Saturday, November 20, 2010
BANGO
CHEREKO ZA KITCHEN PARTY NA SAFARI HII NI KWA NYAMIZI MOHAMED KASSANGA.
WOW!!
WAUKWELI.COM
USAFI JADI YETU MWANAKWETU...
MAPISHI JEH! SEKTA MUHIMU YA KUZALISHA ENERGY KWA FAMILIA.
DECORATION AKA MAPOUDAzz!
SHUGHULI ILIFANYIKA TAREHE 20/JUNE/2010 GADHI HALL MWANZA NA BAADAE HARUSI YA NGUVU. (PICHA ZA HARUSI ZAJA).
FLOWERS WALIPENDEZAJE!!
CHAKULA KITAAAAAM'
ZAWADI NI ZAWADI...!
ALITUNZWA HASWAAA...!!
MABIDADA NA MASHOSTI KIMPONGEZA BI HARUSI MTAJIWA.
Friday, November 19, 2010
BANGO
HII NI REMIX KATIKA STYLE YA KATUNI.
MKUU WA IDARA YA HABARI YA RAISI WA UGANDA YOWERI MUSEVENI AMESEMA KUWA SIFA YA RAISI HUYO IMEHARIBIWA VIBAYA KUTOKANA NA MZIKI WA RAP ALIOUIMBA MWEZI ULIOPITA.
TAMALE MIRUNDI AMESEMA WALAGHAI WAMEHARIBU PICHA ZA MUSEVENI, WAKITUMIA KOMPUTA, NA KUMFANANISHA NA NYOTA WA MUZIKI WA HIPO HOP ANAYEIMBA AKIWA NUSU UCHI.
BAADHI YA PICHA HIZO ZINAONYESHA AMEVALIA MKUFU SHINGONI HUKU AKIWA NA PICHA ALIZOCHORWA MWILINI MAARUFU KAMA ''TATTOOS''..
RAIS MUSEVENI ANAWANIA MUHULA MWINGINE KAMA RAIS WA UGANDA KUPITIA CHAMA CHA NATIONAL RESISTANCE MOVEMENT NRM.
Thursday, November 18, 2010
HABARI
KAIMU KAMANDA WA POLISI MWANZA NONOSIUS KOMBA.
JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KWA KOSA LA KUMILIKI NOTI BANDIA ZENYE THAMANI YA SHILINGI LAKI NANE NA SABINI ELFU.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KAIMU KAMANDA WA POLISI MWANZA NONOSIUS KOMBA AMEMTAJA MTUHUMIWA HUYO KUWA NI BW. SILAS OMOLO (29) MKAZI WA ENEO LA NYEGEZI WILAYA YA NYAMAGANA.
AMESEMA KUWA MNAMO TAREHE 16NOV2010, SAA TISA NA DAKIKA ISHIRINI JESHI HILO LILIFIKA ENEO LA TUKIO NYEGEZI JIJINI MWANZA NA MARA BAADA YA UPEKUZI MTUHUMIWA SILAS OMOLO ALIKUTWA NA NOTI 87 ZA SHILINGI ELFU KUMI, KUMI AMBAPO NOTI 30 ZILIKUWA NA NAMBA AINA MOJA AMBAYO NI AK S802330 NA NOTI 57 ZILIZOSALIA NAZO ZOTE ZILIKUWA NA NAMBA AINA MOJA AMBAYO NI AK S802338.
KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA HUYO PAMOJA NA KIASI HICHO CHA FEDHA KUMEKUJA MARA BAADA YA JESHI HILO KUPATA TAARIFA TOKA KWA WANANCHI WEMA AMBAO WALINASA UWEPO WA NOTI HIZO BANDIA NA HATIMAYE TAARIFA KUZIFIKISHA KATIKA JESHI HILO LA POLISI, NALO BILA AJIZI LIKAFANYA KAZI YAKE.
MTUHUMIWA ANASHIKILIWA NA JESHI HILO NA ANATEGEMEA KUFIKISHWA MBELE YA MAHAKAMA.
Wednesday, November 17, 2010
MICHEZO
JEH! NANI KATI YA HAWA:-ASAMOAH GYAN, ANDRE AYEW, SAMWEL ETO'O, YAYA TOURE AU DIDIER DROGBA?
Una nafasi ya kuamua bingwa atakuwa nani, kati ya sasa hadi tarehe 10 mwezi Disemba, na mshindi atatangazwa wiki moja baada ya hapo, Ijumaa ya tarehe 17 mwezi Desemba, katika matangazo ya moja kwa moja ya michezo kwa lugha ya Kiingereza, Fast Track, saa 1600 GMT.
Hili ni tuzo la pekee linalosifika na ambalo hutoa nafasi kwa wewe kama shabiki kuamua mshindi. Mshindi wa mwaka jana alikuwa ni mshambulizi wa Chelsea, Didier Drogba, na ambaye pia huichezea timu ya taifa ya Ivory Coast.
Unaweza kushiriki kwa kupiga kura kupitia mtandao, au kwa kuandika ujumbe wa SMC.
Shughuli ya upigaji kura itaanza saa 1700 GMT, Jumatatu, tarehe 17 Novemba, na itafungwa saa 1700 GMT, Ijumaa, tarehe 10 Desemba 2010.
Kura za mtandao na zile za ujumbe wa SMS zitachanganywa na kuhesabiwa pamoja, na matokeo ya mshindi yatapatikana katika tovuti ya 'BBC African Fooballer of the Year', ambao pia ina masharti mbalimbali na vikwazo vyote vya kushiriki katika upigaji kura.
ZAIDI JINSI YA KUSHIRIKI SIKILIZA BBC SWAHILI.
Wednesday, November 17, 2010
BANGO
NI MUDA MUAFAKA KATIKA MWAKA KUJUMUIKA PAMOJA KULA CHAKULA NA WATU WOTE WA JAMII INAYOTUZUNGUKA. NAAM! NDANI YA SIKUKUU HII IMEHALALISHWA KUCHINJA, HIVYO KWA WALE WENYE UWEZO INSHAHLAH NI VYEMA KUSHIRIKI KUTIMIZA IBADA.
GLOGU YAKO ILIYOMSTARI WA MBELE KTK JUKUMU LA KUANGUSHA NEWS' (g sengo)INAPENDA KUTOA SALAMU ZA SIKUKUU YA EID KWA WAISLAM WOTE AMBAO WANAUNGANA NA WAISLAM KOTE DUNIANI KUADHIMISHA IBADA YA SIKUKUU YA EID-UL-ADHA.
ASSALAMU ALAIKUM WA RAHMATULLAHI WA BARAKATUH !! SHEREHEKEA VYEMA EID-UL-ADHA.
Tuesday, November 16, 2010
SIASA
Tuesday, November 16, 2010
BANGO
Mchujo wa kuwatafuta wanamitindo wenye sifa za kitofauti yaan i" Giaffe unique model " utafanyika jumamosi hii ya tarehe 20 mwezi wa kumi na moja katika hoteli yenye hadhi ya nyota nne Giraffe ocean view hotel katika ukumbi wa jet 1.
Akiongea na blog zote maarufu nchini Tanzania mratibu wa shindano hilo bwana Magese Methuselah Magese amesema kuwa shindano hilo ni la kizalendo lenye nia mahususi ya kukuza tasnia ya mitindo na wanamitindo wachanga nchini Tanzania kwa kuleta umoja,mafanikio na kuhimiza mapinduzi ili tasnia hii iwe ajira kamili kwa wanamitindo wa hapa nchini kinyume na ilivyo sasa.
Ameongeza kuwa ikiwa vyombo vya habari vitaunga mkono mapinduzi haya kwa kutangaza kwa wingi habari za mitindo, wamamitindo na wabunifu wa ndani, itageuza mtazamo wa watanzania wengi kuondokana na utamaduni wa kuvaa nguo kutoka nje ya nchi pekee badala yake wapende kuvaa nguo zilizobuniwa na wabunifu wa Tanzania.
" Hii itachangia wabunifu kuwa na kipato kikubwa na maonyesho ya mavazi yatakuwa mengi ambapo wanamitindo watafaidika kwa kulipwa kwa kiwango chajuu, aidha vyombo vya habari vikitangaza sana tasnia hii jamii itapenda zaidi hata makampuni mengi yatajitokeza kuwekeza na kujitangaza kwa kudhamini shughuli za mitindo nchini Tanzania kitu ambacho kitaongeza pato la taifa na kpato cha mtu mmojammoja.
Wito umetolewa kwa wasichana wote wenye sifa na vigezo vya kushiriki shindano hilo lenye hadhi ya kitaifa kujitokeza kwaajili ya mchujo tarehe 20 novemba saa sita mchana katika hoteli hiyo iliyopo maeneo ya africana mbezi beach ambapo majaji watakuwa Steven Kanumba, Miriam Gerald, Ali Remtulah, Vitoria Martin na Asia Idarous, watakao shiriki kuchagua wasichana kumi bora wataoingia moja kwa moja katika shindano hilo.