ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 8, 2016

PICHA ZA USHINDI WA CCM NYAMAGANA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA LEO

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) katikati mwenye shati na tai akitoka chumba cha Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza mara baada ya kushinda kesi ya uchaguzi.

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) aliyenyoosha mkono juu (katikati) akiwapungia wananchi wakati akisindikizwa kuelekea ofisi za CCM Wilaya ya Nyamagana baada ya kushinda kesi ya uchaguzi jana kufatia uamuzi uliotolewa na Makakama Kuu Kanda ya Mwanza, kushoto kwake ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ilemela, Acheni Maulid na kulia aliyeinua mkono juu ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Elias Mpanda wakiwa na wafuasi wa CCM. Picha Na Blandina Aristides.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu (kulia) akizungumza na wananchi juu ya uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilioutoa jana ya kuitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya Jimbo la Nyamagana nje ya jengo la ofisi ya CCM Mkoa katikati ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Elias Mpanda na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) baada ya kutoka Mahakamani.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu (kulia) akizungumza na wananchi juu ya uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilioutoa jana ya kuitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya Jimbo la Nyamagana nje ya jengo la ofisi ya CCM Mkoa katikati ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Elias Mpanda na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) baada ya kutoka Mahakamani.

RAIS MAGUFULI AREJEA NCHINI AKITOKEA RWANDA.

Rais Dkt. John Magufuli arejea nchini baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya siku 2 nchini Rwanda. 

ZURI APPOINTS DESPEC AS EAST AFRICAN DISTRIBUTOR FOR SMARTPHONES

zuri_aca4.640
One of the types of Zuri Phones in the Tanzania market, the phones are of quality and high tech among the Smart phones...
Digital lifestyle devices brand Zuri (www.zuri.hk) has appointed DESPEC as a distribution partner for smartphones in East Africa. Under the terms of the deal, DESPEC will distribute Zuri products across three countries: Kenya, Tanzania and Uganda.

As a well-established and fast-growing technology distributor in East Africa, DESPEC provides Zuri with a unique opportunity to rapidly expand its channel reach within the markets covered by the agreement. The two companies will collaborate closely to increase consumer awareness of the Zuri brand throughout East Africa.

Vikash Shah, CEO at Zuri, stated: “East Africa represents a significant growth opportunity for Zuri, with demand for smartphones increasing across the region. We are confident that DESPEC will enable us to build strong routes-to-market across Kenya, Tanzania and Uganda. Zuri is fully committed to building its brand presence in East Africa and DESPEC is the perfect partner to help us achieve this.”

Initially ZURI has launched 4 smartphone models : C41, C46, C52 and S56. The 4.0-inch C41 combines a 4” display with a quad core processor and 4GB Memory and is available in white or black. The C46 is a feature-packed 4.5-inch smartphone with quad core processor, 8GB memory and 8.0MP camera. The 5.0-inch C52 offers an elegant design with rubberised back finish, IPS Display, 8GB Memory and 8 MP Camera powered by a quad core processor.

Completing the line-up is the powerful S56 smartphone, offering a 5.5-inch display, octacore processor, HD IPS display,16GB internal memory,13.0MP camera and dual-SIM capabilities, running Android 5.1 Lollipop. Additionally all devices support dual sim cards. Initially the launch packs also includes Free 8GB Memory card, screen protectors, and phone covers.
Full details of all four smartphones covered by the agreement are available at www.zuri.hk/smartphones/ The phones come with 1 year ZURI warranty and is backed by an extensive after sales network.

Riyaz Jamal, CEO at DESPEC, commented: “We are pleased to add Zuri smartphones to our portfolio and believe the brand has a bright future in East Africa. Channel partners and consumers are looking for smartphone brands that stand out from the crowd. We believe the Zuri message, branding and image – coupled with the quality of the devices – will allow us to build strong sales across Kenya, Tanzania and Uganda.”

The appointment of DESPEC represents the next step in Zuri’s ambitious international expansion plans. DESPEC provides Zuri with access to an extensive channel customer base spanning both reseller and retailer channels across East Africa. The two companies plan to work together on a series of marketing initiatives, branding exercises and social media campaigns in the coming months to build market awareness.

Vikash Shah continued: “Zuri aims to provide consumers with smarter, simpler and stronger ways to realise the full potential of the connected world. Our high quality designs and manufacturing excellence create products that offer a compelling price-performance proposition for users.”

“We look forward to working with operators, retailers and resellers in East Africa to explain the benefits that Zuri provides to consumers and the win-win business proposition for channel partners that align with our strategy,” Shah added.
Watching ..MO tv, for this News here:
DSC_9798
Mr, Vikash Shah , Zuri Ceo (in the middle) Showing one of the phones to members of press(not in the Picture) during the launch of Zuri phones into Tanzania Market, on his left is Despec( zuri phones main distributor in Tanzania) country Manager Mr Amit Tulsidas.DSC_9871
Mr Amit Tulsida, Despec Country manager on the left, holding one of the phones during the launch,Despec are the main distributors of Zuri Phones in Tanzania. On the right is the marketing Manager Mr. Moses Mtwelve.
(All Photo by Andrew Chale, Modewjiblog).

AIRTEL YADHAMINI MASHINDANO YA ICT KWA WASICHANA HAPA NCHINI

Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati) akipiga picha ya pamoja na washindi wa mashindano   ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal  Communications Services Access Funds ) na kushirikisha  wasichana 240 hapa nchini, na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel  ni mdhamini wa mashindano hayo . Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam
Mwanafunzi  Elisia Yohana (kulia) wa shule ya sekondari Nyankumbu iliyopo Geita akielezea jinsi program ya kikundi chao jinsi itakavyokuwa inafanyakazi katika mashindano  ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal  Communications Services Access Funds ) na kushirikisha  wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel  ni mdhamini wa mashindano hayo. Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam
Afisa Mtendaji mkuu wa mfuko wa Mawasiliano kwa wote (Universal  Communications Services Access Funds) UCAF, Eng. Peter Ulanga (aliyesimama) akiongea na wanafunzi  katika  mashindano ya  ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF na kudhaminiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel na kushirikisha  wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu. Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi  wa Sayansi na Teknolojia wizara ya elimu, sayansi, teknolojia na ufundi, Prof. Evelyne Mbede (kushoto) akiongea  na wanafunzi wa kidato cha tatu katika mashindano ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal  Communications Services Access Funds ) na kushirikisha  wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel  ni mdhamini wa mashindano hayo . Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Elimu ya sekondari, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali- Zanzibar bi Asya Iddi (kushoto) akikabidi cheti kwa Aines Mtani (wa tatu kulia) kama mmoja wa washiriki katika mashindano ya ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal  Communications Services Access Funds ) na kushirikisha  wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel  ni mdhamini wa mashindano hayo . Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam 

BREAKING NEWS: WENJE APIGWA CHINI KESI YAKE DHIDI YA MABULA.

Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Mtaturu akimpongeza Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula mara baada ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge iliyofunguliwa na Ezekiel Wenje katika jimbo hilo kufutwa.
Mahakama kuu kanda ya Mwanza imeifuta kesi ya kupinga Matokeo ya Ubunge katika jimbo la Nyamagana iliyokuwa imefunguliwa na mbunge aliyemaliza muda wake Ezekiel Wenje (CHADEMA) baada ya kushindwa kuthibitisha.
Kufutwa kwa Kesi hiyo kumeweza kumpatia ushindi Stanslaus Mabula (CCM) kuwa mbunge halali wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza,ambapo wafuasi wa CCM wanaelezwa kuwapo nje ya Mahakam hiyo huku wakishangilia ushindi wa Mbunge huyo.


Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula akifanya mahojiano na waandishi wa habari jijini Mwanza.
Jembe Fm 93.7 kupitia mwandishi wake Mansour Jumanne iliyekuwa eneo la tukio  Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza na kisha baadaye ofisi za CCM wilaya ya Nyamagana anasimulia kilichotokea kupitia kipindi cha KAZI NA NGOMA
BOFYA PLAY KUSIKILIZA KILICHOJIRI.

Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula akizungumza na wananchi waliojitokeza kumpongeza mbele ya ofisi za CCM Nyamagana, kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Baraka Konisaga.
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana pamoja na marafiki wa Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula walipita mitaa mbalimbali katikati ya jiji la Mwanza kuelekea ofisi za CCM wilayani humo huku wakiimba kusherehekea.
Selfie za makada wa CCM.
Mabangoz.....!!!

Mwaka jana Octoba 25 Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Mabula alitangazwa mshindi wa mbio za ubunge katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza kwa kupata kura 81, 170 dhidi ya Ezekiel Wenje (Chadema) aliyepata kura 79, 280.

MAGAZETI YA LEO> POLISI ANAYEMILIKI NYUMBA 40 ATUMBULIWA. FATMA KARUME AMVURUGA DR. SHEIN. VITA DHIDI YA UFISADI YAIVA. MTOTO WA RAIS MATATANI.


Magufuli amkuna Kagame. Bajeti ya JPM mjadala mkali. Makanisa ya kilokole kuthibitiwa mtaani. CUF yapiga hodi kwa Majaliwa. 

Polisi anayemiliki nyumba 40 atumbuliwa. Fatma Karume amvuruga Dk.Shein. Vita thidi ya ufisadi yaiva. Mtoto wa rais matatani; 

 Lowassa amshukia Magufuli kwa mambo 5. CAG atoboa jinsi alivyokerwa na UDA. Mwanafunzi ajifungua akiwa shuleni .

Thursday, April 7, 2016

PCCB KUCHUNGUZA RUSHWA LIGI DARAJA LA KWANZA

TAKUKURU yaanza kuchunguza sakata la kufungiwa  kwa viongozi na wachezaji wa timu 4 za ligi daraja la kwanza kwa tuhuma za rushwa.

MCHEZAJI KANU WA NIGERIA AZINDUA DUKA JIPYA LA STARTIMES KESHO KWENDA KUTEMBELEA SHULE YA MSINGI MAJIMATITU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM


  Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (kulia),akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la Mkuki Mall Barabara ya Nyerere Dar es Salaam leo mchana. Mchezaji huyo yupo nchini kwa ziara ya siku tano. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao.
 Ofisa Mauzo wa StarTimes Tanzania na mshereheshaji wa uzinduzi huo, Tang Jing Yu 'Juma Shorabaro wa Kichina'  (kulia), akiendelea na majukumu yake.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Mr.Canter, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (wa pili kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

 Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaamleo mchana, baada ya kuzindua duka la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la Mkuki Mall wakati wa ziara yake aliyoianza jana  nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Mr.Canter, Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao, Katibu wa mchezaji huyo, Kingstey Obiekwe na Makamu wa Rais wa StarTimes, Zuhura Hanif.
  Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (katikati), akitia saini yake katika jezi.
 Kanu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa StarTimes na wa jengo la Mkuki Mall baada ya kuzindua duka hilo.
Mmiliki wa Blog ya Full Shangwe, John Bukuku akichukua picha na mchezaji huyo.

Na Dotto Mwaibale


Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Naijeria (Super Eagles) na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu ameshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya StarTimes Tanzania lililopo katika jengo la Mkuki Mall Barabara ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mchezaji Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika ambapo inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya 10 amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kuwepo nchini na atashiriki shughuli mbalimbali za kampuni pamoja na za kijamii.

“Ni mara ya kwanza mimi kuwepo nchini Tanzania, nashukuru nimefika salama na kupokelewa kwa ukarimu mkubwa, kwa kweli sikutarajia. Uwepo wangu hapa ninaiwakalisha kampuni ya StarTimes barani Afrika kama balozi wao na kama balozi ninao wajibu wa kufika kila nchi ambayo kampuni hii ipo. Kwa namna nilivyopokelewa ninaamini kuwa kweli StarTimes ni kampuni kubwa, inapendwa na kujulikana miongoni mwa watanzania wote.” Alielezea Bw. Kanu

“StarTimes wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanafurahia huduma za matangazo ya dijitali kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu. Na hii ni kutokana na falsafa iliyojiwekea kampuni ya kutaka kuhakikisha kuwa kila nyumba ya muafrika inafikiwa na matangazo hayo. Changamoto ni nyingi katika uendeshaji na utoaji huduma za kidijitali lakini kampuni imejizatiti kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika uboreshaji wa vipindi na chaneli zake. Kwa mfano kwa sasa kama mnavyoweza kushuhudia kuwa ligi kubwa barani Ulaya za Bundesliga na Serie A za nchini Ujerumani na Italia zinaonyeshwa moja kwa moja kupitia StarTimes Pekee.” Aliongezea Kanu

“Michezo na burudani ni maudhui muhimu sana ambayo lazima yawekewe mkazo kwani ndivyo vitu vinavyopendwa na kuwavutia wateja wengi hivyo haina budi kuweka mkazo. Ninaamini kuwa uwepo wangu nchini Tanzania utasaidia kwa kukaa chini na uongozi wa kampuni nchini na kuweza kuona wanawaongezea na kuwapatia nini wateja wao. Ninatumaini ninacho cha kuongezea kwa nilichojifunza kutoka nchi kama za Uganda na Kenya ambazo nimetokea huko pia,” alisema na kumalizia Kanu kuwa, “Nashukuru kuwepo Tanzania na ninaamini nitajifunza na kushirikiana kwa mengi kwa kipindi nitakachokuwepo mpaka kuondoka kwangu.”

Naye kwa upande wake akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya ambalo litakuwa ni la saba kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee, Mkurugenzi wa Uendeshaji (Operesheni) wa StarTimes Tanzania, Bw. Carter amebainisha kuwa duka hilo jipya litawarahishia wateja wote wanao kama maeneo ya jirani kama vile Tandika, Mbagala, Temeke, Kurasini, Yombo, Kiwalani, Vingunguti na kwengineko kujipatia huduma na bidhaa kwa urahisi zaidi.

“Leo tunayo furaha kubwa kufungua duka hili jipya ambalo katika kumbukumbu litakuwa limezinduliwa na balozi wetu barani Afrika, Nwanko Kanu. Duka hili litakuwa msaada mkubwa kwa wateja walio maeneo ya jirani na kwingineko na ningependa kuwatoa wasiwasi kuwa litakuwa linatoa huduma zenye ubora sawa na maduka yetu yote hivyo wasiwe na wasiwasi. Ninawaomba wateja wetu watembelee hapa kujipatia huduma kama vile kununua visimbuzi, antena na kebo, vocha za malipo ya mwezi pamoja na huduma kwa wateja.” Alimalizia Bw. Carter.


JUMA NATURE AJIPIGA PINGU JEMBEKA FESTIVAL 2016.

Wakati joto la burudani likiendelea kupanda Kanda ya Ziwa kwa vipindi, habari na matangazo yenye mguso na jamii kupitia kituo cha redio Jembe Fm kinachorusha matangazo yake kutoka jijini Mwanza katika masafa ya FM 93.7, nayo safari ya kuelekea Tamasha kubwa la burudani linalojulikana kama JEMBEKA FESTIVAL 2016 linaufanya ukanda huo joto lake kupanda zaidi kiasi cha kusababisha presha kwa wadau wa Kanda husika. 

Jumamosi, May 21,2016 ndiyo siku litakapopigwa Tamasha la Jembeka Festival ikiwa ni Msimu wa Pili. Utamu wa Jembeka Festival unaanzia kwa Mkali Neyo kutoka nchini Marekani pamoja na Mkali Diamond Platnumz kutoka Tanzania. Pia watakuwepo wasanii wengine kibao.

Wakati huo huo msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania ambaye historia ya muziki wa Bongo Fleva hainogi bila jina lake kutajwa, Juma Nature tayari ameangusha wino kuwa mmoja wa wasanii watakaomwaga burudani kwenye tamasha hilo.

Jina la Sir Nature lilihusishwa mapema kabisa katika mipango ya tamasha hilo kutokana na maombi ya mashabiki wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake kupitia ujumbe mfupi/sms za vipindi tofauti tofauti ndani ya Jembe Fm kiasi cha kuipa presha kamati husika kumuweka mkali huyo kwenye listi ya wakali watakaopanda jukwaa moja na Neyo.

 Licha ya msanii huyo kufanya makamuzi jijini Mwanza mapema mwezi Machi akipanda jukwaa moja na wakali wengine kutoka nchini Nigeria Tekno, Seyi Shey na Ommy Dimpoz kutoka nchini Tanzania nyota yake imeonekana kung'ara tena na tena kuelekea JEMBEKA NA VODACOM "Haijalishi mara ngapi ndani ya mwaka huu Nature kaja Mwanza na tukaenda kwenye show zake. Tunamtaka Nature!!" alisikika mmoja wa mashabiki wa burudani kutoka mkoani humo. 

List ya wasanii wengine watakao husishwa na tamasha hilo mpaka sasa bado haijatajwa rasmi,  licha ya fununu kwa baadhi ya wakali. 

Kumbuka ni katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kiingilio cha Shilingi 10,000, 50,000 na 100,000 so anza kujichanga mapema mwana wa kwetu. Imedhaminiwa na Vodacom Tanzania! Vodacom Kazi ni Kwako. Special Thanks FastJet, EF Outdoor, Ndege Insurance, Syscorp Corporation, KK Security, JembeFm-JembeniJembe, Gsengo Blog, Michuzi Blog, Binagi Blog na wadau wengine. 
Nunua Tiketi yako mapema www.jembenijembe.com

TANZANIA YAMKUMBUKA SHEIKH ABEID AMANI KARUME,MTU WA WATU.SHEIKH Abeid Amani Karume, Rais wa kwanza wa Zanzibar, alikuwa mtu mcheshi mchangamfu aliyependa kujichanganya na watu.
Alikuwa ni mtu mwenye kujisikia raha sana kujichanganya na watu wa kawaida sanjari katika kushiriki nao mchezo wa jadi wa bao. Usafiri aliokuwa akitumia ni Baiskeli.

Mapenzi yake kujichanganya na watu kupita na kudhuru mazingira ya watu wa kawaida na kutobagua watu yalisababisha kuwa njia rahisi kwa maadui zake kumfanyia njama na hatimaye kumuua mnamo tarehe 7 April 1972.

Karume amekufa na kubaki kama shujaa huku miaka yake 8 ya utawala nchini Zanzibar umeacha alama Thabiti ya UMOJA.
In 1964, Karume led a successful revolution which led to the birth of a new Zanzibar and his quick move made the Isles what it is, only about one-hundred days after revolution. Karume was swift in reforms and nation building.
He spared no effort in making sure that Zanzibaris lived decent life: housing improvement, infrastructure development (Roads, Water supply, and Electricity), agriculture, as he declared health and education free of charge for all Zanzibaris.
Many admired and loved Karume for his compassion and integrity, but 44 years after his death, how are Zanzibaris remember him and what does the future hold without him?
Both main rival political parties in Zanzibar: Civic United Front (CUF) and the Chama Cha Mapinduzi (CCM) agree that late Karume was a man of people and a committed leader, his steps worth following.
CUF remembera Karume by playing some of his speeches in public rallies, while CCM fans and leader praise him by implementing his plans. President Ali Mohammed Shein has been doing a lot to get back on Karume's track.

MADRID YAFINYWA, CITY YATOKA SARE NA PSG


Ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea kwa michezo miwili ya robo fainali kuchezwa.
Wolfsburg wakiutumia vyema uwanja wao wa Volkswagen Arena,wamepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Madrid.
Ricardo Rodriguez ndie alianza kuipatia timu yake bao la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Andre Schurrle kufanyiwa madhambi na Casemiro.
Katika dakika ya 18 Max Arnold akaongeza bao la pili na kuwazamisha kabisa vijana wa Zidane.
Nao Man City wakicheza ugenini huko nchini Ufaransa walikwenda sare ya kufunga kwa mabao 2-2, mabao ya Psg yalifungwa na mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic na Adrien Rabiot.
Huku mabao ya Man City yakifungwa na viungo Kevin De Bruyne na Fernandinho, mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic alikosa mkwaju wa penati uliokolewa na kipa Joe Hart.

Wednesday, April 6, 2016

MKUU MPYA WA MKOA WA MWANZA USO KWA USO NA WAANDISHI WA HABARI

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amewaomba waandishi wa habari jijini Mwanza kushirikiana na serikali ya mkoa Taasisi mbalimbali katika kuutangaza mkoa katika nyanja mbalimbali za uwekezaji, utalii, biashara, kilimo na uvuvi ili ukue kiuchumi na kimaendeleo.
Sehemu ya waandishi wa habari waliojitokeza kumsikiliza mkuu huyo.
Mwanahabari Nashon Kennedy kutoka Daily News akichangia kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Sehemu ya wanahabari.
Peter Fabian mwandishi wa habari kutoka gazeti la Mtanzania akifunguka namna ya ushirikishwaji wa waandishi katika kuusaidia umma wa wananachi wa Mwanza kupata elimu itakayowakwamua kuziona kwa jicho la ziada fursa za uwekezaji zilizopo jijini Mwanza.
Sehemu ya wanahabari waliojitokeza kwenye kusanyiko hilo.
Kwa umakiiiiini.
Pointi = Wanahabari wako tayari kushiriki zoezi husika lakini changamoto kuu ni uwezeshwaji pamoja na vitendea kazi, kama mkoa utaamua kuwekeza kwa waandishi kuzibaini changamoto zao na kuzitatua naam tutegemee kuona matokeo chanya.
Sitta Tuma.
Fredrick Katulanda na Mseti.
Vinasio na uchukuaji wa taarifa.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza amesema anahitaji ushirika mzuri na waandishi wa habari katika kubaini na kukabiliana na wimbi la uhalifu kwani kupitia wao i rahisi kupata taarifa za waharifu. 
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.