Kamishna wa kaunti hiyo, Gilbert Kitiyo amethibitisha kutokea
mauaji hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Maleli, eneobunge la Witu,
Lamu Magharibi. Kadhalika magaidi hao wameteketeza kwa moto nyumba
kadhaa katika eneo hilo.
Hata hivyo kamishna huyo hajatoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo, ingawaje anasema maafisa usalama wametumwa katika eneo hilo kudhibiti mambo.
Hii si mara ya kwanza kwa genge hilo la Kiwahabi kushambulia kaunti ya Lamu na kutorokea katika msitu wa Boni ulioko katika kaunti hiyo.
Wanachama wa al-Shabab katika msitu wa Boni, Lamu

Mapema mwezi uliopita wa Julai, wanachama wengine wa al-Shabab
waliwauwa kwa kuwakata vichwa watu 9 katika shambulizi lililofanyika
katika kijiji kimoja cha kaunti hiyo ya Lamu, siku chache baada ya
wanamgambo wa kundi hilo la kigaidi kuua polisi watatu katika kijiji
jirani cha Pandanguo na baadaye wakaua wanafunzi wanne na polisi wanne
katika kijiji cha Kiunga, kaunti hiyo ya Lamu.
Aidha mwezi Mei mwaka huu, maafisa saba wa polisi ya utawala waliuawa
baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa kando ya barabara katika
kaunti ya Lamu, kusini mashariki mwa Kenya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.