Goli la kwanza la Toto Africans. |
Dakika tatu baadaye Polisi Morogoro walisawazisha kupitia mpira wa faulo iliyopigwa na kuwababatiza mabeki wa timu ya Toto hatimaye ukamkuta kwenye nafasi nzuri mfungaji Keneth Masumbuko kuweza kuzifumania nyavu.
Toto walitulia na kuweza kujipatia bao la pili kwenye dakika ya 60 baada ya krosi safi ya Emma Swita kukifikia kichwa cha mfungaji James Magafu aliyeutupia mpira engo ya kushoto mwa lango la Polisi Morogoro.
Uzembe wa kipa wa Toto Africans Erick Ngwengwe aliyeponyokwa na mpira aliokuwa na uwezo wa kuudaka wa shuti la Niko Kabipe uliigharimu timu hiyo kutoa mwanya kwa Polisi kupata bao la pili la kusawazisha kwenye dakika ya 65 ya mchezo.
Hadi mwisho wa mchezo ndani ya dimba la CCM Kirumba Toto 2 Polisi Moro 2.
Kocha wa timu ya Polisi Morogoro Richard Adolf akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo.. Kumsikiliza bofya play.Mashabiki walivamia benchi la wachezaji wa timu ya Toto baada ya kumalizika kwa mchezo kati yake na Polisi Moro na hapa kiwalaumu wachezaji kucheza chini ya kiwango na kutoka sare kwenye mchezo huo... kusikiliza bofya play.
Hapa lilitoka 'buku' tu'''' mwanawane...
Kepteni wa timu ya Toto Africans Hamisi Msafiri akipokea fedha zilizochangwa kwa style ya papo kwa hapo na wadau wa soka kutoka kwa Mwandishi wa habari Philbert Kabago, baada ya wachezaji hao kudai kuwa wako taabani katika kambi yao likiwemo suala la kutolipwa mishahara na posho za michezo mbalimbali kwa zaidi ya miezi minne sasa kiasi cha kuwaathiri mikakati yao ya kupata matokeo mazuri.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.