Watu wasiojulikana wamefukua kaburi na kunyofoa sehemu za siri za mwili wa marehemu Ruben Kasala, aliyezikwa Machi 18, 2023.
Mtoto
wa marehemu Frank Kasala alisema baba yake Ruben Kasala alikuwa akiugua
kisukari na kukumbana na matatizo ya mapafu tangu Machi 2023
Baada ya kupata habari za kifo cha
baba yake asubuhi ya Machi 18, walifanya mazishi baadaye siku hiyo hiyo
Amesema kulingana na mila na desturi zao, ni
lazima warejee walikomzika baba yao asubuhi iliyofuata.Walipofika, walikuta
kaburi limefukuliwa na jeneza limevunjwa.
Waligundua pia marehemu baba yao
mwenye umri wa miaka 74, hakuwa na baadhi ya sehemu za mwili. Lakini baadaye
walizika tena mwili huo upya.
Baadhi ya jamaa wengine wa marehemu
walionyesha masikitiko yao baada ya kupata taarifa hizo na kueleza kuwa bado
hawajabaini sababu kuu iliyopelekea mwili huo kufukuliwa.Walihusisha tukio hilo
na imani za kishirikina na uchawi.
Wakati hayo yakijiri, kule nchini
Kenya nako Jamaa afukua mwili wa shemejiye Katika tukio tofauti la kufanana na hilo,
kulikuwa na kisa cha ajabu katika
kaunti ya Migori baada ya mwanamume mmoja kuufukua mwili wa shemeji yake
uliozikwa katika boma lake miaka 12 iliyopita.
Isitoshe, mwanamume huyo alichukua
mabaki hayo ya shemeji yake na kuweka kwenye gunia na kwenda kuyatupa kwa mke
wake wa zamani Monica Adhiambo.
Ripoti ya polisi ilisema kuwa
mwanamume huyo alitengana na Adhiambo mwaka wa 2020, na alifanya kitendo hicho
cha ajabu kupinga kutemwa na mke wake wa zamani, ambaye dada yake Joan Apondi
alikuwa amezikwa nyumbani kwake
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.