Saturday, August 07, 2010
HABARI
MH. MKUU WA MKOA WA MWANZA ABBAS KANDORO AKIKAGUA JUKWAA LA SILAHA HIZO HARAMU TAYARI KWA KUTEKETEZWA.
MKUU WA MKOA KTK HOTUBA YAKE:-
KUTOKANA NA MATUKIO YANAYOTOKEA MARA KWA MARA KWA WAMILIKI WA SILAHA KUNYANG'ANYWA AU KUSHINDWA KUTUMIA SILAHA WANAPOKABILIANA NA WAHALIFU, BAADHI YA WANANCHI WANAOMILIKI SILAHA NA WAOMBAJI WAPYA WANAHITAJI MAFUNZO MAALUM YA NAMNA YA KUTUMIA SILAHA WANAZOOMBA AU WANAZOZIMILIKI.
MWAKILISHI KUTOKA RECSA BW.FRANCIS AKIHUTUBIA.
AMBAPO SHIRIKA LAKE LIMEONGEZA MASHINE NYINGINE YA KUWEKA ALAMA KATIKA SILAHA ZINAZOMILIKIWA KIHALALI, SAMBAMBA NA UWEKAJI KUMBUKUMBU ZA SILAHA HIZO KATIKA KOMPYUTA.
KAMANDA SIRO KATIKA HOTUBA YAKE:-
ENEO LA KANDA YA ZIWA NI MOJA WAPO YA MAENEO YANAYOKUMBWA NA WIMBI LA UINGIAJI WA SILAHA HARAMU, HILI LIMETOKANA NA WIMBI LA WAKIMBIZI NA NYINGINE HUINGIA KUPITIA MIPAKA YETU NA NCHI JIRANI. KANDA YA ZIWA IMESHUHUDIA VITENDO VYA MATUMIZI MABAYA YA SILAHA HARAMU KUTUMIKA KATIKA MAPIGANO YA KOO, UTEKAJI WA MAGARI, UPORAJI WA FEDHA, MAPIGANO MIGODINI, UPORAJI WAVUVI NA MAUAJI YA ALBINO MATUKIO YALIYOSABABISHA WATU KUPOTEZA MAISHA HUKU WENGINE WAKIBAKI NA ULEMAVU WA KUDUMU.
WAKIELEKEA JUKWAA LA UCHOMAJI SILAHA HARAMU.
MIKOA INAYOONGOZA KWA MATUKIO YA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA KATIKA KANDA YA ZIWA NI MARA MATUKIO 442, TABORA MATUKIO 199, MWANZA MATUKIO 112, SHINYANGA MATUKIO 78 NA TARIME RORYA MATUKIO 76. TAKWIMU KWA KIPINDI CHA MWAKA 2008 HADI JUNI 2010.
MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA MWANZA ABBAS HUSSEIN KANDORO AKIONGOZA ZOEZI LA KULIKAGUA JUKWAA LA SILAHA ZA KUTEKETEZWA.
ZOEZI LA UCHOMAJI.
WADAU WOTE KAMA ASASI ZA KIRAIA, VYOMBO VYA HABARI NA MADHEHEBU YA DINI SOTE TUNAO WAJIBU WA KUPAMBANA KIKAMILIFU KATIKA KUDUMISHA AMANI KWA KUFICHUA VITENDO VYA MATUMIZI MABAYA YA SILAHA.
MOTO ZAIDI.
JESHI LA POLISI TAYARI LIMEANZA KUBORESHA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA SILAHA ZINAZO MILIKIWA NA WATU BINAFSI, TAASISI ZA KISERIKALI PAMOJA NA MAKAMPUNI MBALIMBALI ZA ULINZI AMBAPO HADI SASA SILAHA ZAIDI YA 65,00 ZIMEHAKIKIWA UPYA NCHI NZIMA, KATI YA SILAHA HIZO 67,000 NA ZOEZI LINAENDELEA.
MTANGAZAJI WA SHIRIKA LA HABARI NCHINI TBC ONE RICHARD LEO AKIANGUSHA NONDO ZAKE TUKIONI.
SEHEMU TU YA UMMA WA WAKAZI WA JIJI LA MIAMBA WALIOHUDHURIA TUKIO HILO.
ILI KUPAMBANA NA UHALIFU HUU WA KUTUMIA SILAHA NCHI ZOTE DUNIANI HATUNA BUDI KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA KWA KUWA NCHI MOJA HAIWEZI PEKEE KUPAMBANA NA UHALIFU. NJIA NZURI NIA KUFANYA MISAKO NA OPERESHENI ZA MARA KWA MARA NA KUENDELEZA MFUMO WA UBADILISHAJI TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU PAMOJA NA TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA.
SHUKURANI ZINATOLEWA NA JESHI LA POLISI KWA WAANDAAJI WALIOFANIKISHA ZOEZI HILI MKOANI MWANZA CHINI YA URATIBU WA REGINAL CENTRE ON SMALL ARMS (RECSA) YANYE MAKAO YAKE NAIROBI KENYA. WAFADHILI SERIKALI YA JAPAN AMBAO WAMETOA MSAADA WA FEDHA ZA KUFANIKISHA ZOEZI HILI MUHIMU KWA KUIMARISHA AMANI KATIKA NCHI ZETU ZA AFRIKA MASHARIKI NA NCHI ZA MAZIWA MAKUU NA PEMBE YA AFRIKA.
Saturday, August 07, 2010
HABARI
SILAHA MBALIMBALI ZILIZOKAMATWA KANDA YA ZIWA ZIKITUMIKA KATIKA MATUKIO MBALIMBALI YA UHALIFU NCHINI NA SILAHA ZILE ZILIZO SALIMISHWA, LEO ZITATEKETEZWA JIJINI HAPA.
KWA KARIBU ZAIDI.
TUKIO HILO LINATARAJI KUFANYIKA ASUBUHI HII MAJIRA YA SAA 5 KAMILI UWANJA WA NYAMAGANA JIJINI MWANZA. TAYARI SILAHA HIZO ZIMEPANGWA KATIKA MPANGILIO THABITI KWA AJILI YA KUTEKETEZWA NA MOTO (KAMA PICHA INAVYOONEKANA).
NYOTE MNAKARIBISHWA KUWA MASHUHUDA.
Friday, August 06, 2010
FIESTA
MENEJA MKUU WA UHUSIANO, MAWASILIANO NA JAMII WA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI, TEDDY MAPUNDA AKISHIRIKIANA NA MSANII KUTOKA IVORY COAST AMBAYE ANATAMBA SANA NA WIMBO WAKE WA ALADJI, JEFF DOGOLOBANGO KUPAKA RANGI WODI YA WANAUME.
MPISHI MKUU WA KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI, RALF SCHUSTER AKIPAKA RANGI KUTA ZA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY, KINONDONI JIJINI DAR LEO MCHANA.
MGANGA MKUU HOSPITALI YA MWANANYAMALA, BI ZUHURA MAJAPA AKIPOKEA VIFAA VYA USAFI NA NDOO ZA RANGI KUTOKA KWA MENEJA MKUU WA UHUSIANO NA MAWASILIANO YA JAMII KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI, TEDDY MAPUNDA LEO MCHANA.
MSANII KUTOKA IVORY COAST AMBAYE ANATAMBA SANA NA WIMBO WAKE WA ALADJI- ALADJI, JEFF DOGOLOBANGO AKIWA AMEAMBATANA NA MKALIMALI WAKE PAMOJA NA DENSA WAKE WAWILI ALIPOWASILI NDANI YA HOSPITALI YA MWANANYAMALA KWA AJILI YA KUSHIRIKI ZOEZI LA KUFANYA USAFI NA KUPAKA RANGI LEO MCHANA.
MENEJA MKUU WA UHUSIANO NA MAWASILIANO YA JAMII KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI, TEDDY MAPUNDA AKIPEANA MKONO WA SHUKURANI NA MKUU WA POLISI KINONDONI, ELIAS KALINGA, KULIA NI MMOJA WA WAKURUGENZI WAKUU WA CLOUDS ENTERTAINMENT NA MRATIBU MKUU WA TAMASHA LA FIESTA JIPANGUSE 2010, RUGE MUTAHABA.
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA MICHUZI JR.
www.michuzijr.blogspot.com
NUNUA SASA UFAIDI YALIYOMO.
Friday, August 06, 2010
HABARI
ZIWA VICTORIA NA BANDARI YA JIJI LA MWANZA.
Wanafunzi 18 wanahofiwa kuangamia katika ajali ya mtumbi katika ziwa Victoria mjini Mwanza nchini Tanzania.
Ajali hiyo ni ya tatu katika eneo hilo katika muda wa mwezi mmoja.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, boti hiyo ilikuwa imebeba abiria kupitia kisasi.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema, David Palangyo amesema boti hiyo ilizama kutokana na hali mbaya ya anga.
Palangyo ameongezea kuwa boti hilo lilikuwa limebeba wanafunzi 37 waliokuwa na umri wa kati ya miaka 5 na 14.
20 kati yao waliokolewa na maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wavuvi katika ziwa hilo.
Duru zinasema mtumbwi huo ulikuwa ukielekea kisiwa cha Itendelea kutoka Lukungu.
Kamanda Siro wa jeshi la polisi mkoani Mwanza amesema uchunguzi umeanzishwa ili kubainisha chanzo cha ajali hiyo, lakini amekiri kuwa naodha wa mtumbwi huo amekamatwa na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.
Siku ya jumapili wiki iliyopita mashua iliyokuwa na shehena na samaki na abiria ilizama katika eneo la ziwa hilo, inayomilikiwa na Uganda.
Watu 33 waliangamia kwenye ajali hiyo.
Thursday, August 05, 2010
BANGO
KUBALI KATAA!
HAPA....
GADNA G. HABASH 'KAPITEIIIN' (RUKSA ITAMKE HIVYO HIVYO).
EPHRAIM KIBONDE JAHAZINI.
SI KUINOGESHA TU JIONI YAKO UKAJISIKIA RAHA UKACHEKA BASI KWISHNI', LA HASHA!... JAHAZI NI KIPINDI CHENYE STORI ZA UKWELI UKWELI (nyingine utani kimtindo) ZENYE MWAMKO WA KIRAFIKI ZAIDI KATIKA USIMULIAJI, UTAKAO KUFANYA UBADILIKE NA KUTEMBEA KATIKA MWELEKEO CHANYA.
HEBU CHUNGUZA KWA YOTE WANAYO JADILI, CHUNGUZA KWA YOTE WANAYO KEMEA, CHUNGUZA KWA YOTE WANAYO SIHI YAPATE KUFANYIKA NDANI NA NJE YA JAMII YAKO.
MWISHO WA SIKU UTAUNGANA NA WENGI WENYE KAULI HII:- "TUNUKU WALIYOPEWA VIJANA HAWA NA MOLA YAANI UPEO, UJASIRI, HEKIMA, UJUZI NA MAARIFA, YOTE HAYO KWA PAMOJA YAMELETA MAPUNDUZI YA KIMAENDELEO SI KWA MTU MMOJA MMOJA TU BALI HATA KWA JAMII NA TAIFA LA TANZANIA KWA UJUMLA".
SIKILIZA JAHAZI NDANI YA CLOUDS FM SAA 16:00 HADI 19:00.
HAKIKA HUTO BANDUKA!!!!!
KANBAAAAA!
LIDUMU JAHAZI.
WENU albert g.sengo
Thursday, August 05, 2010
HABARI
Matokeo ya mapema ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya nchini Kenya yanaonyesha kuwa katiba hiyo imeungwa mkono kwa wingi wa kura.
Baadhi ya mapendekezo kwenye katiba hiyo ni kupunguza mamlaka ya rais, kulinda haki za kibinadam za wakenya pamoja na kubuni sera mpya ya umiliki wa ardhi.
Hata hivyo katika maeneo ya mkoa wa Rift Valley ambako ghasia za baada ya uchaguzi ziliathiri wengi, wengi walipiga kura ya kupinga katiba hiyo wakisema kuwa itachochea vurugu za kisiasa katika eneo hilo.
Kura hiyo imefanyika bila vurugu lolote ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo ghasia zilizuka kufuatia na kkuwaacha watu elfu moja miatano wakiwa wamefariki na wengine takriban nusu milioni bila makao.
CHANZO CHA HABARI BBC SWAHILI.
Wednesday, August 04, 2010
SOMA
WAMEVAA VITAMBAA VYEUSI MKONONI WAKIMAANISHA KUWA LAZIMA KIELEWEKE(UCHAGUZI URUDIWE)NA WANACHAMA WOTE WAPATE FURSA YA KUPIGA KURA.
SAKATA LA KUPINGA MATOKEO KWA WAGOMBEA WA CCM KUPITIA NGAZI MBALIMBALI ZA CHAGUZI ZILIZO FANYIKA JUMAPILI NCHINI KOTE LIMEENDELEA TENA LEO JIJINI MWANZA PALE AMBAPO WANANCHI WANACHAMA WA CCM KATA YA MBUGANI WALIPOVAMIA MAKAO MAKUU YA OFISI ZA CCM MKOA WA MWANZA, WAKIDAI KUWA UPIGAJI KURA KATA YA MBUGANI URUDIWE KWANI HAUKUTENDEKA KWA HAKI NA KAMA HAUTORUDIWA, BASI WANACHAMA HAO WATARUDISHA KADI ZAO.
WANANCHI HAO WAMEDAI KUWA UCHAGUZI WA DIWANI KTK KATA HIYO HAUKUENDA KAMA ILIVYOPASWA KWANI WANANCHI WALIO WENGI WALIZUILIWA KUPIGA KURA KWA KUAMBIWA KUWA MAJINA YAO HAYAMO KWENYE DAFTARI LA UANACHAMA.
WAMEENDELEA KUHOJI KUWA IWEJE VIONGOZI WA KATA, TAWI NA WILAYA WAWACHAGULIE KIONGOZI WASIYEMTAKA, ALIYESHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU KTK AWAMU ILIYOPITA KWA KUELEMEA UPANDE WAKE MARA BAADA YA KUGUNDUA KUWA ANGESHINDWA UCHAGUZI, HIVYO MBINU CHAFU ZIKAANZA KUTUMIKA(KAMA HIYO YA KUWAZUIA BAADHI YA WANACHAMA KUPIGA KURA).
DIWANI ANAYELALAMIKIWA KUSHINDA KIMIZENGWE KATIKA KATA HIYO YA MBUGANI NI BW.EMANUEL BAHABE ALIYEKUWA AKICHUANA NA WAGOMBEA WENGINE HUSSEIN MANUMBU, MKANGARA, MABINDO NA MASATU.
Tuesday, August 03, 2010
SIASA
Mchakato huo mkali uliofanyika siku ya Jumapili umesababisha kuanguka baadhi ya wabunge.
PICHANI BALOZI GETRUDE MONGELA.
JIMBO LA UKEREWE (WAGOMBEA 10 WALISHIRIKI). Balozi Getrude Mongela kawasambaratisha akina Joseph Lyato na Oswald masatu Monarch.
JIMBO LA ILEMELA (WAGOMBEA 7). Antony Mwandu dialo kawabwaga kiulaini washindani wake wakubwa John Buyamba na Pastory Masota.
JIMBO LA NYAMAGANA (WAGOMBEA 12). Lawrance Masha kawabwaga bila huruma John Mboje Marogoyi na Joseph Kahungwa.
JIMBO LA MAGU (WAGOMBEA 9). Dk. Festus Limbu kawachakaza Abel Busalama na Boniface Magembe.
JIMBO LA MISUNGWI. Charles Kitwanga kawaangusha Jackob Shibiriti(aliyekuwa mbunge) na Madoshi Makene.
PICHANI MBUNGE ALIYEANGUSHWA JIMBO LA BUSEGA DK. RAPHAEL CHEGENI.
JIMBO LA BUSEGA (WAGOMBEA 4). DK Titus Kamani kampiga chini DK> Raphael Chegeni aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo huku akifuatiwa na Nyandwi Msemakweli.
JIMBO LA KWIMBA (WAGOMBEA 7). Shanif Hiran Mansoor kachukuwa jimbo mikononi mwa Bujiku Sakila ambaye imekula kwake.
JIMBO LA SUMVE (WAGOMBEA 8). Richard Ndassa kapiga kachukuwa akifuatiwa na Richard Mchele.
JIMBO LA BUCHOSA (WAGOMBEA 4). DK. Charles Tizeba kalichukua jimbo akifuatwa kwa karibu na mwanaharakati Erick Shigongo, huku aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Samwel Chitalilo akiacha na sura ya mnuno baada ya kukamata nafasi ya tatu.
JIMBO LA SENGEREMA (WAGOMBEA 4). William Ngeleja kaendelea kutamba akiwaacha mbali Kimasa Shejamabu na Joshua Shimiyu.
JIMBO LA GEITA (WAGOMBEA 6). Donard Max kakwea akiwaangusha Jacob Mtalitinya na Costantine Kanyansu.
JIMBO LA BUSANDA (WAGOMBEA 4). Lolencia Bukwimba akitetea ulaji wake vyema mbele ya Tumaini Magesa na Abdala Mussa.
JIMBO LA NYANG'WALE (WAGOMBEA 4). Hussein Amar Gulamali kachukua jimbo kuwatumikia wananchi akifuatiwa kwa kura na Evarist Ndikilo ile hali aliye kuwa mbunge wa jimbo hilo James Msalika akiangukia pua nafasi ya tatu.
Wagombea hawa wote watalazimika kusubiri kikao cha Kamati Kuu ambacho kina mamlaka na idhini ya kufuta wagombea watakaobainika kuwa wamekiuka taratibu za chama hicho - ikiwa ni pamoja na kutoa rushwa kwa wapiga kura, jambo ambalo limedaiwa kujitokeza mara nyingi katika mchakato wa kura za maoni.
Kamati Kuu itakutana tarehe 14 Agosti.
Tuesday, August 03, 2010
SIASA
Msafara wa magari ukielekea katika ofisi za Tume ya Uchaguzi wakati Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akisindikizwa na wana CCM kwenda kuchukua fomu leo
Mgombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Kikwete (kulia)na Mgombea Mwenza Mh. Mohamed Ghalib Bilal wakisaini fomu zao mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Lewis Makame hayupo pichani katika ofisi za Tume ya Uchaguzi leo hii
Picha Aron Msigwa - MAELEZO na Freddy maro.
Tuesday, August 03, 2010
FIESTA
MSANII DIAMOND ALIONYESHA NINI THAMANI YAKE KUJIITA JINA LA HAYO MADINI KWA KUPIGA SHOW MOJA HATARI.
MSANII TOKA ROCK CITY MNAHELA AKIWA AMEJILIPUA'
BROTHER WA KITENGO CHA MASOKO CLOUDS MWANZA, MR. HUMPHREY SIMON NA UA LAKE 'IN ZA HAUSI'.
FIESTA YA KWANZA MWANZA ILIGONGWA PALE VIWANJA VYA UFUKWENI YATCH CLUB, NA KAMA ILIVYOADA WAKAZI WA MWANZA HAWAKUJIVUNGA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA KULA RAHA.
HAPA LILIPIGWA SONGI NA WANAUME HALISI MWISHO KIKAMALIZIWA KIPANDE CHA AKAPELLA FINITO KWA STYLE. ZIKALIPUKA SHANGWE!!!
TOKA USHUANI HADI USWAZI ILIKUWA NI KUSHEA KITU KIMOJA! HONGERA BONGO FLEVA KWA MAPINDUZI TUYAONAYO, KWANI HAKUNA ALIYEFIKIRIA KUWA MUZIKI HUU UNGEWEZA KUKUSANYA MATAIFA NAMNA HII!!
FLOWERS ZA MWANZA NDANI YA FIESTA YATCH CLUB.
EH BANA UZURI WA FIESTA MWANZA NI MAKALI YAKE PAMOJA NA MADHARI ZA VENUE NDIZO HUSABABISHA MARAFIKI KUTOKA MBALI KUFANYA KILA NJIA KUPATA HUDHURIA. PICHANI MTAYARISHAJI MUZIKI MAARUFU NCHINI, MWENYE HISTORIA YA MAPINDUZI YA MUZIKI WA BONGO FLEVA MASTER J KATIKA POZ NA WANAMUZIKI BEATRICE (KATI) NA SHAA (KUSHOTO).
MTAYARISHAJI MUZIKI WA MWANZA CHINI YA LABEL YA TETEMESHA PRODUCTION, AMBAYE VILEVILE YU MTANGAZAJI MAHIRI RADIO FREE AFRIKA, KID BWAY (ALIYE TUPIA KITU CHA DRAFT NA GLASS) AKIWA NA WADAU WA ROCK CITY NA PHILLY KABAGO (MWENYE CAPE KULIA)
WAKATI NAJIULIZA YU WAPI PIPI YULE ALIYEKUWA AKING'ARA NA BARNABA MAJUZI MAJUZI?! NA HATA NISIJISUMBUE KUPATA JIBU NARIDHIKA TUU! MARA BAADA YA KUKIONA KICHWA KINGINE KIKALI, BINTI MWENYE SAUTI YA UKWELI. KAMA NI KUZIKONGA NYOYO ZA WATU WAZIMA KAMA MIE, BASI MPANGO MZIMA ULIMALIZWA NA VIJANA HAWA TOKA PALE THT BARNABA NA LINA.
KATIKA MOJA NA MBILI (TUMBUIZO ASILIA) MULLY B ANAYEIDHURU MACHINE NA DJ STEVE B (MWENYE CAPE) NDANI YA FIESTA MWANZA.
HIVI NDIVYO JICHO LA M'BLOGISHAJI MAARUFU NCHINI MICHUZI JR LINAPOKUWA KAZINI.
CLOUDS CREW NCHA KALI NA FENHE KITU KINAKWENDA LIVE BILA CHENGA 88.1.
POZI LA NIGHT LA WASTAARABU WA MWANZA.
NYUMA YA JUKWAA HIVI NDIVYO WALIVYOKETI WAKISUBIRI TIME YAO KUMWAGA MAUA YENYE HARUFU YA RAHA, KUANZIA KUSHOTO AMINI, MWENYEJI WAO FID Q, JITAH MAN NA PRODUCER RAMAL.