|
Mechi kati ya Sierra Leone na Seychelles yatibuka kutokana na hofu ya Ebola. |
Mechi kati ya Sierra Leone na Seychelles ya kuwania tikiti ya kushiriki katika kombe la mabingwa barani Afrika mwakani imetibuka.
Hiyo inafuatia hatua ya maafisa wa Ushelisheli kuwanyima Sierra Leone ruhusa ya kuingia nchini humo wakihofia wanaweza kueneza Ebola.
Yamkini timu hiyo ilikuwa ikipania kusafiri lakini maafisa wa usafiri wa ndege katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi wakawaarifu kuwa Ushelisheli haijaidhinisha safari yao kuingia nchini humo.
Timu hiyo ililazimika kurejea hotelini mjini Nairobi Kenya ambako wamekuwa wakipiga kambi tangu Jumatano.
Rais wa shirikisho la soka la Sierra Leone Elvis Chetty ameiambia BBC kuwa amepokea habari kutoka kwa Wizara ya afya ya Ushelisheli kuwa angependa waiahirishe mechi hiyo kutokana na hofu ya kuenea kwa Ebola.
Barua hiyo ya Wizara ya Afya inaelezea hofu ya kisiwa hicho ya kutokea mlipuko wa homa ya Ebola.
Chetty aliendelea kusema kuwa kufuatia tahadhari iliyotangazwa leo na rais wa Sierra Leone kuwa huenda ugonjwa huo ukadhibitiwa katika kipindi cha miezi minne ijayo basi huenda mechi hiyo haitachezwa kamwe.
Hatua hiyo huenda ikasababisha Ushelisheli ikapigwa marufuku ya kushiriki mashindano hayo.
Sierra Leone, ilishinda mkondo wa kwanza mabao mawili kwa nunge .
|
Ebola ilivyoenea Afrika Magharibi. |
Mechi hiyo ilichezwa juma lililopita.
Chetty alisema kuwa kuambatana na sheria za shirikisho la soka barani Afrika CAF, mechi hiyo inasiku 3 tu za kuchezwa vinginevyo wapinzani walistahili kupewa ilani siku 10 kabla ya tarehe iliyopangiwa mechi yenyewe.
''Ninaamini kuwa tayari Mshelisheli ameamua liwe liwalo hatocheza mechi hiyo na hilo huenda likaisababishia taifa hilo marufuku ya kipindi kirefu.
''Kimsingi taifa lote lilikuwa limechangamkia mechi hii na ni jambo la kusikitisha sana''.
CHANZO:BBC SWAHILI.