KAMA MWAKILISHI WA CLOUDS FM ROCK CITY KIPINDI CHA POWER BREAKFAST KILIPOKEA UJUMBE TOKA KWA MOJA YA WASIKILIZAJI WAKE JUU YA HALI ISIYORIDHISHA YA MAZINGIRA YA KISIWA CHA SAA NANE KILICHO NDANI YA ZIWA VICTORIA... UJUMBE ULIKUWA UNASEMA........nimesahau!! DAH! (G.HANDO uliutamka vizuri NITUMIE SMS niuanike kaka) NDIPO WAKUBWA WANGU WA KAZI G.HANDO NAYE BABRA HASSANI (PROTOKO IMEZINGATIWA) WALIPONITUMA NIKATIZAME KUNANI PALE. NI MWENDO WA DK 10 TU TOKA JIJINI, NAMI YULEEEEEE!!
BANDA HILI NI NYUMBA YA CHUI UJENZI WAKE UMEZINGATIA TARATIBU ZOTE ZA KIUSALAMA KUPITIA MAISHA NA TABIA ZA MNYAMA HUSIKA. KUNA KIBAO CHA TAHADHARI KIASI KWAMBA WAWEZA TISHIKA KUINGIA HATA ILE HALI YALIYOMO HAYAMO (HUMO NDANI HAKUNA CHUI). NITAWALETEENI MOJA YA MAWORNING""
ENEO HILI LA MAPUMZIKO AMBALO LIMESANIFIWA KITALII UTALIPATA NDANI YA KISIWA CHA SAA NANE UWANDA WA CHINI KABISA KUELEKEA ZIWANI. KUNA MITI NA UPEPO MWANANA USOKERA KAMA UMEPIMWA KWA RULA TEHE!!
YUKO WAPI YULE NYANI TULOKUWA TUKI MLISHA MAPOCHOPOCHO, KUMSMOKISHA NA KUMNYWESHA DUBAIZ! TEH TEH! MAHALA HAPA ATAPAMISS SANA!! HAPA NI KWA NDNI,, BANDA HILI NDIMO ALIMOKUWA AKIJIVINJARI NA TAIRI KULITUMIA KAMA SEHEMU YA UWANJA WAKE WA BURUDANIZ!
CHINI NI MOJA KATI YA ENEO LA JUU YA MWAMBA WA JIWE AMBAKO UNAPATA FURSA KUJIONEA YAFANYIKAYO ZIWANI HALIKADHALIKA SEHEMU YA JIJI LA MWANZA UTAFAIDI ZAIDI ENEO HILI UKIWA NA DARUBINI MAZEE. JUU NI ENEO LA MBELE BANDA LA SIMBA, HIVI SASA LIKO TUPU LIKIENDELEA KUFANYIWA UKARABATI. YUKO WAPI SIMBA MZEE?