|
Mkuu wa Mkoa wa mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akisikiliza kwa makini Michango ya Wajumbe wa Kamati ya Michezo Mkoa walipokutana kujadili maendeleo. |
|
Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza (kushoto) pamoja na Bw. Kizito Bahati Afisa Michezo wilaya ya Ilemela aliyemwakilisha Mkurugenzi wa wilaya hiyo wakiwa kwenye kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa mikutano ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. |
|
Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Mwanza MZFA Bw. Jackson Songora ambaye ni mmoja kati ya wajumbe wa kamati hiyo akichangia hoja iliyowasilishwa mezani. |
|
Wajumbe wakitafakari kwa makini huku wakiainisha kwenye karatasi zao maoni yao namna ya kuinua michezo mkoa wa Mwanza. |
· Zachangwa Mil. 6
Papo kwa Papo
Na. Atley Kuni -Afisa Habari Mkoa wa Mwanza.
Kamati ya Michezo
Iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, imeazimia kuhakikisha
inainua suala zima la Michezo katika Mkoa huo.
Wakitoa mawazo katika
kikao kilicho itishwa na Mkuu wa Mkoa huo
walisema tatizo kubwa ambalo lipo katika Masuala ya Michezo ni pamoja na
nidhamu ndogo ya michango kwa Viongozi wanao chaguliwa,
Walisema kukwama kwa
michezo katika Mkoa nia tatizo la watu wanaochaguliwa kutokuwa na dhamira ya
dhati katika kuendeleza michezo Mkoani hapa.
Akizungumza katika
Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo amesema,
"kwakweli tufike mahali tumalize tatizo hili lakukwamisha suala la michezo
katika Mkoa huu". Alisema haipendezi watu kugeuza uongozi kama sehemu ya
Miradi yao badala yake tufanye kazi ambayo itakuwa na maslahi kwa wanamwanza
wote.
Kwa upande wake Afisa
Elimu Mkoa wa Mwanza bwana Hamisi Maulid alisema tatizo lililopo ni Umbwe la
uongozi usio zingati maadili ya uongozi hivyo Umefika wakati sasa kamati kama
hii inayo undwa kusimamia kwa dhati na ikiwezekana viongozi wanaochaguliwa wawe
ni wale tu wenye dhamira ya dhati katika kuinua Michezo katika Mkoa huu,
akitolea mfano alisema huko yeye alipotoka waliunnda kamati kama hiyo na
usimamizi wa fedha ukaimarishwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Hata hivyo kamati hiyo
ilitoka na Maazimio Manane yakwenda kuyafanyia kazi, Maazimio yaliofikiwa ni
pamoja, kila halmashauri ya Wilaya kuchangia, Mil.10, Uchaguzi wa vilabu ambao
bado haujafanyika ufanyike ikiwezekana hata kwakulazimishwa, Kamati ya Michezo
ya Mkoa kuwa Mhimili Mkuu wa kusimamia masuala ya michezo, kufungua akaunti
kwaajili ya kuhifadhi pesa itakayokuwa inapatikana, kutunga sheria ndogondogo
kwaajili kukusanya sehemu ya kodi ya leseni kwaajili yakuendeleza michezo
mkoani humo, Aidha kila mjumbe wa kamati hiyo amehimizwa kuwa chachu ya
mabadiliko yakuhakikisha suala la Michezo katika Mkoa huo linarejea kama enzi
za zamani.
Katika hatua nyingine
kamati hiyo Imewachagua Bibi Doroth Mwanyika kuwa Mwenyeki wa Kamati hiyo, huku
bwana Peter Ngongoseke akichaguliwa kuwa Makamu wa Mwenyekiti, huku nafasi ya
Mtunza fedha ikienda kwa bwana Peter Shewio ambaye ni mfanya kazi wa Mamlaka ya
Mapato nchini TRA.
Kabla ya kikao hicho
kumalizika wajumbe hao walikusanya kiasi cha Tshs 6,000,000 kwaajili
yakuanziasha mfuko huo na wadau wengine waka ahidi kuendelea kuchangia mfuko
huo.
Kamati ya Michezo ya Mkoa wa Mwanza inaundwa
na Mkuu wa Mkoa Mwenyewe kama Mlezi, Bibi Dorothy Mwanyika Katibu Tawala Mkoa
wa Mwanza Mwenyekiti, Peter Ngongoseke Makamu wa
Mwenyekiti, wajumbe ni Ernest Mangu,
Christopher Gachuma,Altaf Hilani, Nuru Suleiman, Jeremiah Lusana wajumbe,
wengine ni Leonard Kadashi Mjumbe, L. Japhet,Wilson Kabwe,Zuberi Mbyana Jackson
Songora, Gisiruri Mwihechi, Baraka Ezekiel, Njile Lili, Samwel Nyala wote
wajumbe, taarifa hiyo Imeongeza kuwa wajumbe wengine ni James William, Lameck
Airo, Joseph Kahungwa, Lazaro Ngweleja, na Hamis Salehe wote wajumbe.
Kwa mujibu wa historia
Mkoa wa Mwanza uliwahi kuwika katika Michezo katika vipindi tofauti kati ya
miaka ya sabibi na Themanini, lakini pia Mwanza ndio Mkoa pekee wenye chuo kikubwa
kabisa cha Michezo cha Malya.