Mwandishi Gerlard Robert wa kasi mpya anaandika ...WAKATI VUGUVUGU LA UCHAGUZI LIKIWADIA MAWAZIRI NA WABUNGE KWA TIKETI YA CCM SASA PRESHA ZINAZIDI KUPANDA NA KUSHUKA KATIKA MAJIMBO YAO, HUKU MBUNGE WA JIMBO LA NYAMAGANA MWANZA, BW. LAWRENCE KEGO MASHA ANADAIWA KUWAITA MADEREVA TEKSI KATIKA HAFLA ILIYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA NEW MWANZA HOTEL KWA LENGO LA KUWAOMBA MSAMAHA IWAPO ALIWAKOSEA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE ILIYOPITA. MADEREVA HAO WALIANDALIWA CHAKULA SWAFI + VINYWAJI NA BAADAE KILA MMOJA ALIPATIWA KIFUTA JASHO CHA SHILINGI 10,000/=(unauliza za nini? teheee!). BW. MASHA AMBAYE PIA NI WAZIRI WA MAMBO YA NDANI ALITUMIA FURSA HIYO KUKANUSHA KWAMBA HATAGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA NYAMAGANA NA BADALA YAKE ATAGOMBEA JIMBO LA KARUMO LILILOPO KTK WILAYA YA SENGEREMA, IWAPO JIMBO HILO LITAGAWANYWA KUWA MAJIMBO MAWILI KUTOKA JIMBO LA SASA SENGEREMA. NA BADALA YAKE MH. MASHA AMESEMA ATAGOMBEA UCHAGUZI UJAO KWA TIKETI YA CHAMA CHAKE (CCM) JIMBO LA NYAMAGANA. MBUNGE HUYO ANAYEJIPANGA KWA MTINDO HUU ILI KUJINUSURU NA MCHAKATO ULIO MBELE YAKE KWANI ANAKABILIWA NA KIBARUA KIZITO NDANI YA CHAMA HICHO HASA WAKATI WA KURA ZA MAONI KUTOKANA NA BAADHI YA WAFUASI WA CHAMA HICHO TAWALA KUANZA KUMUACHA NJIA PANDA HASA WAKATI HUU WA KUELEKEA KTK UCHAGUZI MKUU. WANACHAMA WALIOPANIA KUMNG'OA KTK UBUNGE NI PAMOJA NA BW. WILIAM KULWA MVANGA, BW.RAPHAEL SHILATU, MBW. KIZITOMARONGO, BW. JOSEPH KAHUNGWA PAMOJA NA BW. SHANIFU MANSOOR (MOIL)PAMOJA NA BW. MWARUZUKU MAGONGO AMBAYE PIA ANADAIWA KUONESHA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE WA JIMBO HILO........stori inaendelea..
JINAMIZI LA UVAMIZI WA MAENEO YA WAZI YALIYOTENGWA KWA AJILI YA UKUZAJI WA VIPAJI KWA VIJANA HUSUSANI MICHEZO LIMEENDELEA KUTAFUNA MAENEO KWA MAENEO NA SAFARI HII LIMEGEUKIA KIWANJA CHENYE HISTORIA YA KUTOA WASUKUMA KANDANDA MAARUFU NCHINI MUHIMU KWA TAIFA WALIOTAMBA ZAMANI AKINA MBUYI YONDANI,MZEE HALFANI NGASA, HAMADI BILIYOMO(RTC MZ+TOTO) NA WAKALI WA SASA JERRY TEGETE, NGASA,HENRY JOSEPH NAWENGINEO WENGI. NAUZUNGUMZIA UWANJA WA FURAHISHA ULIOKO KIRUMBA JIJINI MWANZA.
WAKATI MHESHIMIWA RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIPIGANA KUFA NA KUPONA KUONA TAIFA LINASONGA MBELE KATIKA NYANJA YA MICHEZO SAMBAMBA NA KUHAKIKISHA KUWA WATU WAKE WANAPATA MISINGI BORA TANGU AWALI KATIKA HATUA ZA KIMICHEZO KUTIMIZA AZMA, TIZAMA HILI LINALOFANYIKA SASA KATIKA ENEO LA WAZI LA UWANJA WA MICHEZO FURAHISHA KIRUMBA JIJINI MWANZA, AMBAPO HALMASHAURI YA JIJI IMEMEGA SEHEMU YA UWANJA HUO KUWA DAMPO.
SI MICHEZO PEKEE ITAKAYOATHIRIKA VIPI KUHUSU AFYA ZETU NA WATOTO WETU? KWANI TAKA HIZI ZIKO KATIKA UWANJA HUU ULIO KARIBU KABISA NA NAKAZI YA WATU.
ETI ENEO HILI NI KWA KUKUSANYA TAKA TU!. NANI KASEMA? KWA MUJIBU WA WAKAZI WA ENEO HILI MKURUGENZI WA JIJI BW. WILSON KABWE NDIYE ALIYE IDHINISHA HILI KUFANYIKA HAPA.
SHULE NYINGI ZA MWANZA MFANO. SHULE YA MSINGI MILONGO JUU, SM KITANGILI, SM. NYAMAGANA, HATA SHULE YA SEKONDARI LAKE HAKUNA VIWANJA, WATOTO WENGI WANACHEZA KWENYE MAWE VIWANJA VYA MICHEZO MASHULENI VIMEJENGWA MADARASA AU OFISI. SASA NI ZAMU YA HIKI TAAAARATIBU TUNAPIGA FENSI KESHO INSHU NYINGINE HAPA HAPA.
WAKIWA MAKUNDI KWA MAKUNDI NDEGE HAWA KWA HIVI SASA ENEO HILI LIMEKUWA YAO MAKAZI.
Wednesday, January 13, 2010
MWANZA