Polisi huko Kabale wanajaribu kusuluhisha mauaji mawili yaliyounganishwa baada ya mwili wa Sarah Naturida, uliotazama chini ukiwa umefungwa mikono kupatikana katika chumba chake cha alichopanga
Babake, Naris Ndanganwa alikuwa na
wasiwasi baada ya kutosikia chochote kutoka kwa bintiye kwa siku mbili na akampigia
simu mwenye nyumba wa Naturida ili kuuliza aliko.
Ni mawazo ya babake ambayo
yalisababisha msako wa polisi. Msemaji wa polisi mkoani Kigezi, Elly Maate,
alithibitisha hilo walipouliza kutoka kwa majirani zake na mwenye nyumba.
Maafisa wa polisi, mwenye nyumba na
babake Naturida walifika chumbani kwake, wakakuta kimefungwa na kuvunja kufuli.
Hapo ndipo maiti yake ilipopatikana.
Kulingana na walioshuhudia kioja
hicho, mrembo huyo alizozana na Denis Arinaitwe; mwanamume anayeaminika kuwa
mpenzi wake Jumapili asubuhi.
Hili liliwashangaza polisi kwa sababu
Arinaitwe tayari yuko chini ya ulinzi wao baada ya kumpiga risasi mpenzi wake, polisi
mwanamke, Caroline Komugisha, katika makazi yake kambini.
Alijaribu kujitoa uhai, lakini
alikamatwa na maafisa wengine wa polisi waliokuja mbio baada ya kusikia milio
ya risasi. Kulingana na gazeti la Monitor, uchunguzi unaendelea ili kubaini
kile ambacho kingeweza kusababisha Arinaitwe kumuua msichana huyo wa polisi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.