MKUU wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian amewahimiza wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani humo kuhakikisha wanatimiza haki yao ya msingi kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Aliyasema hayo wakati akihimitisha zoezi la kuwahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura katika wilaya za Mkinga, Lushoto na Korogwe ambapo alikutana na wananchi wa makundi mbalimbali.
Alisema kwamba ni muhimu wananchi baada ya kwisha zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura wajipange kushiriki kwenye uchaguzi huo kwa kupiga kura ikiwemo kuwania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo.
“Niwashukuru sana wananchi kwa kushiriki kwenye zoezi hili muhimu la kujiandikisha katika Daftari la Wapiga kura ambapo limehimitishwa Jumapili Octoba 20 hivyo sasa nawaomba tujipange katika kuhakikisha tunatimiza haki ya msingi kuwachagua viongozi.
Aidha alisema hivi sasa ni fursa ya kupiga kura kuwachagua viongozi ambao watakuwa chachu ya kuwaletea maendeleo katika maeneo yenu
“Uchaguzi huu ni muhimu hivyo niwaombe wananchi tuhakikisha tunajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura tuweze kupata haki ya msingi ya kuwachagua viongozi ambao watatuletea maendeleo”Alisema
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.