ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 25, 2025

YANGA YAIGAGADUA COPCO FC 5-0 LEO 25/01/2025

 

Ni katika michuano ya CRDB Federation Cup, ushindi wa goli 5-0 unapatikana dhidi ya Copco FC ya jijini Mwanza ambapo magoli ya Yanga Sc yamefungwa na:-

1. Sheikhan Rashid

2. Dube 

3. Max Nzengeli

4. Abuya

5. Mudathir Yahaya

MSIGWA AAGIZA NYARAKA MUHIMU ZA UANZISHWAJI WA BODI YA ITHIBATI YA WAANDISHI WA HABARI ZIKAMILISHWE HARAKA

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa, akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Wakili Patrick Kipangula, alipozitembelea ofisi za Bodi hiyo leo tarehe 23 Januari, 2025, Mtaa wa Jamhuri Posta, Jijini Dar es Salaam.
Bw. Msigwa amefanya ziara hiyo ili kufahamiana na watumishi wapya wa Bodi, kukagua ofisi na kujionea maendeleo ya uandaaji wa nyaraka mbalimbali za Bodi kabla haijazinduliwa rasmi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa pamoja na Watumishi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari wakifuatilia wasilisho la utekelezaji wa uandaaji wa nyaraka mbalimbali za uanzishwaji wa Bodi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo Wakili Patrick Kipangula, wakati wa ziara ya kwenye ofisi za Bodi leo tarehe 23 Januari, 2025 zilizopo Mtaa wa Jamhuri Posta jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa, amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Wakili Patrick Kipangula, kuhakikisha nyaraka zote muhimu zinazohitajika kwa ajili ya uanzishwaji rasmi wa Bodi hiyo zinakamilishwa mapema ili iweze kuanza kufanya kazi yake.

Bw. Msigwa ametoa agizo hilo leo wakati alipozitembelea ofisi za Bodi hiyo leo tarehe 23 Januari, 2024, Mtaa wa Jamhuri Posta, Jijini Dar es Salaam ili kufahamiana na watumishi wa Bodi, kukagua ofisi na kujionea maendeleo ya uandaaji wa nyaraka hizo kabla uzinduzi rasmi haujafanyika.

“Kwanza mimi niwapongeze sana kwa hatua mliyofikia, lakini Kaimu Mkurugenzi hakikisha unasimamia hizi nyaraka zote mlizozitaja zifanyiwe kazi kwa haraka sana na kukamilika, umuhimu wa kuanza kazi kwa bodi hii unaujua na bahati nzuri wewe ni mtu wa Sheria, ulishiriki tangu mchakato wa uandaaji wa Sheria na kanuni zake, hivyo unayafahamu majukumu yake na unafahamu kwa nini tunahitaji Bodi ya Ithibati,” amesema Bw. Msigwa na kusisitiza;

“Serikali ya Awamu ya Sita tunaona umuhimu wa kuwepo kwa hii Bodi, hivyo ni muhimu sana haya yote yaliyopangwa kufanyika yafanyike na yalete tija na manufaa kwa Tasnia ya Habari, ni muhimu sana”.

Bw. Msigwa amesema baadhi ya nyaraka zinazotakiwa kufanyiwa kazi haraka ni pamoja na Muundo Bodi, Mpango Mkakati wa Bodi wa Miaka Miwili (Strategic Plan), Mkakati wa Mawasiliano wa Bodi (Communication Strategy) na Kanuni za Maadili ya Waandishi wa Habari.

Amesisitiza kuwa Mpango Mkakati wa Bodi ndiyo nyaraka na mwongozo muhimu unaoelezea malengo ya Bodi, majukumu yake, umuhimu wake, vyanzo vya mapato na namna gani taasisi itaendeshwa.

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ilitangazwa tarehe 18 Septemba, 2024 baada ya aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry Silaa kuteua Mwenyekiti wa Bodi Bw. Tido Mhando na wajumbe wake sita pamoja na sekretarieti yenye watumishi 6.

Bw. Msigwa amekuwa kiongozi mkubwa wa kwanza kuitembelea Bodi hiyo tangu ilipohamishiwa chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo baada ya mabadiliko ya Wizara yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mwishoni mwa mwaka jana.

Thursday, January 23, 2025

TAZAMA HAPA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2024

 

Bofya Hapa chini kutazama matokeo




Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2024, ambapo watahiniwa 477,262 kati ya wanafunzi 516,695 wenye matokeo wamefaulu kwa kupata madaraja ya I, II, III na IV.

NECTA imesema ufaulu huo umepanda kwa asilimia 3, hivyo kufikia asilimia 92.37 kutoka asilimia 89.36 mwaka 2023.

Aidha kwa mwaka 2024, takwimu zinaonesha idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya I, II na III imeongezeka na kufikia 221,953 sawa na asilimia 43, ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo idadi ilikuwa  197,426 sawa na asilimia 37.4.

Idadi ya watahiniwa waliopata daraja la IV na zero imepungua, hivyo ubora wa ufaulu umepanda kwa asilimia 5.6.

Wednesday, January 22, 2025

LISSU AM'BWAGA MBOWE UCHAGUZI CHADEMA.

Tundu Lissu amechukua usukani wa Chadema, baada ya kumng'oa madarakani Freeman Mbowe ambaye amekiongoza chama hicho kama mwenyekiti kwa takribani miaka 21. 


Mbowe amekuwa wa kwanza kukiri kushindwa na kumpongeza Lissu kupitia mtandao wa X. Timu ya kampeni ya Lissu pia imetumia mtandao wa X kutangaza ushindi wake. 

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo uliofanyika Jumanne usiku yanaonesha kuwa Lissu amepata 51.5% ya kura zote dhidi ya 48.3% alizozipata Mbowe. 


Mara baada ya wagombea wakuu Mbowe na timu ya kampeni ya Lissu kutuma salamu za matokeo kupitia mtandao wa X, wakala wa Lissu kwenye uchaguzi huo na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Godbless Lema aliwaambia waandishi wa Habari kuwa Chadema ndiyo imeshinda. "Chama kimeonesha demokrasia iliyokomaa… huu ulikuwa uchaguzi huru n awa haki kabisa, na umerushwa mubashara na vyombo vya habari. 

Watu wote wameliona hilo," amesema Lema. 


 Lissu ampongeza Mbowe 
Mwenyekiti mpya wa Chadema Tundu Lissu baada ya kutangazwa mshindi amesema chama hicho kimeweka kiwango cha dhahabu cha demokrasia ya ndani na kuvitaka vyama vingine vya siasa nchini humoi kuiga mfano wao. 

Lissu amesema uchaguzi huo ulikuwa wa wazi, huru na haki bila mizengwe japo amekiri kuwa kulikuwa na misuguano na kasoro za hapa na pale. "Tumefanya jambo ambalo halijawahi kufanywa toka chama chetu kianzishwe… tumeweka kiwango cha dhahabu – tunawaambia vyama vingine kama vinaweza viige," ameeleza Lissu. 

 Lissu pia alitumia hotuba yake hiyo ya kwanza kama mwenyekiti kumshukuru mtangulizi wake Freeman Mbowe akisema alichukua kjiti cha uongozi wa chama hicho wakiwa na wabunge watano na katika uongozi wake amekifanya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania. 

 Lissu pia amesema Mbowe ndiye aliyefanikisha uchaguzi wa jana na leo kuwa huru na haki na anastahili pongezi. "Historia ya chama chetu itakapoandikwa, watatambua huu mchango wako mkubwa uliotoa." Mwenyekiti huyo mpya amesema Mbowe hajastaafu na ataendelea kuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya chama hicho kama ambavyo katiba ya Chadema inavyoainisha. 


 Mbowe 'amuagiza' Lissu kutibu majeraha 
Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema anayemaliza muda wake baada ya kushindwa katika uchaguzi na Tundu Lissu amesema mchakato wa uchaguzi huo umekiacha chama hicho na majeraha. 

 Mbowe amesema japo uchaguzi umefanyika katika misingi ya uhuru, haki na uwazi kama ambavyo aliahidi awali lakini amesema mchakato wa kampeni umeacha majeraha na amemtaka Lissu na viongozi wengine waliochaguliwa kuleta maridhiano ndani ya chama. "Mimi niliahidi kuwa kama ningeshinda ningeliunda kamati ya ukweli na maridhiano ili watu wazungumze na kutibu majeraha yaliyoletwa na kampeni … sasa kama mnaniheshimu kama baba, basi nawaagiza Lissu na viongozi wenzako wapya mlete maridhiano baada ya majeraha yaliyoletwa na kampeni," amesema. 

 Mbowe pia amewataka viongozi wapya kusimama na katiba ya chama hicho na kujizui kuwa na kiburi. Kuhusu mustakabali wake kisiasa, Mbowe amesema anachukua likizo na ataendelea kujikita katika kufanya biashara zake na kuendelea kukishauri chama.

 "Nimepewa likizo ya lazima, na nitaenda kwenye biashara zangu nitafute pesa ana nitaendelea kutoa ushauri kwa chama…Nashukuru nimepewa likizo hii kidemokrasia na katika mfumo ambao nimeujenga mwenyewe… kuna watu waliniambia nijitoe kwenye uchaguzi nitaadhirika, nikawaambia nitafia demokrasia." 

Jinsi kampeni zilivyokuwa za vuta nikuvute, rarua nikuraruwe. Kumalizika kwa uchaguzi huu kunahitimisha takribani kipindi cha mwezi mmoja cha kampeni kali kati mwenyekiti Mbowe anayeondoka madarakani dhidi ya makamu wake, Lissu. 

Lissu aliendesha kampeni zake akijielekeza kwenye kuleta mabadiliko ya namna Chadema inavyopendesha shughuli zake za kisiasa. 

 Anamtuhumu Mbowe akidai amebadilika mno tangu alipotoka gerezani alikokuwa ameshkiliwa kwa miezi 8 akikabiliwa kesi ya Ugaidi. 

 Pia anamtuhumu Mbowe kwa kupokea fedha kutoka kwa watu walio karibu na serikali, japo hakuwahi kutoa ushahidi wowote. Mbowe alikuwa akisema kuwa bado ana kazi ya kufanya kukiimarisha zaidi chama huku akimwita Lissu muongo anayewachafua watu bila ushahidi 

 Hata hivyo, wawili hao waliuambia mkutano mkuu wa chama wakati wa kuomba kura kuwa watabakia ndani ya chama bila ugomvi, bila kujali matokeo ya uchaguzi.

 Lakini wafuatiliaji wa masuala ya siasa za Tanzania wanasema kuna hatari ya Chadema kudhoofika na kugawanyika kutokana na tuhuma ambazo viongozi hao wawili walitupiana wakati wa kapeni za uchaguzi.

BODI YA NAMAPWIA AMCOS YAVUNJWA VIONGOZI WAKAMATWA NA POLISI

 

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akitoa amri ya kukamatwa kwa viongozi wa AMCOS ya Namapwia kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali za AMCOS hiyo.
Baadhi viongozi wa AMCOS ya Namapwia waliokamatwa 
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Nachingwea iliyokabidhiwa viongozi wa AMCOS ya Namapwia kwa ajili ya uchaguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa mali za AMCOS hiyo.


Na Fredy Mgunda, Nachingwea Lindi.

Viongozi wa AMCOS ya Namapwia wamekamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi kufuatia uchunguzi uliofanywa kuhusu ubadhilifu wa fedha za wakulima na upotevu wa mazao. 

Uchunguzi huo ulifanywa baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wanachama wa chama hicho, na ripoti ya ukaguzi kubaini kwamba viongozi hao walihusika katika ufisadi wa mazao na malipo yasiyostahili kwa wakulima.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo alitoa agizo la kuchukuliwa kwa hatua za kisheria dhidi ya wahusika na kusema kuwa wote watapelekwa polisi kwa mahojiano zaidi.
 
Agizo hilo lilitolewa wakati wa ziara yake  kata ya Namapwia ambapo alikabidhiwa ripoti ya ukaguzi iliyofanywa na timu ya ukaguzi iliyoongozwa na Afisa Ushirika Wilaya ya Ruangwa, Patrobas.

Ripoti ya ukaguzi iliyofanywa kati ya tarehe 15 hadi 22 Oktoba 2024 ilibaini upotevu wa tani 21 za mazao, pamoja na ulipaji wa fedha kwa wakulima ambao hawajauza mazao yao kupitia AMCOS hiyo. 

Vilevile, ilibainika malipo ya zaidi ya milioni tatu msimu wa ufuta ambazo hazikuingizwa kwenye akaunti rasmi ya AMCOS, huku baadhi ya malipo hayo hayakuwa yameidhinishwa na kamati ya chama hicho,upotevu wa fedha shilingi milioni 60 ambazo walizilipa kwa kugawana wajumbe wote.

Kiongozi wa timu ya ukaguzi, Patrobas, alieleza kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho walitengeneza wakulima feki na kufanya malipo ya fedha za mazao ambayo hayakuuzwa. 

Patrobas aliongeza kuwa mfumo wa biashara wa chama hicho ulikuwa na dosari, hali iliyosababisha upotevu mkubwa wa fedha.

Kwa upande wake Mrajisi wa Vyama Ushirika Mkoa wa Lindi, Keneth Shemdoe, aliifuta bodi ya AMCOS ya Namapwia na kuunda kamati ya mpito ili kuendeleza shughuli za chama hicho. 

Shemdoe pia alitoa agizo la kuwaajiri meneja wenye kiwango cha elimu cha stashahada au shahada ili kuendana na mahitaji ya sasa, huku akisisitiza chama hicho kuandaa akaunti rasmi ikiwa na orodha ya hisa za wanachama pamoja na daftari la taarifa zao ndani ya muda wa mwezi mmoja.

Diwani wa kata ya Namapwia, Mheshimiwa Omari Muhamed Lingumbende, amepongeza kwa hatua zilichukuliwa kwa kukamatwa viongozi ha

Monday, January 20, 2025

PPRA YAENDESHA MAFUNZO MODULI MPYA MFUMO WA NeST MWANZA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

MAMLAKA ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) inaendesha Mafunzo kuhusu Sheria mpya ya Ununuzi pamoja na Moduli mpya za Mfumo wa NeST kwa watumishi wa umma kutoka kada na Taasisi mbalimbali nchini, 

Mafunzo hayo yaliyoanza rasmi hii leo Januari 20, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Rock City Mall Jijini Mwanza, yamehudhuriwa na washiriki zaidi ya 200 wa kada mbalimbali wakiwemo Maafisa Ununuzi, Maafisa Sheria, Wakuu wa Vitendo vya Ununuzi, na wengineo.

Meneja wa Kujenga Uwezo na Huduma za Shauri PPRA Gilbert C. Kamnde amesema, muendelezo wa utoaji mafunzo hayo ni utekelezaji wa jitihada za Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma, ya kuhakikisha wanawajengea uwezo wadau wa Ununuzi wakiwemo Maafisa wa Serikali pamoja na wazabuni ili kuhakikisha weledi na uzoefu wa matumizi ya mfumo unaongezeka ili kurahisisha utendaji kazi katika michakato ya Ununuzi wa Umma Nchini.

JESHI LA POLISI LAMKAMATA KIJANA ALIYESAMBAZA PICHA FEKI ZA UTUPU KWA WANAFUNZI WA BAOBAO

 MWANDISHI NA. VICTOR MASANGU/PWANI

SAUTI NA. ALBERT G.SENGO


JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali na kufanikiwa kumkamata  mtu mmoja ambaye anadaiwa kuhusika katika kutengeneza picha  za mjongeo  za utupu zenye maudhui machafu ambayo ni kinyume kabisa na maadili na sheria za nchi na kuamua kuzisambaza katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Pwani Salim Morcase amesema kwamba mtuhimiwa huyo  baada ya kufanya uchunguzi na kwamba alitengeneza picha hizo za utupu kwa kutengengeneza na kuunganisha na baadhi ya picha za majengo ya shule ya sekondari  Baobab kwa lengo la kuaminisha umma kuwa vitendo hivyo vimefanyika shuleni hapo kitu ambacho sio cha kweli hata kidogo.
  
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shule ya sekondari Baobab Shani Swai amekanusha vikali na kusema kwamba  kwamba wamesikitishwa sana na kitendo cha baadhi ya watu kuamua kuwachafua taasisi yao  kwa kusamabaza picha hizo za utupu  katika mitandao ya kijamii na kusababisha kuleta hali ya sintofahamu na taharuki kubwa katika maeneo mbali mbali hasa kwa wazazi na walezi.
 
Naye Kaimu mkuu wa shule taalamu Alphonce Kamisa na  Mwenyekiti wa Bodi ya Talaamu wa shule ya hiyo wamesema kutokana na jambo hilo limeweza kuleta taharuki kubwa licha ya kwamba wanafunzi tayari wamesharipoti shule kwa ajili ya kuanza na masomo yao.

VIA AVIATION YACHANGIA MITI 100,000 KWA WILAYA YA MAGU KUPITIA MRADI WA VIA GREEN

 NA ALBERT GSENGO/MWANZA

WAKATI Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mohamed Ramadhani akitoa maagizo kwa kitengo cha lishe katika halmashauri hiyo kuandaa program maalumu ya upandaji wa miti ya matunda katika kila shule za msingi na sekondari zilizopo wilayani humo ili kuwezesha wanafunzi kupata virutubisho mbalimbali ndani ya eneo lao la shule.
Agizo alilolitoa katika kikao maalumu kilicholenga kujadili Mapendekezo ya Rasimu ya Mpango kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa kamati ya lishe ya wilaya, tayari kampuni inayoongoza katika mbinu endelevu za usafiri wa anga, imetangaza kwa fahari mchango wake wa miti 100,000 kwa Wilaya ya Magu kama sehemu ya mradi wake mahiri wa VIA Green. Collen Muguyo ni Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Via Aviation akizungumza wakati wa zoezi la upakiaji wa miti hiyo kutoka katika shamba la upandaji miche lililopo Kamanga wilayani Sengerema mkoani Mwanza anasema Mradi wa VIA Green, unalenga kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa, na kuijenga Tanzania ya kijani kibichi.