Saturday, September 03, 2011
huzuni
Saturday, September 03, 2011
SOMA
Watu hukaa katika majumba ya kifahari meza zikisheheni kila aina ya tunda nayo kwa mafungu makubwa makubwa.
Wakichinja kila aina ya vitoweo, wapishi katika masufuria makubwa walipika vyakula kwaajili ya sherehe yenye nia moja tu nalo ni kupongezana.
Vyakula vya nafaka kwa shehena vikapikwa.
Nao hula na kunywa hata kusaza.
Mara baada ya sherehe chakula kingi kilichosalia humwagwa hata kisibakie kwani marufuku kula kiporo.
Kikimwagwa majalalani kama taka.
Chakula choote hutupwa.
Hayo yakifanyika hebu fikiria juu ya ndugu zetu wengine, wakiishi kama ndege kuokoteza.
Upande wa pili wa dunia unadhoofika kwa kukosa lishe.
Hali si hali kwa kukosa hata kipande cha chakula.
Mtizame mama yule anayenyonyesha.
DON'T WASTE FOODS ANY MORE, Kusanya peleka kwa wenye uhitaji.
Let this be remembered.. . each time we throw away Foods!
People who live in rich countries,, don't know this,, don't want to know
this,, never understand this!
but U,, please U,, understand this .........
Saturday, September 03, 2011
MICHEZO
Friday, September 02, 2011
huzuni
Thursday, September 01, 2011
BANGO
TAARIFA YA MABADILIKO YA JINA NA LINK YA TONE INTERNET RADIO KWENDA TONE ONLINE RADIO
Tone Multimedia Company Limited inapenda kuwapa taarifa wananchi wote popote Duniani kuwa tumefanya mabadiliko ya jina la Radio pia jina la Tovuti ambapo mala ya kwanza ilikuwa inaitwa Tone Internet radio na Jina la Tovuti lilikuwa ni www.toneinternetradio.blogspot.com, Kutokana na Sababu za kimsingi za kuingiliana kwa mtandao na Radio moja iliyopo USA inakwenda kwa jina la Tune Internet Radio ndio sababu iliyo tupelekea kubadilisha jina na kuzaliwa kwa jina jipya la Tone Online Radio ambapo tovuti yake sasa itakuwa ni www.toneonlineradio.blogspot.com na ikumbukwe pia Tone Online Radio ni Radio inayo tumia internet Pekee hatuna Frequency za aina yoyote. asanteni sana atakae pata link hii ampatie na mwenzake.pia kwa wanamuziki watume na maproducer watume kazi zao kupitia toneonlineradio@live.com Kwa pamoja tunaendelea kuleta maendeleo ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia. Tone Online Radio Tumekufikia popote Duniani.
Natanguliza Shukrani kwa niaba ya Uongozi,
Imetolewa na,
Joseph Mwaisango
Mkurugenzi wa Mawasiliano
Tone Multimedia Company Limited.
KUSIKILIZA TONE ONLINE RADIO BOFYA HAPA: www.toneonlineradio.blogspot.com
Thursday, September 01, 2011
HABARI
RAIS Jakaya Kikwete amelikataa ombi la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) la kuitaka serikali iwarejeshee shule ambazo walikuwa wakizimiliki kabla ya kutaifishwa miaka michache baada ya uhuru.Kikwete alitoa msimamo huo ambao alikiri kwamba unaweza ukawakera baadhi ya Waislamu wakati akihutubia kwenye Baraza Kuu la Iddi lililofanyika kitaifa katika Msikiti wa Gaddafi mjini Dodoma jana.
Badala yake, Rais Kikwete alizitaka taasisi za Kiislamu kuweka msisitizo katika kuzijenga shule mpya kwani maombi yao ya kutaka warejeshewe shule walizokuwa wakizimiliki yamekuja yakiwa yamechelewa.
Alisema uamuzi wowote wa kuzirejesha shule za Waislamu leo unaweza ukasababisha mgogoro mzito kutokana na ukweli kwamba wakati wa utaifishwaji serikali ilichukua shule zilizokuwa zikimilikiwa na taasisi tofauti za kidini na watu wa rangi tofauti.
Akifafanua, Rais Kikwete aliwalaumu Waislamu kwa kuwa mstari wa mbele kunung’unika kwamba wanaachwa nyuma katika masuala ya maendeleo kama yale ya elimu tangu mwaka 1992 pasipo kuchukua hatua zozote.
Kikwete aliyeonekana kuzungumza kwa namna iliyoonyesha kuchukua msimamo mkali na wa wazi dhidi ya maombi ya BAKWATA yaliyowasilishwa kupitia katika risala yao, iliyosomwa na Sheikh Mkuu wa Dodoma, alisema serikali kama si juhudi kubwa zilizofanywa na waasisi wa taifa hili hali ya ustawi wa elimu uliopo leo usingefikiwa.
“Tumeshirikiana vema na taasisi za dini, naamini bila ushirikiano huo baadhi ya maeneo wasingepata huduma za afya, elimu, maji na miundombinu…napenda kuwahakikishia kuwa hakuna kitu chochote ambacho serikali itatoa na kuwabagua wengine.
“Baada ya uhuru Mwalimu Nyerere alitaifisha shule hizo ili kuweka uwanja sawa kwa watoto wa rangi, dini na kabila zote kwa sababu zilikuwa za serikali.
“Ninyi kama mnataka jengeni shule na vyuo serikali itawasaidia kama inavyofanya kwenye shule na vyuo vya wenzetu Wakristo, shule za Azania na Kihindu…mfano ni mkopo unaotolewa na serikali kwa wanafunzi waliopo katika vyuo vya Wakristo.
Alisema wanaomcha Mungu ni watu wa upendo siku zote kwa sababu wanawahudumia vema wananchi wanaowahubiria amani na upendo, hali inayovipunguzia kazi ya kupambana na uhalifu vyombo vya dola.
Aidha, aliwataka Waislamu kuunda Mahakama ya Kadhi bila kuitegemea serikali huku akibainisha kwamba ushauri huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Profesa Ibrahim Juma, ambaye ni mtaalamu wa Sharia na Sheria za Kiislamu.
Alisema mahakama hiyo ya kadhi itakayoundwa haitahusika na kesi za jinai na kwamba haitakuwa na utaratibu wa kutoa hukumu kama zile za kukatwa mikono kwa wezi na za watu kupigwa mawe hadi kufa ambazo zimekuwa zikitumika katika mataifa yanayofuata Sheria za Kiislamu (Sharia).
Hata hivyo, aliwaomba viongozi wa dini kuacha kukashifiana na kubainisha kwamba njia bora ya kufikia malengo ya mafanikio ni kupitia meza ya mazungumzo huku akiwataka kutimiza wajibu wao bila woga wala kuoneana.
Aliwataka viongozi wa dini zote kurejesha utaratibu wa mazungumzo katika meza moja na kubainisha kwamba nguvu ya dola inatumika pale amani inapotoweka.
Aliipongeza BAKWATA kwa utaratibu bora wa kila mwaka kuwapeleka Makka Mahujaji na kuwatia moyo waendeleze utaratibu huo ili ifike mahali baraza hilo liwe chaguo la hiyari la mahujaji.
Kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya, aliwataka viongozi wa dini zote kuwahamasisha waamini wao kushiriki bila kuwepo kwa ushabiki wa kidini na kusema suala hilo linawezekana iwapo viongozi hao wataamua na kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.
Alitumia fursa hiyo kuwaonya waumini wa Kikristo na Kiislamu kutougeuza mjadala wa mabadiliko ya Katiba kuwa mdahalo au malumbano ya kutaka kuingiza masilahi ya dini hizo mbili ndani ya katiba.
Akizungumzia tatizo la dawa za kulevya, Rais Kikwete alisema tatizo hilo lipo kila mahali, hivyo serikali imejipanga kukabiliana nalo huku akiomba ushirikiano kwa viongozi wa dini ambao miongoni mwao wanahusika.
Akionyesha namna tatizo hilo linavyokua, alisema wafanyabiashara hao wameshaanza kuwalenga vijana wa vijijini, ambapo iwapo hatua za kudhibiti hali hii hazitachukuliwa, hasa na viongozi wa dini, basi tatizo litazidi kuongezeka na kukithiri.
“Ni tatizo la kweli, hakuna mji ulionusurika, sasa hivi wanakwenda kuwauzia vijana wa vijijini…kazi iliyo mbele yetu ni ushirikiano mkubwa kati ya viongozi wa dini na waumini wao.
Alitumia fursa hiyo kuwajibu viongozi wa dini akiwamo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakimtaka awataje hadharani viongozi wa dini aliosema wamekuwa wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Akirejea kauli alizopata kuzitoa katika maeneo mawili tofauti ya Kanisa Katoliki, Rais Kikwete alisema alifanya hivyo kama njia ya kutoa rai na tahadhari baada ya kupata taarifa ambazo zimekuwa zikiwataja viongozi wa dini kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
“Nilisema hili kama tahadhari, tumewakamata masheikh, wachungaji, maalhaji. Mmoja alikuwa anakwenda Brazil akakamatwa na kesi ipo mahakamani. Sikusema maaskofu bali watumishi wa Mungu…maaskofu na viongozi wa dini, niliwaomba tushirikiane..Nikaona wengine wanachukia,” alisema Kikwete pasipo kutaja jina la kiongozi yeyote wa dini.
Alisema wito wake huo kwa viongozi wa dini haukuwa na lengo la kuwakejeli au kuwashutumu bali alifanya hivyo kutokana na kutambua namna walivyo na uwezo wa kuvuta hisia za watu wengi wanaohudhuria mahubiri yao.
“Sikuwakejeli wala sina sababu ya kuwakejeli viongozi wa dini, sasa hili mkiliona baya wenzangu mnanikatisha tamaa na ninyi mnasikilizwa kwa sababu mna uwezo wa kukusanya watu wengi, mkawahubiria wakawaelewa,” alisema.
Hisani ya Tanzania Daima.
Tuesday, August 30, 2011
BANGO
URBAN PULSE inawaletea video fupi ya Notting Hill carnival iliyofanyika jumapili 28.8.11
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE wakishiriana Miss Jestina Blog
The Ngorongoro Crater is often called ‘Africa’s Eden’ and the ’8th Natural Wonder of the World,’ a visit to the crater is a main drawcard for tourists coming to Tanzania and a definite world-class attraction. Within the crater rim, large herds of zebra and wildebeest graze nearby while sleeping lions laze in the sun.
G.Sengo looking at the Mbuga'z...
At dawn, the endangered black Nyumbu'z returns to the thick cover of the crater forests after grazing on dew-laden grass in the morning mist. Just outside the crater’s ridge, tall Masaai herd their cattle and goats over green pastures through the highland slopes, living alongside the wildlife as they have for centuries.
Tembo aka Elephant is the largest living land animals on Earth today. This male weighed about 11,000 kg.
Tembo na misafara yao.
Twiga (Girafe).
Kiboko na wenzie' basi tuwaite Viboko kwasababu wako wengi.
Swala.
Ukungu, umande yaaani ni full baridi humu mbugani.
Katika eneo hili la Hotel ya Serena iliyozungukwa na maadhari ya aina yake ya kuvutia, kila utakachokitizama kitakuwa na mvuto kwa macho yako, ardhi, nyasi, miti, utunzaji wa mazingira ololooo!
Kama Directory vile.
The Ngorongoro Crater and the Ngorongoro Conservation Area are without a doubt some of the most beautiful parts of Tanzania, steeped in history and teeming with wildlife.
Nikiwa Ngorongoro Serena Lodge.
Much respect kwa mwongoza huu msafara Dreva Abdul 'Masafari' aliyekuwa akinimwagia maifomesheni', mahistoria ya pori na makila kingafrengwa.
Lango kuu kuingia Hifadhi ya Taifa Serengeti National Park A Word heritage Site.