Zao la Karafuu
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka
Hamdu Shaka akipanda miti aina ya Mikoko Kwa ajili ya kutunza
Mazingira wakati wa ziara yake katika eneo la Mwambe Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka
Hamdu Shaka akiwasili katika eneo la Mwambe Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba kwa ajili ya kujionea hali ya upandaji miti aina ya Mikoko unavyoendelea.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka
Hamdu Shaka akizungumza jambo na Mdhamini wa Shirika la Bodi ya Taifa ya Biashara Zanzibar mara baada ya kutembelea ofisi hizo kujionea hali ya ukusanyaji wa zao la karafuu Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Zao la Karafuu likiwa limehifadhiwa ghalani chini ya Shirika la Bodi ya Taifa ya Biashara Zanzibar
Vijana wakijishughulisha na shughuli za ubabeji mizigo katika ghala la kuhifadhia zao la Karafuu, Wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Shaka
Hamdu Shaka akisikiliza maelezo mbalimbali ya Mdhamini
wa Shirika la Bodi ya Taifa ya Biashara Zanzibar mara baada ya
kutembelea ofisi hizo kujionea hali ya ukusanyaji wa zao la karafuu
Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba wakati wa ziara ya kikazi ya
kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Na Mathias Canal, Pemba
Zanzibar ni maarufu kwa uzalishaji
wa karafuu ulimwenguni kwa zaidi ya karne
mbili sasa. Uzalishaji huo ulikuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia tani
35,000 mwaka 1830 na kumiliki soko la karafuu duniani kwa asilimia 90.
Iliongoza katika uzalishaji wa zao
hilo kuanzia mwaka 1830 hadi 1940 kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na
Indonesia.Tathmini iliyofanywa hivi karibuni ya Sensa ya Miti (Woody Biomass
Survey 2013) imeonesha kwamba Zanzibar kwa sasa ina idadi ya mikarafuu 4,131,783,
ambapo Unguja pekee ina zaidi ya mikarafuu 277,196 na Pemba zaidi ya mikarafuu 3,854,587.
Tathmini ya mwaka 1997 ilionesha
idadi ya mikarafuu 790,400 kwa Unguja na
mikarafuu 5,042,700 kwa upande wa Pemba, ikifanya idadi ya mikarafuu yote kuwa
ni 5,833,100
Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg Shaka Hamdu Shaka amelitaja zao la karafuu kuwa
ni zao muhimu kwa uchumi wa taifa ambalo huongeza kwa kiasi kikubwa kipato kwa
wananchi.
Alisema katika kuimarisha zao la karafuu Zanzibar, pamoja na kupambana na
mabadiliko ya tabia ya nchi kuna haja ya kupandwa mikarafuu na minazi maskulini,
ili wanafunzi waweze kupata uwelewa zaidi wa kutunza na kulienzi zao hilo, kwa
maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Shaka alisema hayo wakati alipotembelea na kupanda miti aina ya Mikoko Kwa
ajili ya kutunza Mazingira ili kuhuisha uoto wa asili na kuepuka mmomonyoko wa
ardhi katika eneo la Mwambe lenye asili ya Watumbatu Wilaya ya Mkoani na Mkoa
Ni Kusini PEMBA .
Pia
aliwasisitiza wananchi kuhusu kupanda miche ya mikarafuu na minazi na kutotupa
taka ovyo ili kuzuia mmomonyoko wa ardhi.
Alisema
kuwa serikali inajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa inaandaa sheria kali
itakayokuwa maalumu kwa kuwachukulia hatua wananchi wanaokata miti ovyo kinyume
na utaratibu.
Katika hatua nyingine Shaka alitembelea shirika la Taifa la Biashara Zanzibar
kujionea hali ya ununuzi wa zao la karafuu ambapo alimpongeza Mdhamini wa wa
shirika hilo Ndg Seif Suleiman Kassim kutokana na kiwango kikubwa cha
ukusanyaji wa zao hilo ambapo katika msimu huu hadi kufikia Mwezi Julai 13,
2017 tayari 2203 sawa na Kilogramu 99180.0 zilikuwa zimehifadhiwa kwa ajili ya
kupelekwa Unguja.
Alisema
uzalishaji wa zao la karafuu, katika Wilaya ya Mkoani unaongoza kwa zaidi ya
asilimia 60 ya uzalishaji wa zao hilo kwa zanzibar, na amewataka wananchi
kuendelea kutunza mikarafuu, kwani ndio pato la Taifa.
Zanzibar ni visiwa vinavyosifika kwa uzalishaji wa karafuu bora duniani. Katika
miaka 30 ya nyuma pia ilisifika kwa uzalishaji karafuu nyingi, wastani wa tani
8,605 zilikuwa zikizalishwa kwa mwaka.
Jamii ya wakati huo walikuwa wakizijali, wakizithamini na wakizipenda sana
karafuu ukilinganisha na kizazi cha sasa. Walihakikisha karafuu zao wakiuza
vituoni tena zinakuwa safi, zimekauka vizuri na zinapata daraja la kwanza.
MWISHO