ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 20, 2022

RC MGUMBA SENSA INA UMUHIMU MKUBWA SANA KWA VIJANA

 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba katika akiongoza matembezi maalumu ya kuhamasisha  zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika nchini Agosti 23 mwaka huu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema na kushoto  ni Mkuu wa wilaya Tanga Hashim Mgandiliwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillooo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba katika akiongoza matembezi maalumu ya kuhamasisha  zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika nchini Agosti 23 mwaka huu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema na kushoto  ni Mkuu wa wilaya Tanga Hashim Mgandiliwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillooo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba katika akiongoza matembezi maalumu ya kuhamasisha  zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika nchini Agosti 23 mwaka huu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema na kushoto  ni Mkuu wa wilaya Tanga Hashim Mgandiliwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillooo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba katika akiongoza matembezi maalumu ya kuhamasisha  zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika nchini Agosti 23 mwaka huu kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema na kushoto  ni Mkuu wa wilaya Tanga Hashim Mgandiliwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillooo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza wakati wa matembezi hayo leo
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa akizungumza kuhusu namna walivyojipanga kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi




NA OSCAR ASSENGA,TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema Sensa ya watu na makazi ina umuhimu mkubwa sana kwa vijana kwa sababu wao ndio Taifa la leo na kesho hivyo mipango mingi inayopangwa inawagusa kwa sababu jambo hilo sio la kila mwaka bali ni kila baada ya miaka 10.

Mgumba aliyasema hayo leo wakati wa matembezi kwa ajili ya kuhamasisha zoezi Sensa ya Watu na Makazi iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga ambapo alisema sensa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Alisema kwa hiyo mipango ya miaka 10 ijayo itategemea idadi ya watu na makazi na shughuli zitakazobainika baada ya Sensa hiyo kukamilika hivyo ndio maana Rais Samia Suluhu ametoa siku hiyo kuwa ya mapumziko kutokana na umuhimu wake.

"Nimeamini Tanga hatuna dogo na jambo la mama ni letu wana Tanga mmedhihirisha kwa vitendo hili lililofnyika Tanga linafanyika na wilaya nyengine lengo ni kuhamasishana tujitokeze kwa wingi kushiriki kwenye katoka zoezi la sensa ya watu na makazi kwani ni muhimu kwa maendeleo yetu ua mkoa na Taifa na itatusaidia kupata takwimu sahihi shughuli za watu na kufahamu uchumi wa watu hivyo kusaidia serikali kupanga mpango wa maendeleo

Alisema wasipopata idadi kamili ya watu itakuwa ni vigumu kwa serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa watu wake na baadae wao watalalamika kwamba serikali inapendelea na inapeleka miradi mingi mikoa fulani kwa sababu kule ndio walijitokeza kwa wingi wakati huo.

Alisema suala la sensa halina mahusiano yoyote na imani za kidini,kijadi wala kimila bali ni kupanga maendeleo kwa watanzania hususani wakazi wa mkoa huo wa Tanga

Hata hivyo aliwataka wakazi wa mkoa huo kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23 mwaka huu hapa nchini

Awali akizungumza wakati wa matembezi hayo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alisema matembezi hayo yalikiwa ni muhimu kwa ajili ya uhamasishaji watu kujitokeza kwenye zoezi sensa ambapo wametembea umbali wa kilomita 7 kutoka kwenye viwanja vya urithi kuzunguka maeneo mbalimbali Jijini humo na kurejea walipoanzia.

Alisema wameanzisha mpango wa mtaa kwa mtaa Tanga na Sensa 2022 wana vijana 40 madensasi wanapita kila mtaa yote ya Tanga na kutoa burudani kwa dakika tano na kutoa ujumbe wa sensa anasma wanaamini kupitia mpango huo wanaweza kuwafikia watu wengi Jijini humo

Friday, August 19, 2022

RC MALIMA ATAJA SABABU MIFUGO YA TANZANIA KUTOUZIKA NJE.

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima amewataka wazalishaji wa bidhaa ikiwemo wazalisha wa nyama nchini kuacha kulalamika kwamba hakuna soko la nyama nje ya nchi badala yake wazingatie vigezo vya kimataifa vya uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Malima ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua Semina ya Kuhamasisha Masuala ya Ushidani na Udhibiti wa Bidhaa Bandia kwa wazalishaji mkoani Mwanza iliyoandaliwa na Tume ya Ushindani nchini.

Thursday, August 18, 2022

MAANDAMANO YA WANANCHI MESERANI YAWANYWESHA MAJI.

 

Bertha Ismail.

Arusha .  Zaidi ya wananchi 40,000 kutoka vijijini saba vya Tarafa ya Meserani wanatarajia kuanza kunywa maji safi na salama baada ya serikali jana kumkabidhi mkandarasi mradi wa kuanza ujenzi wa miundo mbinu ya maji itakayogharimu jumla ya bilioni 1.7.

Hatua hiyo imefikia baada ya hivi karibuni wananchi hao kuandamana hadi barabarani na kuzuia msafara wa waziri wa Maji Jumaa Aweso aliyekuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji agost 1 mwaka huu.

Wananchi hao walimlilia wakiwa na ndoo kichwani wakidai kuwa wamechoka kutembea umbali mrefu kusaka maji ya mabwawa na vidimbwi kwa matumizi ya nyumbani ikiwemo kunywa hali inayopelekea kuugua kila kukicha.

Akizungumza katika kamabidhiano hayo, meneja wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini ‘RUWASA’ Neville Msaki alisema kuwa maandamano yenu yamezaa matunda ya kufanikisha serikali kupitisha bajeti ya bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya maji katika vijiji saba vya kata ya Esilalei na majengo.

 

“Baada tu ya kupokea fedha hizi, serikalii ilituagiza kumtafuta mkandarasi haraka na kusaini mkataba ambavyo vyote tiyari na kama mnavyoomuona tumekuja kwenu kumtambulisha na kumkabidhi eneo la mradi ambapo anaanza kazi kesho ya kusambaza mabomba na kuhakikisha anaukamilisha mradi na kuukabidhi baada ya miezi sita ukiwa na mafanikio ya wananchi kuanza kutumia maji safi” alisema Msaki.

 

Alisema kuwa mradi huo unaotoa maji kutoka chanzo cha mto wa Mbu unatarajia kutoa kiasi cha lita milioni moja kwa siku ambayo yanatosha kwa matumizi ya kawaida ya wananchi wote wa vijiji hivyo na vya jirani.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi mkandarasi eneo hilo la kuanza mradi, mkuu wa wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe alisema kuwa mradi huo uliokuwa uanze siku nyingi ulikwama kutokana na fedha hazikufika hivyo ziara ya waziri imeleta mafanikio hayo.

 

“leo mradi unaanza ni mafanikio makubwa sana hivyo nimualike afisa wa TAKUKURU hapa na kamanda wa polisi wilaya washirikiane na wataalamu hawa mradi ukamilike ndani ya muda, kwani wananchi hawahitaji siasa bali maji pekee na sitaki kuja kusikia kuna mahali nyumba zimerukwa hazina maji, hakika hatutaelewana” alisema Mwaisumbe

 

Mwaisumbe pia alimtaka meneja wa RUWASA kuzivunja jumuiya zote za watumia maji zilizopo na kuunda chombo kimoja ndani ya siku 21 kitakachosimamia miradi yote ya maji ili kurahisisha ufuatiliaji na uwajibika katika utendaji na utekelezaji.

Nae mwenyekiti wa baraza la halmashauri ya Monduli, Isack Kadogoo alishukuru serikali kwa mradi huo na kuwataka wananchi hao kutoa ushirikiano wa ulinzi wa vifaa na miundombinu ya mradi visiibiwe.

“Tumemuomba mkandarasi vibarua wote watoke hapa eneo la mradi ili hata mama zetu wapike chakula wauze lakini na nyie mtoe ushirikiano mzuri wa kutunza na kulinda hivi vifaa, jamani msiibe tukaanza kukamatana na vyombo vya sheria tukachelewa kunywa maji mazuri”

 

Nae mkandarasi huyo, Fauz Eshaq kutoka kampuni ya ‘Skywords construction Ltd’ alisema kuwa amepokea mradi na kuahidi kuutekeleza ndani ya mda kwa uaminifu mkubwa hivyo kuomba ushirikiano wa karibu na viongozi wa serikali wa ngazi zote za vijiji hadi wilaya.

SERIKALI YATANGAZA MAPUMZIKO SIKU YA SENSA.

SENSA PIC 2
 Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia Agosti 23, 2022 kuwa siku ya mapumziko.

 Lengo ni kuwezesha Watanzania kushiriki Sensa ya Watu na Makazi. Awali ilitangazwa kuwa siku hiyo haitakuwa aya mapumziko.

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa iliyotolewa leo Alhamisi Agosti 18, 2022 kupitia akaunti yake ya Twitter imesema, Rais Samia ameridhia siku hiyo iwe ya mapumziko.


“Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameridhia tarehe 23 Agosti 2022 iwe siku ya mapumziko ili Watanzania wawepo majumbani na waweze kuwapokea makarani wa sensa na kutoa maelezo sahihi,” amesema Msigwa

CHANZO: MWANANCHI.

MBUNGE KOKA ASHIRIKI KONGAMANO LA UWT KIBAHA.

 

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akizungumza Jambo na mamia ya wanawake walioshiriki katika kongamano hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake waliofika katika kongamano hilo.

Na Victor Masangu, Kibaha

Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewahasa umoja wa wanawake (UWT)  Wilaya ya Kibaha mjini kuhakikisha kwamba wanajitokeza kwa wingi katika zoezi la watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.


Koka ameyasema hayo wakati wa kongamano maalumu lililoandaliwa na uongozi wa (UWT) Kibaha mji ambalo limehudhuliwa  na wanawake zaidi ya mia tano kutoka kata zote 14 za Jimbo la Kibaha mjini na kuwashirikisha viongozi mbali mbali wa serikali.


Mbungu huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo amesema wanawake pamoja na wananchi wote wanapaswa kujitokeza siku hiyo kwa lengo la serikali kuweza kupata idadi kamili ya watu wake ili iweze kuweza kupanga bajeti yake kwa usahihi.


"Kwanza kabisa napenda kuwashukuru wanawake wote wa UWT katika jimbo langu la Kibaha mjini kwa kuweza kujiitokeza kwa wingi katika kongamano hili kwa ajili ya sensa ya watu na makazi kwa hili Jambo ni muhimu Sana,"alisema Koka.


Pia Mbunge Koka alisema kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha kwamba inatambua idadi ya watu wake wote ili iweze kuleta maendeleo katika nyanja mbali mbali hivyo ni muhimu wananchi wakajitokeza katika zoezi hilo.


Pia Koka amesema kuwa ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi wake wa Jimbo la Kibaha mjini katika kuhakikisha anawaletea chachu ya maendeleo katika miradi mbali mbali.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Elina Mngoja amesema kwamba lengo la kuandaa kongamano hilo ni kwa ajili kuweza kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi kwa wanawake mbali mbali wa Kibaha.


Pia alisema kwamba katika kongamano hilo litaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuwapatia wanawake hao waweze kupata fursa ya kujifunza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la sensa ya watu na makazi.


Naye Mbunge wa viti maalumu Subira Mgalu aliwasihi wanawake wote wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la sensa ya watu na makazi na kuongeza kwamba kufanya hivyo kutaisaidia serikali iweze kupanga mipango yake ya kimaendeleo.


Nao baadhi ya wanawake ambao wamehudhulia katika kongamano hilo wametoa pongezi kwa uongozi wa UWT pamoja na kumshukuru Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuweza kuweza kuwakutanisha kwa pamoja na kuwapatia elimu ya umuhimu wa sensa.


Kongamano hilo maalumu ambalo limeandaliwa na UWT Wilaya ya Kibaha limehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na viongozi wa chama Cha mapinduzi wakiwemo wabunge pamoja na madiwani.

NAIBU WAZIRI MARYPRISCA MAHUNDI ATOA SIKU SABA USAMBAZAJI WA MAJI KIJIJI CHA MSOMERA


NAIBU Waziri wa Maji MarryPrisca Mahundi akizungumza mara baada ya kukagua  mradi wa maji katika Kijiji cha Msomera Kata ya Misima wilayani Handeni ikiwemo kutembelea tenki lenye uwezo wa kuhifadhia maji lita 167,000 unaotekelezwa na Serikali ili kuhakikisha wananchi waliohamia kutoka wilaya ya Ngorongoro wanapata huduma ya maji safi na salama.
MKUU wa wilaya ya Handeni Siriel Mchemba akizungumza wakati wa ziara hiyo

Na Oscar Assenga,

NAIBU Waziri wa Maji Marry Prisca Mahundi ametoa siku saba kwa Meneja wa Ruwasa wilaya ya Handeni Mhandisi Hosea Joseph kuhakikisha anamsimamia mkandarasi wa Kampuni ya Mponela Dicksona Mwipoo anayetekeleza mradi wa maji katika Kijiji cha Msomera wilayani humo kuhakikisha maji yanafika kwenye tenki na kuyasambaza kwa wananchi.

Agizo la Naibu Waziri huyo alilitoa leo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji katika Kijiji cha Msomera Kata ya Misima wilayani Handeni ikiwemo kutembelea tenki lenye uwezo wa kuhifadhia maji lita 167,000 unaotekelezwa na Serikali ili kuhakikisha wananchi waliohamia kutoka wilaya ya Ngorongoro wanapata huduma ya maji safi na salama.

Alisema kwamba thamani ya hilo tenki ni kuhakikisha linatoa maji na yapelekwa kwa wananchi waliopo kwenye Kijiji hicho ili kuweza kuwaondolea changamoto ambazo wanakumbana nazo kusaka huduma hiyo muhimu kwa maendeleo yao na jamii zinazowazunguka.

Aidha alisema wao kama Wizara ya Maji mahali popote wanapoona wananchi wanakwenda kujenga kuishi wanahitajika kupatiwa huduma ya maji na kwa hapo Msomera maji yalikuwa yanapatikana kwa wingi kwa jitihada ambazo zimefanywa na Tanga Uwasa na Ruwasa.

“Niwapongeze Ruwasa ambao wanasimamiwa na Mhandisi Upendo Omari ambaye anafanya kazi nzuri sana hapa tulipo kuna tenki kubwa ambalo lililetwa kutoka nje lengo kuhakikkisha jamii ya msomera inapata maji toshelevu na kwa kupata tenki hili visima vilivyochimbwa hapa vinakwenda kutumika vizuri”Alisema

Naibu Waziri huyo alisema kuna kisima ambacho kinatoa maji mengi na wanategemea ndani ya wiki moja kutoka leo hiikitaanza kusafirisha maji kutoka eneo hilo na kwenda kwenye tenki na baadae usambazaji wa  maji kwa wananchi wataohamia hapa Msomera wanapata huduma ya maji.

“Niwahakikishie kama Serikali kupitia Wizara ya Maji muwe na uhakika mtapata maji kwa matumizi ya majumbani ya uhakika na jamii ina mifugo kwa sababu ya hilo tumejenga maeneo ya kunyeshea mifugo msomera matatu ili kuhakikisha wanyama wanapata maji ya kutosha na tunatambua kenye kundi hili kuna wakulima tayari waziei wa Kilimo atakuja lengo la kuhakikisha pia tunapata wakulima kupitia kilimo cha Umwagiliaji”Alisema Naibu Waziri huyo.

Alisma kwa sababu unjengeji wa nyumba unendelea katika eneo hilo watendelea usambaji wa maji na wanancji wanaendelei kupata maji karibu kwa sababu ujengeji nyuma unaendeleo kusambaa wengine watajikuta wanakuwa mbali na vichoeta maji vyao  watawafuata walipo lengo kuhakikisha maji yanapatikana kwa wingi kwa wananchi.

Hata hivyo alisema kwamba maji yakishafika kwenye tenki yatakwenda kwenye usambazaji wa vichotea maji na kwa wananchi watakaokuwa na uhitaji wa kuyavuta kwenye majumba yao watapewa vigezo vya na masharti nafuu ili waweze kuvuta maji,

“Lakini nitoe wito kwa wakandarsi wote ambao mnapewa kazi nchi mhakikisha mnafanya kazi kwa kujituma bila kuangali malipo yamelipwa kwa wakati au yamechelewa huyu mkandarsi hapa amefanya kazi nzuri tutaendelea kufanya naye kazi Wizara ya maji ipo chini ya Waziri Jumaa Aweso na Rais Samia Suluhu imedhamiria kuhakikisha inamtua mama ndoo kichwani ili waweze kufanya shughuli nyengine za kuchangia kwenye pato la Taifa kwa kufanya shughuli za uzalishaji “Alisema

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Omari alimueleza Naibu Waziri huyo kwamba wamepokea maelekezo hayo na wao watahakikisha kwamba ndani ya siku tatu wananchi wa eneo hilo wanapata maji.

Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Mchemba alisema kuwa kabla ya kuingia Serikali ya awamu ya sita hali ya upatikanaji wa maji ili kuwa chini ya asilimia 34 ambapo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja hali ya upatikanaji wa maji umefikia asilimia zaidi ya asilimia 50.

Aidha alisema Wilaya hiyo imefanikiwa kupata zaidi ya Bil 10 ambapo bil 1 inatokana na fedha zitokanazo na uvico ambzo kwa ajili ya Handeni Mjini na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa ajili ya kuondoa tatizo la maji ambalo lilikuwa linaikumba Wilaya hiyo.

Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Handeni Hosea Joseph alimuhakikishia Naibu Waziri wa Maji kuwa amepokea agizo la kumsimamia Mkandarasi Mponela Construction and co,ltd anaetekeleza ujenzi wa mradi wa maji Kijijini hapo  kuwa utamalizika kwa wakati kama agizo lilivyotolewa.

Hata hivyo alisema mbali ya agizo hilo la siku saba alisisitiza kutokana na umuhimu wa huduma hiyo ya maji atahakikisha ndani ya siku tatu wananchi wa kijiji hicho watakuwa wanapata huduma hiyo ya maji ili kuondoa kero iliyopo ndani ya makazi hayo ya wananchi waliohamia katika eneo hilo.

Wednesday, August 17, 2022

TAKUKURU PWANI YAFANYA UCHUNGUZI WA KINA MIRADI 32 YA MAENDELEO.

 

VICTOR MASANGU, PWANI 

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  Mkoa wa Pwani imefanya uchunguzi na  kukagua  miradi 32 ya maendeleo yenye thamani ya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni Saba na kubaini miradi  nane kuwa na kasoro na mapungufu mbali mbali ambazo zimesababishwa na kamati kutowajibika ipasavyo.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Christopher Myava wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa majukumu katika robo ya tatu  ambapo  amesema kuwa baadhi ya miradi umechelewa kutokana na uzembe wa wahusika kutofanya kazi kwa kuchelew.


Aidha Mkuu huyo alibainisha kuwa katika miradi mingine Kuna tabia ya baadhi ya mafundi kujichukulia vifaa vya ujenzi bila ya kukabidhiwana wanakamati hali ambayo inapelekea upotevu wa vifaa vya ujenzi hivyo kuathiri suala zima la ubora wautekelezaji wa miradi hiyo.

"Katika uchunguzi wetu ambao tumefanya Takukuru tumeweza kubaini miradi nani ya maendeleo kuwepo kwa mapungufu na kasoro mbali mbali ambapo kwa sasa tunaendelea na uchunguzi zaidi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wale wote ambao watabainika kuhusika na vitendo vya rushwa.

Pia alisema kuwa katika kukabiliana na winbi la mianya ya rushwa wataendelea kuweka mipango madhubuti kwa kuendelea kutoa elimu kwa umma na kufanya uchunguzi wa Mara kwa Mara katika sekta mbali mbali lengo ikiwa ni kudhibiti vitendo vya rushwa.

,
"Ili kuweza kudhibiti mianya ya rushwa katika idara za serikali pamoja na sekta binafsi jumla ya chambuzi za mifumo ipatayo Saba zimefanyika kwenye sekta za elimu.huduma za jamii,madini.mapato,kilimo ,ardhi pamoja na maji,"alisema Christopher.

Alifafanua zaidi aliongeza kuwa pia wamegundua kuwepo kwa ukwepaji wa kulipa ushuru katika eneo la madini ya ujenzi ambapo wamebaini kwamba maeneo mengi ya uchimbaji wa madini hasa ya mchanga hakuna udhibiti wa kutosha.



Aidha Mkuu huyo wa Takukuru amesema kuwa pia wamebaini kuwepo kwa maduka ya dawa muhimu kuendesha shughuli zao kinyemela  bila ya kuwa na leseni kitu ambacho ni kinyume kabisa na Sheria na taratibu za nchi.



Pia katika hatua nyingine ametoa onyo Kali kwa baadhi ya watu ambao ni wabadhilifu katika mali za umma na kuwahimiza wananchi wa Mkoa wa Pwani kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

POLISI WAPATA KANDA YA CCTV INAYOONYESHA HATUA ZA MWISHO ZA AFISA WA IEBC ALIYETOWEKA EMBAKASI.

Polisi wamepata kanda ya CCTV ambayo inaonyesha hatua za mwisho za Afisa Msimamizi wa Uchaguzi wa Embakasi Mashariki Daniel Musyoka, kabla ya kutoweka Alhamisi, Agosti 11. 

Zaidi ya saa 48 baada ya Musyoka kuripotiwa kutoweka katika kituo cha kuhesabia kura cha East African School of Aviation (EASA) jijini Nairobi bado hajulikani mahali aliko.

Picha za CCTV kutoka jengo la karibu na kituo hicho zinaonyesha Musyoka, mwenye umri wa miaka 53, akitoka nje siku ambayo aliripotiwa kupotea.

Kulingana na afisa anayefuatilia uchunguzi huo, Musyoka alionekana ametulia alipokuwa akielekea kwenye kituo cha basi kilichokuwa karibu. 

"Tumegundua kuwa yeye (Musyoka) hakupiga au kupokea simu wakati alipotoka nje. Uhakiki wetu wa CCTV hauonyeshi mtu yeyote au gari ambalo lingeweza kumfuata mtu huyo," afisa huyo aliambia gazeti la The Standard. 

Ripoti za awali zilidai kuwa afisa huyo wa IEBC alijinafasi ili kupokea simu kabla ya kutoweka kwa njia isiyoeleweka. 

Uchunguzi zaidi katika akaunti za pesa za simu za Musyoka haukuonyesha jambo lolote la kutiliwa shaka. Kaka yake afisa huyo wa IEBC, Shadrack Musyoka aliambia The Standard kwamba walikuwa wametembelea takriban hospitali zote jijini Nairobi lakini bado hawajampata jamaa wao. 

Msako huo pia uliendeshwa hadi kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti karibu na jiji la Nairobi lakini haukuzaa matunda. 

Binti yake Musyoka, Prudence Mbolu, alisema mara ya mwisho kuzungumza na baba yake ilikuwa Jumanne, Agosti 9, asubuhi ambayo ilikuwa siku ya uchaguzi.

Lakini mazungumzo kati yaoyalikuwa mafupi kwani Musyoka alikuwa akiratibu uchaguzi. 

Mke wake naye alieleza kuwa kuwa mumewe ambaye amekuwa akifanya kazi na tume ya uchaguzi tangu 2009, aliondoka nyumbani kwao Nakuru kuelekea Nairobi mnamo Julai 10 baada ya kuhudhuria ibada katika kanisa la AIC Lanet Umoja.

 “Nilimpigia simu mnamo Agosti 11 mwendo wa saa nane asubuhi lakini hakupokea simu. Binamu yake ambaye pia anaishi Nairobi alinipigia simu alasiri akiniuliza ikiwa nimezungumza naye. Afisa wa IEBC ambaye alikuwa rafiki yao walimfikia kwa swali sawa,” alisema Tabitha. 

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alisema kuwa tume hiyo ina hofu kubwa kuhusu tukio hilo la kusikitisha. 

Tume hiyo imetoa ripoti katika kituo cha Polisi cha Embakasi kuhusu afisa huyo aliyepotea kwenye daftari la matukio nambari 24/11/8/2022.

Cheukati alisema Musyoka aliondoka nyumbani kwake saa 9.00 alfajiri na kusindikizwa na mlinzi wake hadi ofisini katika kituo cha kujumlisha kura cha East African School of Aviation (EASA) ambako ni mahala pa kuhesabia kura na kujumlisha matokeo ya uchaguzi. 

“Afisa huyo aliomba kutoka nje ya chumba cha kuhesabia kura saa 9.45 asubuhi lakini hakurejea afisini,” alisema Chebukati. 

TAARIFA ZA KUPATIKANA KWAKE.

Vyombo vya habari vya Stechitegist vimekusanya kuwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Embakasi Mashariki aliyetoweka, Daniel Musyoka, alipatikana amekufa kwenye kichaka huko Mariko, Oloitoktok, Kajiado.

 

Kifo cha Musyoka kilitangazwa alfajiri ya Jumanne na mwanablogu maarufu wa Kenya, Robert Alai.

 

Familia ilithibitisha kuwa Musyoka alipatikana amefariki katika bustani ya Amboseli, kaunti ya Kajiado.

 

Maafisa wa polisi kutoka Loitoktok, kaunti ndogo ya Kajiado Kusini walithibitisha kupokea arifa baada ya mwili wa mwanamume wa makamo kupatikana msituni.

Mwili ulitambuliwa vyema na dada zake; Mary Mwikali na Ann Mboya katika hifadhi ya maiti ya kaunti ndogo ya Loitokitok.

 

Afisa wa polisi wa Loitoktok Kipruto Ruto alithibitisha kuwa familia hiyo iliweza kumtambua Musyoka na kumaliza msako wa siku 5 wa kumtafuta afisa wa uchaguzi Embakasi Mashariki aliyetoweka.

 

Polisi wanaamini Musyoka aliuawa kwingine na mwili wake kutupwa msituni. Kulingana na maafisa hao, mwili wake ulikuwa na dalili zinazoonekana za mateso na mapambano lakini wanasubiri uchunguzi wa maiti.

Uvumi ambao umekuwa ukienea na kuenea virusi una hivyo

 

“Daniel Musyoka, Msimamizi wa Uchaguzi wa IEBC aliyetoweka amepatikana amefariki mahali fulani Loitoktok.

 

"Matokeo ya Embakasi Mashariki yanapaswa kuchunguzwa na kubainishwa ikiwa mbunge aliyechaguliwa alishinda bila matokeo au kwa vitisho."

 

“Ni dhahiri kuwa mwathiriwa aliuawa kwingine na mwili kutupwa bondeni. Mwili una makovu yanayoashiria kuteswa kabla ya kifo. Huenda alikufa kifo cha uchungu,” Bw Ruto alisema.

 

Mwili huo ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Loitokitok ukisubiri kutambuliwa baada ya maafisa wa polisi kukusanya alama za vidole.

 

"Tunawasiliana na familia ambazo zimepoteza wapendwa wao ili kuja kutambulishwa tunaposubiri kushughulikiwa kwa alama za vidole," alisema mkuu wa polisi ambaye aliongeza kuwa hawawezi kubashiri juu ya utambulisho wa marehemu.

RAILA ODINGA AKATAA MATOKEO YA URAIS, KUELEKEA MAHAKAMANI.


Kinara wa Azimio Raila Odinga amekataa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotolewa na mweyekiti wa tume ya uchaguiz nchini IEBC. 

Raila alisema uamuzi mzito kama vile kutangazwa kwa kura ni jambo la makamishna wote kuketi na kukubaliana kuhusu litakalotangazwa. 

Alizungumzia kesi ya hapo awali ambayo iliwahi kutolewa na mahakama ya Juu kuhusu uamuzi wa IEBC. "Uamuzi wa suala lolote ni lazima liwe la maafisa wote kukubaliana au kwa wingi wa idadi baada ya makamishna kupiga kura," alisema Raila. 

Mgombea huyo wa Azimio alisema kutokana na kuwa matokeo ya urais jana yalitolewa na makamishna watatu baada ya wanne kujiondoa, basi hakuna linaloweza kukubalika. "Hatukubali matokeo yaliyotolewa hapo jana. 

Na kwa hivyo, tunajua hakuna mshindi aliyetangazwa akiwa amechaguliwa kihalali au Rais Mteule," Raila alisema.

Kiongozi huyo wa Azimio alimkashifu Wafula Chebukati akisema aliendesha shughuli za IEBC kwa njia ya kifua bila kuwahusisha makamishana wengine. "Kama si wafuasi wetu kujizuia kuzua fujo, taifa kwa sasa lingekuwa katika hali baya kama ilivyokuwa 2007. 

Hatutakubali mtu mmoja ajaribu kubadilisha yale Wakenya wameamua," alisema Raila huku akiitaka mahakama kubadili kilichotanagzwa na Chebukati. 

Kero la kiongozi huyo ni kutokana na mpinzani wake William Ruto kutanagazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne Agosti 9. 

Ruto alitangazwa mshindi na asilimia 50. 49 ya kura ambazo zilipigwa na hivyo kufikisha vigezo vya kikatiba vinavyohitajika. 

Hata hivyo, makamishna wanne walimhepa Chebukati wakisema wao hawawezi kusema wanajua lolote kuhusu matokeo hayo. 

Katika kikao na wanahabari Jumanne Agosti 16, naibu mwenyekiti wa IEBC Juliana Cherare, mmoja wa makamishna hao wanne, alisema matokeo ya urais ni ya Chebukati na wala si ya tume ya IEBC. 

Tuesday, August 16, 2022

HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO YAPOKEA MSAADA WA MAABARA YA KISASA KUTOKA SERIKALI YA UJERUMANI KUPITIA GIZ

 

Na Oscar Assenga,TANGA.

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo imepokea msaada wa maabara ya kisasa ya kufanyia uchunguzi wa ugonjwa wa Uviko 19 yenye thamani ya Milioni 225 kutoka kwa Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika lake la Maendeleo ya GIZ

Akizungumza mara baada ya kuifungua mara baada ya ukaguzi wa maabara hiyo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisema kwamna maabara hiyo ina uwezo wa kutoa majibu ndani ya masaa nane hivyo kuwa mwarobaini wa changamoto zilizokuwepo awali.


Alisema kuwa pia kupitia uwepo wa maabara hiyo utasaidia hata wananchi kutoka nchi jirani ya Kenya ambao wataingia nchini kufanyiwa vipimo kwa haraka na majibu kupatikana kwa wakati.

Alisema uwepo wa maabara hiyo itaondoa changamoto iliyokuwepo ya kusafirtisha sampuli kwenda kwenye maabara nyengine ambapo ilikuwa inasababisha ucheleweshwaji wa majibu na wakati mwengine vipimo vilikuwa vinachelewa.

"Kwa niaba ya serikali tunawashukuru wenzetu wa Ujerumani kwa kutusaidia katika sekta ya Afya kama mnavyofahamu hospitali hii ilijengwa na wajerumani miaka 100 iliyopita lakini bado wanaendelea kutoa fedha nyingi katika kusaidia sekta ya afya nchini ikiwemo hospital yetu ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo wanatupatia fedha kwaajili ya kuimarisha afya ya uzazi ,mama na mtoto pamoja na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona "Alisema

Alisema kuzinduliwa kwa kituo hicho cha kupima sampuli za Corona kitasaidia na kuokoa muda kwani awali ilikuwa inawalazimu sampuli zinazochukuliwa hospital Bombo kwenda kupimwa Dar es salaam kwenye maabara ya Taifa na baada ya masaa 48 ndio majibu kupatikana ambapo sasa majibu yatakuwa yanapatikana ndani ya masaa 8 na kuwarahisishia wanaosafiri kwenda nje ya nchi kupata majibu kwa haraka zaidi.

Waziri Ummy alisema pia fedha walizitoa zitatumika kwaajili ya kuimarisha mapambano dhidi ya Uviko -19 na ndio maana katika hospitali ya rufaa ya mkoa Bombo wamefungua kituo cha kupima sampuli za Corona kwa kutumia kipimo hicho.

Awali akizungumza Waziri wa Ushirikiana wa Uchumi na Maendeleo kutok Serikali ya Ujerumani Dkt Barbel Kofler alisema kuwa wakazi wa Tanga pamoja na wageni kutoka nje sasa wataweza kutumia maabara hiyo kwa ajili ya vipimo vya UVIKO.

Alisema wanajisikia furaha kuona kituo hiki cha kupimia sampuli za Covid 19 kinaanza kufanya kazi kwaajili kuimarisha afya ya jamii ya watu wa Tanga na ni muhimu sana kwa serikali ya ujerumani kuendelea kusaidia sekta ya afya katika mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Alieleza kwa sababu wote hatuko salama muda wowote hivyo wanapaswa kushirikiana kusaidia katika kuimarisha afya ya jamii kwa ujumla kwa Tanzania na ulimwengu mzima pia

Dkt. Kofler alisema mbali na fedha hizo wamesaidia kuwajengea uwezo wataalamu wa afya katika kutoa huduma bora huku wakingia Dolla za kimarekani 15.3 kwaajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto na wasichana ili kupambana, kupunguza au kutokomeza kabisa vifo vitokanavyo na uzazi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa maabara kuu ya Taifa ya Afya ya Jamii  Medard Beyanga alisema kuwa  Serikali inaendelea kuziimarisha maabara zote hapa nchini kwaajili ya kupelekea huduma karibu na  wananchi  ambapo baadhi ya vituo hapa nchini vimeanza kufunguliwa  ikiwemo kilichopo katika  hospital ya rufaa mkoa wa Tanga  Bombo.

Alisema kwamba hivi sasa wanaendelea na mpango wao wa kuziimarisha maabara  za upimaji wa Uviko - 19 na Serikali inafanya jitihada za  kuongeza upimaji  ili kupeleka huduma karibu na wananchi kuliko kusubiri majibu kutoka Dar es salaam kwenda maabara kuu ya Taifa ,na hii maabara haitakuwa ya kupima Corona bali itapima na magonjwa mengine.

Aidha alieleza pia Serikali ya Ujerumani pia imeendelea kuwa na mchango mkubwa hapa nchini kupitia sekta ya afya ambapo inasaidia kulipia bima ya afya na mtoto inayotambulika kama 'Tumaini la mama', kuchangia mapambano dhidi ya kifua kikuu pamoja na malaria.

“Serikali ya Ujerumani imedhamini miradi ya afya ya Nchini Tanzania kwa gharama ya shilingi dola za kimarekani za zaidi ya shilingi bilioni 7 ikihusisha miradi ya mama na mtoto na Uviko 19”Alisema.

RAIS SAMIA ATOA SALAMU ZA PONGEZI KWA RAIS MTEULE WILLIAM RUTO KWA USHINDI.


 Rais wa Tanzania Samia Suluhu amempongeza Rais mteule William Ruto kwa ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu wa 2022. 

Rais Samia Suluhu Ampongeza William Ruto Baada ya Kutangazwa kuwa Rais Mteule. Picha: Samia Suluhu. Chanzo: Twitter Katika taarifa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii siku ya Jumanne, Agosti 16, Suluhu alimpongeza Ruto kwa ushindi wake na kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwa rais mteule. 

Suluhu pia aliwasifu Wakenya kwa kudumisha amani wakati wa mchakat mzima wa uchaguzi na kuahidi kuendelea kufanya kazi na Kenya. "Ninapenda kuwapongeza kwa dhati wananchi wa Kenya kwa kushiriki uchaguzi wao mkuu kwa amani na utulivu, ambapo matokeo yake ni Dkt William Ruto kutangazwa kuwa Rais mteule wa Kenya.

Tanzania itaendeleza undugu na ushirikiano wa Kihistoria na Kenya uliodumu miaka na mikaka," alisema. 

Suluhu pia aliahidi kuendelea kufanya kazi na Kenya ili kueneza uhusiano wao kidiplomasia. Rais huyo alibainisha kuwa Kenya na Tanzania zina uhusiano wa kihistoria kama majirani, akiongeza kuwa mataifa hayo mawili yameungana. 

Ruto apokea kongole kote duniani Baada ya kutangazwa rais mteule, William Ruto amekuwa akipokea jumbe za kongole kutoka kwa viongozi tofauti ulimwenguni. 

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alisema anaamini kuwa Ruto atahudumia Wakenya bila upendeleo. 

Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamed alisema anatazamia kufanya kazi na Ruto katika kuendeleza maslahi ya pande zote mbili za Nairobi na Mogadishu.

 Ubalozi wa Marekani ulitaja kuchaguliwa kwa Ruto kuwa rais wa tano kama hatua muhimu huku ukizitaka pande ambazo hazijaridhika na matokeo kupinga matokeo hayo kupitia mifumo iliyopo ya kutatua mizozo. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alimtakia kila la heri Ruto akiahidi kufanya kazi naye kwa karibu ili kuboresha uhusiano baina ya nchi hizo mbili. 

PIA SOMA Magazetini Agosti 16: William Ruto Alizungumza na Raila Kabla ya Kutangazwa Rais Mteule Katika salamu zake za pongezi, rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema anatazamia uhusiano thabiti kati ya Nigeria na Kenya. 

MEDALA HIGH SCHOOL YAUNGA MKONO ROYAL TOUR KUCHANGIA WAANDISHI IRINGA KUTEMBELEA HIFADHI YA RUAHA

Mkurugenzi wa Medala High school Emmanuel Mfikwa akiongea na waandishi wa habari ambao walikuwa wamefika shuleni hapo wakati wakiendelea na ziara ya Iringa Journalist's Ruaha The Royal Tour na kuongea na mkurugenzi huyo aliyeunga mkono ziara hiyo ya kutangaza na kutembelea hifadhi ya Ruaha.Mkurugenzi wa Medala High school Emmanuel Mfikwa akiongea na waandishi wa habari ambao walikuwa wamefika shuleni hapo wakati wakiendelea na ziara ya Iringa Journalist's Ruaha The Royal Tour na kuongea na mkurugenzi huyo aliyeunga mkono ziara hiyo ya kutangaza na kutembelea hifadhi ya Ruaha.Baadhi ya wanafunzi wa Medala High School wakiwa kwenye picha ya Pamoja Mbele ya Jengo la Utawala la shule hiyoMuonekano wa juu wa Majengo ya Medala High School

Na Fredy Mgunda, Iringa.


Uongozi wa  Medala High school iliyopo mkoani Iringa imeunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutangaza utalii wa kutembea hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa walipotembelea shule ya Medala iliyopo tarafa ya Idodi wakati wakiwa kwenye ziara ya Iringa Journalist's Ruaha The Royal Tour, mkurugenzi wa Medala High school Emmanuel Mfikwa alisema kuwa ameamua kuunga mkono juhudi za waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa kwa kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Mfikwa alisema kuwa anatambua mchango wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo inapambana kuvitangaza vivutio vilivyopo nchini kwa njia mbalimbali ikiwemo filamu ya Royal Tour ambayo imeigizwa na Rais Samia Suluhu Hassan hivyo kitendo cha waandishi wa habari Iringa kutembelea hifadhi hiyo kunaongeza chachu ya kukuza utalii wa ndani.

aliongeza kuwa uongozi wa Medala High School kwa ushirikiano na mkurugenzi walitoa katoni kadhaa za maji ya kunywa na kiasi cha fedha kwa ajili ya waandishi wa habari kujikimu wakati wanafanya utalii na kuanda habari za kuitangaza hifadhi ya taifa ya Ruaha.                                                                                                                                                         

Alisema kuwa Medala High school iliyopo kata ya Idodi wilaya ya Iringa imekuwa na utaratibu wa kuwapeleka wanafunzi wa shule hiyo mara kwa mara kwenda kutalii katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha na wamepanga kuwapeleka wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika hifadhi hiyo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii.

Mfikwa alisema kuwa wanafunzi wa Medala High school wamekuwa wanafundishwa kwa ubora ambao unatakiwa na kuwafundisha uzalendo wa kutembelea hifadhi na vivutio vilivyopo nchini kwa kuwajengea uwezo wa kupenda kwenda kutalii.

Aidha mkurugenzi wa Medala High school Mfikwa alisema kuwa malengo ya shule hiyo ni kutoa elimu ilivyo bora kwa wanafunzi ambao watakuwa wanasoma hapo kwa kuajili walimu na wafanyakazi wenye taaluma inavyotakiwa kila idara ili kuhakikisha Wanafunzi akitoka hapo anakuwa bora kila eneo.


Alisema kuwa wanampango wa kuajili walimu wenye ubora kutoka pande zote za Africa Mashariki ili mradi awe amefikia ubora wa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa shule hiyo kama ambavyo walimu waliopo wanavyofanya hivi Sasa.

"Waandishi wa habari angalieni hili shule inamazingira yaliyo bora na tulivu kumpa kumuwezesha mwanafunzi kusoma akiwa huru kwa kuwa mahitaji yote muhimu yanapatika hapo shuleni kwa wakati hivyo si dhani kama Kuna mzazi atakataa mtoto wake asisome katika shule yangu ya Medala High school"alisema Mfikwa

Mfikwa alisema kuwa Medala High school inapokea wanafunzi wa bweni kutoka na mazingira shule iliyopo na lengo ni kuhakikisha wanatoa elimu iliyo bora na kufanya mapinduzi ya kitaaluma kwa shule zilizopo mkoa wa Iringa na nje ya Iringa kwa namna ambavyo amekuwa na walimu bora na nguli wa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

Mkurugenzi wa Medala High school alimazia kwa kusema kuwa wamekuwa wakiwasomesha bure baadhi ya wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha nne na darasa la saba wanaotoka katika kata ya Idodi na tarafa ya Idodi kwa ujumla huku lengo kubwa likiwa ni kukuza elimu ya wananchi wa eneo hilo ambao asili yao kubwa ni wafugaji.

Medala High school inapatikana mkoani Iringa wilaya ya Iringa kata ya Idodi karibu na hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo unaweza kuwapigia kwa namba hizi hapa 
0736313180, 
0715817236, 
0678122682, 
0713961069 na 
0758313180 muda wote wanapatikana.

Kwa upande wao baadhi ya waandishi wa habari Iringa walimpongeza mkurugenzi wa Medala High school kwa uwekezaji ambao unatija kwa maendeleo ya elimu kwa wananchi wa Tanzania kutokana mazingira yalivyojengwa kwa ubora unatakiwa.


Walisema kuwa wamevutiwa na mazingira ya Medala High school na watakuwa mabalozi wa shule hiyo ya bweni ambayo inamajengo yanayotakiwa na kuliziwa na mzazi yoyote yule kumpeleka mtoto wake akasome katika shule hiyo.


Waandishi wa habari walimalizia kwa kumshukuru mkurugenzi wa Medala High school na wafanyakazi wote kwa mchango wao kufanikisha ziara ya Iringa Journalist's Ruaha The Royal Tour ambayo ilikuwa na lengo la kwenda kutalii na kuendelea kuitangaza hifadhi ya Taifa ya Ruaha.