ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 7, 2010

MKUU WA MKOA WA MWANZA AONGOZA ZOEZI LA KUTEKETEZA SILAHA HARAMU.

MH. MKUU WA MKOA WA MWANZA ABBAS KANDORO AKIKAGUA JUKWAA LA SILAHA HIZO HARAMU TAYARI KWA KUTEKETEZWA.

MKUU WA MKOA KTK HOTUBA YAKE:-

KUTOKANA NA MATUKIO YANAYOTOKEA MARA KWA MARA KWA WAMILIKI WA SILAHA KUNYANG'ANYWA AU KUSHINDWA KUTUMIA SILAHA WANAPOKABILIANA NA WAHALIFU, BAADHI YA WANANCHI WANAOMILIKI SILAHA NA WAOMBAJI WAPYA WANAHITAJI MAFUNZO MAALUM YA NAMNA YA KUTUMIA SILAHA WANAZOOMBA AU WANAZOZIMILIKI.

MWAKILISHI KUTOKA RECSA BW.FRANCIS AKIHUTUBIA.

AMBAPO SHIRIKA LAKE LIMEONGEZA MASHINE NYINGINE YA KUWEKA ALAMA KATIKA SILAHA ZINAZOMILIKIWA KIHALALI, SAMBAMBA NA UWEKAJI KUMBUKUMBU ZA SILAHA HIZO KATIKA KOMPYUTA.

KAMANDA SIRO KATIKA HOTUBA YAKE:-

ENEO LA KANDA YA ZIWA NI MOJA WAPO YA MAENEO YANAYOKUMBWA NA WIMBI LA UINGIAJI WA SILAHA HARAMU, HILI LIMETOKANA NA WIMBI LA WAKIMBIZI NA NYINGINE HUINGIA KUPITIA MIPAKA YETU NA NCHI JIRANI. KANDA YA ZIWA IMESHUHUDIA VITENDO VYA MATUMIZI MABAYA YA SILAHA HARAMU KUTUMIKA KATIKA MAPIGANO YA KOO, UTEKAJI WA MAGARI, UPORAJI WA FEDHA, MAPIGANO MIGODINI, UPORAJI WAVUVI NA MAUAJI YA ALBINO MATUKIO YALIYOSABABISHA WATU KUPOTEZA MAISHA HUKU WENGINE WAKIBAKI NA ULEMAVU WA KUDUMU.

WAKIELEKEA JUKWAA LA UCHOMAJI SILAHA HARAMU.

MIKOA INAYOONGOZA KWA MATUKIO YA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA KATIKA KANDA YA ZIWA NI MARA MATUKIO 442, TABORA MATUKIO 199, MWANZA MATUKIO 112, SHINYANGA MATUKIO 78 NA TARIME RORYA MATUKIO 76. TAKWIMU KWA KIPINDI CHA MWAKA 2008 HADI JUNI 2010.

MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA MWANZA ABBAS HUSSEIN KANDORO AKIONGOZA ZOEZI LA KULIKAGUA JUKWAA LA SILAHA ZA KUTEKETEZWA.

ZOEZI LA UCHOMAJI.
WADAU WOTE KAMA ASASI ZA KIRAIA, VYOMBO VYA HABARI NA MADHEHEBU YA DINI SOTE TUNAO WAJIBU WA KUPAMBANA KIKAMILIFU KATIKA KUDUMISHA AMANI KWA KUFICHUA VITENDO VYA MATUMIZI MABAYA YA SILAHA.

MOTO ZAIDI.

JESHI LA POLISI TAYARI LIMEANZA KUBORESHA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA SILAHA ZINAZO MILIKIWA NA WATU BINAFSI, TAASISI ZA KISERIKALI PAMOJA NA MAKAMPUNI MBALIMBALI ZA ULINZI AMBAPO HADI SASA SILAHA ZAIDI YA 65,00 ZIMEHAKIKIWA UPYA NCHI NZIMA, KATI YA SILAHA HIZO 67,000 NA ZOEZI LINAENDELEA.

MTANGAZAJI WA SHIRIKA LA HABARI NCHINI TBC ONE RICHARD LEO AKIANGUSHA NONDO ZAKE TUKIONI.

SEHEMU TU YA UMMA WA WAKAZI WA JIJI LA MIAMBA WALIOHUDHURIA TUKIO HILO.

ILI KUPAMBANA NA UHALIFU HUU WA KUTUMIA SILAHA NCHI ZOTE DUNIANI HATUNA BUDI KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA KWA KUWA NCHI MOJA HAIWEZI PEKEE KUPAMBANA NA UHALIFU. NJIA NZURI NIA KUFANYA MISAKO NA OPERESHENI ZA MARA KWA MARA NA KUENDELEZA MFUMO WA UBADILISHAJI TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU PAMOJA NA TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA.

SHUKURANI ZINATOLEWA NA JESHI LA POLISI KWA WAANDAAJI WALIOFANIKISHA ZOEZI HILI MKOANI MWANZA CHINI YA URATIBU WA REGINAL CENTRE ON SMALL ARMS (RECSA) YANYE MAKAO YAKE NAIROBI KENYA. WAFADHILI SERIKALI YA JAPAN AMBAO WAMETOA MSAADA WA FEDHA ZA KUFANIKISHA ZOEZI HILI MUHIMU KWA KUIMARISHA AMANI KATIKA NCHI ZETU ZA AFRIKA MASHARIKI NA NCHI ZA MAZIWA MAKUU NA PEMBE YA AFRIKA.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. hii fasheni ya kuchoma moto viwanjani na sherehe juu naona imeshika kasi

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.