ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 28, 2020

Masauni:Tumedhibiti Matukio ya Uporaji Fedha

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Mkutano wa  Mashauriano ulioandaliwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji,ukiwajumuisha  wafanyabiashara na wawekezaji katika mkoa wa Simiyu.
Na Mwandishi Wetu, Simiyu
Serikali imesema imefanikiwa kudhibiti matukio ya uporwaji fedha kwa wafanyabiashara na wawekezaji huku ikiwa na mkakati maalumu wa kuhakikisha wawekezaji na wafanyabiashara wanafanya shughuli zao za maendeleo kwa amani na utulivu pasina shaka yoyote.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati akizungumza katika mkutano wa mashauriano ulioandaliwa na Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji,Angellah Kairuki ukiwaalika wafanyabiashara na wawekezaji katika mkoa wa Simiyu.
“Kuanzia Januari mwaka jana mpaka sasa tulipo matukio ya unyang’anyi kwa kutumia silaha yameripotiwa kuwa ni tukio moja moja katika Mkoa wa Songwe,Tabora,Njombe,Mjini Magharibi,Temeke na Kinondoni na tayari watuhumiwa ishirini na mbili washamakamatwa na kesi zao ziko mahakamani zikiendelea na utaratibu wa kisheria” alisema Masauni

Masauni aliweka wazi sababu ya mafanikio hayo ni mafunzo mbalimbali waliyopewa askari wa Jeshi la Polisi ambayo yanawawezesha kupambana na aina tofauti za uhalifu hali inayopelekea kupungua na kuisha kwa matukio hayo.
“Kipindi cha nyuma mmeshuhudia wafanyabiashara na wawekezaji wakivamiwa na majambazi na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha aidha wakiwa wanaenda kuzihifadhi benki au kwa kuvamiwa nyumbani,Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kwa kupitia intelijinsia wamekua wakifanikiwa kiudhibiti matukio hayo na sasa tumeona katika Awamu hii ya Serikali ya Tano matukio hayo yamepotea kabisa na niwaombe wawekezaji pamoja na wafanyabiashara nchi nzima waendelee na shughuli zao pasina kuwa na shaka yoyote” alisema Masauni
Akitaja idadi ya matukio ya unyang’anyi wa fedha kuanzia Januari mwaka jana mpaka Februari mwaka huu Naibu Waziri Masauni alisema kwa nchi nzima ndani ya muda huo ni matukio nane tu huku akilipongeza jeshi la polisi kugundua na kudhibiti mianya ya uhalifu huo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara na wawekezaji walisifu juhudi zinazofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuwalinda hali inayowafanya wafanye shughuli zao kwa amani na usalama.

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MSIKITI WA BAKWATA

Rais John Magufuli leo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti mkubwa wa BAKWATA unaojengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Msikiti huo unajengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco baada ya kuombwa na Rais Magufuli alipofanya ziara hapa nchini Oktoba 2016.

KITUO CHA AFYA NYAKALIRO SULUHISHO LA ADHA WALIOKUWA WAKIIPATA WAJAWAZITO KUSAFIRI UMBALI MREFU.Wakazi wa kata ya Nyakaliro Halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wameipongeza Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha Nyakaliro na kuondoa adha ya akina mama wajawazito waliokuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma ya afya. Pongezi hizo wamezitoa mara baada ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya ilani ya uchaguzi 2015 -2020 inayotekelezwa na Serikali kuu mkoani Mwanza. Wananchi hao wamebainisha kuwa awali wajawazito walilazimika kutembea umbali wa zaidi wa kilomita 20 kutafuta huduma ya afya hospitali ya wilaya - Sengerema kiasi cha kusababisha baadhi yao kujifungulia njiani huku wengine wakifariki dunia kutokana na kushindwa kuhimili. Deus Gakamwa ni Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Nyakaliro amesema kituo hicho kimejengwa kea gharama ya Tsh. Milioni 400 na kituo kimekamilika kwa asilimia mia moja huku akidai baadhi ya majengo yameanza kutumika.
 


Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema kituo hicho ni kati ya vituo vya afya 16 ambavyo mkoa wa Mwanza ilipata fedha zake huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo akitoa maelekezo kwa mkuu huyo wa mkoa kufuatilia ujenzi wa jengo la halmashauri ya Buchosa lililosimama. Ujenzi wa kituo hicho cha afya cha Nyakaliro ni miongoni mwa vituo vingine vya afya, zahanati na hospitali vinavyoendelea kujengwa nchini ambavyo Serikali ilitoa fedha zake zaidi ya Tsh. bilioni 300.

Thursday, February 27, 2020

DC BAGAMOYO AWAPIGA STOP WANAOKESHWA USIKU KWENYE VIGODORO


 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa akizungumza na wananchi wa Kata ya Nianjema kuhusiana na kupiga marufuku ngoma za usiku maarufu kama Vigodoro wakati wa Mkutano wake wa kikazi kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

 Baadhi ya Wananchi wa Wilayani Bagamoyo wakiwa wametulia kwa makini kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo ambaye aliitisha Mkutano maalumu kwa ajili ya kuzungumzia mambo mbali mbali ya maendeleo kwa wakazi wa kata ya Njia njema pamoja na kuwasikiliza changamoto zao.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa ambaye pi ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amepiga marufuku kuwepo kwa ngoma  na miziki ambayo inafanyika nyakati za usiku bila utaratibu  maarufu kama ‘Vigodoro’ kwani zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili kwa wananchi.
Agizo hilo amelitoa  wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Nina njema, wadau wa maendeleo pamoja na wakuu mbali mbali wa idara wakati wa mkutano wake wa kikazi kwa ajili ya kusikiliza kero na changamoto mbali mbali za wananchi kwa lengo la kuweza kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kuweka mipango  madhubuti kwa ajili ya kuleta chachu ya maendeleo.
Zainabu alisema kwamba  katika baadhi ya maeneo ya Wilaya yake kumekuwepo  wimbi la ngoma ambazo zinachezwa nyakati za usiku na kupelekea kero na usumbufu mkubwa kwa watu wengine hivyo ameamua kuchukua hatua ya  kupiga marufuku hali hiyo kwa lengo la kuondokana na mambo mbali mbali ambayo yamekuwa yakijitokeza hasa katika wakati wa usiku.

“Kuanzia leo katika mkutano huu napenda kusema napiga marufuku kabisa mambo ya vigodoro vya usiku kwani vimekuwa ni kero sana na vinachangia kwa kiasi kikubwa katika kunjunja maadili ya Mtanzania na kwamba katika hili nitahakikisha ninalisimamia kwa ukaribu mno ili kukomesha kabisa kuwepo kwa hali hii kayika Wilaya ya Bagamoyo,”alifafanua Zainabu.
Aidha Mkuu huyo alibainisha kwamba wananchi wa Bagamoyo kwa sasa wanatakiwa kubadilika na kuwa na mtazamo chanya kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za miradi ya maendeleo kuliko kutumia muda wao mwingi katika kukesha nyakati za usiku wakicheza ngoma ambazo hazina faida yoyote katika Taifa la Tanzania.
“Mimi kikubwa ninachotaka kuwaambia hasa wananchi wa Wilaya ya Bgamoyo tuachane kabisa na kujikta zaidi katika kukesha kwenye vigodoro. kabisa  ni vema zaidi mkatumia fursa mbali mali zilizopo mkajishughulisha katika shughuli za kujipatia kipato ili kuweza kuondokana na  wimbi la umasikini hivyo ni rai yangu wote tukashirikiana katika kuleta maendeleo na sio kukesha kwenye vigodoro ambavyo ni havina faina yoyote ile,”alisema Zainabu.
Pia Mkuu huyo wa Wilaya alifafanua kwamba mtu yoyote ambaye anahitaji kufanya shughuli yake ya usiku ni lazima apatiwe kibali maalumu kutoka katika Ofisi yake kwa kuzingatia sheria na utaratibu ambao utakuwa umewekwa,ili kuhakikisha mambo yote ambayo yanakuwa yanajitokeza nyakati za usiku ikiwemo masuala ya  uharifu  na wizi yanakomeshwa kwa kiasi kikubwa.
Katika  hatua nyingine ametoa onyo kali kwa wale wote ambao watabainika kukiuka agizo lake ambalo amelitoa na kwamba atahakikisha anawachukulia hatua kali za kisheria wale wote ambao watabainika bado wanaendeleo kinyemela  kujihusisha na  masuala ya kupiga ngoma za usiku na vigodoro bila ya kuwa na kibali maalumu.
Nao baaadhi ya wananchi ambao hawakuta kutaja majina yao walimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa hatua ambayo ameifanya ya kupiga marufuku kabisa mambo ya vigodoro hasa katika nyakati za usiku kwani yamekuwa ni tatizo kubwa kutokana na kuwepo kwa matukio mbali mbali ambayo yanasabisha momonyoko wa maadili hasa kwa vijana.

“Kwa kweli sisi kama wananchi wa Wilaya ya Bgamoyo hili agizo la Mkuu wetu kupiga marufuku ngoma za usiku maarufu vigodoro sisi tunamuunga mkono kwa asilimia mia moja kwani imekuwa ni kero sugu ya siku nyingi na wakati mwingine yani watu hatulali kabisa na kingine kuna baadhi ya matukio ambayo yanafanyika hivyo kwa hatua hii itaweza kusaidia kuondoa na kupunguza kabisa changamoto amabzo zimekuwa zikijitokeza katika maeneo ambayo tunaishi,”walisema.
Kwa upande wake mmoja wa wadau wa maendeleo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nianjema Abdul Pyalla alisema kwamba suala hilo la vigodoro  ni kweli limekuwa ni kero kubwa kwa wananchi hivyo atahakikisha kushirikiana bega kwa bega na Mkuu wa Wilaya  pamoja na wananchi husika katika mitaa mbali mabli kwa lengo la kuwaelimisha zaidi kuhusu umuhimu wa kutumia muda wao katika shughuli za maendeleo kuliko kukesha kwenye ngoma.
                                                      

WANAFUNZI WALIOLAZIMIKA KUPANGA NYUMBA ZA WAGENI ILI KUPATA ELIMU SASA BASI.


Ni katika ziara ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Diallo kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali kama sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015 - 2020. Dkt. Diallo akiwa wilayani hapa kwenye ziara ya Chama hicho akiiongozana na kamati ya siasa ya CCM mkoa wa Mwanza anashiriki ujenzi wa shule ya sekondari Sukuma inayojengwa wilayani Sengerema kwa fedha za Wananchi wakishirikiana na Serikali ambapo licha ya kuwapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu katika kuisaka elimu pia hatua hiyo imewanusuru kukatisha masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama sanjari na mimba. Shule ya sekondari Sukuma inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Mwezi April mwaka 2020.

Wednesday, February 26, 2020

WAFANYABIASHARA MWANZA WAOMBA HURUMA YA JPMZaidi ya Wafanyabiashara wadogo 100 maarufu kama machinga waliopo mtaa wa Rwagasore eneo la Kariakoo jijini Mwanza wamemuomba Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kuingilia kati mgogoro uliopo baina yao na mtendaji wa kata ya Pamba kufuatia kutakiwa kuondoka katika eneo hilo ndani ya siku saba.

RC HAPI MARUFUKU KUOSHEA MAGARI ENEO LA NDIUKA.

 Mkuu  wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa katika eneo la Ndiuka ambako ndio chanzo cha maji yanayotumiwa na wakazi wa manispaa ya Iringa kwa kiasi kikubwa yanazalishwa hapo.
Mkuu  wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akieleza jambo kuhusiana na marufuku aliyoitoa  
FREDY MGUNDA,IRINGA.

KUTOKANA  na  uchafunzi wa Vyanzo vya maji,Afya za wananchi wapatao  laki 1.78 wanaoshi katika Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa na  pembezoni mwa mji  ziko hatarini  kukumbwa na magonjwa mbalimbali.

Hayo yamebainika kwenye ziara ya awamu ya mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ya awamu ya pili ya iringa mpya.

Mkuu wa mkoa alipokuwa akipokea taarifa kutoka kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (IRUWASA) moja ya changamoto iliyotajwa nipamoja na kazi  ya kuosha magari inayofanywa na vijana  katika chanzo cha maji Ndiuka.

 Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (IRUWASA) Girbelt Kayange akitoa  taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka hiyo kwa mkuu mkoa alisema kuwa moja kati ya changamoto ambazo zinaikabiri mamlaka hiyo ni uharibifu wa chanzo hicho kutokana na shughuli za kiuchumi zinazofanywa unaweza sababisha madhara makubwa kiafya kwa binadamu kutokana na gari zinazooshwa baadhi ya gari kubeba mafuta na kemikali za viwandani.

“Kwa zaidi ya miaka 10 shughuli  za kuosha magari katika chanzo cha maji ndiuka kimekuwa ni changamoto kubwa ambayo inaweza kuathiri afya za wananchi wanaotumia maji hayo” alisema

Aliongeza kuwa zipo taasisi  za serikali ambazo zinakawamisha utendaji kazi wa mamalaka hiyo ikiwemo magereza jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za mamlaka hiyo kutokana na kudaiwa fedha nyingi  za fedha.

‘’Bado tasisi za serikali hazijamaliza madeni yake licha ya  baadhi ya kuliapa taratibu madeni hayo.lakini magereza wanadaiwa kiasi cha milioni 300.

Akitaja mafaniko ambayo mamlaka hiyo imeweza kupata nipamoja na kuongezeka kwa mapato,mamlaka imeweza kupanua mtandao wa maji safi na taka ukilinganisha na hapo awali  na kusababisha  kuwafikia wakazi wengi zaidi hasa wanaoishi pembezoni mwa Manispaa hiyo. 

Akikagua  mradi wa maji  katika eneo la Ndiuka  mkuu  wa mkoa wa Iringa Ally Hapi  alipiga marufuku shughuli za  uzalishaji mali  na za kibidamu kufanyika katika maeneo ya vyanzo vya maji na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuanza kuwachukulia hatua madereva    ambao watabainika kusimamisha magari yao katika eneo la ndiuka  kwa ajili ya kuoshwa na wakiwemo waoshaji.

Alisema gari nyingine zinabeba kemikali kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali  viwandani pamoja na mafuta,kuendelea kuruhusu magari kuoshwa katika vyanzo vya maji ni kuatarisha usalama wa watu  na afya zao.

‘’Napiga marufuku kuanzia leo shughuli za kuosha magari  katika vyanzo vya maji pia naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata na kuwashukulia hatua stahiki madereva na wale wote watakaobainika kuosha magari kuanzia leo’’

Omary Mkangama Ofisa Utumishi Manispaa ya Iringa akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Manispaa alisema baada ya kupokea taarifa ya zuwio watatafuta eneo mbadala ambalo litatumika na vijanahao kufanya shughuli zao ambazo wamekuwa wakizifanya.

Alisema kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wanajishughilia na kazi ya kuosha magari katika eneo ambalo ni chanzo cha maji,jambo ambalo linatishia usalama wa afya wananchi wa  mkoa wa Iringa.

Katika ziara hiyo alikagua miradi ya maji iliyo chini ya usimamizi wa IRUWASA katika eneo la Ndiuka ambalo ni chanzo cha maji, kukagua usambazaji wa maji katika eneo la Tosamaganga, mradi wa usambazaji wa maji kalenga ,kukagua  mradi wa uboreshaji wa huduma  ya maji mtwivila pamoja na  kuzungumza na kupokea kero   wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Isakalilo.

VIJANA WAWEKEZAJI KWENYE KILIMO WATAPATIWA ARDHI SONGWE

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akifunga Kongamano la Vijana katika Kilimo lililofanyika Mkoa wa Songwe na Kuhusisha vijana takribani 700 kutoka Mikoa ya Songwe, Rukwa, Mbeya na Katavi ambapo ameahidi kuwapatia ardhi vijana wanaotaka kuwekeza katika Kilimo.
Vijana takribani 700 kutoka Mikoa ya Songwe, Rukwa, Mbeya na Katavi wakiwa katika Kongamano la Vijana Katika Kilimo ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali na kuwekeana maazimio yatakayo boresha ushiriki wa vijana katika Kilimo.
Vijana wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya kilimo Mkoani Songwe wamepewa ahadi ya kupatiwa ardhi kwa ajili ya shughuli za kilimo ndani ya muda mfupi baada ya kuwasilisha maombi yao.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amtoa ahadi hiyo leo wakati akifunga Kongamano la Vijana  katika Kilimo lililofanyika Mkoa wa Songwe na Kuhusisha vijana takribani 700 kutoka Mikoa ya Songwe, Rukwa, Mbeya na Katavi.
Brig. Jen. Mwangela amesema Mkoa wa Songwe unayo ardhi ya kutosha kwa ajili ya shughuli za Kilimo ambayo bado haijatumika hivyo kijana yeyote mwenye nia ya kuwekeza katika Kilimo afike ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
“Mkoa una hekta Milioni mbili, mpaka sasa tumetumia asilimia 30 kwa ajili ya kilimo na asilimia ndogo kwa ajili ya makazi na misitu hivyo tunalo eneo la kutosha, mvua za kutosha na ardhi nzuri pia tunazo hekta elfu 18 zinazofaa kwa ajili ya kilimo cha umwgiliaji hivyo ardhi bado ipo ya kutosha.”, amesema Brig. Jen. Mwangela.
Ameongeza kuwa kijana mwenye nia ya kuwekeza kwenye Kilimo akifika ofisi ya Mkuu wa Mkoa ata taja Wilaya anayotaka kewekeza ili aelekezwe isipokuwa kijana hatatakiwa kuchagua mwenyewe eneo maalumu ambalo tayari linamilikiwa na watu wengine.
Brig. Jen. Mwangela amewasisitiza Vijana kuchangamkia fursa ya kumiliki ardhi kihalali kwakuwa bado inapatikana kwa urahisi ili baadaye wasihangaike kuitafuta wakati wa uzee na kuongeza kuwa waache kulalamikia wazazi au serikali kutokana na umasikini bali wajikite katika Kilimo.
Amesema asilimia 67 ya nguvu kazi ni vijana ambao hawana ajira ambapo nguvu kazi hii ikibaki bila ajira ni aibu kwa vijana na taifa hivyo mkakati wa Wizara ya Kilimo wa Kuhakikisha vijana wanajikita katika Kilimo ni mzuri na utainua uchumi wa taifa kwa haraka.
Brig. Jen. Mwangela ameongeza kuwa vijana wakishiriki kikamilifu katika Kilimo uchumi utakua, viwanda vitaongezeka na wataweza kuyafurahia maisha kwakuwa Kilimo hakijawahi kumtupa mtu na pia wasiache kuangalia fursa katika sekta za ufugaji na uvuvi.
Aidha Brig. Jen. Mwangela amewaeleza Vijana waliohudhuria Kongamano hilo kuwa Serikali itawaunganisha na taasisi zinazotoa mikopo ya Kilimo isipokuwa watatakiwa kuwa waamini na kurejesha mikopo hiyo.
Ameongeza kuwa wapo baadhi ya watu ambao walipatiwa mikopo ya Kilimo na baadhi ya benki lakini wamekuwa sio waaminifu kwa kutorudisha mikopo hiyo au kuwa wasumbufu katika kurejesha mikopo hiyo hivyo vijana hao wasiige mifano yao.
 Naye Afisa Programu kutoka Jukwa la Wadau wa Kilimo (ANSAF) Rehema Msami amesema wamefanya utafiti kuhusu namna ambayo halmashauri zimekuwa zikitoa asilimia 10 ya mapato yao kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu.
Msami amesema utafiti wao umebaini kuwa vijana wengi wenye sifa hawapati mikopo hiyo na hivyo kushindwa kuwa na mitaji ya kuwekeza katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo, pia baadhi ya vijana wanaopewa mikopo hawana sifa na hivyo kushindwa kurejesha mikopo hiyo.
Nelusigwe Kibona kijana Mkulima wa Mbogamboga kutoka Rungwe Mkoani Mbeya amesema Kongamano la Vijana limempa elimu na mbinu nyingi za Kulima kisasa pamoja na kutafuta masoko ya mazao yake.
Kibona ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Songwe kwa kuwasaidia vijana kupata ardhi kwa ajili ya Kilimo na kuiomba mikoa mingine iige mfano huo.
Kenedy Kyando Kijana Mkulima Kutoka Vwawa Songwe amesema kuwa Vijana wengi hawataki kujishughulisha na Kilimo kwa kukosa uvumilivu na kutaka fedha za haraka huku akiiomba Serikali kufanya makongamano kama hayo mara kwa mara.

Monday, February 24, 2020

SWALI LA MWANAFUNZI BWILU GIRLS LAMPA SABABU MKAPA KURUDIA KITABU CHAKE KWA LUGHA MAMA 'KISWAHILI'Swali la mwanafunzi toka Shule ya Sekondari wasichana Bwiru Mwanza lamuamsha Mkapa kukiandika kitabu chake kwa lugha mama ya Kiswahili.

KABENDERA AKUTWA NA HATIA, AHUKUMIWA KULIPA FIDIA NA FAINI MILIONI 273


Mahakama ya Kisutu imemuhukumu Mwanahabari Erick Kabendera kulipa fidia na faini ya Sh. Mil 273 baada ya kukiri makosa ya utakatishaji fedha na kukwepa kodi, tayari ameshaingiza Tsh. Mil 100 kwenye akaunti ya Serikali na ameachiwa huru huku akitakiwa kulipa fedha iliyobaki ndani ya miezi sita.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega baada ya Kabendera kusota rumande kwa takribani miezi sita.

Katika kesi hiyo Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa TSh.Mil 173.

MKAPA AKANUSHA DHANA KUWA ALIANDALIWA NA BABA WA TAIFA AJE KUWA RAIS“Nawashukuru viongozi wa mkoa wa Mwanza kwa kuwezesha kuja kutambulsha kitabu hiki baada ya uzinduzi wake Dar es salaam, ni heshima ambayo mlistahili na hasa nikikumbuka vile mlivyoandaa sherehe zile za Uhuru 9 Disemba mwaka jana (2019), zikafana sana pamoja na nyimbo za kwaya ile, nasema hii ni heshima kubwa kwangu. Hongereni sana kwa matayarisho ninyi ni hodari sana” Asema Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin W. Mkapa katika hafla ya utambulisho wa kitabu chake 'MY LIFE, MY PURPOSE' uliofanyika ukumbi wa Hotel Malaika jijini Mwanza. “Kwanini niliamua kuandika kitabu hiki? Ni kwasababu ninalaumiwa sana katika jamii hasa wanasiasa kutokana na sera nilzokuwa nikizitekeleza wakati wa uongozi wangu” “Ninasemwa kuwa mtu jeuri, najiona sana, sasa n jukumu lenu someni kile kitabu halafu muamue kweli huyu ni jeuri” “Kuna dhana inayosemwa kwama Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliniandaa toka mwanzo ili nije kuwa rais wa nchi, HII SI KWELI” Amesisitiza Mhe. Mkapa.