Friday, April 22, 2022
Benki ya CRDB yafuturisha wateja wake jijini Mwanza, yatoa zawadi kwa watoto
Wednesday, April 20, 2022
WAZIRI MBARAWA APANIA UJENZI WA DARAJA KUBWA LA MTO WAMI KUKAMILIKA MWEZI JUNI
Wazari wa ujenzi wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawe wa kulia akigagua mradi wa ujenzi wa daraja la mto wami ambalo limejengwa kwa kiasi cha shilingi bilioni 75.1 kushoto kwake ni balozi wa china nchini Tanzania Mingijian Cheni alipofanya ziara ya kukagua mradi huo.
Balozi wa china nchini Tanznaia Mingijian Cheni wa kulia akizungumza jambo na Waziri wa ujenzi na Uchukuzi wakati walipofanya ziara ya pamoja kwa ajili ya kuweza kukagua mwenendo na maendeleo ya ujenzi wa daraja la mto wami.
Waziri wa ujenzi na uchukuzi akiwa katika picha ya pamoja na balozi wa china nchini Tanzania sambamba na baadhi ya viongozi wa Tanrods pamoja na wakandarasi wa mradi huo.
Waziri Mbarawa pamoja na balozi wakiwa wanatembea kujionea maendeleo ya ujenzi huo wa mradi mkubwa wa daraja la mto wami.
Picha ya pamoja na Waziri Mbarawa pamoja na Balozi wa china nchini Tanzania pamoja na watendaji wengine mara baada ya kuutembelea mradi wa ujenzi wa daraja la mto wami.
NA VICTOR MASANGU, PWANI
SERIKALI imesema kwamba kukamilika kwa mradi mkubwa wa ujenzi na daraja jipya la mto wami Julai mwaka huu kutakuwa ni mkombozi mkubwa wa kupunguza wimbi la vifo kwa wananchi ambavyo vimekuwa vikitokana mara kwa mara kutokana na kukithiri kwa changamoto ya kutokea kwa ajali za barabarani kutokana na kuwepo kwa miundombinu finyu katika daraja hilo la zamani.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ambapo amemuagiza mkandarasi wa Power Construction kukamilisha ujenzi wa daraja hilo ifikapo mwezi Juni mwaka huu badala ya mwezi novemba 21 mwaka huu kama ilivyokuwa katika mkataba.
Pia waziri Mbarawa amemtaka mkandarasi Power Construction kukamilisha ujenzi wa Daraja la Mto Wami ifikapo Juni badala novemba mwaka huu ambapo daraja hilo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni 75.1 mara litakapo kamilika.
Aliyasema hayo jana kwenye ujenzi wa Daraja hilo jipya lililopo Wami-Chalinze Wilayani Bagamoyo ambapo aliambatana na Balozi wa nchi ya China Ming Jian Chen na kuwa angependa arudi Juni 15 na kupita na gari kwenye daraja jipya na siyo la zamani.
Mbarawa alisema kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutasaidia kuokoa maisha ya watu ambao walikuwa wakipoteza maisha pamoja na mali kuharibika kutokana na ufinyu wa barabara hiyo kwani magari hayawezi kupishana tofauti na daraja jipya ambalo litakuwa na urefu wa mita 500.
"Daraja la zamani limejengwa mwaka 1959 ni jembamba na ni la njia moja ningefurahi kuona muda mliopanga kukamilisha Julai usifike mmalize Juni ijapokuwa mwanzo ilipangwa kukamilika Novemba mwaka huu kwani watu wengi wamekuwa wakipata shida kwenye daraja la zamani,"alisema Mbarawa.
Kwa upande wake Balozi wa china nchini Tanzania amesema kwamba wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika miradi mbali mbali ya maendeleo na kwamba daraja hilo la mto wami litasaidia kupunguza kasi ya ajali kwa wananchi mbali mbali wa Dar es salaam, Pwani pamoja na nchi nyingine za jirani.
Aidha balozi huyo alifafanua kuwa mradi huo wa Maendeleo unaunganisha Mji wa Kibiashara wa Dar es Salaam na mikoa ya Kaskazini na kuleta maendeleo na nchi yake itaendelea kushirikiana bega kwa began a serikali ya Tanzania katika kusaidia miradi mbali mbali ya ya maendeleo.
Naye Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANRODS) Injinia Hussen Mativila amebainisha kwamba mradi wa daraja hilo ambalo lina urefu wa mita 5.15 limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 75.1 na kwamba daraja la zamani ni chakavu na nifinyo kutokan ana na magari kupita kwa shida kwani limejengwa tangu manamo mwaka 1959.
Kadhalika mtendaji huyo mkuu wa Tanrods alisema kuwa mradi huo unagharimiwa na serikali na unatumia Teknolojia ya madaraja marefu kuna nguzo nne ambapo mbili zina urefu wa mita 19 nyingine ikiwa na urefu wa mita 37 na huku moja ikiwa na urefu wa mita 44.
Kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa daraja hilo jipya la mto wami lililopo katika halmashauri ya Chalinzi Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kutaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi pamoja na kupunguza wimbi za ajali ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara na kupoteza maisha ya watu.
WAFANYABIASHARA IRINGA WALALAMIKIA KUTOZWA KODI KUBWA
Na Fredy Mgunda,Iringa.
WAFANYABIASHARA waliopanga katika jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Iringa lililopo karibu na Stendi ya zamani ya Mabasi ya Mkoani wamelalamikia kutozwa kodi kubwa kutoka ofisi ya Halmashauri hiyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari wafanyabiashara hao walisema kuwa wanalipishwa kodi kubwa kuliko biashara ilivyo katika eneo ambalo kwasasa halina wateja kama ilivyokuwa awali.
Walisema kuwa wamekuwa na majadiliano ya mara kwa mara na ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo lakini wamekuwa hawapati ushirikiano wa kutosha kutatua changamoto hiyo.
Raphati kaberege ni mfanyabiashira aliyepanga katika jengo hilo alisema kuwa wameandika barua ya kuomba kukutana na viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa toka mwaka 2017 na hawajawahi kujibiwa.
“Kwa kweli mamlaka hawajahi kutupa ushirikiano licha ya kuwaandikia barua, Pia tumewahi kuwaalika katika eneo la biashara lakini hawajahi kufika, na ukiangalia mazingira ya biashara hayaridhishi kwani vyoo wakati mwingine vimejaa na mitaro imeziba jambo linalohatarisha afya zetu”alisema kaberege
Alisema kuwa wameitwa na mkurugenzi ili kufanya kikao cha majadiliano lakini mkurugezi hakufanikiwa kufika katika kikao hicho ambacho ofisi yake ilikiitisha kwa ajili ya majadiliano.
Kaberege alisema kuwa vyumba vya biashara ambavyo vinapangishwa na halmashauri ya Manispaa ya Iringa na vyumba vya biashara vya CCM Iringa ni gharama nafuu Zaidi kuliko halmashauri ya wilaya ya Iringa.
“Mfano CCM wanalipa wanatoza kiasi cha shilingi 50,000 hadi 70,000 na maeneo mengine yanayotazamana na jengo hilo wafanyabiashara wanalipa kwa gharama ya shilingi laki moja (100,000) hadi laki moja na nusu (150,000) kwa mwezi,tofauti na sisi” alisema kaberege
Isaack Steven ni Miongoni mwa wapangaji katika jengo hilo amesema kuwa kwa wafanyabiashara waliopanga milango ya mbele wanalipa shilingi laki tatu na nusu (350,000) huku waliopanga milango ya nyuma wakitozwa kodi ya shilingi laki Moja (100,000).
Alisema kuwa kodi hizo ni kubwa sana kwa kuwa eneo hilo kwa sasa halina mzunguko wa biashara baada ya standi kuhamishiwa eneo la igumbilo ambapo pia mazingira ya jengo hilo siyo rafiki kwani choo wanachotumia wanatozwa fedha nyingi.
Mfanyabiashara Alice Ngwale alisema kuwa licha ya kuchajiwa fedha kubwa ya pango ya mwezi pia wanashindwa kuendesha biashara zao kwani wamekuwa wakitoa fedha katika vyanzo vingine vya mapato ili waweze kulipia majengo hayo.
Wapangaji hao kwa kauli moja waliamua kuondoka katika Ofisi za Siasa ni kilimo baada ya Mkurugenzi wa halmashauri kushindwa kufika katika kikao hicho huku wakiiomba serikali kuwawekea utaratibu mzuri wa kulipa kodi kila mwezi au kila baada ya miezi mitatu na siyo kila baada ya miezi 6 jambo ambalo linawafanya washindwe kumudu gharama hizo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Stephen Mhapa alisema kuwa kama wanaona kuwa kodi waliyopangiwa ni kubwa bora wakaachia vyumba hivyo kwa kuwa wanafanya biashara sio kutoa huduma kwa wananchi.
Mhapa alisema kuwa hata ukienda kwa watu binafsi inaendana na gharama ambazo halmashauri inapangisha kwa wafanyabiashara waliopanga katika jengo hilo.
Alisema kuw malalamiko ya kushuka kwa biashara hayana mashiko kwa kuwa changamoto hiyo ipo na bado wafanyabiashara wengine wa jirani wanafanya biashara kwanini wawe wao.
Mhapa alimazia kwa kusema kuwa kama kuna changamoto ya kutosikilizwa basi wanapaswa kurudi tena kwenye ofisi yake ili watafutiwe njia mbadala ya kujibiwa kero hizo.