|
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya vifurushi vya kimataifa ndani na nje ya nchi, vitakavyomwezesha mteja kupiga simu kwenda nchi zaidi ya 20 kwa gharama nafuu. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kimataifa wa Airtel, Prisca Tembo na Meneja wa kitengo hicho, Alice Paulsen. |
|
Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kimataifa wa Airtel, Prisca Tembo (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya vifurushi vya kimataifa ndani na nje ya nchi, vitakavyomwezesha mteja kupiga simu kwenda nchi zaidi ya 20 kwa gharama nafuu. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando na Meneja wa kitengo hicho, Alice Paulsen. |
Airtel yazindua vifurushi vya kimataifa ndani na nje ya nchi
· sasa wateja kununua vifurushi vya kupiga simu za kimataifa kwenda nchi zaidi ya 20
· wateja kujitengenezea vifurushi vya intaneti pindi wanapotembelea nchi ambazo Airtel inazofanya biashara barani Afrika
Dar es Salaam, Alhamis 10 Novemba 2016, Airtel Tanzania leo imetangaza ofa kabambe itakayowawezesha wateja wake nchi nzima kununua vifurushi wavipendavyo na kupiga simu kwenda nchi zaidi ya nchi 20 kwa gharama nafuu
Pamoja na vifurushi vya kupiga simu nje ya nchi , Airtel pia imezindua vifurushi vya intaneti vya roaming mahususi kwa wateja wanaotembelea nje ya nchi vijulikanavyo kama “Safari Internet Roaming” vitakavyowapatia uhuru wateja wake kupanga matumizi yao ya intaneti pindi wanapotembelea nchi ambazo Airtel inafanya biashara zake barani Afrika. Nchi hizo ni pamoja na Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Kenya, Gabon, Ghana, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Uganda na Zambia.
Akitangaza ofa hiyo Meneja Biashara za Kimataifa wa Airtel, Prisca Tembo alisema” Tunayofuraha kutangaza ofa nyingine kabambe itakayowapa wateja wetu uhuru katika mahitaji yao ya mawasiliano na kuwawezesha kuwasiliana na familia, marafiki na wafanyabiashara wenzao barani Afrika na kimatifa kwa urahisi zaidi. Ofa yetu ya kupiga simu nje ya nchi inamhakikishia mteja thamani ya pesa yake na urahisi katika huduma za mawasiliano na kupata faida lukuki za kujiunga na timu SIBANDUKI. Vifurushi vyetu vya kupiga simu nje ya nchi zinapatikana kwa siku, wiki au mwezi kwa kupiga *149*13# au kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60#. Mteja anaweza kujinunulia kifurushi akipendacho na kupiga simu kwenda zaidi ya nchi 20 kwa gharama nafuu”
Tembo aliongeza kwa kusema “vifurushi vipya vya intaneti vya roaming yaani wateja wanaotembelea nje ya nchi zinaenda sambamba na dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma za mawasiliano za kibunifu, gharama nafuu na zenye ubora kwa watanzania zinazovuka zaidi ya mipaka ya nchi. Idadi ya watanzania wanaosafiri nje ya nchi kibiashara na safari za kawaida inakuwa kwa kasi, vifurushi vyetu vipya vya nje ya nchi vitawawezesha kupanga matumizi yao na kuwaepusha na ankra kubwa na kuwahakikishia mawasiliano mahali popote waliko”
Ofa hizi za kupiga simu nje ya nchi na vifurushi vya intaneti nje ya nchi ni kwa wateja wa malipo ya awali yaani ”prepaid” nchi nzima
Nchi ambazo mteja anaweza kupiga simu nje ya nchi kwa kununua vifurushi vya kimataifa ni pamoja na Zambia, Malawi, DRC, South Africa, India, China, USA, Canada, Uganda, Rwanda, Kenya, Oman, UAE, Saudi Arabia, Yemen, Lebanon, Pakistan, Qatar, Uingereza, Itali na Ujerumani.