MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa aliyevaa suti katika akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Insha wakiwa wamebeba zawadi zao na vyeti wakiwa na watumishi wa Shirika la World Vision |
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa aliyevaa suti katika akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Insha wakiwa wamebeba zawadi zao na vyeti wakiwa na watumishi wa Shirika la World Vision
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MKUU wa wilaya ya Tanga mkoani Tanga Hashimu Mgandiliwa amelitaka Shirika la World Vision kuhakikisha linaendelea kuwajengea uwezo mkubwa vijana walioshindanishwa kwenye usomaji wa Insha na uandishi wa Ishana kuibuka washindi ili kuwaendeleza vipawa mungu alivyowajalia ili kufika mbali zaidi kimaendeleo.
Mgandilwa aliyasema hayo wakati wa kilele cha sherehe za uandishi wa Insha kwa shule za Msingi mkoa wa Tanga iliyohusisha wilaya nne za mkoa wa Tanga iliyandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania iliyoambatana na utoaji wa zawadi
Alisema vipaji ambavyo vimepatikana visiishie hapo bali viendelezwe ili viweze kufika mbali ikiwemo kuhakikisha fedha wanazowapa wazazi zisaidie kuwaendeleza kimasomo na kununua mahitaji ya shule.
Alisema Shirika hili limelenga kusaidia jamii na kusaidia kutimiza ndoto za watoto kusoma vizuri basi ni vyema kujikita zaidi katika kuibua vipawa na kuviendeleza katika masomo yao ili kufikia ndoto zao na kujikwamua kiuchumi endapo watahakikisha wanapata elimu bora itakayowasaidia kufika hadi vyuo vikuu na kupata wandishi wazuri wa Insha.
Aidha aliwataka watoto waliopata zawadi baada ya kuibuka washindi wa Uwandishi wa Insha kwamba wazingatie vigezo kabla ya kuhariri kazi zao wazingatie kuwashindanisha walichokiandika wenyewe badala ya kubadilisha maana na uhalisia wa mtoto ili kuweza kufanikiwa kupata washindi halisi badala ya kubadilisha maana na mantiki ya Insha yake.
“Kubadilisha maana ya uhalisia wa maana ya Insha kunaweza kusababisha mtoto kushindwa kufanya mwenyewe vizuri na kukosa kujiamini wakati wa kuwasilisha alichokiandika mwenyewe hivyo zingatieni hilo ili kuweza kupata vipawa vingi katika maeneo tofauti kwenye Halmashauri zetu.
Pia alisema watoto hao wanatakiwa kuhakikishiwa wanasoma vizuri na kuwekeza nguvu katika kusaidia familia zao kwani wengine wanatoka katika familia duni na kushindwa kutimiza malengo yao hivyo ni vyema kuliona hilo nalo ili kuhakikisha wanafika mbali zaidi na kupata wandishi wazuri kama watajengewa misingi imara kutokea wakiwa wadogo hadi kufika chuo kikuu.
Alisema Shirika linauwezo wakuwasomesha watoto hao hadi kufika vyuo vikuu nivyema kuhakikisha wanaunga nguvu ya pamoja katika kukuza vipawa hivyo alivyovitunuku vyeti vya sifa katika viwanja hivi vya Usagara.
Awali akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa Kitengo cha Jinsia na Uchchemuaji Makao Makuu Shirika la World Vision Tanzania Esther Mongi alisema wao kama shirika wameanzisha kampeni hiyo tokea mwaka 2017 ya kupinga mimba za utotoni.
Alisema lakini baada ya kutekeleza kampeni hiyo wakaona hapana mimba pekee haitoshi changamoto iliyopo kwenye jamii kuna mimba na ndoa za utotoni hivi sasa wana kampeni yao jukumu lao sote kupinga mimba za utotoni na ndoa na mwaka huu wamekuja na zoezi la uandiskiha wa insha kwa mikoa 12 Tanzania.
Aidha alisema wapo mkoani Tanga kutoa zawadi kwa washindi wa ngazi ya wilaya za mkoa na wamepata washindi watatu ngazi ya wilaya kwenye wilaya tatu na katika mkoa wa Tanga leo washindi watatu baada ya hapo mshindi wa kwanza katarasi yake itapelekwa Tamisemi Dodoma ili kupata mshindi wa kwanza na pili na tatu.
,Sisi kama Shirika la World Vision tunaamini kabisa ni jukumu lao wote kupinga mimba za utoto na ndoa iwe mzazi,mlezi, kiongozi wa dini na serikali kupitia insha tumewajenga uwezo watoto wameweza kuwa na ujasiri kusoma insha zao mbele ya wenzao”Alisema
Hata hivyo alisema kupitia zoezi na insha wamefikia shule 544 na kwa mkoa wa Tanga wamezifikia shule 72 hivyo wanaamini kwenye mikoa iliyopita wamefanya kazi kwa karibu na waandishi na elimu hiyo itasamba na wanaamini washindi watakuwa mabalozi wazuri.
Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza ngazi ya wilaya alipata 300,000 na cheti pamoja na baiskeli,mshindi wa pili 200,000,cheti na baiskeli,mshindi wa tatu 100,000 cheti na baiskeli ili kuweza kuwasaidia katika masomo yao.
Hata hivyo washindi kwenye ngazi ya mkoa,mshindi wa kwanza kutoka wilayaani Korogwe Sarah Juma Mussa alipata 500,000 na cheti,mshindi wa pili 400,000 na cheti huku mshindi akipata 350,000 na cheti.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.