Wakazi wa kata ya Nyakaliro Halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wameipongeza Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya cha Nyakaliro na kuondoa adha ya akina mama wajawazito waliokuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma ya afya. Pongezi hizo wamezitoa mara baada ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza kufanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya ilani ya uchaguzi 2015 -2020 inayotekelezwa na Serikali kuu mkoani Mwanza. Wananchi hao wamebainisha kuwa awali wajawazito walilazimika kutembea umbali wa zaidi wa kilomita 20 kutafuta huduma ya afya hospitali ya wilaya - Sengerema kiasi cha kusababisha baadhi yao kujifungulia njiani huku wengine wakifariki dunia kutokana na kushindwa kuhimili. Deus Gakamwa ni Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Nyakaliro amesema kituo hicho kimejengwa kea gharama ya Tsh. Milioni 400 na kituo kimekamilika kwa asilimia mia moja huku akidai baadhi ya majengo yameanza kutumika.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema kituo hicho ni kati ya vituo vya afya 16 ambavyo mkoa wa Mwanza ilipata fedha zake huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo akitoa maelekezo kwa mkuu huyo wa mkoa kufuatilia ujenzi wa jengo la halmashauri ya Buchosa lililosimama. Ujenzi wa kituo hicho cha afya cha Nyakaliro ni miongoni mwa vituo vingine vya afya, zahanati na hospitali vinavyoendelea kujengwa nchini ambavyo Serikali ilitoa fedha zake zaidi ya Tsh. bilioni 300.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.