutokana na kwamba wanafanya kazi nzuri hasa juu ya usimamizi na ufuatiliaji wa mradi huu.

“Rais Samia ni Rais wa nchi nzima lakini ametambua kiu ya wananchi wa Pangani miaka ya nyuma ukitaka kwenda Pangani kutoka Tanga unacheza kiduku mpaka unafika Pangani kutokana na miundombinu mibovu ya barabara lakini ujenzi huo utaondosha changamoto hizo”Alisema.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) Mhandisi Zuhuru Amani alisema ujenzi wa barabara ya Tanga –Pangani kilomita 50 uligharimu kiasi cha Sh. bilioni 66.853 ambayo ilikuwa ni gharama za awali lakini imeongezeka na sasa kuwa Bilioni 67.458 kutokana na mabadiliko ya usanifu,

Mradi huu ulipangwa kukamilika Novemba 14 mwaka 2021 lakini kutokana na sababu mbalimbali za kimkataba mufa wa kukamilika kwa mradi huo umeongezwa hadi Desemba 5,2022 na kazi hiyo inafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100.

Alisema mradi huo mwanzoni ulikuwa ukisimamiwa na Mhandisi Mshauri M/S TECU (TANROADS Engineering Consulting Unit) hadi Desemba 5 mwaka 2020 na kwa sasa unasimamiwa na Mhandisi Mshauri M/S Dotch LTD ya Tanzania kwa gharama ya Sh.Bilioni 2.246 na utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimai 42.3 na hadi sasa mkandarasi amelipwa hati nne za madai zenye jumla ya Sh.Milioni 8,

Alisema awamu ya pili ya mradi huo ni ujenzi wa daraja la Mto Pangani lenye urefu wa mita 525 utahusisha ujenzi wa barabara ya maungio ya daraja yenye kilomita 14.3,barabara ya mchepuko ya kwenda ushongo kilomita 5.9 na barabara za Pangani mjini zenye urefu wa kilomita 5.4.

Mhandisi Zuhura alisema mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkataba umesainiwa kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroad) na Mkandarasi M/s Shandong Luqiao Group Co.Ltd kutoka Chini Mei 5 mwaka huu kwa gharama zaidi Sh. Bilioni 82 kwa muda wa miezi 36 ya ujenzi na miezi 36 ya kipindi cha uangalizi kwa upande wa daraja ni miezi 12 kwa upande wa barabara.

Hata hivyo alisema kwa upande wa barabara ya Tungamaa –Mkwaja-Mkange kwa kiwango cha Lami (Km 95.2) ikijumuisha na barabara ya mchepuko ya Kipumbwi yenye kilomita 3.7 unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mradi huo ulishasainiwa na mtendaji mkuu wa wakala wa barabara nchini.

Alisema na mkandarasi M/s China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G) kutoka china kwa gharama za zaidi ya Sh.Bilioni 94 na kwa sasa muda wa miezi 36 ya ujnzi na miezi 12 ya kipindi cha uangalizi na kazi ya ujenzi imeanza Aprili Mosi mwaka huu na inatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 31 2025 na zaidi ya Bilioni 14 zimelipwa kwa mkandarasi na mpaka sasa ikiwa ni malipo ya awali ya Mhandisi Mshauri kuidhinisha malipo hayo na utekelezaji wake umefikia asilimia 5.1.

NIGERIA : WASHUKIWA WA BOKO HARAM WATOWEKA BAADA YA JELA KUVAMIWA.

 


Mamlaka nchini Nigeria, zimesema washukiwa wa kundi la kijihadi la Boko Haram, wametoweka katika gereza  la Kuje, jijini Abuja, baada  ya watu wenye silaha kuvamia gereza hilo, usiku wa kuamkia leo.

Hata hivyo mamlaka nchini humo hazijasema idadi wa washukiwa waliotoweka wakati wa uvamizi huo, ambao jeshi la Nigeria limesema lilifanikiwa kuuthibiti.

Kwa miaka ya hivi karibuni makundi ya kijadi yamekuwa yakivaimia magereza nchini Nigeria, zaidi ya wafungwa 5,000 wakifakiwa kutoroka tangu mwaka 2020.

Tukio hili limejiri muda mfupi baada ya watu wenye silaha kushambulia msafara wa rais Muhammadu Buhari, kaskazini mwa taifa hilo.

POLISI NIGERIA WAANZISHA MSAKO KWA MAPADRI WALIOTEKWA.

 


Polisi nchini Nigeria wameanzisha msako kuwatafuta mapadri wawili wa kanisa katoliki waliotekwa mwishono mwa juma, katika jimbo la Edo.

Mapadri hao Udo Peter na Philemon Oboh, walitekwa na watu wenye silaha katika barabra kuu ya Benin- Auchi.

Kisa hiki kinajiri siku chache baada ya watu wenye silaha kumteka na kumuua padri mwingine Christopher Odia, karibu na mji wa Auchi.

Katika hatua nyingine mamlaka katika jimbo la Zamfara, kuko huko nchini Nigeria zimesajili vijana 9, 000, ambao wamejukumiwa kulinda jamii na kupambana na majambazi.

Mwishoni mwa mwezi uliopita gavana wa zamfara, Bello Muhammad, aliwataka raia kununua silaha ili kujilinda dhidi ya uvamizi wa makundi ya watu wenye silaha.

AFRIKA KUSINI : MAZIKO YA VIJANA 21 WALIOFARIKI NDANI YA KLABU KUFANYIKA LEO.

 

Ibada ya pamoja ya maziko ya vijana 21, waliofariki katika mazingira tatanishi kwenye klabu moja nchini Africa kusini, inafanyika leo.

Ibada  ya vijana hao wanaodaiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 13-17, inafanyika katika bustan ya Scenery, mashariki mwa jiji la London.

Rais wa Africa Kusini ,Cyril Ramaphosa, maafisa wa serikali na mafariki ni baadhi ya wageni 3,000 wanaotarajiwa kuhudhuria mazishi ya leo.

Hakuna taarifa rasmi ambayo imetolewa kuhusiana na chanzo kamili cha vifo vya vijana hao wanaodaiwa kufariki wakati wakisherekea kumalizika kwa mitihani yao.

Hata hivyo uchuguzi wa awali umebaini kuwa huenda vijana hao walivuta hewa yenye sumu.

Tuesday, July 5, 2022

WANAFUNZI 10 BORA MASOMO YA SAYANSI KIDATO CHA SITA 2022 HAWA HAPA.

matokepoiicc 

Kaimu Katibu wa Baraza Hilo, Athuman Amas amemtaja Catherine Alphonce Mwakasege kutoka shule ya St.Mary's Mazinde Juu kuwa kinara wa matokeo hayo katika masomo ya sayansi mchepuo wa PCB.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Lucy E Magashi kutoka shule ya St. Mary's Mazinde Juu Tanga kutoka PCB. Muhewa Charles Kamando kutoka Tabora Boys, PCB akishika nafasi ya tatu akifuatiwa na Minael Simon Mgonja kutoka St.Mary's Mazinde Juu mkoani Tanga PCB, aliyeshika nafasi ya nne.

Nafasi ya tano imechukuliwa na Norah Eliaza Kidjout kutoka shule ya St.Mary's Mazinde Juu (Tanga) PCB, akifuatiwa na Jennifer Martin Chuwa aliyeshika nafasi ya sita kutoka St Mary's Mazinde Juu, PCB.

Pauline Ildephonce Mabamba kutoka St.Mary's Mazinde Juu Tanga PCM akichukua nafasi ya saba, Rachel Joachim Moshy amechukua nafasi ya nane kutoka St.Mary's Mazinde Juu Tanga, akichukua mchepuo wa PCM.

KIKOPE NI NINI? Sababu, matibabu na kuzuia tatizo la kuvimba kope (sekela)

 Kikope (stye) ni uvimbe mwekundu unakuwa juu au ndani ya ukingo wa kope ya jicho lako, uvimbe huu unaouma huwa unaaanza kuvimba na kuongezeka ukubwa ndani ya siku kadhaa.

Uvimbe huu huw unatokana na maambukizi ambayo huwa yameanzia kwenye shina la unywele wa kope . Inaweza ikawa ngumu kufungua jicho au unaweza kuanza kujihisi kama kuna kitu ndani ya jicho, hasa unapo fumba na kufungua jicho. Jicho lako linaweza kuwa linatoa machozi na mwanga unaweza kuwa unakuumiza ukiuangalia. Kikope huwa kinakua na baadae kinapasuka, kinapopasuka maumivu huanza kupungua, japo kuna baadhi ya vikope huwa vinaisha tu vyenyewe hata kabla ya kupasuka.

TFS WAPONGEZWA KWA KUPAMBANA NA MATUKIO YA MOTO

 

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana akisalimiana na baadhi ya watumishi wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) shamba la miti la Sao Hill wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Baadhi ya watumishi wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) shamba la miti la Sao Hill wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana wa katikati alipowasili katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Mufindi kwa ajili ya ziara ya siku moja.
Baadhi ya watumishi wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) shamba la miti la Sao Hill wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa katika kitengo cha moto.

 

 Na Fredy Mgunda,Iringa. 

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana amewapongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kuweka mkakati wa kupambana na majanga ya moto na kuendeleza utamaduni wa kulinda kwa kutoa elimu ya uhifadhi wa misitu kwa wananchi ambao wanayazunguka mashamba ya mimi ya TFS.


Akizungumza wakati wa ziara ya siku moja katika ofisi za Shamba la Miti SaoHill wilayani Mufindi mkoani Iringa Balozi Dkt.Chana alisema kuwa anatoa pongezi kwa uongozi na wafanyakazi wa TFS kwa kuendelea kutoa elimu ya majanga ya moto na amekikipongeza kitengo cha moto kwa kukabiliana vilivyo na majanga ya moto.


Dkt.Pindi Chana amewataka watumishi wa TFS kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa ajili ya kuendelea kulinda hifadhi za misitu


Alisema kuwa licha ya kazi kubwa wanayoifanya kulinda misitu lakini bado wamefanikiwa kutoa ajira zaidi ya 4000 katika shamba la miti ya kupanda la Sao Hill jambo ambalo linasaidia serikali kuendelea kutoa ajira kama ilivyokuwa kwa serikali kuwa ajira limekuwa swala la kipaumbele katika awamu hii ya sita ya uongozi.


Dkt.Pindi Chana aliwapongeza TFS  Sao Hill kwa kufanikiwa kutatua migogoro kumi na mbili na kubakiwa mitatu ambayo anaamini kuwa watatafuta nyia ya kuimaliza migogoro hiyo kama ambavyo wamefanya kwenye kutatua migogoro mingine.


Lakini pia Dkt.Pindi Chana aliwata TFS Sao Hill kuanza kutafuta bidhaa mpya za zao la misitu ambayo yatakuwa na faida kwa wananchi na taifa kwa ujumla.


Katika ziara hiyo Balozi Dkt.Chana ametembelea kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki kilichopo Shamba la Miti SaoHill na kuipongeza TFS kwa kazi nzuri ya uzalishaji wa mazao yanaotokana na misitu ikiwemo asali.


Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi TFS Prof.Dos Santos Silayo amesema katika kuunga mkono juhudi za serikali kwenye sekta ya utalii TFS imeandaa mpango wa kuzifanya hifadhi kuwa ni sehemu ya utalii


Prof.Silayo alisema kuwa katika shamba la miti la Sao Hill wamekuwa wakifanya utalii wa kutembea kwa miguu,utalii wa pikipiki na baiskeli akaongeza kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaanzisha utalii wa farasi jambo ambalo wanaamini litakamilika hivi karibuni.


Naye Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi amesema  sekta ya Misitu ina mchango mkubwa kwa wananchi hasa wa Mafinga kwa kutoa  ajira nyingi na mchango mkubwa kwenye Mapato ya Halmashauri hiyo kwa asilimia 60,  hivyo yeye kama mwakilishi wa wananchi ataendelea kushirikiana  na Wizara katika uhifadhi wa Maliasili hiyo.

Chumi alisema kuwa asilimia 85 ya wananchi wa wilaya ya Mufindi na Jimbo la Mafinga Mjini wanategemea mazao ya misitu kukuza uchumi wa wananchi wa Mufindi


Alisema kuwa anawapongeza TFS kupitia shmba la miti la Sao hill kwa kuwa wamekuwa na mchango mkubwa wa kimaendeleo kwa kusaidia ujenzi kwenye sekta ya afya elimu na biashara kwa kuboresha miundombinu katika maeneo hayo.

RAIS SAMIA ATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZOTE ZA KOMBE LA YAMLEYAMLE

 





Na John Mapepele.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan ametoa vifaa vya michezo kwa timu zote 45 zinazoshiriki mashindano ya kombe la Yamleyamle Zanzibar ili timu ziweze kufanya vizuri hatimaye  kuwapata wachezaji bora na wenye  vipaji ambao wataunganishwa  kwenye timu ya Taifa.


Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa, Julai 3, 2022 wakati akizindua mashindano hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Amani Zanzibar ambapo amesema Mhe. Rais ametoa mipira 45 kwa ajili ya timu hizo na jezi.


“Niwaombe  tunapojipanga kwenda kuandaa mashindano ya AFCON,  tuleteeni orodha  ya  vijana wanaofanya vizuri tutahakikisha tunawaingiza kwenye time zetu za taifa, tutawaendeleza, tutakuza vipaji vyao kwa maslahi  ya Serikali zote mbili SMT na SMZ”. Amesisitiza Mhe, Mchengerwa.


Amewapongeza kwa kuandaa mashindano hayo ambapo amefafanua kwamba dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaandaa mashindano ya AFCON  2027 na kusisitiza kuwa inawezekana iwapo kila  mdau atachukua wajibu wake.


Aidha, amefafanua kuwa eneo la soka ndilo eneo pekee ambalo  linaweza  kuwaunganisha watanzania wote bila kujali itikadi ya dini zao, rangi wala  makabila yao.