Kinara wa Azimio Raila Odinga amekataa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotolewa na mweyekiti wa tume ya uchaguiz nchini IEBC.
Raila alisema uamuzi mzito kama vile kutangazwa kwa kura ni jambo la makamishna wote kuketi na kukubaliana kuhusu litakalotangazwa.
Alizungumzia kesi ya hapo awali ambayo iliwahi kutolewa na mahakama ya Juu kuhusu uamuzi wa IEBC. "Uamuzi wa suala lolote ni lazima liwe la maafisa wote kukubaliana au kwa wingi wa idadi baada ya makamishna kupiga kura," alisema Raila.
Mgombea huyo wa Azimio alisema kutokana na kuwa matokeo ya urais jana yalitolewa na makamishna watatu baada ya wanne kujiondoa, basi hakuna linaloweza kukubalika. "Hatukubali matokeo yaliyotolewa hapo jana.
Na kwa hivyo, tunajua hakuna mshindi aliyetangazwa akiwa amechaguliwa kihalali au Rais Mteule," Raila alisema.
Kiongozi huyo wa Azimio alimkashifu Wafula Chebukati akisema aliendesha shughuli za IEBC kwa njia ya kifua bila kuwahusisha makamishana wengine. "Kama si wafuasi wetu kujizuia kuzua fujo, taifa kwa sasa lingekuwa katika hali baya kama ilivyokuwa 2007.
Hatutakubali mtu mmoja ajaribu kubadilisha yale Wakenya wameamua," alisema Raila huku akiitaka mahakama kubadili kilichotanagzwa na Chebukati.
Kero la kiongozi huyo ni kutokana na mpinzani wake William Ruto kutanagazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne Agosti 9.
Ruto alitangazwa mshindi na asilimia 50. 49 ya kura ambazo zilipigwa na hivyo kufikisha vigezo vya kikatiba vinavyohitajika.
Hata hivyo, makamishna wanne walimhepa Chebukati wakisema wao hawawezi kusema wanajua lolote kuhusu matokeo hayo.
Katika kikao na wanahabari Jumanne Agosti 16, naibu mwenyekiti wa IEBC Juliana Cherare, mmoja wa makamishna hao wanne, alisema matokeo ya urais ni ya Chebukati na wala si ya tume ya IEBC.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.