ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 25, 2023

"HAKUNA KURUDI NYUMA" RAILA AWEKA NGUMU, ASEMA MAANDAMANO YA JUMATATU YAKO PALE PALE.

 


Kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga amesema maandamano ya Jumatatu Machi 27 yataendelea kama yalivyopangwa. kiongozi wa ODM Raila Odinga alisema atakuwa kwenye maandamano. 

Akiongea eneo la Kisii ambapo alikuwa akihudhuria mazishi, Raila alisema kama serikali inataka asitishe maandamano lazima ifungue mitambo ya Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi. "Sisi haturudi nyuma, kama wanataka tusitishe wewe fungua servers. Kama unaamini ulishinda kwa nini unakataa kufungua servers," alisema Raila. 

Alizungumza wakati ambapo kuna presha kutoka kwa serikali na viongozi wa kanisa kuhusu maandamano. 

 Raila alisema ni haki yake na kila Mkenya kikatiba kuandamana na kushinikiza serikali kutii matakwa yao. "Ni haki yetu kikatiba kuandamana, na ndio manake naambia Wakenya wote wakuje Jumatatu kwenye maandamano," Raila alisema. 

Alitaka kuundwa kwa kamati mpya ya uchaguzi nchini IEBC kwa ajili ya 2027 kuwahusisha wote. "Kwa kamati mpya ya IEBC kuundwa ni lazima Kenya Kwanza na Azimio waketi chini na kuelewana, na pia kama wewe ulishinda fungua servers," aliongeza. 

Akizungumza Kisii, Rais William Ruto alimtaka Raila kukomesha maandamano yake mara moja na kumpa nafasi ya kuwahudumia Wakenya. Wacha kiburi. Mtu wa kubishana na mtu wa kitendawili ni mimi, badala ya kukabiliana na mimi ameanza kusumbua raia. Wewe unauliza nini Mama Mboga? Mwenye alikushinda ni mimi. 

Kama uko na shida kuja ukabiliane na mimi. Achana na mambo ya wananchi wadogo," Ruto amesema.

MSHINDI WA NACHINGWEA POLISI JAMII KUJINYAKULIA MBUZI.

 

Wa kwanza kushoto ni mkaguzi msaidizi wa Polisi Frank Mwanisi na mwa mwisho kulia ni OCD wa wilaya ya Nachingwea mrakibu mwandamizi wa Polisi James Chacha akikagua timu kabla ya mechi za Mashindano ya Polisi jamii cup yakiendelea wilaya ya Nachingwea.
Mechi ya kimashindano ikiendelea

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

WANANCHI wa wilaya ya Nachingwea wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuanzisha Mashindano ya Polisi jamii ambayo yenye lengo la kuendeleza mahusiano mazuri na Jeshi hilo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Polisi jamii wilaya ya Nachingwea, mwenyekiti wa waendesha pikipiki (bodaboda) wilayani Nachingwea Hashim Awadhi alisema kuwa lengo la Mashindano hayo ni kuimarisha mahusiano baina ya wananchi na Jeshi la Polisi.

Awadhi alisema kuwa Polisi na wananchi wakiwa na mahusiano mazuri vitendo vya uharifu vitapungua kutokana na Jeshi hilo kupata taarifa Mara kwa Mara kutoka kwa raia wema.

Alimazia kwa kumpongeza OCD wa wilaya ya Nachingwea James Chacha kwa kuwa na mahusiano mazuri na wananchi Jambo ambalo limesaidia kupunguza vitendo vya uharifu wilaya ya Nachingwea.

Kwa upande wake OCD wa wilaya ya Nachingwea mrakibu mwandamizi wa Polisi James Chacha alisema kuwa lengo la Mashindano ya Polisi jamii ni kuimarisha mahusiano na wananchi wa Nachingwea.


Chacha alisema kuwa wameanzisha Mashindano hayo kwa kuwashirikisha vijana zaidi kwa kuwa kundi hilo ndio limekuwa linatumika kufanya vitendo vya uharifu mtaani.


Alisema kuwa ukitoa elimu ya madhara ya uharifu kwa jamii kupitia vijana basi hapo baadae kutakuwa na kizazi bora ambacho kitakuwa tayari kupambana na uharifu wowote ule.

Chacha alisema kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia Mbuzi mmoja,ya jezi seti moja na mpira mmoja, mshindi wa pili atapata jezi seti moja na mpira mmoja na mshindi wa tatu atapata jezi seti moja.

Hivyo Mrakibu mwandamizi wa Polisi James Chacha kuomba wananchi kujitokeza kwenye mechi za Mashindano hayo ili kupata elimu mbalimbali kutoka kwa Jeshi la Polisi wilaya ya Nachingwea.


Friday, March 24, 2023

SHERIA MPYA YA KUTOBADILI IMANI YA KIDINI NCHINI INDIA YALALAMIKIWA


Viongozi ya makundi ya walio wachache nchini India wanasema kwamba sheria mpya ya kutobadili Imani iliyopitishwa katika baadhi ya majimbo inalenga kuadhibu na kukandamiza makundi ya wakristo na waislamu nchini humo.

Hayo yamejiri wakati tume ya Marekani ya Uhuru wa kimataifa wa dini, USCRIF, ikieleza wasiwasi wake kutokana na sheria hiyo, na kuomba ibatilishwe.

USCRIF kupitia ripoti imesema kwamba sheria hiyo mpya inavuruga uhuru wa kidini nchini India, ambao tayari ulikuwa hatarini, na kwamba hatua hiyo ni kinyume na sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Makundi ya kihindu pamoja na chama tawala cha Hindu Nationalist Bharatiya Janata, wanadai kwamba wamishonari wa kikristo wanabadili Imani za watu kote nchini kwa kutumia nguvu au ushawishi usiofaa.

 

Katika miaka ya karibuni, wamedai kwamba waislamu wamekuwa wakivuta watu kwenye dini yao kupitia njia haramu.

 

Kufikia sasa majimbo 12 kati ya 28 yaliopo nchini humo yamepitisha sheria hiyo, wakati baadhi ya yaliobaki yakitathimini kufuata nyayo .

KIJANA ALIYEKWEPA KWENDA SHULE ILI AMTEMBELEE MPENZI AFARIKI KATIKA NYUMBA YA DEMU


Kijana aliyekwepa kwenda shuleni kwa lengo la kumtembelea mpenzi wake ameaga dunia katika nyumba ya binti huyo eneo la Northrise, mjini Ndola huko Zambia.

Emmanuel Kayuni mwenye umri wa miaka 21 anasemekana kuzirai na kuaga dunia katika nyumba ya mpenzi wake huku wazazi wake wakidhani kuwa alikuwa katiak shule ya bweni kule Mansa.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa eneo hilo Peacewell Mweamba, amesema tukio hilo lilitokea machi  22 ambapo plisi walipokea taarifa kutoka kwa baba wa marehemu, bwana John Kayuni

Taarifa fupi kuhusu suala hilo ni kwamba   marehemu alienda shuleni kule Mansa mwezi Januari 2023 lakini akatoka shule kukutana na mpenzi wake Princess Mwaba mwenye umri wa miaka 20,

Marehemu Emmanuel alikuwa amerejea kutoka shule ya bweni na kujificha kwa  mpenzi wake ili wazazi wake ambao waliamini kuwa alikuwa bado yuko shule wasijue.

Machi 21, 2023, marehemu na princess    walienda katika loji ya Executive kule Northrise ambako walilala na alikuwa anakilalamika kuhusu matatizo ya moyo.

Asubuhi, wawili hao walitoka loji na kwenda katika nyumba yao Princess ambako marehemu alimuacha demu wake mwendo wa saa tatu asubuhi ili aende gengeni kununua nyanya sokoni.

Saa moja baadaye, marehemu alizirai kwenye mlango alipokuwa akirejea kutoka kununua nyanya ambapo mfanyakazi wa kutunza maua na mashamba eneo hilo alimshuhudia akianguka.

Princess  alielezwa kilichotokea kwa Emmanuel na usafiri ukawasilishwa ili kumkimbiza hospitalini lakini akawa amefariki.

HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO KUANZISHA KLINIKI ZA KIBINGWA ZA JIONI

 

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhan


HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo inatarajia kuanzisha huduma za Kliniki za Kibingwa wakati wa muda wa ziada wa jioni itakayoanza kuanzia Aprili 9 mwaka huu katika hospitali hiyo.

Akizungumza leo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Juma Ramadhan amesema huduma hizo zitaaza saa tisa na nusu jioni mpaka muda ambao wagonjwa watamalizika ambao watapata fursa ya kuonana na madaktari bingwa waliopo kwenye hospitali hiyo.

Dkt Juma alisema kwamba katika kliniki hiyo huduma mbalimbali za kibingwa ikiwemo magonjwa ya ndani,magonjwa ya ya upasuaji,magonjwa ya wakina mama,magonjwa ya watoto,magonjwa wa koo,pua pamoja na sikio .

Aidha alisema kwamba huduma hizo zitatolewa kwa wagonjwa wote wenye bima bila kujalia aina gani ya bima lakini pia wale wagonjwa wanaofanya malipo ya keshi yatapokelewa.

Hata hivyo alisema huduma hiyo itatolewa siku Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa tisa na nusu mpaka pale watakapomalizika.

Dkt Juma aliwahimiza wananchi wa mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kuhudhuria kliniki hizo ili kuweza kukutana na madaktari bingwa wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga

Hata alisema uwepo wa kliniki hiyo utasaidia kutoa fursa kwa wagonjwa kuweza kukutana na madaktari bingwa ambao wataweza kuwasaidia hivyo watumie nafasi hiyo kuweza kuonana na madaktari hao bingwa waliopo kwenye hospitali hiyo.

Thursday, March 23, 2023

WEZI WAFUKUA KABURI NA KUIBA SEHEMU ZA MWILI SAA CHACHE BAADA YA MAZISHI


Watu wasiojulikana  wamefukua kaburi na kunyofoa sehemu za siri za mwili wa marehemu Ruben Kasala, aliyezikwa Machi 18, 2023.

Mtoto  wa marehemu Frank Kasala alisema baba yake Ruben Kasala alikuwa akiugua kisukari na kukumbana na matatizo ya mapafu tangu Machi 2023

Baada ya kupata habari za kifo cha baba yake asubuhi ya Machi 18, walifanya mazishi baadaye siku hiyo hiyo

 Amesema kulingana na mila na desturi zao, ni lazima warejee walikomzika baba yao asubuhi iliyofuata.Walipofika, walikuta kaburi limefukuliwa na jeneza limevunjwa.

Waligundua pia marehemu baba yao mwenye umri wa miaka 74, hakuwa na baadhi ya sehemu za mwili. Lakini baadaye walizika tena mwili huo upya.

Baadhi ya jamaa wengine wa marehemu walionyesha masikitiko yao baada ya kupata taarifa hizo na kueleza kuwa bado hawajabaini sababu kuu iliyopelekea mwili huo kufukuliwa.Walihusisha tukio hilo na imani za kishirikina na uchawi.

Wakati hayo yakijiri, kule nchini Kenya nako Jamaa afukua mwili wa shemejiye Katika tukio tofauti la kufanana na hilo,

kulikuwa na kisa cha ajabu katika kaunti ya Migori baada ya mwanamume mmoja kuufukua mwili wa shemeji yake uliozikwa katika boma lake miaka 12 iliyopita.

Isitoshe, mwanamume huyo alichukua mabaki hayo ya shemeji yake na kuweka kwenye gunia na kwenda kuyatupa kwa mke wake wa zamani Monica Adhiambo.

Ripoti ya polisi ilisema kuwa mwanamume huyo alitengana na Adhiambo mwaka wa 2020, na alifanya kitendo hicho cha ajabu kupinga kutemwa na mke wake wa zamani, ambaye dada yake Joan Apondi alikuwa amezikwa nyumbani kwake

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU APATIKANA AMEFARIKI NYUMBANI KWAKE SIKU CHACHE BAADA YA KUGOMBANA NA MPENZIWE

 

Polisi huko Kabale wanajaribu kusuluhisha mauaji mawili yaliyounganishwa baada ya mwili wa Sarah Naturida, uliotazama chini ukiwa umefungwa mikono kupatikana katika chumba chake cha alichopanga

Babake, Naris Ndanganwa alikuwa na wasiwasi baada ya kutosikia chochote  kutoka kwa bintiye kwa siku mbili na akampigia simu mwenye nyumba wa Naturida ili kuuliza aliko.

Ni mawazo ya babake ambayo yalisababisha msako wa polisi. Msemaji wa polisi mkoani Kigezi, Elly Maate, alithibitisha hilo walipouliza kutoka kwa majirani zake na mwenye nyumba.

Maafisa wa polisi, mwenye nyumba na babake Naturida walifika chumbani kwake, wakakuta kimefungwa na kuvunja kufuli. Hapo ndipo maiti yake ilipopatikana.

Kulingana na walioshuhudia kioja hicho, mrembo huyo alizozana na Denis Arinaitwe; mwanamume anayeaminika kuwa mpenzi wake Jumapili asubuhi.

Hili liliwashangaza polisi kwa sababu Arinaitwe tayari yuko chini ya ulinzi wao  baada ya kumpiga risasi mpenzi wake, polisi mwanamke, Caroline Komugisha, katika makazi yake kambini.

Alijaribu kujitoa uhai, lakini alikamatwa na maafisa wengine wa polisi waliokuja mbio baada ya kusikia milio ya risasi. Kulingana na gazeti la Monitor, uchunguzi unaendelea ili kubaini kile ambacho kingeweza kusababisha Arinaitwe kumuua msichana huyo wa polisi

MWANAHABARI WA UFARANSA ALIYESHIKILIWA NA WANAMGAMBO NCHINI MALI KWA MIAKA SABA AREJEA NYUMBANI.

 


Mwanahabari Olivier Dubois  mwenye umri wa miaka 48 kutoka Ufaranasa Jumanne amerejea nyumbani baada ya kushikiliwa kwa karibu miaka 7 kwenye eneo  la Sahel.

Mwanahabari huyo alilakiwa na familia yake pamoja na rais Emmanuel Macron, kwenye uwanja mmoja wa ndege karibu na mji mkuu wa Paris.


Dubois akiwa na mfanyakazi wa kutoa msaada Jeffery Woodke mwenye umri wa miaka 61 kutoka Marekani walikamatwa kusini magharini mwa Niger Okotoba 2016, na waliwasili kwenye mji mkuu wa taifa hilo wa Niamey Jumatatu baada ya kuachiliwa huru.


Video iliyotolewa awali na watu waliokuwa wamemshikilia inasema kwamba walikuwa ni kutoka kundi la Support Group for Islam and Muslims, GSIM, ambalo linajumuisha makundi ya kigaidi ya Sahel, na linalohusishwa na lile la Al-Qaeda.

Dubois alikuwa akiishi nchini Mali tangu 2015 wakati akiwa mwanahabari huru wa gazeti la Ufaransa la Liberation, pale alipokamatwa. Hakuna taarifa za kina zilizotolewa kuhusu Dubois na mwenzake Woodke.

Wednesday, March 22, 2023

POLISI IRINGA WAMEKAMATA BAJAJI 446 KWA MAKOSA MBALIMBALI

 

 
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Allan Bukumbi akizungumza na madereva bajaji ambao bajaji zao zimekamatwa kutokana na makosa ya kutotii sheria za barabarani.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Allan Bukumbi akizungumza na madereva bajaji ambao bajaji zao zimekamatwa kutokana na makosa ya kutotii sheria za barabarani.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa Acp Allen bukumbi akionyesha GPS iliyoibwa katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Iringa .

Na Fredy Mgunda, Iringa.


JESHI la Polisi Mkoani Iringa wamekamata bajaji 446 kutokana na sababu mbalimbali huku likiwataka madereva bajaji kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuondokana na ajali zinazohatarisha maisha yao 

Amesema kuwa ni vyema vijana hao wakazingatia sheria kwani wamekuwa wakihatarisha maisha yao kutokana na kutotii sheria za barabarani hali ambayo imesababisha moja ya dereva bajaji kupata madhira ya ajali 

“katika operesheni hiyo bajaji yenye namba za usajili mc 677 BZL aina ya TVS ilikutwa imetelekezwa katika eneo la kitanzini ndipo walipofika katika eneo hilon na kuikuta bajaji hiyo na kuipeleka katika kituo cha polisi ilipofika majira ya saa sabab mchana askari waliokuwa katika doria maeneo ya samora walipata taarifa kuwa kuna mtu ameonekana mteremko wa kisima cha bibi mlima wa ipogoro ameumia ndipo walipomchukua na kumpeleka hospitalini kijana aliyefahamika kwa jina la Esau Hosea Kilawa ambaye mpaka taarifa za leo asubuhi bado yupo ICU"

Alisema kuwa ni vyema kila mtu akafuata sheria kwani bila hivyo inaweza pelekea jeshi la polisi kudhami dereva bajaji anayekimbia anauhalifu mwingine alioufanya 

Katika hatua nyingine Jeshi la polisi mkoani Iringa watu kadhaa kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali ikiwa ni pamoja na manyoya ya mkia wa tembo ,kichwa cha mnayama pundamilia pamoja na nyama ya swala 

Hili linakuja baada ya msako wa jeshi la polisi kwa kushirikiana na askari uhifadhi katika msako na hivyo kuwakamata felician modestus mwenye umri wa miaka 46 ,efrahim esiyo mwenye umri wa miaka 51 ,ezekiel remigus umri wa miaka 45 kwa makosa ya kuwa na nayara za serikali .

“Ndugu waandishi wa habari Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori Hifadhi ya Taifa Ruaha tumefanikiwa kuwakamata Efrahim Esiyo  ambaye alikutwa na kichwa,mkia na nyama ya pundamilia na silaha moja aina ya gobole,baruti,shoka na panga ndani ya hifadhi ya Ruaha , Ezekiel Remigus mkazi wa kisinga ,Jimale Chilala umri wa miaka 41 mkazi wa nyamakuyu feliecian modestus mponzi mwenye umri wa miaka 46 mkazi wa igangidung’u kwa makosa ya kukamatwa na mfuko wa salfeti wenye manyoya ya tembo"

Aidha ACP Allan Bukumbi alibainisha kuwa wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita kwa kosa la kuwa na mali za wizi 

“ tumemkamata fadhili lulandala miaka 31 mkristo fundi simu mkazi wa malingumu amour zahoro miaka 32 muislam mkulima mkazi wa lugalo kelvin mussa miaka 52 mkristo mkulima mkazi wa nyamahanga ,niko nyakunga miaka 40 mkazi wa ilole, baraka mtandi umri wa miaka 36 kutoka malingumu mafinga na ayub sanga miaka 20 mkazi wa ifunda kwa kosa la kuwa na ving’amuzi vinne ,tv tatu aina ya hometech inch 24 redio sub woofer remote mbili za tv simu janja 8 GPS MOJA NA TABLET MOJA"

BENKI YA CRDB, SILENT OCEAN ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUWASAIDIA WAFANYABIASHARA

 

 
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul (kushoto) kwa Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji Mizigo ya Silent Ocean, Salah Mohammed wakisaini hati ya makubaliano ya kuwawezesha wafanyabiashara ambao wanaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia Kampuni hiyo waweze kukidhi mahitaji ya soko na wakati huo huo kuepuka gharama za ziada zinazotokana na mzigo kukaa muda mrefu bandarini, ambapo wafanyabiashara hao watawezeshwa mkopo wa riba nafuu kwa kipindi cha kuanzia mwezi mmoja hadi miezi sita, katika hafla iliyofanyika leo Machi 21, 2023 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Benki ya CRDB, Pascal Mihayo (kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo. Mauzo wa Silent Ocean, Godfrey Mbowe.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul (kushoto) akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji Mizigo ya Silent Ocean, Salah Mohammed, muda  mfupi baada ya  kuzisaini ikiwa ni makualiano ya kuwawezesha wafanyabiashara ambao wanaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia Kampuni ya Silent Ocean ili waweze kukidhi mahitaji ya soko na wakati huo huo kuepuka gharama za ziada zinazotokana na mzigo kukaa muda mrefu bandarini, ambapo wafanyabiashara hao watawezeshwa mkopo wa riba nafuu kwa kipindi cha kuanzia mwezi mmoja hadi miezi sita, katika hafla iliyofanyika leo Machi 21, 2023 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja wadogo na wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul akizungumza katika hafla ya kuingia makualiano ya kuwawezesha wafanyabiashara ambao wanaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia Kampuni ya Silent Ocean ili waweze kukidhi mahitaji ya soko na wakati huo huo kuepuka gharama za ziada zinazotokana na mzigo kukaa muda mrefu bandarini, ambapo wafanyabiashara hao watawezeshwa mkopo wa riba nafuu kwa kipindi cha kuanzia mwezi mmoja hadi miezi sita, katika hafla iliyofanyika leo Machi 21, 2023 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha  Biashara wa Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbagu akizungumza katika hafla ya kuingia makualiano ya kuwawezesha wafanyabiashara ambao wanaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia Kampuni ya Silent Ocean ili waweze kukidhi mahitaji ya soko na wakati huo huo kuepuka gharama za ziada zinazotokana na mzigo kukaa muda mrefu bandarini, ambapo wafanyabiashara hao watawezeshwa mkopo wa riba nafuu kwa kipindi cha kuanzia mwezi mmoja hadi miezi sita, katika hafla iliyofanyika leo Machi 21, 2023 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya  CRDB, Mussa Lwila akizungumza katika hafla ya kuingia makualiano ya kuwawezesha wafanyabiashara ambao wanaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia Kampuni ya Silent Ocean ili waweze kukidhi mahitaji ya soko na wakati huo huo kuepuka gharama za ziada zinazotokana na mzigo kukaa muda mrefu bandarini, ambapo wafanyabiashara hao watawezeshwa mkopo wa riba nafuu kwa kipindi cha kuanzia mwezi mmoja hadi miezi sita, katika hafla iliyofanyika leo Machi 21, 2023 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es salaam.
Meneja wa Benki ya  CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd akizungumza katika hafla ya kuingia makualiano ya kuwawezesha wafanyabiashara ambao wanaagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kupitia Kampuni ya Silent Ocean ili waweze kukidhi mahitaji ya soko na wakati huo huo kuepuka gharama za ziada zinazotokana na mzigo kukaa muda mrefu bandarini, ambapo wafanyabiashara hao watawezeshwa mkopo wa riba nafuu kwa kipindi cha kuanzia mwezi mmoja hadi miezi sita, katika hafla iliyofanyika leo Machi 21, 2023 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wafanyabiashara na wageni waliohudhulia hafla hiyo wakiendelea kufuatilia tukio hilo.






NACHINGWEA KUKAMATAA WOTE WALIO KULA PESA ZA ASILIMIA 10

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Adinani Mpyagila ametangaza vita na vikundi vyote ambavyo vimekuwa havirudishi mikopo ya asilimia 10 wanayokopeshwa na Halmashauri hiyo kwa mujibu wa sheria za nchi.


Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya LAAC, Mwenyekiti huyo alisema kuwa kumekuwa na vikundi vingi vinakopa lakini vinashindwa kurudisha fedha hizo kwa wakati au mara nyingine wasirudishe kabisa fedha hizo hivyo kamati ya LAAC imewapa nguvu ya kuwakamata wote ambao hawajarudisha fedha hizo na kuwapeleka mahakamani.

Mpyagila alisema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea itaendelea kutoa kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vyote kama ambavyo serikali imeagiza lakini watakuwa makini na wakali kwa wanavikundi wote wadanganyifu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Injinia Chionda Kawawa alisema kuwa watakuwa makini mno wakati wa kutoa mikopo ya asilimia 10 ili kuepukana na usumbufu ambao wamekuwa wakiupata kutoka kwa wananchi waliokopa kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.

Injinia Kawawa alisema kuwa kamati ya LAAC imewapa nguvu na njia muhimu za kufuatilia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ili kila kikundi kinarejesha mkopo kwa wakati na vikundi vingine viendelee kukopa.

Naye mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka wafanyakazi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea kuacha mara moja kufanya kazi kwa mazoea ili kuendana na Kasi ya serikali ya awamu ya sita.


Moyo alisema kuwa hatakuwa tayari kumvumilia mtendaji yoyote yule atakaye fanya kazi kwa mazoea katika wilaya ya Nachingwea.

Tuesday, March 21, 2023

TANGA UWASA KUFUFUA VISIMA VYOTE VYA MAJI VILIVYOKUWA VIKITUMIKA

 Mhandisi wa Tanga Uwasa Salum Ngumbi wakati wa ziara ya wateja na mabalozi wa maji kutembelea miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo ili kujifunza na kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya maji.


Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla akizungumza wakati wa ziara ya wateja na mabalozi wa maji kutembelea miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo ili kujifunza na kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya maji.

 

Na Oscar Assenga,TANGA.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi Mazingira (Tanga Uwasa) umeweka bayana mikakati waliokuwa nayo kwa sasa wa kufufua  visima vyote vya maji zilivyokuwa vinatumika ili kupunguza kero ambazo zinaweza kuzuilika.

Mkakati huo uliwekwa hadharani na Mhandisi wa Tanga Uwasa Salum Ngumbi wakati wa ziara ya wateja na mabalozi wa maji kutembelea miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo ili kujifunza na kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya maji.

Alisema visima hivyo vipo katika  maeneo ya uwanja wa ndege,na Mwakileo ikiwa ni mbadala wa maji kwa wananchi,ikitokea kupungua kwa maji ili waweze kuvitumia kwa ajili ya kuwafikia wananchi pasipo kuwepo na kizuizi chochote.
Alisema pamoja na kufufua visima hivyo lazima watahakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ambao wamekuwa wakiwahudumia kila siku ili kuondosha vikwazo ambavyo wanaweza kukutana navyo.

"Mpango tulionao kwa sasa ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata maji kukidhi mahitaji muhimu kwa wananchi,pia tuna mpango wa kuanza miradi ya maendeleo katika mamlaka ya maji ikiwemo mradi wa ujenzi wa kutanua bwawa la mabayani na tunatarajia uanze septemba mwaka huu".

Upatikanaji wa maji kwa siku katika maeneo yote ni lita 30,000,ambapo kwa sasa mtambo uliopo ni kwa ajili ya kutanua uzalishaji kufikia lita 45,000 ambayo itasaidia kukidhi haja kwa wananchi wote.

“Kwa sasa upo mradi uliogharimu zaidi ya sh.Bilioni 10 ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji katika jamii kwani tunafanya hivi kuhakikisha yaliyojitokeza kwa wananchi kukumbana na changamoto ya huduma hii hayajitokezi tena na hali iliweza kuwaathiri wakazi katika maeneo mbalimbali Jijini Tanga kutokana na mvua kutokunyesha kwa kipindi kirefu na kusababisha Bwawa la Maji kupungua”Alisema

"Tuna mitambo minne ambayo miwili ndio inatumika Kwa Sasa ns inasaidia kupandisha Maji mpaka kuwafikia wananchi na mingine miliwi ipo kwa ajili ya akiba kama ikitokea mmoja kati ya hii ikiharibika" 

 Mhandisi salum aliwashauri pia wakazi wa Tanga kupanda miti itakayosaidia kutunza mazingira muda wote na kusababisha kunyesha mvua za mara Kwa mara Ili kuwepo na upatikanaji wa Maji

“Suala la miti kuwa michache katika maeneo yetu tunayoishi ni Changamoto niwaombe wananchi kupanda miti Ili kusaidia mazingira yetu muimarika na Hata mvua ziweze kunyesha Ili tupate maji muda wote”Alisema

Akielezea changamoto ya ukosefu wa Maji tokea mwezi Novemba Mwaka jana ambapo alieleza mpaka kufikia mwezi Machi mwaka huu hali hiyo imeweza kuimarika hivyo amewaomba wakazi wote kutumia Maji kwa umakini na ikiwemo kujenga utamaduni ya kuyahifadhi kwa ajili ya kuwasaidia katika maatumizi yao.

"Kuanzia machi Mwaka huu hali ya upatikanaji wa Maji imeanza kuwa shwari ingawaje haijafikia asilimia 100 , maeneo mengi yanapata maji na vilevile Tanga Uwasa tumejipanga kutatua changamoto iliyokuwepo"Alisema Mhandisi Salum

Naye kwa upande wake Mtaalamu wa Maabara kutokea kwenye mtambo wa kutibu Maji wa Mowe Amos Rwehangana alisema kwa sasa hali ya kutoka kwa Maji ipo vizuri katika maeneo mbalimbali yakiwa masafi na hayawezi kuleta athari yoyote katika jamii na hiyo inatokana na juhudi walizonazo .

MWANAMKE AFARIKI DUNIA WAKATI AKISHIRIKI NGONO KICHAKANI KAUNTI YA HOMA BAY.

Mwanamme mwenye umri wa miaka 37 anakabiliwa na mashataka ya mauaji baada ya mpenzi wake aliyefahamika kama Milca na mwenye umri wa miaka 48 kufariki wakati wakifanya ngono kichakani eneo bunge la Mbita kaunti ya Homa Bay.  

Mtuhumiwa anasemekana kumrithi marehemu baada ya kifo cha mume wake kama ilivyo tamadumi ambapo mwanamke anaruhusiwa kurithiwa baada ya kifo cha mume wake

.Wawili hawa wanasemekana kuwa walionekana wakibugia pombe katika kilabu kimoja eneo hilo jioni ya kabla ya kuondoka kuelekea nyumbani.

Wakiwa njiani hapo ndipo wasia wa kuyatia mahanjam katika mapenzi yao iliwajia na kisha wakaamua kuingia kichakani eneo la Got Rateng na kushiriki tendo la ndoa wasijuwe lilokuwa linawasubiri.

Mtuhumiwa huyo aliyekutwa na kisa hicho amesemekana kuwa alijaribu kuuzika mwili wa Milca.

Kulingana na chifu wa Lambwe Mashariki Bernard Ouma wawili hawa walikuwa wameonywa dhidi ya kubugia pombe na kuwa mshukiwa hakutarajia kuwa mpenzi wake angefariki wakati wa ngono.

Amatuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kukiri kuwa marehemu alifariki wakati walipokuwa wanashiriki ngono

Chifu wa eneo hilo amesema kuwa alikuwa amefanya kikao na wawili hao awali na kuwaonya dhidi ya hulka yao ya kufanya mapenzi kiholela  baada ya kubugia vileo.

Mwili wa mwendazake umepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Homa Bay uchunguzi zaidi ukitarajiwa kufanywa.

MALAWI INAKABILIWA NA HATARI YA ONGEZEKO LA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU KUFUATIA UHARIBIFU ULIOSABABISHWA NA KIMBUNGA FREDDY AMBACHO KIMEHARIBU MIFUMO YA MAJI NA VYOO, WIZARA YA AFYA ILIONYA JUMATATU.



Nchi hiyo ambayo ilikuwa tayari ikipambana mlipuko mkubwa wa kipindupindu ambao haujawahi kurekodiwa wakati dhoruba ya kimbunga Freddy ilipotua wiki iliyopita, na kusababisha maporomoko ya matope na mafuriko, ambapo watu 476 walipoteza maisha na wengine takribani nusu milioni kukoseshwa makazi.

Mlipuko wa kipindupindu nchini humo uliozuka mwaka jana, ambapo watu zaidi ya 30,600 waliambukizwa na wengine zaidi ya 1,700 kupoteza maisha.


Baada ya mashambulizi ya kimbunga hicho kilichovunja rekodi, dhoruba hiyo ilisababisha vifo vya watu 579 katika nchi tatu za kusini mwa Afrika zikiwemo Msumbiji na Madagascar.

Malawi ni nchi iliyoathirika zaidi wakati kimpunga Freddy kiliposababisha mafuriko na maporomoko ya udongo ambayo yalisomba nyumba, barabara na madaraja – na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ya maji nchini humo.



..................................................................................................................................................................................................................................................................................


WAKATI HUO HUO KUTOKA NCHINI MSUMBIJI


WAZIRI WA AFYA WA MSUMBIJI ALISEMA IJUMAA KUWA MLIPUKO WA KIPINDUPINDU KATIKA ENEO LILILOPIGWA NA KIMBUNGA FREDDY KIMEUA WATU WANANE WIKI HII NA WENGINE 250 WAMELAZWA HOSPITALI – IKIWA NI SEHEMU YA WATU 600 AMBAO NI WAGONJWA TANGU KUTUA KWA KIMBUNGA KATIKA ENEO HILO MWEZI FEBRUARI.

 

Waziri wa Afya Armindo Tiago amekiambia Radio Msumbiji inayomilikiwa na serikali kwamba waathirika wa kipindupindu walikuwa katika mji wa bandari wa Quelimane, mji mkuu wa Jimbo la Zambezia, eneo lililokuwa limeathiriwa sana na kimbunga hicho.

Tigao alisema hatua ya kuzuia kipindupindu imelengwa katika vituo 133 vya mji huo ambavyo vinatoa hifadhi kwa takriban watu 50,000 waliokoseshwa makazi kutokana na mafuriko. Ameongeza kuwa juhudi zaidi zinahitajika katika majimbo mengine yaliyokumbwa na Kimbunga Freddy, kimbunga cha historia ambacho kimepiga katika eneo hilo tangu Februari.

Tiago alisema kila mtu lazima afanye juhudi kudhibiti mlipuko huo kwa kuchemsha maji ya kunywa, kusafisha na kuosha chakula, na kutupa takataka inavyotakiwa – hususan choo cha binadamu. Iwapo watu wana dalili kama vile kuharisha na kutapika, lazima wafike katika vituo vya afya.


POLISI WAMUUA MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MASENO BAADA YA KUTUMIA RISASI KUWATAWANYA WAANDAMANAJI


Chuo kikuu cha Maseno kimempoteza mwanafunzi wa mwaka wa tatu William Mayange (pichani aliye chuchumaa) aliyekumbana na kifo chake baada ya polisi kutumia risasi kuwatawanya wanafunzi wa chuo hicho waliokuwa wakiandamana kulalamikia hali ngumu ya kiuchumi.

Mayange anasemekama kudhibitishwa kuwa amefariki alipofikishwa katika hospitali ya Coptic alikokuwa amepelekwa kupata huduma ya kwanza.


Marehemu  anasemekana kupigwa risasi shingoni alipokuwa amejumuika na wenzake nje mwa lango kuu la chuo hicho wakati wa maandamo yaliyokuwa yameitishwa na muungano wa Azimio ili kuishurutisha serikali kupunguza gharama ya maisha

Mayange alisoma katika shule ya upili ya Ringa Boys kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Maseno miaka mitatu iliyopita.

Polisi wamesema kuwa maandamano ya wanafunzi hao yalizua rapsha na kupelekea maafisa wa usalama kutumia risasi baada ya kuishiwa na vitoa machozi.

Maafisa wa usalama wamesema kuwa wanafunzi waliokuwa wakiandamana walionekana kuwashinda nguvu jambo ambalo lilichangia utumiaji wa risasi.

Maandamano ya Jumatatu 20 yameshuhudia makabiliano makali kati ya polisi wa wafuasi wa Azimio kote nchini.

 Kinara wa Azimio Raila Odinga ametangaza kuwa kila Jumatatu itakuwa ni siku ya maandamano hadi pale serikali itakaposhughulikia matakwa yao

ADUI MKUBWA WA BARABARA ZA LAMI NI MAFUTA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Jeh ni muda gani wa kikomo kwa gari likiharibika barabarani linatakiwa kuondoshwa? Na vipi kunapokuwa na misafara ya viongozi wa kitaifa na wakuu wa nchi, na gari lako likaharibika njiani? Sikiliza, fuatilia maswali ya wanafunzi wa Victoria Nganza High School na majibu toka kwa maafisa wa #TANROADS

MADAKTARI,WAUGUZI WAKIWEMO WATOA HUDUMA HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO WAPEWA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MITUNGI YA OXYGEN

 Mhandisi wa  Vifaa tiba wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Mhandisi Gabriel Mringi kulia akitoa elimu juu ya Matumizi sahihi ya mitungi ya Oxygen kwa wagonjwa iliyokuwa ikitolewa kwa wauguzi na madaktari wakiwemo watoa huduma hospitalini leo kwenye hospitali hiyo lengo kuongeza ujuzi kwa watumiaji wa mitungi  hiyo kwa wagonjwa wa pili kutoka kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Naima ZakariaMhandisi wa  Vifaa tiba wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Mhandisi Gabriel Mringi kulia akitoa elimu juu ya Matumizi sahihi ya mitungi ya Oxygen kwa wagonjwa iliyokuwa ikitolewa kwa wauguzi na madaktari wakiwemo watoa huduma hospitalini leo kwenye hospitali hiyo lengo kuongeza ujuzi kwa watumiaji wa mitungi  hiyo kwa wagonjwaMhandisi wa  Vifaa tiba wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Mhandisi Gabriel Mringi kulia akitoa elimu juu ya Matumizi sahihi ya mitungi ya Oxygen kwa wagonjwa iliyokuwa ikitolewa kwa wauguzi na madaktari wakiwemo watoa huduma hospitalini leo kwenye hospitali hiyo lengo kuongeza ujuzi kwa watumiaji wa mitungi  hiyo kwa wagonjwa  wa pili kutoka kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Naima Zakaria


Mhandisi wa Vifaa tiba wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Mhandisi Gabriel Mringi kulia akitoa elimu juu ya Matumizi sahihi ya mitungi ya Oxygen kwa wagonjwa iliyokuwa ikitolewa kwa wauguzi na madaktari wakiwemo watoa huduma hospitalini leo kwenye hospitali hiyo lengo kuongeza ujuzi kwa watumiaji wa mitungi hiyo kwa wagonjwa
Mhandisi wa  Vifaa tiba wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Mhandisi Gabriel Mringi kulia akitoa elimu juu ya Matumizi sahihi ya mitungi ya Oxygen kwa wagonjwa iliyokuwa ikitolewa kwa wauguzi na madaktari wakiwemo watoa huduma hospitalini leo kwenye hospitali hiyo lengo kuongeza ujuzi kwa watumiaji wa mitungi  hiyo kwa wagonjwa,Picha na Bombo Hospital