ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 20, 2024

MBUNGE UMMY APITA VIJIWENI KUHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA NA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

 

Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini (CCM) Mhe Ummy Mwalimu  Octoba 18 mwaka 2024 ametembelea vijiwe mbalimbali katika mitaa ya Mwambani, Mchukuuni, Mwahako, Mwakidila na Mwang'ombe katika kata za Tangasisi na Masiwani kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la mkazi na pia kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakao fanyika tarehe 27/11/2024.


Akizungumza mara baada ya kuvitembelea vijiwe hivyo amesema  kuwa mitaa ndio chimbuko la Amani na Maendeleo kwa Wananchi hivyo ni muhimu kila wananchi wa Tanga Mjini kushiriki.
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini (CCM) Mhe Ummy Mwalimu akisikiliza maoni ya wananchi wake, na kutathimini uelewa wao kwa masuala ya umuhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini (CCM) Mhe Ummy Mwalimu akipokea mawazo ya mmoja wa vijana baada ya kutoa elimu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la orodha ya uchaguzi serikali ya mtaa.
Wavuvi mpo tayari!!....Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini (CCM) Mhe Ummy Mwalimu.

Boda boda mpooo!!...
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini (CCM) Mhe Ummy Mwalimu na wananzengo.

KOKA AONGOZA MAMIA YA WANANCHI ZOEZI LA HAMASA YA KUJIANDIKISHA

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewahimiza wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika kushiriki zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la makazi kwa ajili ya kumwezesha kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Koka ameyasema hayo wakati alipokwenda kutimiza haki yake ya msingi ya kwenda kujiandikisha katika daftari hilo katika ofisi ya serikali ya mtaa kituo cha Mkoani 'A'


Aidha Koka mbali na kujiandikisha alitumia fursa ya kuweza kuzungumza na wananchi mbali mbali na kutoa hamasa juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari hilo.

"Leo nimeweza kushiriki kikamilifu katika zoezi la kujiandikisha na nimeungana na wananchi wangu na kutoa hamasa waweze kujiandikisha "alifafanua Mbunge Koka.

Aidha Mbunge huyo alifanya ziara ya kutembelea vituo vya kujiandikishia ambapo amedai mwamko wa wananchi ni mzuri na kuwahimiza waendelee kujitokeza.


Mbunge huyo aliweza kutembea kwa miguu na kupita maeneo kadhaa likiwemo la stendi ya Loliondo,Soko la mnarani na kuwatembelea wafanyabiashara wa bidhaa mbali mbali na mafundi magari.

Koka aliwahiza wananchi kutofanya makosa na kuhakikisha kwamba wanamchagua viongozi mwenye sifa na uwezo ambaye ataweza kusikiliza changamoto zao na kuwaletea chachu ya maendeleo.