NA ALBERT GSENGO/MWANZA
WAKATI Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mohamed Ramadhani akitoa maagizo kwa kitengo cha lishe katika halmashauri hiyo kuandaa program maalumu ya upandaji wa miti ya matunda katika kila shule za msingi na sekondari zilizopo wilayani humo ili kuwezesha wanafunzi kupata virutubisho mbalimbali ndani ya eneo lao la shule.
Agizo alilolitoa katika kikao maalumu kilicholenga kujadili Mapendekezo ya Rasimu ya Mpango kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa kamati ya lishe ya wilaya, tayari kampuni inayoongoza katika mbinu endelevu za usafiri wa anga, imetangaza kwa fahari mchango wake wa miti 100,000 kwa Wilaya ya Magu kama sehemu ya mradi wake mahiri wa VIA Green.
Collen Muguyo ni Mkuu wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Via Aviation akizungumza wakati wa zoezi la upakiaji wa miti hiyo kutoka katika shamba la upandaji miche lililopo Kamanga wilayani Sengerema mkoani Mwanza anasema Mradi wa VIA Green, unalenga kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa, na kuijenga Tanzania ya kijani kibichi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.